Rais Museveni anachochea chuki baina ya Tanzania na Kenya

Tujenge tu bomba, Museveni akitukubali tufanye naye business, akitukataa tunalibadilishia matumizi liwe bomba la maji, lisaidie kusambaza maji vijijini

Wala siyo ya Maji tu! Gesi je? Situnaweza wauzia Uganda,Burundi,Rwanda?.
Serikali iweke offer nzuri mezani na Uganda! Tuna nafasi kubwa na Kenya hawawezi kushindana na sisi!
 
Mkuu, ninafahamu vizuri hoja yako na sina tatizo katika msingi wa hoja yako.

Tatizo ninaloliona ni maamuzi tofauti kati ya wawekezaji na serikali ya Uganda ambayo yanajenga sintofahamu na kutoaminiana kati ya Tanzania na Kenya.

Mixed statements zinaleta confusion lakini pia zinajenga ufa katika nchi zilizoko ndani ya jumuiya ya EAC.

Statements za Boss wa TOTAL na Rais Museveni zinapishana!

Mkuu pamoja na statements za hao wawili kupishana Nd. Yoweri Kaguta hana ujanja hapo, he is trying to rescue the situation on his part. Maji ya shingo yamemfika.
 
Mazee hii ishu si yamchezo.Pini waliyopigwa leo wakenya pale airport ya Tanga si mchezo.Waziri wa nishati wa uganda leo amekuja tanga kwa usafiri wa anga.Kumbe wakenya nao wamejileta ili wasome ramani za kila kitu kinachoendelea. Tena mpka gharama za huyu waziri pamoja na wao wenyewe imelipwa na wizara ya nishati ya kenya.Sasa walivofika tu airport migration wako kama mvua.Kilichofanyika ni kuwaruhusu wananchi wauganda na wazungu wao kupita lakini wote wale wakenya walinyang'anywa passport zao na kuambiwa mtangoja hapa VIP LOUNGE,mpaka hawa wengine warudi. So waganda na uongozi wa gvt ya tanzania walienda kufanya yao.Waziri wao wa nishati na timu yake walibaki wanatoa macho.Mazee tz tuiache ilivo...hili tikio leo lilikuwa lakimafya sana sana.Ni mengi..ila chkueni hayo machache.
Mkuu, Thanks kwa kutuletea habari ambayo inakuja kuwa ni habari ya kweli!

Tanzania itajengwa na Watanzania!
 
Aksante kaka kwa kunipa cheo nisichokitamani duniani, labda kiswahili chako kimekuzwa katika mapokeo yenye mushkeli na "ashki" zinazotaka kukugombanisha na wenza. Hii inajionyesha jinsi unatumia meneno vibaya bila hata kufikiria, kwa mfano neno strategy kiswahili ni mkakati, sasa sijui ashki zako zinakutuma tofauti na sie wenzako.
Na pia katika biashara hakuna mkakati wa kukufanya upoteze dhamira na heshma yako, sio kila biashara unairukia bila kutizama nini kitakachojiri baadae. Nakupa mfano mmja tunalo bomba la TAZAMA Pipeline mbona wakati likijengwa hatukusikia chokochoko au mikakati ya kinafiki?
Hii ni biashara na ukumbuke Kenya suala la ardhi ni gumu saaana. Wenye maeneo ni watu wazito na wanajua utamu wa hii biashara. Mtu hakubali kupitisha bomba kwenye ardhi yake hivihivi, wanataka kukodisha ardhi sio kuuza vipande vya ardhi bomba likapowakuta watu walio hodhi ardhi.
Nyinyi mnataka kukurupuka kama kawaida yenu ili watu wenye maeneo yatayopitiwa na mradi yauzwe. Lazima mfikiri vizuri, kama umebahatika kuhodhi eneo liliwekwa mnara wa simu utakubailiana nami kwamba ni ujinga kuuza eneo. Dunia hii imebadilika leo hii vijiji linakopita lile bomba la TAZAMA hawapati hata pingili ya shilingi. Wewe unang'ang'ania fitna zisizo na mashiko.

