Rais Mstaafu Benjamin Mkapa atajwa katika kesi ya kina Mramba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa atajwa katika kesi ya kina Mramba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 3, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Date::11/3/2009Rais Mstaafu Benjamin Mkapa atajwa katika kesi ya kina Mramba
  [​IMG]

  Rais Mstaafu awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, jina lake limetajwa katika kesi ya akina Mramba.

  Na Tausi Ally
  Mwananchi

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana ilielezwa kuwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa ndiye aliidhinisha mchakato wa kuiajiri Kampuni ya Alex Stewart uendelee kwa haraka.

  Hayo yalielezwa mbele ya jopo la mahakimu watatu lililokuwa likiongozwa na hakimu John Utamwa wakati Wakili Hurbet Nyange alipokuwa akimhoji shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka Godwin Nyelo (4.


  Nyelo ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria na masuala ya Uchumi wa Wizara ya Nishati na madini ni shahidi wa kwanza kwa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wake katika kesi ya kutumia madaraka vibaya na kuisababishia hasara ya zaidi ya Sh 11 bilioni serikali inayowakabili Mramba, Daniel Yona na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Gray Mgonja.

  Hata hivyo shahidi huyo alisema Rais Mkapa alihusika katika kukubali mchakato huo uendelee haraka baada ya Wakili Nyange kumuonyesha dokezo na kumtaka asome sehemu ya dokezo hilo naye kufanya hivyo mahakamani hapo.


  Dokezo hilo lilikuwa limeandikwa kutoka kwa Daniel Yona ambaye kwa wakati huo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini kwenda kwa Rais huyo wa serikali ya awamu ya tatu.

  Akimhoji shahidi huyo, Wakili Hurbert na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:


  Wakili Nyange: Waziri wako Daniel Yona alikuwa na wajibu wa kutii wakubwa wake?.

  Nyelo: Ndiyo.

  Wakili Nyange: Mkubwa wake wa kazi akisema jambo hili lina uharaka na wewe unasema halina uharaka atamsikiliza nani?.

  Nyelo: Mkubwa wake.

  Wakati mahojiano hayo yakiendelea Wakili Nyange alimuonyesha Nyelo dokezo aliloliandika Yona kwenda kwa Rais na kumtaka shahidi huyo asome jibu linalodaiwa kuwa ni la Rais.

  Shahidi huyo alilisoma kuwa “Nakubali endeleeni haraka.

  Wakili Nyange: Baada ya kusoma Waziri angeweza kusitisha huo mchakato?.

  Shahidi: Waziri asingeweza kusitisha huo mchakato kwa sababu ya uharaka.

  Wakili Nyange: Uliwahi kuuona mkataba uliotengenezwa na kwenye upande wa malipo ulikuwa na tofauti na jinsi mlivyopendekeza kama kamati?.

  Shahidi Nyelo: Hapana.

  Wakili Nyange: Katika ule mkataba ambao serikali iliingia na Alex Stewart uliona kama kuna kipengele kilikuwa na matatizo au tofauti na mlivyokubaliana?.

  Shahidi: Kipengele kilichokuwa na matatizo ni cha ada tu vingine vilikuwa sawa.

  Wakili Nyange: Maneno yako ya kuwa hapakuwepo na bajeti kati ya mwaka 2003 na 2004 ya kuilipa kampuni ya Alex Stewart, wewe na ripoti ya bunge kipi ni sahihi?.

  Shahidi: Yote ni sahihi.

  Wakili Nyange: Nikikwambia kuwa kampuni ya Alex Stewart ilishindwa kufanya kazi yao kutokana na makampuni ya madini kukataa kukaguliwa hadi hapo walipoonywa na waziri wa fedha?.

  Shahidi: Ni sawa kabisa waziri wa fedha aliwaonya.

  Wakili Nyange: Unakumbuka kampuni ya Alex Stewart ilikataa taarifa za hesabu za makampuni yaliyoonyesha hasara?.

