RAIS Obama Adaiwa Kuisaliti Ndoa Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAIS Obama Adaiwa Kuisaliti Ndoa Yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 3, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,080
  Likes Received: 5,556
  Trophy Points: 280
  Obama Adaiwa Kuisaliti Ndoa Yake
  [​IMG]
  Vera BakerMonday, May 03, 2010 3:47 AM
  Rais Barack Obama wa Marekani amekumbwa na skendo la kuisaliti ndoa yake kwa kujivinjari na mwanamke aliyekuwa mstari wa mbele kwenye kampeni zake za uchaguzi wakati alipokuwa akigombea useneta miaka sita iliyopita.Rais Barack Obama wa Marekani anadaiwa kuisaliti ndoa yake na Michelle Obama kwa kujirusha na mrembo wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Vera Baker.

  Mwaka 2004 wakati Obama akipiga kampeni za useneta ilidaiwa kuwa alijivinjari chumba kimoja hotelini na mrembo Vera Baker ambaye wakati huo alikuwa ana umri wa miaka 29.

  Wakati huo Vera alikuwa mdau wa karibu wa Obama kwenye kuchangisha fedha za mfuko wa kampeni na alifanikiwa kuchangisha mamilioni ya dola.

  Miaka sita ikiwa imepita bila ya ushahidi hata wa picha kutolewa, jarida maarufu la Marekani National Enquirer limeliibua upya soo hilo likisema kwamba lina ushahidi wa video kuthibitisha kuwa Obama aliisaliti ndoa yake.

  Jarida hilo ambalo lilijipatia umaarufu mkubwa mwaka jana baada ya kuibua skendo la mgombea urais John Edwards kuwa anajivinjari kwa siri na mrembo Rielle Hunter na kwamba amezaa naye mtoto mmoja.

  Skendo hilo lilipoibuliwa wakati huo, Edwards alikanusha vikali lakini ilipogundulika kuwa ni kweli, jarida la National Enquirer lilijipatia umaarufu mkubwa sana na kugeuka kuwa chanzo cha habari kwa vyombo vingine vya habari.

  Hivi sasa National Enquirer linasema kwamba lina ushahidi wa video za kamera ya ulinzi kwenye hoteli ya jijini Washington D.C ambayo Obama na Bi Vera wanadaiwa kupumzika kwenye chumba kimoja.

  Jarida hilo limesisitiza kuwa iwapo watu wataziona video walizo nazo basi wataamini kuwa rais Obama aliisaliti ndoa yake na Michelle Obama.

  Obama hajasema chochote tangia National Enquirer lilipoliibua tena skendo hili ingawa Vera alishawahi kukanusha kuwepo kwa uhusiano wowote wa kimapenzi kati yake na Obama.

  Wafuasi wa chama cha Democratic cha rais Obama wanaamini kuwa skendo hili ni njama za Republican kummaliza kisiasa rais Obama.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,080
  Likes Received: 5,556
  Trophy Points: 280
  Mhhhh jamani hata hivyo kimwwaana kinalipa ngozi nyeusi si mchezo
   
 3. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wanalipa wangapi dunia hii?
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wazungu wanahangaika sana juu ya Obama lakini bado tu hawakubali kuwa amekuwa rais wao...hahaaa wamarekani bana
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  KAazi kwer kwer
   
 6. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  angalia historia ya wademocrats, huwa kuna pepo la ngono linawafuata siku zote. clinton alishashindwa kwenye jaribu hilo, obama ataweza wapi. inawezekana alifanya kweli. lisemwalo lipo...
   
 7. Causin

  Causin Member

  #7
  May 4, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sina uhakika na jibu lako,coz navyoona hata Michelle yupo juu sana tu,labda kama alitaka mambo mengine ambayo cyajui
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  May 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Wazungu wanahangaika kivipi sasa wakati wao ndio waliomweka madarakani? Au hujui kuwa wazungu bado ni overwhelming majority Marekani? Mtu kashinda majimbo kama Iowa, Oregon, Wisconsin n.k. ambako wazungu ni zaidi ya asilimia 90 ya population nzima halafu bado unadai wazungu wanahangaika? Ujinga kitu kibaya sana.....ungesema wapinzani wake kisiasa ungekuwa na hoja...lakini hii ya wazungu huna hoja kabisa maana wazungu kwa wingi sana walimpigia kura. Bila wazungu asingeweza kuwa raisi....hivi unalijua hilo? I doubt it.....
   
 9. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mukulu Nyani NGABU.. Lainisha lugha kidogo na punguza jazba TAFADHALI.. TUMEKUSOMA...
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  tehteh Nyani bana umetumia neno safi sana UJINGA ila sio UPUMBAVU...haya wanayoyasema sasa walikuwa na muda wa kuyasema wakati wa kampeni...sasa sielewi wanachozungumza sasa.Nakumbuka mpaka kuna mmoja alisema cheti cha kuzaliwa cha Obama ni cha ku forge sasa sijui aliishia wapi?anyway kweli mimi mpumbavu
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sie tushamzoea huyu wala si mgeni kwetu...
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,493
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Mh, ingekuwa na hapa kwetu yanachimbuliwa hayo, Mheshimiwa ange............!!!?? tehetehe
   
 13. B

  Baba Ubaya Senior Member

  #13
  May 4, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili jibu nilipenda jamaa bado ana fikra za kibaguzi huyu.
   
 14. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kawaida hiyo sioni cha ajabu
   
 15. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  kwani aki-do nje ya ndoa inakula vipi kwako zaidi ya michel!?
   
 16. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi wewe unafikiri ubaguzi umeisha?Unaishi dunia gani?Tusiwe wanafaki kujaribu kupindisha mambo,tujaribu ku-acknowledge baadhi ya mambo.Ulimwengu mzima unasema ubaguzi hakuna hilo linabaki kwenye maandishi na mazungumzo lakini ukweli hupo katika mambo mengi tu!Kuanzia South Africa,United States haya mambo yapo kote huko na uthibitisho hupo sema mabeberu wanahukumu kila mtu anayetaka kuonesha ubaguzi uliopo.

  Kwa hiyo inawezekana wazungu walimpigia kura Obama na wakamfanya ashinde lakini je hii pekee yake inatosha kusema hawa jamaa si wabaguzi?Siasa si kitu cha mchezo,kampeni huwa zinabadili watu toka mtazamo mmoja kwenda mwingine hivyo mtu anaweza aka-vote kwa Obama kwasababu nyingine lakini bado akawa shaka na uwezo wa Obama kama raisi mweusi wa kwanza....hili linaweza kuwa suala la ubinadamu tu lakini pia hali hiyo inaweza kuashiria namna ya ubaguzi. Je,si kweli kuwa baada ya muda mfupi wa uongozi wa Obama baadhi ya waliompigia kura hawampendi tena na sababu za rangi ziko pale?  Huo unaonekana kwenye hii video sio ubaguzi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Duh.aisee hebu subiri kwanza twende polepole..hiyo clip hebu tupe kidogo nani ni nani hapo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  huyu mzungu si ndy walewale na yule aliyemwagwa mav, wabaguzi masalia. ningekuwapo mimi ningemuumua manundu mbele ya kadamnasi
   
Loading...