Rais, Majaji na wote wasiokatwa kodi kwenye mishahara yao ni muda muafaka nao waanze kulipa kodi

nnhhh, nimejaribu kupitia sheria za kodi ya mapato (Second Schedule), sikuona mahali majaji wamesamehewa kulipa kodi ya PAYE. Ni Rais wa URT na yule wa Zanzibar ndio wamesamehewa. Labda kama kuna kitu kinafichwa, ambacho tecnically ni illegal
 
Uko sahihi....kodi ni swala la kizalendo kwa kila raia...kama kweli ni uzalendo. Na kila mtu alipe kutokana na kipato chake. Majaji, Wabunge na vigogo wote walipe, maana wao ndio wazalendo zaidi wanajiita.
 
Hii nchi ni kichwa cha mwenda wazimu wanaochukua mishahara mikubwa na marupurupu wao hawalipi kod et walim manes polis n.k
 
Rais halipi kodi kwasababu inchi na pesa yote ni yake pamoja na hii hewa na pumnzi yetu ni mali yake

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 

Enyi wanufaika wa malipo bila kodi stahiki oneni japo aibu basi?
 
Hakuna namna inabidi nao walipe kodi.

Hatuwezi kuwa na Taifa la "walipa kodi" na "watumia kodi". Lazima usawa uwepo kwenye kulipa kodi, sote tujenge nchi

Kibaya zaidi hao waliopewa upendeleo wa kutokulipa kodi, ndio sehemu ya kukandamiza haki za wananchi wengine!
 
Ni kweli kabisa. Katika mataifa mengine uzalendo hupimwa kwa namna mtu anavyochangia katika uchumi kwa njia ya kulipa kodi. Tanzania misamaha imewekwa kwa wale wenye kipato cha mshahara mkubwa, misamaha ya kosi kwenye mishahara, ankara za umeme, simu na maji wanalipiwa Hapa kwetu ukwepaji kodi na misamaha ya kodi ndiyo kipimo cha ukaribu na wale wanaojiita wazalendo kwa maana wale waliokaribu na watawala wanaoweza kutoa maelekezo kwa watoza kodi kwa kupiga simu au vimemo. Mzigo mkubwa anatwishwa mlalahoi.
 
Mbali ya kutolipa Kodi, anakula bure, ananunuliwa nguo, kila kitu bure tu
 
Uzalendo uanze na viongozi wenyewe

Walipe Kodi kwanza kwanini wao hawalipi???

Kwa maoni yangu wanaopaswa kuwa exempted na Kodi ni Watu wa vyombo vya Ulinzi Na Usalama tu.
 
Uko sahihi mkuu, kama wanatangaza kulipa kodi ndo uzalendo basi na wao walipe kodi maana wanatuibia mchana kweupe halafu wanatulaghai eti tuwe wazalendo, nyooooo....!!!!! Machinga endeleeni kuchukua bidhaa kutoka kwenye maduka makubwa muuze bila kuzilipia kodi maana ni ujambazi tunafanyiwa na Rais, Majaji, Wabunge, Askari na wengineo wasiolipa kodi
 
Labda Kwa KATIBA MPYA sio hii ya CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…