Naona hujawahi fanya biashara wewe, na hauwajui wakenya wewe.
Au wewe ni miongoni mwa watu walioonja kadhia ya kuzuiliwa kuingiza magari ya kubeba watalii pale JKIA na hivyo unaogopa watawatimua tena?
Unajua kwa nini waliruhusu haraka kurejewa kwa utaratibu wa awali?
Unadhani ni kwa nini Kenya walishadiriki kutangaza kuwa Mt Kilimanjaro ipo kwao?
Unashangaa ni kwa nini tunachukulia kawaida kupigana nao vikumbo kwenye hili dili?
Yeyote anayekuja na mawazo ya kuturudisha nyuma ktk hili dili mimi namshuku kuwa ni mkenya, na iwapo anaposti hapa itakuwa ni kwa unafiki.
Kama wewe si mkenya basi unafiki haukuhusu lkn mwenyewe fikiria Serikali ya Kenya inagharamia safari ya officials wa Uganda kuja kuservey Tanga port na wao wanajichanganya humo, why? Na wao ni stakeholders ktk huu mradi? Kwa mawazo yako ulitaka na wao waruhusiwe kuservey bandari?
Aisee nakushangaa sana
 
Ikumbukwe kuwa Jumuiya hii mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 na kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).

Kile ambacho Uganda inakifanya kwa sasa kuhusu ‘’umalaya’’ katika maamuzi unajenga chuki kati ya Tanzania na Kenya.

Uganda inakuwa kama mwanamke anayetongozwa na wanaume wawili kutoka katika familia moja huku akimkubali kila mmoja. Mbaya zaidi, anajitokeza mbele ya kandamnasi na kusema huyu pia ni mwanamme wangu. Wananchi wengine wanabaki wanashangaa na kujiuliza, what’s going on?

Kinachotia wasiwasi, hatufahamu huyu mwanamke anaongea nini zaidi wakati akiwa ndani ya chumba kuhusu mwanamme mwingine anayedai pia anampenda.

Huu ujenzi wa bomba la mafuta unaweza kuleta matatizo makubwa katika mahusiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kuwa, Mwezi August, 2015 tulihabarishwa kuwa Kenya na Uganda wamekubaliana na kuweka saini kujenga hilo bomba la kusafirisha mafuta. Less than two months, on Oct 2015 tukaambiwa Uganda and Tanzania have signed an agreement to explore the possibility of building a crude oil pipeline between the two countries.

Mwezi March 1, 2016, Rais Magufuli na Rais Museveni wakaonekana mbele ya waandishi wa habari wakisema wamekubaliana kuhusu mpango wa kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka bandari ya Tanga, Tanzania hadi Uganda.

March 14, 2016, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo alienda Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumuhakikishia Rais Magufuli kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

March 21, 2016, Tukaambiwa tena, Rais Kenyatta na Rais Museveni walikutana jijini Nairobi kujadili tena ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huu ulifanyika siku chache tu baada ya Uganda na Tanzania kuafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda.

Kwa sasa jopo la wataalam wa Uganda wamebaki Kenya wakitembezwa huku na kule ili kujionea hali halisi ya fursa zitakazopatikana baada ya kujengwa bomba.

Kuna wengine wanaweza kudhani hili ni suala la kawaida lakini mimi ninaliona ni suala hatari sana katika mstakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ningemwelewa Rais Musevevi kama angekuwa anafanya huu ''umalaya'' kwa nchi ambazo haziko ndani ya EAC.

Rais Museveni anachochea ugomvi/uhasama sio kwa Marais wa Tanzania na Kenya pekee bali hata kwenye Mstakabali wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Rais Musevevi asikubaliwe kufanya biashara kwa mgongo wa kujenga chuki kati ya Tanzania na Kenya. Huu ni unafiki na uzandiki wa kiwango cha juu.

Someone must tell Rais Museveni to stop it, just play fair business game. He doesn't have to do all that mumbo jumbo.

