Rais Samia aagiza Wazazi waliofiwa na watoto 4 kwenye ajali watibiwe kwa VIP Class Muhimbili, JK, MOI na Hospital zote nchini!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,133
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Chalamila amesema Rais Samia ameumizwa sana na vifo vya wanafamilia 4 waliofariki kwenye ajali huko Mbwewe Chalinze.

Chalamila amesema Rais Samia anajua kuwa Mzee Msuya na mkewe walikuwa wanawategemea watoto wao hawa waliofariki, hivyo ameagiza wazazi hawa wawe wanatibiwa kwa huduma ya VIP Class pale Muhimbili, JK, MOI na Hospital zote za Serikali.

Kadhalika kesho ujumbe wa Serikali utatembelea familia moja moja za marehemu hawa kutoa rambirambi rasmi za Serikali.

RIP Sia Msuya na ndugu zako.

Pia soma: Pwani: Magari yagongana uso kwa uso, wanne wafariki
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM mh Chalamila amesema Rais Samia ameumizwa Sana na Vifo vya Wanafamilia 4 waliofariki Kwenye Ajali huko Mbwewe Chalinze

Chalamila amesema Rais Samia anajua Kuwa Mzee Msuya na mkewe walikuwa wanawategemea Watoto wao hawa waliofariki hivyo ameagiza Wazazi hawa Wawe Wanatibiwa kwa huduma ya VIP Class pale Muhimbili, JK, MOI na Hospital zote za Serikali

Kadhalika Kesho Ujumbe wa Serikali utatembelea familia Moja Moja.za marehemu hawa kutoa rambirambi rasmi za Serikali

RIP Sia Msuya na ndugu zako
Ni jambo jema lakini nia hii njema iliyojaa utu izindue mfuko wa hisani wa majanga na matibabu kwa wazee wengine wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa Rais,

Na wazazi wa wengine ambao hawajulikani, na wamezungukwa na lindi la Umasikini wanaweza kupata hii Ofa yako tafadhali?

Na haya maagizo huwa unayatoa kwa kushauriwa na Mtu ama ni utashi wako mwenyewe Mheshimiwa Rais?

Asante.
Mapendo,
TANMO.
 
Hayo maamuzi yanaongonzwa na emotions.
Ni jambo zuri lakini sasa aangalie bima ya afya kwa wote. Kuondoa kifurushi cha watoto ni pigo kubwa kwa raia. Ninwachache watakaomudu kama kina Sia ambao sasa wazazi wanapewa matibabu bure. Mhe umefikiria hawa watoto wa masikini ambao leo wanatakiwa waingie kwenye kifurushi cha wazazi mpaka tzs 1,500,000 kutegemea na idadi ya watoto? Hamna anaelizungumzia hili la bima ya watoto, si wabunge, si wanasiasa, si Serikali.
Mafuta yamepanda tzs 400 kwa lita, dola imepanda dhidi ya shilingi, bidhaa zilishapanda bei zamani.
NHIF wanajua pesa zinakopotelea, posho kwa wajumbe, mishahara, ofisi kila mkoa au wilaya (nyingi wanapanga), magari, mafuta, matengenezo bila kusahau malipo hewa kwa mahospitali (inasemekana)
Sina uhakika kama wanawekeza popote hayo malipo ya wanachama. Tabu tupu
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM Chalamila amesema Rais Samia ameumizwa Sana na Vifo vya Wanafamilia 4 waliofariki Kwenye Ajali huko Mbwewe Chalinze.

Chalamila amesema Rais Samia anajua Kuwa Mzee Msuya na mkewe walikuwa wanawategemea Watoto wao hawa waliofariki hivyo ameagiza Wazazi hawa Wawe Wanatibiwa kwa huduma ya VIP Class pale Muhimbili, JK, MOI na Hospital zote za Serikali.

Kadhalika Kesho Ujumbe wa Serikali utatembelea familia Moja Moja.za marehemu hawa kutoa rambirambi rasmi za Serikali.

RIP Sia Msuya na ndugu zako
Hizo ni ahadi za kitapeli. Mara nyingi ahadi zinazotolewa kwenye misiba huwa zina hisia ya siku husika kwenye msiba, baada ya hiyo simanzi kuisha hakuna utekelezaji wowote. Labda kwa mbali rais angesaini mahali kwenye hiyo ahadi yake. Inshort ni utapeli wa kizamani.
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM Chalamila amesema Rais Samia ameumizwa Sana na Vifo vya Wanafamilia 4 waliofariki Kwenye Ajali huko Mbwewe Chalinze.