  Shahidi: Hilo sikumbuki.

  Wakili Nyange: Unakumbuka sababu iliyoongeza mkataba wa Alex Stewart toka mwaka 2005 hadi 2007 ili kuwawezesha kumaliza kazi yao ni kutokana na ukosefu wa ushirikiano kati yake na wachimbaji hao.

  Shahidi: Hiyo ni moja ya sababu.

  Wakili Nyange: Unafahamu Nyaraka zaidi ya 6000 zilifichwa ili kampuni ya Alex Stewart isizione katika kuhakiki?.

  Shahid: Inawezekana ikawa hata zaidi ya hiyo.

  Wakili Nyange: Hivi una habari nyaraka hizo zilikuwa zikifichwa na kampuni hizo kwa ajili ya kukwepa kodi na kwamba hilo liligunduliwa na kampuni ya Alex Stewart?.

  Shahidi: Hilo najua.

  Wakili Nyange: Unajua kama kampuni ya Alex Stewart iligundua kampuni za Blacr Dom na kampuni ya Resolute zilishindwa kuthibitisha matumizi yao ya dola 160 ambayo yalikuwa hayaeleweki kwa sababu nyaraka husika zilikuwa katika makao makuu yao ambayo hayapo hapa Tanzania?.

  Shahidi: Hapana.

  Wakili Nyange: Unajua Nyaraka hizo ilitakiwa zibaki hapa hapa nchini.

  Shahidi: Najua

  Wakili Nyange: Wewe ulishauri vipi?.

  Shahidi: Alex Stewart asipewe mkataba.

  Wakili Nyange: Unamsaliti Waziri , Katibu Mkuu na kamati nzima mliyokaa?.

  Shahidi: Hapana.

  Wakili Nyange: Picha unayotaka mahakama iioneni ipi?.

  Shahidi: Kile nilichokishauri kwenye kamati ndicho nilichomshauri Waziri.

  Kwa upande wa mahojiano kati ya wakili Casbert Tenga na Shahidi Nyelo yalikuwa kama ifuatavyo;

  Wakili Tenga: Hayo mapendekezo uliyoyatoa yanaashiria zoezi zima lifutwe?.

  Shahidi: Sawa.

  Wakili Tenga: Unakubali kuwa mapendekezo hako ya kufuta zoezi zima na wakati wa kusaini mkataba ulikuwa umefika hiyo aina madhara kwa kamati?.

  Shahidi: Itakuwa na madhara.

  Hakimu Utamwa aliiahirisha kesi hiyo hadi leo mahojiano hayo kati ya mawakili wa upande wa utetezi na shahidi yatakapoendelea.

  Shahidi huyo wa kwanza kwa upande wa mashtaka ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa kampuni ya madini ya Uranes Tanzania Limited awali akitoa ushahidi wake alidai ushauri wake wote alioutoa kuhusiana na mchakato huo wa kuiajili kampuni ya Alex Stewart haukuzingatiwa kwa sababu mambo mengi aliyaona katika utendaji wa kampuni ya hiyo na kwamba aligundua hawakusaidia kuimarika kwa udhibiti na usimamizi wa maandizi.

  Alidai hakukuwepo na mabadiliko yoyote katika utendaji uliokuwepo awali kabla ya kampuni hiyo kuajili, ilipoajiliwa na ilipomaliza muda wake na kufanyiwa tathmini(Evaluation).

  Alidai katika dokezo la Mei 26,2003 la majadiliano ya kuweka mfumo wa kudhibiti uzalishaji wa dhahabu kuwa kutokana na mambo yalikuwa yanajitokeza ilibidi kufanywe mabadiliko kwenye zabuni za awali ili ziendane na matakwa yao.

