Rais Samia alivyochochea ukuaji wa uwekezaji kwenye sekta mbalimbali nchini

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetoa taarifa kuhusu mwenendo wa hali ua uwekezaji nchini katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais wa awamu ya sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kueleza kwamba jumla ya miradi 575 imesajiliwa sawa na ongezeko la asilimia 26.

Mchanganuo wa Kisekta wa Miradi iliyosajiliwa Machi 2021- Feb 2023

1. Kilimo - miradi 47 na kutoa ajira 9,133

2. Ujenzi/ Majengo ya Biashara- miradi 44 na kutoa ajira 4,452

3. Miundombinu- miradi 5 na kutoa ajira 17,233

4. Nishati- miradi 2 na kutoa ajira 95

5. Taasisi za kifedha- miradi 4 na kutoa ajira 2,869

6. Rasilimali Watu - miradi 17 na kutoa ajira 1,434

7. Viwanda- miradi 280 na kutoa ajira 44,664

8. Huduma- miradi 30 na kutoa ajira 2,479

9. Mawasiliano- miradi 2 na kutoa ajira 85

10. Utalii- miradi 48 na kutoa ajira 3,2111

11. Usafirishaji- miradi 96 na kutoa ajira 1,532

Katika kipindi cha Awamu ya Sita, Machi 2021 hadi Feb 2023 ikilinganishwa kipindi kama hicho Machi 2019 hadi Feb 2021, thamani ya mitaji ya miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa TIC imeongezeka kwa asilimia 173 kutoka Dola za Marekani 3.16 bilioni hadi Dola za Marekani 8.64 bilioni. #MamaYukoKazini
 
Hiyo miradi toka imeanza imetatua changamoto gani za ajira?

Umeiona hiyo miradi ikifanya kazi ama unadanganywa na taarifa za kwenye makaratasi?
 
Kwa mujibu ya huo taarifa watu zaidi ya 73,000 wapata ajira.
Kama ni hivyo mbona kilio bado ni kikubwa sana, au sio ajira rasmi?
 
Tanzania ndio nchi pekee ambayo inafanya uwekezaji kwenye makaratasi na safari za rais kwenda kutafuta wawekezaji,uku ikiwa na mifumo mibovu ya sheria na kodi.

Enyi chawa wa Dr Samia mwambieni abadili sheria za kodi na kuweka mazingira bora ya uwekezaji , wawekezaji watakuja wenyewe.

"Wajinga hukubali ujinga na ujinga huo huwa kweli"
 
Back
Top Bottom