Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,285
Kama kulipa kodi ni uzalendo, basi rais wa nchi ndiye anayepaswa kuwa mzalendo namba moja.
Kama Tanzania ni nchi ya Usawa, basi haiyumkiniki wawepo watu katika nchi hii wawe ni wavuja jasho, wanaokamuliwa kodi kwenye mishahara yao lakini kuna jingine la watanzania haohao mfano rais na Majaji ambao hawakatwi kodi kabisa kwenye mishahara yao
Majuzi hapa waziri wa fedha amesema bungeni kuwa katika mwaka huu wa fedha wameweka kodi kwenye laini ya Simu, kwamba watu watakuwa wakikatwa kuanzia shilingi 10 hadi 200 kila siku kulingana na uingizaji wao wa salio, wao wanaita eti kodi ya "Uzalendo".
Waziri wa fedha anasema eti pesa hizo zinatakiwa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa mahospitalini. Ngoja nimkumbushe Waziri wa fedha Chanzo kizuri cha mapato ya serikali, Waziri ajue kuwa kuna wananchi nchi hii hawalipi kodi kwenye mishahara yao mfano ni RAIS na MAJAJI.
CCM huwa wanapenda kujitangaza kuwa nchi hii ni nchi ya kijamaa, Umewahi kuona ujamaa wa wapi wenye matabaka ya wazi ya namna hii ikiwemo ukosefu wa Usawa kwenye kulipa kodi?
Yaani sisi walalahoi kila siku tukamuliwe kodi ila top Class wao wale tu mishahara itokanayo na kodi zetu lakini wao wasilipe kodi, hii fairness ya wapi?
Tunataka sheria ibadilishwe, Kila anayepaswa kulipa kodi alipe kodi. Rais alipe kodi, Majaji walipe kodi na yeyote yule aliyepewa kinga ya kulipa kodi alipe.
Haiwezekani ionekane eti rais kulipa kodi ni kitu kibaya kwake lakini eti kiwe wajibu kwa raia wa kawaida!