Rais Magufuli yashamshinda?

Rais Magufuli yashamshinda?

hahahaha! eti kwa heshima! wakat huyu aliyechukua kijiti analilia kaachiwa nchi imeoza! kuozesha nchi ndo heshima?!
heshima kwako ni ipi? mlisema hatamaliza mda wake akamaliza tena na kuwaadhibu na dubwasha lenu.
 
CHADEMA ingekuwa imara kama zamani huyu DIKTETA UCHWARA easily angeondoka 2020
Lkn kwa upinzani huu wa hovyo hovyo wa kutowasikiliza wanachama na kujiona viongozi kama Mungu watu
Wapinzani wanawatumia wanachama wao kwenye maadamano tu
Kwenye teuzi wanapuuzi kauli za wanachama wa kawaida
Wao na CCM hamna tofauti
Magufuli atashinda 2020 hata kukiwa na TUME HURU
Mark my words

Duh! Zamani gani hiyo ambayo CDM ilikuwa imara? Labda wengine tulikuwa hatujazaliwa. Lakini kama CDM hii iliyoanzishwa baada ya vyama vingi kuruhusiwa tena mwaka 1992, has never been stronger.
 
Acha hivyo hivyo...kuna watu wanapenda hii hali...na wanafaida nayo. Kiukweli kabisa kabisa...watu wengi hawawezi vya kuchinja!!

offcourse wengi wanahaha hata kusema neno chai achilia mbali lunch au dinner.
 
Nchi haieleweki kesho itaamkaje,labda tutaambiwa tuliooa wanawake weupe tuachane nao!!

Wawekezaji/wafanyabiashara wameficha hela zao benki wakisubirk hali ya kibiashata iwe predictable.

Watumishi wa umma hawana security of tenure,yeyote anaweza kumfukuza yeyote mahali popote kwa sababu yeyote.

Wenye biashara hawajui TRA wataamkaje maana hata mahesabu ya kodi nasikia yanazidishwa ili kufikia lengo.

Bodaboda na trafic ni shida
Tuliambiwa elimu bure Leo tunachanga madawati
Sekta ya umma iko stagnant hakuna anayekubali kubuni kitu cha manufaa, hakuna viwanja vinavyopimwa wala nini,watumishi wanafanya conventional works,shughuli za kawaida za kila siku

Ndani ya Mwaka biashara nyingi zitakuwa zimefunga anzia grocery mpaka mahoteli na MADUKA madogo kwa makubwa!!
Magenge ya wapeleka umbeya ndio yanapewa nafasi kubwa kuliko kukaa na kusikiliza wataalam wanasemaje
 
Zungumza na wenye maduka Kkko hadi Posta...

Wao ndio "sample" ya utafiti wako?

Kama ndiyo hivyo wakosoaji wa Magufuli mna kazi kubwa.

Kama ndiyo hoja zenu hizo mi naweza kuja na kukwambia zungumza na wakulima na wafugaji uone wanavyomsifia na kumpongeza Magufuli na Serikali yake.
 
Nyani Ngabu urais ni taasisi ukimuona rais anatoa maamuzi ujue information zote anazo

Kuwa na information ni kitu kimoja na application of that information ni kitu kingine kabisa, info isipochambuliwa kwa kina na kuangalia -ves na +ves zake kwa tafakuri tunduizi kunaweza kuzaa mis_application of the information.
 
Duh! Zamani gani hiyo ambayo CDM ilikuwa imara? Labda wengine tulikuwa hatujazaliwa. Lakini kama CDM hii iliyoanzishwa baada ya vyama vingi kuruhusiwa tena mwaka 1992, has never been stronger.
CHADEMA ilijipanga vyema sana 2010-2015 kabla Mbowe na akina Lissu hawajatuharibia mchakato wa kura za maoni

Kumtoa Dr Slaa kwa sababu za ajabu na baadae kuteua wabunge viti maalum ambao hata hawakuwa wana CHADEMA ndiyo kumeua chama hiki
 
I agree with you. Hata wafanyakazi wengi wa umma hawana furaha na staili hii ya Magu. Na hili la kuhamia Idodomya fasta ndio usiseme.
Kwani hao wafanyakazi wa umma wapo dar tu watu tupo chip tunapiga maji kisimani na mavi ya ng'ombe, acha iwe hivo
 
Ukipita mitaani watu washachoka na story zake...
biashara haziendi.....mood iliyopo ni kusubiri labda mambo yatanyooka soon...
sasa sijui yasiponyooka itakuaje....
mkuu uko sawa kabisa,biashara iko down sana, kila siku afadhali ya jana,kila mtu analalamika
 
Kwani Cuba wana vyama vingapi na wana maisha gani? Hata Tanzania tutarudi kwenye chama kimoja na tutakuwa na maisha mazuri sana kama Cuba hakuna shaka. Demokrasia haiji kwa kulazimisha inabidi watu wawe tayari ama sivyo ufalme uendelee. Usiwe na shaka.

Cuba wana maisha mazuri...? Labda unaongelea Cuba nyingine siyo hii ya Fidel Castro!
 
Hujaainisha vizuri mkuu ni kipi kilichomshinda na kipi kizuri!
Ungefafanua vyema ingependeza zaidi.
 
tena atashinda kwa kura nyingi mnoo. hawa wapinzani hawana ajenda pumzi imekata mapema sana. wamebaki kufanya siasa za kinafiki mitandaoni
Hebu tutajie umri wako kwanza kabla hatujaanza mjadala Tusije kukaushana mate hapa kumbe MTU mwenyewe bado hujajielewa!
 
Hebu tutajie umri wako kwanza kabla hatujaanza mjadala Tusije kukaushana mate hapa kumbe MTU mwenyewe bado hujajielewa!
unajua masharti ya kujiunga hili jukwaa? au umekupuka tu kujiunga huku?
 
Hivi anaweza kuamua kulipiga mnada ziwa victoria au mlima Kilimanjaro? Maana naanza kupata hofu......au akaagiza bahari ya Hindi ihamie Dodoma Mara moja??🙄🙄🙄😵😵😵🙄
 
Wao ndio "sample" ya utafiti wako?

Kama ndiyo hivyo wakosoaji wa Magufuli mna kazi kubwa.

Kama ndiyo hoja zenu hizo mi naweza kuja na kukwambia zungumza na wakulima na wafugaji uone wanavyomsifia na kumpongeza Magufuli na Serikali yake.

Unajua kitu kinachoitwa 'multiplier effect'?

Wafanyabiashara wanaathiri kila mtu..
wao ndo wanaathiri TRA na mapato.. na mapao ndo bajeti inapoanzia.....
kama unataka niseme watanzania wote.....wanalalamika...
siwezi sema hivyo
najua kuna watu 'mioyo yao inakoshwa na Magufuli'

swali je hao wanaokoshwa hawataguswa na hiyo 'multiplier effects?
 
Back
Top Bottom