Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Mkuu kaongea vizuri kama Mbeya hawana ardhi ya kutosha ekari 500 basi hilo tawi la UDSM litaenda kuanzishwa mikoa mingine kama Rukwa, Katavi na kwingineko kwenye mapori meengii tuu yasiyo na mwenyewe.
Waje Rukwa tuu hapa maeneo yapo ya kutosha.
 
Hiyo Ardhi Mbeya hawezi kuipata maana wilaya ambazo zina Ardhi kidogo ya akiba ni Chunya na Mbarali lakini 500-1000 too much hata UDSM main campus hawana eneo la hivyo
Ipo ya kutosha,Chuo cha kilimo na Tanganyika packers na TBC Wana maeneo makubwa Sana.Unalima.maharage mjini Ili iwe nini?

Chuo cha kilimo uyole kihame pale mjini liende mkoa kama Rukwa ndiko wapewe maeneo ya kufanyia utafiti sio mjini .
 
Acha ufala na ujinga wa kujitungia vitu vya kufikirika ambavyo Mbeya haifanyi..
 
Mawazo mengine ktk nchi za kiafrika ni ya kuchekesha sana,suala la kutaka eneo si muhimu sana kama ilivyo muhimu kutathmin elimu inayotolewa pale USDM.Tutajidai kwa kuwa na vyuo vzr lkn tujue vyuo hv vinavyotengeneza viongozi ombaomba na watembeza bakuli kila kukicha kiongozi anapanga akaombe fedha nchi huko ulaya,hv vyuo vyetu lzm tukubali kwamba vimefeli maana elimu inayotolewa haijakidhi mahitaji ya taifa ndio maana tuna wasomi ambao si creative hata kidogo,hivyo tusiangaike kusumbua watanzania huko Mbeya eti ili kutafuta eneo la kujenga tawi la UDSM ni UPUUZI tu.
 
Kichwa habari utafikiri ameomba binafsi kumbe kwa ajili yachuo muemnaandika ilimueleweke
 
Hizo heka 500 wanazo hapa dar, au ni kutafuta kiki tu.....yaani mnyanga'nye wananchi maeneo yao ili mjenge chuo kikuu uchwara, aka. jalalani........basi nendeni katafute huko kwengine mlipoziweka. Kuna mapori tabora huko hayakaliwi na watu zaidi ya mbung'o kajengeni huko, ebooo!
 
mbeya kuna dhahabu labda wanataka kuimarisha ulinzi.
[/QUOTE]
Dhahabu si ni chunya kule, kikwete anazungumzia mpaka maeneo ya Forest, au nishaisahau Mbeya mara hii. Hayo maeneo ya Forest kuna chuo cha mzumbe kimebanana kwelikweli na makazi ya watu, hiyo forest anayozungumzia Kikwete ni ipi? 1000 hectas?
 
Mkuu Hiki ulichoandika Indio UPUUZI sasa. Hivi una taarifa kwamba tuna upungufu sana wa wahudumu wa Afya nchi hii?

FYI Kitivo cha Tiba UDSM sio kwamba ndio kinaanza , program ilianzi tangu mwaka 2015/2016 pale pale UDSM main campus. Yule bwana aliwahi kuishi magogoni kwa sasa amelala huko chato alipinga uwepo wa kozi ya Medicine UDSM kwa kuna tayari kuna hiyo program Muhimbili. Ikabidi kitivo kihamishiwe Mbeya, Kwanini? Kwa kuwa ili uweze kutoa mafunzo bora kwa madaktari unahitaji MADAKTARI BINGWA kwenye fani mbalimbali kuweza kuwafundisha hawa wanafunzi. Hawa unaweza kuwapata Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya. Its as SIMPLE as that hakuna siasa hapa. Mwaka Jana 2020 wamehitimu zaidi ya madaktari 100 watakua wamekamilisha Internship now tayari kukuhudumia huko kwenu.

Sasa Kwa maono ya UDMS sio kuwa na Lecture halls tu, wanahitaji kuwa na Hospitali Kubwa ya Kisasa kuweza kutoa huduma na kutoa mafunzo ndio maana wanahitaji eneo kubwa la kuweka hizo miundombinu. Nenda Katembee Mloganzila Hospital ndio utaelewa kwanini JK anahitaji eka Hizo kule Mbeya. Hiyo Hospitali ya Mloganzila ni mpango/mradi wa chuo cha Muhimbili Kiliamua kuwa na Hospitali Yake kutoa huduma na kufundishia. Again, yule mwanasiasa wa Chato akawaambia Hiyo Hospitali iwe chini ya Management ya Muhimbili National Hospital. Ikabadilishwa jina toka MUHAS Medical Academic Centre to Muhimbili National Hospital-Mloganzila. Unaweza kuona MUHAS wako Upanga lakini ilibidi watafute eneo nje ya Mji karibu kilomita 30 kujenga Hospitali ya kutoa mafunzo. Ukiniuliza sababu nitakwambia "Poor planning from the very beginning".​
 
Na yeye ameanza kuvimba
Havimbi bali atakuwa ameshauriwa na chuo chenyewe. Kuna kitu watakuwa chuo hawajaridhika wamekiona hakiendi sawa, ikabidi wapeleke hoja zao kwa mkuu wa chuo.
Tuache siasa kwenye elimu, hasa hizi muhimu zinazohusu uhai wa binadamu moja kwa moja. Mimi nilitarajia wangekua wamepewa eneo lenye ukubwa ambao wao wenyewe chuo wangeamua kulikataa na kurudisha sehemu yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…