Chalamila amesema Rais Samia anajua Kuwa Mzee Msuya na mkewe walikuwa wanawategemea Watoto wao hawa waliofariki hivyo ameagiza Wazazi hawa Wawe Wanatibiwa kwa huduma ya VIP Class pale Muhimbili, JK, MOI na Hospital zote za Serikali.

Kadhalika Kesho Ujumbe wa Serikali utatembelea familia Moja Moja.za marehemu hawa kutoa rambirambi rasmi za Serikali.

RIP Sia Msuya na ndugu zako
Pole sana Mzee Msuya, na Rais kafanya jema.
lkn Mmoja alikuwa anagawa pesa, mwingine hajui kama wako wazee wengi vijijini ambao wamebaki wakiwa kwa kufiwa ghafla na watoto wao. Mi nawafahamu wawili, mmoja wanae wote6 walizama majini ukerewe. Mwingine watoto wake 5 wamekufakatika shughuli za ulinzi wa taifa maeneo mbali mbali. Tupata namba ya Rais tumtumie hawa nao awakumbuke
 
Kiongozi mzima wa nchi anatoa maagizo ya kibaguzi kwa kuwagawa wananchi kwamba hawa wapewe huduma hii wale wengine wasipewe eti kisa tu wamefiwa! Sasa hao amesikia msiba wao je wale wengine ambao hakusikia masaibu yaliyowakuta na wafanyeje wakati nchi yao ni hii hii na Rais wao ni yeye? Viongozi waache unafiki na waache ubaguzi kwa sababu huko mitaani kuna wazee kibao ambao hali zao mbaya na hawana watu wa kuwasaidia kiafya wala mahali pa kulala pia wapo watoto wengi sana wanaohitaji matibabu wazazi wao wamebaki kuzurura mitaani na kwenye vyombo vya habari kuomba misaada bila mafanikio.
Binafsi natoa wito kwa serikali kuboresha zaidi sekta ya afya kwa kuwekeza zaidi katika vifaa tiba,wataalamu wa afya na huku wakiweka gharama ambazo wengi watazimudu na pale inapotokea wachache miongoni mwetu wameshindwa kulipia gharama za matibabu basi kuwe na utaratibu maalum wa kuwasaidia kupata matibabu kama wengine lakini hii tabia ya kujifanya mwema kwa watu wachache tena bila ya vigezo vilivyo wazi,usikute ni kutokana na uhusiano binafsi kwa mmoja wa hao marehemu ndio kigezo kilichotumika.
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM Chalamila amesema Rais Samia ameumizwa Sana na Vifo vya Wanafamilia 4 waliofariki Kwenye Ajali huko Mbwewe Chalinze.

Chalamila amesema Rais Samia anajua Kuwa Mzee Msuya na mkewe walikuwa wanawategemea Watoto wao hawa waliofariki hivyo ameagiza Wazazi hawa Wawe Wanatibiwa kwa huduma ya VIP Class pale Muhimbili, JK, MOI na Hospital zote za Serikali.

Kadhalika Kesho Ujumbe wa Serikali utatembelea familia Moja Moja.za marehemu hawa kutoa rambirambi rasmi za Serikali.

RIP Sia Msuya na ndugu zako

Maamuzi ya Kisiasa tu haya.
 
Ni jambo zuri lakini sasa aangalie bima ya afya kwa wote. Kuondoa kifurushi cha watoto ni pigo kubwa kwa raia. Ninwachache watakaomudu kama kina Sia ambao sasa wazazi wanapewa matibabu bure. Mhe umefikiria hawa watoto wa masikini ambao leo wanatakiwa waingie kwenye kifurushi cha wazazi mpaka tzs 1,500,000 kutegemea na idadi ya watoto? Hamna anaelizungumzia hili la bima ya watoto, si wabunge, si wanasiasa, si Serikali.
Mafuta yamepanda tzs 400 kwa lita, dola imepanda dhidi ya shilingi, bidhaa zilishapanda bei zamani.
NHIF wanajua pesa zinakopotelea, posho kwa wajumbe, mishahara, ofisi kila mkoa au wilaya (nyingi wanapanga), magari, mafuta, matengenezo bila kusahau malipo hewa kwa mahospitali (inasemekana)
Sina uhakika kama wanawekeza popote hayo malipo ya wanachama. Tabu tupu
Hawa wazazi hizo pesa tu za mtoto wao Sia,kumbuka Sia hakuwa na watoto wala mme.So pesa ya mafao ya kazini kwake yote itakwenda kwa wazazi wake.Na ingetosha kuwakatia bima mpaka mwisho wa maisha yao .Hao wazee si choka mbaya.
 
Back
Top Bottom