Rais Mteule Barack H. Obama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Mteule Barack H. Obama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 3, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,453
  Likes Received: 5,703
  Trophy Points: 280
  Ewe mola unaesikia sala za watu wako wa jf na mafisadi bila kubagua twaomba kwa nguvu zako na uwezo wako
  mbariki kijana wetu barack obama ashinde atika uchaguzi huu na
  kuwa rais wetu mtarajiwa wa jamuhuri ya muungano wa dunia.
  Twakuomba ee bwana
  amin
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna mamilioni ya watu katika bara letu ambalo wanasubiri kwa hamu ushindi unaotarajiwa wa Obama kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huko Marekani. Kuna tafrija na sherehe zilizoandaliiwa sehemu mbalimbali ambapo watu weusi watasimama kufurahia ushindi wa Obama.

  Sitoshangaa wengi wanaosubiri huo ushindi wa Obama wanafanya hivyo si kwa sababu wanakubaliana na sera zake zote (kuongeza kodi, kugawanya utajiri n.k) au misimamo yake ya kijamii (kuunga mkono utoaji mimba au haki za mashoga n.k) bali wanafanya hivyo kwa sababu Obama ni "mweusi mwenzetu".

  Hili hata hivyo linanikumbusha jinsi watu walivyomshabikia Kikwete mwaka 2005 licha ya kuwa hakuwa na rekodi yeyote, hakuwa tayari kufanya midahalo na wagombea wenzake na alikuwa na maneno matamu ya "change" yaliyotumiwa kwa mbiu ya "ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya".

  Wapo watu wale wale ambao leo wanamgeuka Kikwete ndio leo wanakumbatia kwa haraka maneno ya "change" na ya kuwa "Yes we can". Lakini nyuma ya ushabiki huu Watanzania na watu wa mataifa mengi ya dunia wanachoshabikia kule Marekani kwa kweli ni Rangi; kwamba hatimaye Taifa lenye watu wengi weupe likaongozwa na mtu mweusi!

  hapa najikumbusha maneno ya Mwalimu "Sisi bwana hatutukuzi rangi, tunatukuza mtu bwana"!

  Yawezekana ulimwengu ukakosea katika ushabiki wake wa Obama kama Watanzania asilimia 80 ya wapiga kura walivyokosea walipomshabikia Kikwete. Kweli Obama ataweza kutimiza ahadi yake ya "kuibadili Marekani, na kuibadili dunia"?

  Yawezekana kiongozi ambaye watanzania na nchi za ulimwengu wa tatu zilipaswa kumshabikia ni McCain na siyo Obama kama wangeamua tu kuweka rangi pembeni? Well, masaa 24 yajayo will give us a clue.
   
 3. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Correction...
  He is not pro abortion but pro-choice.
   
 4. J

  Janejo Member

  #4
  Nov 4, 2008
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sikubaliani na wewe pale unapomlinganisha Obama na Kikwete.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Nov 4, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  You are parsing words....
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo...Obama amefanya nini afikie kulinganishwa na baba wa taifa? ama sababu ya rangi kama alivyobainisha MMKJJ!! Ushabiki mwingine ovyoooooooo...
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Nov 4, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Huo ushindi hautarajiwi. I don't care what the pundits say. We are going to defy them tomorrow. McCain is going to win this damn thing
   
 8. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Not necessarily a bad thing now,is it?
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ur missing something mkuu...nimekuuliza Obama kafanya nini? ama ni babu kubwa sababu ya kuwa babu kubwa....!! Kama huoni mchango wa Nyerere kwa taifa licha ya mabaya yake kama walivyo wanasiasa wengine unakazi mzee unashabikia usichokijua....
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mbona hivyo!!!....nilitegemea labda ungenisaidia Obama kafanya nini kuwa baab kubwa....ama ungekuja na hizo tangible FACTS za kuwa yeye ni zaidi ya Nyerere...hakuna cha U-Genius hapo...

  All the best bro
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Uchambuzi wako Mwanakijiji sidhani kama ni sahihi.
  Kwanza kama wewe unadhani sera za Bush ni nzuri...Then ni wazi sitoshangazwa unapomfagilia Mc Cain.

  Jambo moja uelewe...Sera za Bush na Obama ni tofauti so as vs Mc Cain.

  MKJJ huo utajiri unaodai utasambazwa ni upi huo? Mbona ndani ya miaka nane ya Bush walishushiwa kodi lakini bado makampuni yaka outsource biashara zao? Republican hawataweza kushusha kodi kiwango cha kupambana na lets say Mexico, China na hata India.

  Uchaguzi huu Mc Cain naye anaweza kushinda, hilo la washabiki kufanya hayo si jambo la ajabu....Hata hivyo umenishangaza sana kwasababu hujatilia maanani historia ya Taifa hili...Kwao uchaguzi huu ni wa tofauti sana na wanautilia maanani sana na matokeo yataonyesha ni kwa jinsi gani wananchi wa marekani wamejihusisha na siasa kwa kiwango kisicho cha kawaida.

  Watu wameshapiga kura na bado wanapiga kura kwa viwango vya kuvunja rekodi....Yani kila mtu ni simulizi. Ukizungumza na wamarekani hata ambao si weusi kama unavyodai na wao pia ni jambo la kihistoria kutokana na historia ya Taifa hili.