  Kwa mujibu wa dokezo hilo, Nyelo alidai majadiliano waliyofanya na wadau wengine yalionyesha kuwa hawakuwa na uharaka wa kuingia mkataba na kampuni hiyo kabla ya kuona utaratibu uliokuwa unatumiwa na nchi nyingine. Alidai kwa kuwa lengo lilikuwa ni kuongeza mapato ya serikali kulipa kampuni asilimia 1.9 ni sawa na kupunguza mapato na hivyo kuondoa maana ya zoezi zima na kwamba kwa kuwa kunadalili ya kampuni hiyo ya Alex Stewart kutokuwa wawazi kwa maelezo yao alipendekeza wasipewe kazi hiyo.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo ya nchi yetu ni kwamba sawa katajwa lakini ata fanywa chochote? Majina kibao yamesha tajwa yaki husishwa na tuhuma mbali mbali lakini wangapi wao wame chukuliwa hatua? Sawa Mr. Mkapa can "rest" as JK keeps insisting but I hope he won't rest in peace.
   
 3. patriot1

  patriot1 Member

  #3
  Nov 3, 2009
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 5
  haya mambo si lazima yaende haraka kama kila mtu anavyofikiri ni mambo sensitive na ndo maana hata serikali itapochukua hatua yoyote haipaswi kupelekwa na hisia tu jamani tuipe mda...
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I'm glad you are very optimistic but I doubt anything substantial will be achieved and history will support me on this. Nchi yetu inaendeshwa kisanii mno mkuu.
   
 5. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aaaah ..Ndugu yangu. Hizi kesi ni zakupotezeana muda tu..Haina tofauti na yakina Zombe..!!
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Something is better than nothing!..inasaidia kuondoa ndege wengi wasile mpunga shambani kwa bibi...
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Goodluck if you have any positive expectation.
   
 8. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo utasikia wanasema "ya!, Mr Mkapa has been implicated in the scheme to defraud the government"

  Jibu ni kwamba ndio lakini ana kinga dhidi ya mashtaka yoyote yale.

  Kuanza kumuongelea raisi mstaafu ni moja ya njia ya kulegeza nguvu za mashataka lakini sitarajii kuona kwamba mgosi Hubert Nyange anakubali kuyumbishwa.
   
 9. k

  kawekamo Member

  #9
  Nov 4, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumeliwa! Mbona naona huyu shahidi wa kwanza wa mashitaka aliye muhimu anakubali hoja za mawakili wa utetezi zenye kulenga katika kuonesha kuwa Mramba hakukosea?
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hatuna kesi... kesi zote za Mramba na Yona zitafutwa maadam Mkapa amehusika kutoa shinikizo hilo..Sababu kubwa, kama sikosei ni kwamba Mkapa kama rais mstaafu anyo kinga kisheria inayomlinda ktk maamuzi alofanya akiwa rais wa nchi.
   
 11. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Lakini kesi inaweza kuendelea na hawahawa walikamatwa yaani Mramba, mgonja na wengine.

  Baadae sheria ianweza kurekebishwa kwa kutumia hoja kwamba kinga ya uraisi ni kunyume na matakwa ya demokrasia kwamba kila hakuna ale juu ya sheria.
   
 12. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yote kupotezeana wakati tu. Kila kitu kinaonyesha wazi Mkapa ni fisadi, lakini panya hawezi kumfunga paka kengele.

  Leka
   
 13. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  I don't think if there is something tangible gonna happen in this issue.
   
 14. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ebu tusome vizuri sehemu hii ya maojiano:
  "Wakati mahojiano hayo yakiendelea Wakili Nyange alimuonyesha Nyelo dokezo aliloliandika Yona kwenda kwa Rais na kumtaka shahidi huyo asome jibu linalodaiwa kuwa ni la Rais.

