Rais punguza safari, jikite kujenga nchi

Sioni ubaya wowote wa Raisi kusafiri,ila ubaya uko kwenye uchoyo wake wa Katiba mpya ya wananchi.
View attachment 2005449
Hiyo katiba unataka eabafili nini humo? Wabadili nini? Wengi hawakujua Kama VP anaweza kuwa Rais maana they never read it and they don’t even know when it was changed.
I don’t blame her for that, katiba katiba to change what? It’s too general just Katiba. Tell her what you want changed in there!!!!
 
Nawasalimu kwa Jina la Mungu muumba wa mbingu na ardhi.

Jamani, kusafiri ni jambo jema katika kujenga diplomasia na mahusiano ya nchi na nchi. Haipingwi wala haina neno.

Lakini hii kutwa mama wa nchi kukimbizana angani kila wiki inakuaje?

Leo yuko Scotland, kesho Cairo, kesho kutwa Ubelgiji!! HAPANA.

Kitu chenyewe anachokifuata huko ni kujadili kuhusu sijui wingi wa joto angani!!

Jamani, mama yetu tunakupenda sana. Wazungu wako mbali mno, wana muda wa kujadili petty issues. Wewe huo muda hauna.

Wazungu walishajenga nchi zao, sasa hivi wamebaki kujadili kuhusu masuala mepesi mepesi, mara sijui joto angani, mara sijui hali ya upepo jangwa la saharaa!!

MAMA, achana na hao. Jikite kujenga TANZANIA. Maji, Umeme, Ajira, Bei ya bidhaa, Kilimo, Miradi, Miundombinu, usafirii...

Acha mambo ya kubembea Ulaya, hayakusaidii wala hayaisaidii nchii.

Tunakupenda sana na tusingefurahi uharibikiwe. Jenga nchii, jenga uchumi utaepuka kukopa kopa hovyo na kutengeneza tozo za ajabu ajabu zisizoeleweka kisheria wala kimantiki.

Raise taxes, madini simamia, maliasilii, nidhamu kazini na maofisini, pambana na ufisadi. Jenga nchi.

Itakusaidia. Wazungu hawawezi kukujengea nchi. Watakupiga bao wakati wewe unazubaa angani na hiyo midege kila wiki... angani... vuuuu.... vuuuu .... vuuuu... vuuuu...nenda rudi... vuuuu .... vuuuuu... kila wiki... vuuuu .... vuuuu... vuuu....

Wao wanasomba madini, wewe unabembea kwenye ndege. Mafisadi yanaitafuna nchi wewe uko angani unaenda kunywa juisi Ulaya.

Ngoma ikivuma sana iko mbioni kupasuka.

Wasalaam.

5E9E0D75-EEF9-43A8-8F77-845CEBE2416D.jpeg
 
Hiyo ni husda tu inakusumbua. Mahusiano yetu kimataifa yalikua yamekwisha kabisa. Mama anasafiri na anafanya yote hayo ya afya, maji, miundombinu etc etc. Umekimbilia tu kulaumu lakini rejea kiwango cha uwekezaji tangu mama ashike dola ambacho kimeongezeka mara dufu kitokana na mahusiano mazuri mama aliyoyarejesha.
 
Hiyo katiba unataka eabafili nini humo? Wabadili nini? Wengi hawakujua Kama VP anaweza kuwa Rais maana they never read it and they don’t even know when it was changed.
I don’t blame her for that, katiba katiba to change what? It’s too general just Katiba. Tell her what you want changed in there!!!!
Mbona mapendekezo yamo kwenye rasimu ya Warioba
Unaweza kuyapitia ndugu wa Mwime ya ilindi
 
Huyo kichaa wenu msimfananishe na Mama, nambie Rais yupi ambae hasafiri kujadiliana na wenzie?? Hata baba ktk familia huwa anatoka kutafuta mkate kwa watoto, nyie misukule ya dikteta mmevurugwa
Ukiona Baba/Mama,wana Mashamba alafu wakati wa kulima yeye ni kudhurula kwa jirani,jua huyo mzazi wako ni mvivu na amwezi pata maendeleo yeyote, mwisho wa siku utasikia amelikodisha hilo shamba ili mwisho wa siku apewe mazao kidogo ambayo hayawezi kutosheleza family, mwisho hiyo family itakuwa ombaomba.
 