UPDATE:
Niliyokuwa nahofia kutokea katika mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kwa sababu ya ''umalaya'' wa Serikali ya uganda yameanza kutokea baada ya Waziri wa Kenya na kundi lake kuzuiwa na TISS kwenda kwenye Bandari ya Tanga baada ya kuwasili Airport.

Kwa habari kamili gonga hapa;

Tanzania ijipange kubuni na kutekeleza mipango yake kwanza. Badala ya kushabikia ya majirani hata kama ni ya EAC. Kumbukeni kwamba Kenya na Uganda njia yao moja kuelekea bahari ya Hindi kwa reli na barabara, hivyo hata iweje, miundombinu hiyo watailinda sana. Sisi mambo yetu hayaeleweki, badala ya kuimarisha zaidi reli ya kati na bandari ya DSM sijuwi nani katulazimisha kujenga bandari ingine Bagamoyo! Mradi wa bomba la mafuta ya Uganda huenda ukatuyumbishwa bure na kutuvurugia mambo yetu ikiwa Museveni hana msimamo. Hatuna sababu ya kuyumbishwa. Tuna resources nyingi kuweza kufanya yetu. Tuachane na project za kisiasa kama daraja labaharini just for the sake of it! Hivi kweli tunajenga daraja la ku-divert traffic ili magari yapite juu ya bahari tu? Magorofa ya anasa tena kwa pesa za mifuko ya pensheni za wafanyakazi ambao wakistaafu wanasotea haki zao kama ombaomba! Ngoja niseme kidogo tu kuhusu hizi flyovers. Hizi flyovers lazima ziwezeshe transit traffic kuupita mji juu kwa juu, kutoka upande mmoja wa jiji kwenda upande mwingine bila kuchanganyika na trips za ndani ya jiji. Kwamfano kuwe na barbara ya inayomuunganisha mtu atokae Tanga na Bagamoyo moja kwa moja aunganishe Kilwa road to Lindi, au na Morogoro road to Mbeya na Dodoma nk. Siyo atoke Oysterbay kwenda city centre kupitia baharini! Hiyo siyo flyover kwa mantiki ya njia ya kupitiliza juu kwa juu.
 
Mbaya zaidi, nchi zilizoko kwenye EAC ndio zinapambana zenyewe kwa zenyewe!

Hii ni kama vita ya wenyewe kwa wenyewe!

Kwa mtaji huu, EAC itasalimika?

..wa-Tz inatakiwa tubadili fikra zetu kuhusu EAC. jumuiya imekaa kiushindani zaidi kuliko kiushirikiano.

..lingine tunatakiwa tumuelewe Raisi Museveni wa Uganda. Kenya, Uganda, na Rwanda, walikuwa na mradi wao wa reli. sasa hapo katikati Museveni kaamua kuwatupa mkono Rwanda, badala yake ameamua kuunganisha reli na South Sudan. Wakati wowote ule anaweza kutugeuka.

..Katika mradi huu wa bomba la mafuta wa-Tz tunapaswa kuwa makini zaidi. Tusiridhike mpaka pale mkandarasi wa mradi atakapokuwa yuko site, na bomba la kwanza limetandikwa.
 
