Rais Mstaafu Mwinyi Mahakamani Kisutu

Caren

JF-Expert Member
Feb 12, 2010
278
91
Nimepewa taarifa na shuhuda kuwa Rais Mwinyi amefuata nyanyo za Rais Mkapa kwa kutinga mahakama ya Kisutu kutoa ushahidi.

Kwa mujibu wa mtoa habari Rais Mwinyi bado yuko Kisutu maana motorcade yake bado inaonekana. Aliye karibu ajongee pale na kutujuza. Hii imefanywa kwa siri na haijatangazwa.

Kesi gani siwezi kuisema kwa sasa.

SIKU kadhaa baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kufika mahakamani kumtetea aliyekua Balozi wa Tanzania Italia, Prof. Costa Ricky Mahalu, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi naye leo ametinga mahakamani kutoa ushahidi kwenye kesi aliyoibiwa zaidi ya Sh 37 milioni.

Wote wawili (Mkapa na Mwinyi) wamefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kutoa ushahidi.

Katika kesi hiyo, yenye namba 201 ya mwaka huu inayosikilizwa na Hakimu Mkazi, Geni Dudu, Mwinyi ndiye anatajwa kuibiwa Sh milioni 37 na mtu anayetajwa kuwa ni wakala wake, Abdallah Nassoro Mzombe (39). Mtuhumiwa huyo ni mfanyabiashara na mkazi wa Kinondoni Mkwajuni.

Katika kesi hiyo inadaiwa kwamba Mzombe alimuibiwa Mwinyi jumla ya Sh 37, 440,000 zikiwa ni kodi ya pango katika nyumba mbili zinazomilikiwa na rais huyo mstaafu.

Hata hivyo, kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa, Mwinyi aliingizwa kwenye chemba namba moja kwa ajili ya kuandaliwa na Wakili wa Serikali, Charles Anindo.

Mshatakiwa Mzombe alipandishwa kizimbani saa 5:05 asubuhi, kabla ya kesi kuanza kusikilizwa huku waandishi wa habari wakijiandaa kuingia kabla ya kuzuiwa na maofisa hao wa usalama waliowahoji wao ni akina nani.

Pamoja na malumbano kati ya waandishi na walinzi hao, bado waandishi walizuiwa kuingia ndani ya chumba cha mahakama kwa maelezo kwamba kesi hiyo "haiwahusu".

Waandishi wa habari walisubiri hadi saa 6:21 ndipo Mwinyi alipoondoka mahakamani hapo ndani ya gari aina ya Toyota, Land Cruiser T914 BJT.

Nyaraka za kesi hiyo iliyofunguliwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agost 21, mwaka huu, Mzombe anadaiwa kufanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 258 na 273 (b) (e) cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Ilidaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2011 na Julai 2012 huko Mikocheni , Mzombe akiwa Wakala wa rais huyo mstaafu, alimwibia Sh 17,640,000 ambazo ni pato la kodi ya nyumba yake iliyopo eneo la Mikocheni wilaya ya Kinondoni.

Iliendelea kudai kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho Mzombe alimwibia Mwinyi kilikuwa ni kodi ya pango la nyumba namba 481, iliyopo kwenye ploti A huko Mikocheni ya mwaka 2011/2012 na 2012/2013.

Mbali na shtaka hilo, pia anadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, mwaka 2011 na Julai 10, mwaka huu huko Msasani Village wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa huyo alimwibia tena rais huyo mstaafu Sh 19,800,000 ambayo ilikuwa ni kodi ya nyumba namba 55 iliyopo kwenye Kitalu C .

Kiasi hicho cha fedha kilikuwa ni kodi ya pango la nyumba hiyo la mwaka 2011/2012 na 2012/2013.


CHANZO: FikraPevu.com
 
Nimepewa taarifa na shuhuda kuwa Rais Mwinyi amefuata nyanyo za Rais Mkapa kwa kutinga mahakama ya Kisutu kutoa ushahidi. Kwa mujibu wa mtoa habari Rais Mwinyi bado yuko Kisutu maana motorcade yake bado inaonekana. Aliye karibu ajongee pale na kutujuza. Hii imefanywa kwa siri na haijatangazwa.

Kesi gani siwezi kuisema kwa sasa.

Hakuna maana kama hujui kesi inahusu nini. Leta taarifa iliyokamilika.
 
Twasubiri Dec 2015 ifike maana tutsjua mengi na kuwasubiria sana waende kutoa ushahidi au hata kujibu tuhuma zao nyingi sana kwa wakati huo...usimsahau Mamam nae maana yuko active akiwa mwenyewe 'stand alone'sio chini ya kivuli...cha ngao hapana!nae atasimama kama mjasirimali mchumia tumbo
 
Ungefanya utafiti kidogo kabla ya kusema amefuata nyayo za Mkapa. Unajuaje? Labda kaenda kuweka dole gumba hati ya kuuza shamba.......

Mimi nimetimiza wajibu wangu kwa kutoa taarifa. Sidhani kama nilikuwa na jukumu la kufanyia taarifa hiyo utafiti na ndio maana nimeomba mwenye dukuduku aende pale. Kuhusu kufuata nyayo za Mkapa hilo ndio focus yangu maana inacreate precedents (hasa kwa sisi wanasheria). Huko mbele ya safari hakuna rais mstaafu atayeshindwa kuja mahakamni kutoa ushahidi kama hawa wawili wamekuja including mjomba.
 
Mimi nimetimiza wajibu wangu kwa kutoa taarifa. Sidhani kama nilikuwa na jukumu la kufanyia taarifa hiyo utafiti na ndio maana nimeomba mwenye dukuduku aende pale. Kuhusu kufuata nyayo za Mkapa hilo ndio focus yangu maana inacreate precedents (hasa kwa sisi wanasheria). Huko mbele ya safari hakuna rais mstaafu atayeshindwa kuja mahakamni kutoa ushahidi kama hawa wawili wamekuja including mjomba.

Taarifa gani umetoa hapa? Nani ana haja ya kujua gari la Mwinyi limepaki wapi? Watu wanataka kujua anafanya nini au anasema nini kinachohusiana na wananchi. Ndio maana ulipaswa kufuatilia habari kamili ili uweke taarifa iliyoshiba
 
Of course hizo no precedents tosha kabisa. Sisi tunamsubiri mjomba atueleze habari ya Richmund at al akiwa ndani ya kibanda cha watuhumiwa
 
Nani kakwambia atasimama mahakamani?..2015 anahamia kwa Bush na sidhani kama Republican wakishika dola ya USA watamtoa ashitakiwe..Hujui watamlinda
 
Mleta mada, bado mpaka muda huu hujapata taarifa kamili utujuze???
 
Katiba mpya ifute immune kwa Rais!!! Akivurunda tu akiwa madarakani basi akione cha moto. Hii itasaidia kulinda heshima ya nchi pale Rais anapotumia Ikulu kifalme na kujipatia utajiri wa kisiasa na mali!!!!!
 
Waacheni waanza kupata uzoefu na vile vilinge maana soon very soon wataanza kuvikabili.
 
Rais Mwinyi alimkabidhi mtu mmoja nyumba zake mbili awe anazitunza na kukusanya kodi. Badala ya ile kodi kuiwasilisha mwa mwenye nyumba, huyo mtu akazitafuna, Ndipo Mwinyi kaenda polisi na polisi wakafungua kaesi ya madai dhidi ya huyo mshtakiwa (note: bado sijalipata jila la mshtakiwa)
 
Back
Top Bottom