BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,013
Carter na Clinton walisaidiaje dunia, Afrika, na Tanzania?
Watanzania hatumuungi mkono mgombea Urais wa Marekani kwa kutegemea kwamba ataisadia dunia, Afrika na Tanzania. Kuwa na Rais wa US ambaye hatatumia majeshi ya Marekani kuanzisha vita visivyokuwa na kichwa wala miguu ni sababu tosha kabisa ya kumuunga mkono Rais kama huyo maana vita hivyo vinaathiri dunia nzima kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta na athari nyingine mbali mbali.
Bush hizo pesa zake zote alizoahidi kuisadia Afrika ikiwemo Tanzania hazitatoka kwanza kutokana na hali ya uchumi wa US na pili Rais anayeingia kipaumbele chake kitakuwa siyo kuisaidia dunia, Afrika au Tanzania bali kuwasaidia Wamarekani kwanza ili kuujenga tena uchumi wa Marekani ambao umegubikwa na unemployment inayokuwa kwa kasi kubwa sana, budget deficit ya $500 billion and counting na deni la nje la $10.4 trillioni. Mpaka hapo uchumi wa Marekani utakapotengamaa nchi yeyote duniani isitegemee msaada toka US hata baadhi ya wananchi wameanza kuhoji umuhimu wa kuwapa Israel $3 billioni kwa mwaka wakati nchi yao iko katika hali mbaya ya kiuchumi.