Tanzania ijipange kubuni na kutekeleza mipango yake kwanza. Badala ya kushabikia ya majirani hata kama ni ya EAC. Kumbukeni kwamba Kenya na Uganda njia yao moja kuelekea bahari ya Hindi kwa reli na barabara, hivyo hata iweje, miundombinu hiyo watailinda sana. Sisi mambo yetu hayaeleweki, badala ya kuimarisha zaidi reli ya kati na bandari ya DSM sijuwi nani katulazimisha kujenga bandari ingine Bagamoyo! Mradi wa bomba la mafuta ya Uganda huenda ukatuyumbishwa bure na kutuvurugia mambo yetu ikiwa Museveni hana msimamo. Hatuna sababu ya kuyumbishwa. Tuna resources nyingi kuweza kufanya yetu. Tuachane na project za kisiasa kama daraja labaharini just for the sake of it! Hivi kweli tunajenga daraja la ku-divert traffic ili magari yapite juu ya bahari tu? Magorofa ya anasa tena kwa pesa za mifuko ya pensheni za wafanyakazi ambao wakistaafu wanasotea haki zao kama ombaomba! Ngoja niseme kidogo tu kuhusu hizi flyovers. Hizi flyovers lazima ziwezeshe transit traffic kuupita mji juu kwa juu, kutoka upande mmoja wa jiji kwenda upande mwingine bila kuchanganyika na trips za ndani ya jiji. Kwamfano kuwe na barbara ya inayomuunganisha mtu atokae Tanga na Bagamoyo moja kwa moja aunganishe Kilwa road to Lindi, au na Morogoro road to Mbeya na Dodoma nk. Siyo atoke Oysterbay kwenda city centre kupitia baharini! Hiyo siyo flyover kwa mantiki ya njia ya kupitiliza juu kwa juu.
Kumbe tuko wengi tunaoshangaa daraja la baharini...
Yani mi najiuliza sipati jibu..
Nadhani ndio shida ya kutegemea misaada...
Huyo balozi wa nadhani Japan ameona umuhimu wa hilo daraja sababu anakaa O'bay...sa sijui ni msaada au mkopo???!!!
Tuna shida za barabara kibao hapa Dar haikuwa na umuhimu wa kupitisha njia baharini...hizo ni mbwembwe zenye gharama...
Comment yako nimeipenda bure
 
Total ndiye mtoa hela na mtafuta wateja, anajua namna atakavyojenga bomba, namna atakavyo pump mafuta na namna atakavyoyauza.
Museveni ni politician na Total ni mtendaji....
Kwa maana nyingine, huu mradi umeingiza siasa na kutokana na hali hiyo, we are fighting with two huge competing forces!
 
Hao wamarekani na ndugu zao waingereza kila siku wanaingiliana tender za kutengeneza vifaa vya vita deal za zaidi $100 billion au wafaransa na wamerakani kwenye vita ya supply za ndege, tender za natural resources; huko kila mtu anaangalia maslahi yake.

Vitu kama hivi uwezi kuona wakiita ugomvi wakati kila mtu anapigania maslahi binafsi sio muda mrefu waingereza wamechukua tender kubwa sana ya marekani kutoka UAE ya vifaa vya vita kwa kuwa kila serikari ina majukumu yake.

Sasa wewe ukijiingiza katikati kwenye yale wanayosimamia pamoja wote wanakuja kukutwanga kwa pamoja ata kama ulinunua bidhaa kutoka nchi moja wapo au uliwapendelea wengine wakati wanakuja kukulamba miguu.

Tujifunze kujenga kesi za ushawishi kwenye maendeleo kama wakenya wanavyofanya kutoa argument za kiuchumi, security na cost; sio kutegemea free ride the world doesn't work like that. Huu ni ushidani wa kimaslahi tu watanzania swala zima washalipa interpretation nyingine kabisa na historia ndefu ya nyuma isiyo naulizima wa kuzijua tabia za wakenya which has no meaning whatsoever given the situation.
 
Hakuna anayekataa lakini matendo yake yanahitaji angalizo ili yasiwe sumu katika nchi za EAC.

..mbona sumu imekuwepo siku nyingi sana ktk eac.

..kila siku wa-Kenya wako busy kuihujumu Tanzania, na kututangaza vibaya.

..sasa dawa yao ni kuhakikisha wa-Tanzania tunayafanyia kazi mapungufu yetu ambayo kila siku Kenya huyatangaza huko nje.
 
Ikumbukwe kuwa Jumuiya hii mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 na kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).

Kile ambacho Uganda inakifanya kwa sasa kuhusu ‘’umalaya’’ katika maamuzi unajenga chuki kati ya Tanzania na Kenya.