Kwenda kusaini mikataba kama alivyofanya Kikwete. All contracts tunawafuata. Get ready 10 years ya Samia nchi itafilisika. Mabenki ya I Swiss yatajaa hela za wantszania. Get rid of her, she is useless. Rudisheni Zanzibar. Si make wa 4 huyo kwa mime wake, any woman accepting poligamy is sick not fit to be a leader. Hawezi kuongoza hata mtaa.
Wacha mfilisike hizo zote ni laana ya kuivamia Zanzibar Na kumwaga damu. Dua ya mwenye kudhulumiwa hairudi hata bado
 
Hiyo ni husda tu inakusumbua. Mahusiano yetu kimataifa yalikua yamekwisha kabisa. Mama anasafiri na anafanya yote hayo ya afya, maji, miundombinu etc etc. Umekimbilia tu kulaumu lakini rejea kiwango cha uwekezaji tangu mama ashike dola ambacho kimeongezeka mara dufu kitokana na mahusiano mazuri mama aliyoyarejesha.
Miundombinu ipi?maji kila siku shida tuko kwenye mgao, umeme ndio usiseme,tumerudi enzi hizo wakati haya Mambo tulisha yasahau,Samia amechaguliwa na Watanzania sio Wazungu, hivo akatutue shida za Watanzania sio kila siku angani.
 
Ukiona Baba/Mama,wana Mashamba alafu wakati wa kulima yeye ni kudhurula kwa jirani,jua huyo mzazi wako ni mvivu na amwezi pata maendeleo yeyote, mwisho wa siku utasikia amelikodisha hilo shamba ili mwisho wa siku apewe mazao kidogo ambayo hayawezi kutosheleza family, mwisho hiyo family itakuwa ombaomba.
mungu wenu wa Chatttle kwakuwa alikuwa anaogopa kusafiri,mnataka kila mtu amuige yeye,niambie Nchi gani ambayo Rais wake anajifungia ndani tu hasafiri kukutana na wenzie!? Wa mwisho na wa Kwanza alikuwa huyo ambae mnamuabudu
 
Katika kitu alichofanikiwa bwana mkubwa kukaririsha watu,Marais wote jirani zetu wasafiri,TZ sio kisiwa Mwalimu alisafiri,MAMA acha apige kazi,kila akienda sehemu matokeo yake yanaoekana.
 
mungu wenu wa Chatttle kwakuwa alikuwa anaogopa kusafiri,mnataka kila mtu amuige yeye,niambie Nchi gani ambayo Rais wake anajifungia ndani tu hasafiri kukutana na wenzie!? Wa mwisho na wa Kwanza alikuwa huyo ambae mnamuabudu
Kikwete alisafiri dunia mzima na sehemu nyingine alirudia mala mbili au tatu, Nchi ilifaidika na nini?kama sio madeni na ufisadi aliotuachia! kudhurula ni ishara ya uvivi tu,yeye mbona atembelewi?bora Magufuri waliokuwa wanakuja wenyewe
 
Yule alipokuwa hasafiri tulikuwa tuna lalamika

Sahivi SSH ana safiri tuna complain

Wabongo hatujuwi tunataka nini

Ova
Hakuna Raia wa kawaida walilalamika JPM kutosafiri
Waliolalamika ni CHADEMA, kwa sababu ya kutafuta Mambo ya kumkosoa Rais.
 
mama anafungua nchi....hahahaaha.

yule jamaa kuna watu wanasema hakukuwa na demokrasia alikuwa mnyama mara hasafiri kajifungia tu, lakini watu wale wale leo wanasema nchi ina deni kubwa jamaa alikopa sana....sasa sijui wazungu walimkopeshaje mtu asiyefuata demokrasia wala haki za binadamu na wala hatembei kwenda kuomba misaada...
Definitely
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom