Rais Putin: Kama mnataka vita iishe acheni kuipa Ukraine silaha

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Bomu.JPG
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema mataifa ya Ulaya yanatakiwa kusaidia kumaliza vita dhidi ya Ukraine kwa kuweka shinikizo kwa Rais Volodymyr Zelensky na kusitisha kumpelekea silaha.

Rais Putin amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ambaye alikuwa akishawishi kumaliza vita hiyo baada ya Urusi kuivamia kijeshi Ukraine.

Nchi za Magharibi zimekuwa zikiisaidia Ukraine kwa vifaa vya kujilinda na kupigana na Urusi, jana Mei 2, 2022 Uingereza kutoa msaada wa vifaa vya dola 376m ikiwemo vifaa vya kielektroniki vya vita, mfumo wa rada, vifaa vya GPS na vifaa vya kuona usiku.

Maelfu ya watu wakiwemo raia wa kawaida wameuawa au kujeruhiwa katika vita hiyo tangu ilipoanza Februari 24, 2022.

Rais Macron ndiye aliyempigia simu Rais Putin na kusema yupo tayari kusaidia kumaliza mgogoro huo.


Source: BBC
 
ugomvi wa kuchangiwa hata wakiwa watoto wadogo wanaweza kukupiga.
kwani mzee Gaddafi kaangushwa na Nani?kama sio hao wamarekani na wazungu waliowapa silaha raia
Lakini Putin aliyajua haya yote,alijua anakwenda kulipiga Taifa dhaifu kijeshi kuliko yeye,na Ukraine kusaidiwa alilijua mapema tu ndiyo maana akatoa lile onyo,sasa tunachoshangaa kwa nini asitekeleze kwa vitendo lile onyo lake kwa watakaomsaidia Ukraine?
 
Naona watu mumesoma heading tu, bila content mkaanza comments. Putin kapigiwa simu na macron akiombwa asitishe vita, siye yeye aliyeomba Bali Macron. Naye jibu lilikuwa ni kumwambia macron vita itaendelea unless waache kuipa Ukraine silaha Kama kweli wanataka vita iishe.
 
Alijua Vita itakuwa ndogo tu.
Sasa kila siku anaona jamaa wanapewa misaada yeye yupo peke yake.
Lakini Putin aliyajua haya yote,alijua anakwenda kulipiga Taifa dhaifu kijeshi kuliko yeye,na Ukraine kusaidiwa alilijua mapema tu ndiyo maana akatoa lile onyo,sasa tunachoshangaa kwa nini asitekeleze kwa vitendo lile onyo lake kwa watakaomsaidia Ukraine?
 
mwandishi uliyeleta hii mada naona wachangiaji wengi hawajakuelewa.. wengi wanafikiri Putin ndo ameziomba nchi za magharibi zisitishe kutoka siraha kwa Ukraine.. kumbe Putin Alikuwa anamjibu macroni awambie ndugu zake waache Ku supply silaha ndo vita itakoma!
 
Back
Top Bottom