Uganda inakuwa kama mwanamke anayetongozwa na wanaume wawili kutoka katika familia moja huku akimkubali kila mmoja. Mbaya zaidi, anajitokeza mbele ya kandamnasi na kusema huyu pia ni mwanamme wangu. Wananchi wengine wanabaki wanashangaa na kujiuliza, what’s going on?

Kinachotia wasiwasi, hatufahamu huyu mwanamke anaongea nini zaidi wakati akiwa ndani ya chumba kuhusu mwanamme mwingine anayedai pia anampenda.

Huu ujenzi wa bomba la mafuta unaweza kuleta matatizo makubwa katika mahusiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kuwa, Mwezi August, 2015 tulihabarishwa kuwa Kenya na Uganda wamekubaliana na kuweka saini kujenga hilo bomba la kusafirisha mafuta. Less than two months, on Oct 2015 tukaambiwa Uganda and Tanzania have signed an agreement to explore the possibility of building a crude oil pipeline between the two countries.

Mwezi March 1, 2016, Rais Magufuli na Rais Museveni wakaonekana mbele ya waandishi wa habari wakisema wamekubaliana kuhusu mpango wa kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka bandari ya Tanga, Tanzania hadi Uganda.

March 14, 2016, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo alienda Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumuhakikishia Rais Magufuli kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

March 21, 2016, Tukaambiwa tena, Rais Kenyatta na Rais Museveni walikutana jijini Nairobi kujadili tena ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huu ulifanyika siku chache tu baada ya Uganda na Tanzania kuafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda.

Kwa sasa jopo la wataalam wa Uganda wamebaki Kenya wakitembezwa huku na kule ili kujionea hali halisi ya fursa zitakazopatikana baada ya kujengwa bomba.

Kuna wengine wanaweza kudhani hili ni suala la kawaida lakini mimi ninaliona ni suala hatari sana katika mstakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ningemwelewa Rais Musevevi kama angekuwa anafanya huu ''umalaya'' kwa nchi ambazo haziko ndani ya EAC.

Rais Museveni anachochea ugomvi/uhasama sio kwa Marais wa Tanzania na Kenya pekee bali hata kwenye Mstakabali wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Rais Musevevi asikubaliwe kufanya biashara kwa mgongo wa kujenga chuki kati ya Tanzania na Kenya. Huu ni unafiki na uzandiki wa kiwango cha juu.

Someone must tell Rais Museveni to stop it, just play fair business game. He doesn't have to do all that mumbo jumbo.

UPDATE:
Niliyokuwa nahofia kutokea katika mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kwa sababu ya ''umalaya'' wa Serikali ya uganda yameanza kutokea baada ya Waziri wa Kenya na kundi lake kuzuiwa na TISS kwenda kwenye Bandari ya Tanga baada ya kuwasili Airport.

Kwa habari kamili gonga hapa;

No. Katika biashara mambo haya yapo. Isitoshe kwa kweli Wakenya wameionea sana Tanzania katika kuwanyang'anya tonge. Hakuna urafiki katika biashara, ni maslahi tu. Kama Uganda itaona maslahi yake yapo Tanzania, so be it. Si sawa kuzungumzia Umalaya hapa.
Ninavyoelewa Uganda siku zote ingependelea Tanzania, ila tulikuwa na rais uozo aliyejali safari za kuomba nje tu. Lau na yeye 'angetupa mshipi wake' tangu mwanzo mafuta yalipogunduliwa Uganda, sokomoko hii isingetokea kamwe.
 
CeS1xrIWIAAknZa.jpg

Bye bye Kenyans........
Nimerudi Tanzania kujenga bomba letu
 
Sometimes Do Nothing may be another Alternative to solve Problems we have.
Fursa za kibiashara ndani ya nchi washirika wa EAC isije ikawa ni sababu za
utengano au hujuma za kuvunjana nguvu.
Si vyema mtu mmoja akawa-drive watu wawili eti kwa sababu tu yeye ana fursa
fulani ya uchumi.