  Shahidi huyo alilisoma kuwa “Nakubali endeleeni haraka. "


  Dokezo lilitoka kwa Yona kwenda kwa Rais, na rais akakubali akisema "Nakubali endeleeni haraka."
  Hatujui rais alikubali nini kwani hatujaelezwa dokezo lililotoka kwa Yona likuwa linamweleza nini rais! Labda Yona alimdanganya rais? Tupeni hilo dokezo in full ili tuweze kujadili kitu halisi maana hapa tunajadili jibu la rais bila kujua swali/dokezo lilisemaje!,hata shahidi alitakiwa asome jibu tu la rais (kumtaka shahidi huyo asome jibu linalodaiwa kuwa ni la Rais.)
  na siyo dokezo na jibu!, huu ni ujanja wa kijinga wa mawakili!

  Kuhusu kinga kwa rais mstaafu: Wanasheria tuelezeni, ni sheria ipi inayompa rais mstaafu kinga?, ni katiba au kuna sheria tofauti? Tuelezeni
  Katiba inasema hakuna aliye juu ya sheria, na kama katiba hiyohiyo itasema fulani yuko juu ya sheria basi ni contradiction; na kama kuna sheria tofauti na katiba ikasema fulani yuko juu ya sheria, basi sheria hiyo inakuwa batili kwa kuwa inapingana na katiba.
  Fuatilia yaliyotokea kwa waziri mkuu wa Italia!
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,765
  Likes Received: 4,980
  Trophy Points: 280
  Kamakabuzi,

  ..hoja hapo ni kama uamuzi wa kuingia mkataba "ni wa Raisi", au "una baraka za Raisi."

  ..sasa hiyo ni challenge kwa upande wa Mwendesha Mashtaka.

  ..mpambano utakaofuatia ni kuonyesha kama serikali iliingia hasara au la. naona tayari mawakili wa utetezi wameanza kupambano na hilo. hoja yao ni kwamba Alex Stewart walifichua hujuma za makampuni ya madini dhidi ya serikali/Tanzania.

  ..halafu litakuja suala la kupuuza ushauri wa Wataalamu. sasa hapa napo kutakuwa na mpambano kama huo ushauri walioukataa washtakiwa ulikuwa na mantiki ya kitaalamu.

  ..washtakiwa wanaweza kudai kwamba walipokea ushauri wa kitaalamu toka sehemu nyingine. mwendesha mashtaka anapaswa kuieleza mahakama ni jinsi gani ushauri wake ulikuwa better kuliko ushauri/uamuzi waliochukua washtakiwa.

  NB:

  ..upande wa Mashtaka unahitaji ushahidi ambao utawatenganisha kina Mramba na ofisi ya Raisi.

  ..je, Mkapa atakuwa tayari kutoa ushahidi dhidi ya mawaziri wake, kwamba hakuwashinikiza, au alichokuwa amewaagiza sicho walichokwenda kutekeleza?
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Patakuwa matamu ikiwa Mkapa ataitwa mahakamani kama shahidi..Na nijuavyo mimi Mkapa atawaruka! Hatakubali kuhusishwa na uchafu huu kama shahidi na hawezi kuchunguzwa kwa sababu ya kinga..
  Nina hakika hawezi kuchukua lawama hizi baada ya kustaafu akiwa na heshima kubwa ya rais aliyetuongoza vizuri kiuchumi..
   
 17. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hii mijitu inalindana kwani haukuna wa kumnyooshea mwenzake kidole. Ni nini kilichositirika kuwa BWM ni fisadi? Hata akifikishwa maakamani haukuna litakalo endelea. Wameshindwa kuwahukumu kina RA,Chenge,EL na wengine wengi walio husika kweny ufisadi wa EPA na sehemu nyingine, leo wampeleke BEN mahakamani?
  Kama wameshindwa kuwachukulia hatua watu walio kuwa ngazi za chini, je ni huyu aliyekuwa ngazi za juu?
   
 18. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Kutajwa Raisi mstaafu Benjamin Mkapa ni sawa kabisa!!Kwani unadhani hawa wote waliopo mahakamani ni kweli ndio wahusika halisi?No!!! Its Mkapa who is been represented in the names of Mramba&Yona.
   
Loading...