Rais ndiye kiongozi mkuu wa nchi tumempa nafasi tumwache afanye kazi yake, kelele za nini?

Environmental Security

Senior Member
May 21, 2020
181
261
Kwanza nianze kwa kusema mimi ni mtu ninayeamini katika kutii mamlaka na kuiheshimu.

kwakusema hivyo namuunga mkono rais na serikali na ninatii na kuheshimu hatua wanazochukua katika kuongoza taifa letu.

Watu tusijifanye tunajua sana kuhusu corona kiasi cha kuona kama rais na serikali wamepotea na hawajui lolote ktk kupambana na corona. Kama mna mbinu zitajeni na mueleze wapi ambapo zimefanya kazi, mbona kwote wanapambana tu na hakuna aliyefika bado. Acheni dharau kwa serikali yenu ndugu zangu.

Umekaa tu kwenye keyboard unajiona unakila haki ya kuona serikali haiwezi, mengi mnayoshauri mnaiga tu kwa nchi nyingine zinavyohangaika wala hakuna mwenye jipya na mjue nayo serikali inaona huko wanavyofanya lakini haikurupuki tu kama wewe eti wakiona wale wamefanya hivi hapo hapo nasisi tuseme waTz fanyeni hivi. Acheni zenu.

Magufuli kama anajua chanjo na mabarakoa yanaondoa kabisa corona anaanzaje kuyazuia tena itamnufaisha nini yeye kukataa chanjo we jiulize usikurupuke tu kujidai unajali Watanzania kuliko rais na serikali.

Tumempa nafasi tumwache afanye anachokiamini ni kwaajili ya manufaa ya taifa ili akikosea au akipatia iwe lawama kwake au hongera kwake sio miluzi mingi kila mtu anataka rais afanye analotaka yeye hapo itakuwa nyie ndio rais sio yeye.

wote tunajua Mungu anaweza yote rais kasema tumuombe Mungu. Wewe tii kama huamini tumia hizo mbinu zako. Mimi na nyumba yangu tutamtegemea Mungu aliyetuvusha atatuvusha na rais na serikali yote tutakuwa salama kwa jina la Yesu. Amen.

hongera rais kwa kutuongoza njia sahihi, tupo tunaokuunga mkono na kutii mamlaka ya serikali.

Mungu akulinde Rais wetu Magufuli na serikali yako na atatuvusha salama wote tunaomwamini. Asiyeamini hata kama yupo serikalini atajua mwenyewe.

Utukufu kwa Mungu juu, na amani iwe duniani kwa wote aliowaridhia.

Amen
 
Rais ni kinyago chetu timekichonga wenyewe, HATUPASWI kukiogopa kamwe.

Rais ni mtumishi wa watu, yeye ndiye atasikia sisi tunataka nini. Kama ni suala la Chanjo asitusemee, atuache tuchague wenyewe. Wanaotaka wakachanje, wasiotaka wasichanje.

Ila asidhani yeye ndiye mwenye akili kuliko Watanzania wote, LA HASHA yeye wa kawaida sana na kuwa kwake RAIS wa Tanzania ni BAHATI tu wala siyo kwamba ana hekima au maono kuliko Watanzania wengine.
 
Nimecheka kwa nguvu huu uhuni ulioandika hapa, eti umpe fundi kandarasi ya kukujengea nyumba kisha uone anaharibu, uamue kukaa kimya mpaka amalize ndio uongee! Kumbuka yeye ni kiongozi tu, na anatawala kwa matakwa ya wananchi na sio kwamba amekabidhiwa watoto wadogo awavushe barabara.

Tumeshaumwa na nyoka. Enzi za JK tulipiga kelele kuhusu mradi wa gas kuwa kuna ufisadi ndani yake. Watetezi waliokuwa kwenye ulaji wakati huo ikiwemo Magufuli walikuwa kimya, na wengine wakitetea kama ww ulivyofanya hapa. Na lugha zilikuwa hizi hizi kuwa rais anajua kuhusu huo mradi hivyo tumuache afanye kazi. Alipoingia Magufuli anasema gas sio yetu tumepigwa na wajanja, sasa hivi yuko anajenga umeme wa maji kwa mkopo wa 6.5t ambao tuliambiwa tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi, na kundi hili hili la kina Magufuli. Halafu unataka tukae kimya kwa watu wa aina hiyo?

Unasema tumempa kazi Magufuli, kwanza hakuna uhakika kama alishinda uchaguzi, ana hata kama alishinda ni kwa kura kiasi gani. Wote tulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, na wizi mkubwa ikiwemo mauaji na vilema hasa wapinzani. Kwa ujumla yuko madarakani kwa wizi wa kura na sio kwa ridhaa ya wananchi. Hii ndio maana anaongea kwa kushurutisha, na sio kwa ushawishi wala utaalamu wa kisayansi. Kama unamuamini muamini ww maana unafaidika na madaraka yake.
 
Kwenye vifo hakuna siasa. Mwenzako anasema haogopi wakati anatembea na wanajeshi kila mahali!

Tatizo la mfumo mbaya ni hili sayansi ingetakiwa kutegemea idara za kisayansi sio mwanasiasa ameamkaje. Vilevile rais ukisema kitu weka ushahidi.
 
Nikweli ila Raia wanakumbuka katiba inavyo tuongoza inasema Serikali haina dini ila watu wake wana dini ndio maana hakuna wizara ya mambo ya dini bali dini ni kisehem ktk wizara ya sheria. Ila mwisho nikweli kwa katiba yetu no way zaid yakutii anayosema mkuu maana katiba imempa mamlaka so tuwe wapole.
 
Rais ni kinyago chetu timekichonga wenyewe, HATUPASWI kukiogopa kamwe.

Rais ni mtumishi wa watu, yeye ndiye atasikia sisi tunataka nini. Kama ni suala la Chanjo asitusemee, atuache tuchague wenyewe. Wanaotaka wakachanje, wasiotaka wasichanje.

Ila asidhani yeye ndiye mwenye akili kuliko Watanzania wote, LA HASHA yeye wa kawaida sana na kuwa kwake RAIS wa Tanzania ni BAHATI tu wala siyo kwamba ana hekima au maono kuliko Watanzania wengine.
Kwanza tunajuta kwa kuwa na jitu kama hili linalotaka matamanio yake yawe ya sisi wote.
 
Back
Top Bottom