  Kwamba imetokea kuwa ni mweusi hilo ni jambo la kihistoria hilo halina ubishi....Kwamba ana sera nzuri inategemea na kama wewe ni tajiri mkubwa mwenye uchu na asiyewajali masikini ambao uwezo wao wa kuspend ndio unausukuma uchumi.
  Hao matajiri wanaotaka kuwekeza hapa marekani na kupata faida ya kuwatosha huku taifa likineemeka ndio matajiri wazuri ambao wako nyuma ya Obama...Matajiri ambao wanasema kama marekani iliweza kuutokomeza ugonjwa wa malaria hapa marekani ni kwanini isiwezekane Afrika?
  Uchaguzi wa kesho ni wa kihistoria na yeyote kati ya Mc Cain na Obama anaweza kushinda...Lakini yeyote kati yao atakayechaguliwa atafanya tofauti kabisa na atakalofanya mpinzani wake kama angechaguliwa.
   
 12. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mzee Mwanakijiji

  Sioni hoja iliyosimama uliyotumia kumlinganisha Obama na Kikwete.

  Dunia inamshabikia Obama kwa sababu ya ubabe ambao Bush ameufanya duniani.

  Waafrika na wengine, popote pale wanaomshabikia Obama kwa sababu ya weusi wake, wana haki hiyo ili mradi sio wao wanaompigia kura.
   
 13. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  OBAMA BIDEN > McCAIN,PALIN THATS ALL THERE IS TO IT!!
  SINA UHAKIKA BADO KAMA WAZUNGU WATAMPA TICK MTU MWEUSI THOUGH.
   
 14. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  OBAMA BIDEN > McCAIN,PALIN THATS ALL THERE IS TO IT!!
  SINA UHAKIKA BADO KAMA WAZUNGU WATAMPA TICK MTU MWEUSI THOUGH.
   
 15. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mzee Mwanakijiji napingana na wewe, sio kwamba anashabikiwa na Wa-Tanzania au watu weusi tuu bali ni dunia nzima, Japan, China na duniani koote wanamshabikia Obama nadhani uliona Germany watu walivyojaa (Kwa nini? sijui) lakini jamaa ni dunia nzima, labda kwa sababu ya msg yake na ya kampeni yake. Na sioni sababu ya watu utokumshangilia yeye kwa sababu ni haki yao kuchagua. Na hiyo kuongeza Kodi , sasa isipoongezwa nani atalipia hiyo miradi inayotegemewa? au mwenzetu una-make more than $ 250,000 ndio maana umechukia kodi yako itaongezwa nini? na suala la kutoa mimba kashasema kwamba sio kwamba anapenda litokee ila inabidi kuangalia afya ya mama na kama mtu amebakwa na ni chaguo la mama anayetaka kutoa na daktari wake. Maana watu wa dini wanapenda kupigia Republicans kwa sababu ya hivyo vitu viwili tuu gays na abortion, na Bush alipigiwa sana na watu wa dini na hana dini yeyote. Ila ndio hivyo waache wabongo wachague wanayemtaka.
   
 16. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Yaani unataka uambiwe kuwa Obama kasaidia kuleta uhuru wa Tanganyika na baadhi ya nchi za kiafrika ndo uamini kuwa ni zaidi ya Nyerere???Mbona waliosaidia kuleta uhuru wa Tanganyika kina Kambona bado mliwaona wasaliti na kuwabeza.Yaani wewe unataka kuambiwa mazuri ya obama aliyofanya,ok kwa nini usianze kutwambia mabaya ya Obama kama unayajua??

  Hivi kweli wa`wewe MM unathubutu kumlinganisha Obama na Kikwete anaesema hajui hata kwa nini Tanzania inakuwa maskini????Haya bana
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Nov 4, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  ni kawaida ya democraps kupendwa na dunia lakini tujiulize, wameifanyia nini dunia....mauaji ya halaiki yaliyotokea rwanda na burundi hivi raisi wa marekani alikuwa nani?

  halafu hiyo ya $250,000 naona sasa imeshuka hadi $120,000....
   
 18. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kuhusu kushuka naomba uende Welcome to Obama for America kuangalia kama imeshuka. na jiulize baada ya Sept 11, ni nani walikuwa madarakani wakaenda kumpiga mtu ambaye hausiki na mashambulizi na hakuwa na kitu walichosema anacho WMD? na pia mambo ya darfur yametokea chini ya utawala wa nani? na hiyo 120,000 nani kakuambiaa?
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Watanzania kamwe hatumuungi mkono mgombea Urais wa US kwa kuangalia rangi yake bali sera zake. Ndiyo maana katika miaka ya nyuma tuliwaunga mkono akina Clinton, Kerry, Al Gore, Jimmy Carter ambao hawakuwa weusi lakini sera zao zilikubalika na Watanzania wengi ukilinganisha na sera za wagombea wa Republicans

  Sasa hivi Obama anaungwa mkono dunia nzima isipokuwa Israel tu. Japan, China, East and West Europe, Canada, Russia, North and South Korea, Middle East na Africa yote mgombea wanayemuunga mkono ni Obama. Kwa hiyo utaona kwamba Obama ana mvuto mkubwa sana duniani kote na kama angekuwa anagombea katika nchi yoyote ile duniani with exception ya Israel angeshinda ushindi wa kishindo kikubwa sana. Walimwengu wengi watakuwa katika majonzi kama Obama akishindwa. Kila la heri Obama.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Nov 4, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Carter na Clinton walisaidiaje dunia, Afrika, na Tanzania?
   
Loading...