Kwa niavyo kama hali hii itaendelea ni dhihili kabisa jumuiya hii haitakuwa
na uhai mrefu.(rejea historia ya EAC).

Katika hili yatupasa kuwa makini kama watanzania kwani yawezekana
ubeberu tayari umepitia mlango wa mafuta kutuvurugia utawala wetu.

Wenye mamlaka ya uchunguzi na wachunguze hili suala kwa makini sana
maana kukaa madarakani kwa muda mrefu kwa baadhi ya marais/viongozi wa ki-Afrika ni kutekeleza maelekezo ya mabeberu,lakini pia nina imani kuwa shetani huyu kama yupo
na akashindwe kabisa kwa jina la aliye juu ya yote.
 
Wakati Tz inatangaza kujenga bandari ya Bagamoyo kenyatta alibwata sana kwa sababu aliona kapigwa bao na ubora wa bandari ya mombassa itakuwa sio kitu kwa bandari ya bagamoyo.Mwaka mmoja baadae kenyatta kaanza kujenga bandari ya kisasa kama itakavyokuwa ya Bagamoyo huko lamu.Kenyatta na wabongo wengine walemavu wa akili wakabwata sana kusema hakuna umuhimu wa bandari ya bagamoyo,sasa kenyatta anataka kutupiga bao sisi tunalalama na hii ndio tabia ya wabongo ,wenzetu wanasonga sisi ni kubwabwata tu.Kenya wametupiga bao mlima kilimajaro sisi ni kubwabwata tu,juzi juzi tumepigwa bao la olduvai g sisi ni kubwabwata tu oooh kenya ,kenya wenzetu message sent.
Mr Pombe soma ujumbe huu kisha uelewe bongo tunasifika kwa kubwabwata na unafiki wenzetu wanasonga mbele.Wenzetu wapo kwenye business sisi tunasubiri tupewe sifa.
Uwekezaji kenya unasifa sisi huku ooh JK ,ooh JK nenda Rwanda uone uwekezaji unakuwaje ni mazingira ya kuvutia kenya wanataka kutumia ubora wa miundombinu yao kuchukua tender ya bomba Wake up maaaaan
 
Naona hujawahi fanya biashara wewe, na hauwajui wakenya wewe.
Au wewe ni miongoni mwa watu walioonja kadhia ya kuzuiliwa kuingiza magari ya kubeba watalii pale JKIA na hivyo unaogopa watawatimua tena?
Unajua kwa nini waliruhusu haraka kurejewa kwa utaratibu wa awali?
Unadhani ni kwa nini Kenya walishadiriki kutangaza kuwa Mt Kilimanjaro ipo kwao?
Unashangaa ni kwa nini tunachukulia kawaida kupigana nao vikumbo kwenye hili dili?
Yeyote anayekuja na mawazo ya kuturudisha nyuma ktk hili dili mimi namshuku kuwa ni mkenya, na iwapo anaposti hapa itakuwa ni kwa unafiki.
Kama wewe si mkenya basi unafiki haukuhusu lkn mwenyewe fikiria Serikali ya Kenya inagharamia safari ya officials wa Uganda kuja kuservey Tanga port na wao wanajichanganya humo, why? Na wao ni stakeholders ktk huu mradi? Kwa mawazo yako ulitaka na wao waruhusiwe kuservey bandari?
Aisee nakushangaa sana
Kimsingi mimi sikatai hilo dili ninachokataa ni kutaka 'kusacrifice' uhuru na heshma ya Tanzania ili kupata dili la kibiashara. Kuna watu wapo humu wanapendekeza kuwe na 'kickbacks' kwa wajumbe wa Uganda. Haya ni maadili ya Kitanzania? Mbona tunataka kupotoka, kama ipo ipo tu, kama Muumba anataka biashara iwe yetu tutaipata tu, lakini sio kuilazimisha hata kwa kukiuka maadili. Sasa kama mtu anapendekeza tufanye biashara kinyume na baadhi ya watu wanashabikia, hilo halikubaliki na huo si uzalendo!
 
Back
Top Bottom