Samahani kwa kupost vipande lakini nitaweza kuedit baadae:
Mzombe aliyaeleza hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Gane Dudu wakati akitoa utetezi dhidi ya mashitaka hayo yanayomkabili. Katika kesi hiyo, mshitakiwa Abdallah Mzombe anadaiwa kumwibia Rais huyo wa awamu ya pili, zaidi ya sh 37.44 million baada ya kuaminiwa na kufanywa wakala wa kukusanya kodi za pango la nyumba za Rais Mwinyi
"ununuzi wa nyumba hizo ulikuwa ni wa siri baina yetu sisi wawili na baada ya kukamilisha ununuzi, walizifanyia matengenezo ya na kuweka wapangaji.
Mshitakiwa huyo, alitaja miongoni mwa kazi alizokuwa akimfanyia Mwinyi, ikiwamo ya kumtafutia nyumba alizokuwa akitaka kununua eneo la Mikocheni, Msasani na kisha kumkabidhi fedha za kununulia nyumba hizo ambazo zilikuwa ni zaidi ya sh. 300 million.
"vitu vingi vya Mzee Mwinyi tulivifanya kwa siri hata familia yake ilikuwa haijui, nilikuwa na uwezo wa kumuibia feza za ununuzi wa nyumba alipokuwa ananikabidhi lakini sikufanya hivyo". Alidai Mzombe wakati akiendelea kutoa utetezi mahakamani hapo.
Source: Mwananchi, Januari 11, 2013
My take:
Hapo kwenye red/underline pamenishtua wakuu!!!!