Rais Magufuli yashamshinda?

tena atashinda kwa kura nyingi mnoo. hawa wapinzani hawana ajenda pumzi imekata mapema sana. wamebaki kufanya siasa za kinafiki mitandaoni
Katika hili mi naweka akiba ya maneno. Wakati utasema, hatimaye!
 
Ukipita mitaani watu washachoka na story zake...
biashara haziendi.....mood iliyopo ni kusubiri labda mambo yatanyooka soon...
sasa sijui yasiponyooka itakuaje....
Watumishi tuko hoi lakini wateule wameamuru tuchangie mbio za mwenge.
 
Nimeona post yako nikachefukwa
 
na wenye akili ndio walikua wanatafuna Nchii hii. sasa Magufuli anawanyoosha. vyovyote iwavyo ataawanyosha tu na Nchi itanyoka
Thubutuu amnyooshe nani? Watu wanajuwa ni roho yake mbaya hawezi kufanya lolote.sisi tunachoshindwa kumuelewa matamko yake hayaeleweki.
 

Swahiba...

Kitu ambacho sikielewi kabisa ni hiki: tokea tupate uhuru hatujawahi kuongozwa na chama kingine chochote kile zaidi ya CCM [tukizingatia na ubadilishwaji wa jina].

Kwa msingi huo, CCM ndo inawajibika moja kwa moja na hali tuliyonayo leo - dhiki iliyokithiri, huduma za jamii mbovu zilizo chini ya viwango, ufisadi, rushwa, maradhi, na mengineyo.

Cha ajabu, chaguzi baada ya chaguzi watu huishia kuwapa kura walewale ambao ndo wameileta hali tuliyonayo licha ya kutuaminisha kwamba eti sisi ni nchi tajiri sana. Tunaenda kufikia miaka 60 ya kutawaliwa na chama kilekile. Aibu.

Sasa, mtu unaweza kujenga hoja ya kwamba CCM huwa hawashindi kihalali kwa sababu mazingira ambayo chaguzi hufanyika si ya huru, haki, na uwazi.

Sawa, hiyo ni hoja nzuri na yenye mashiko. Lakini mimi binafsi bado naamini kabisa kuwa kwamba watu kwa umoja wetu tukiamua kabisa kutokuipigia kura CCM tunaweza, hata kama CCM itaamua kuchakachua matokeo au kuleta mizengwe [kama ilivyofanyika Zanzibar].

Na ikitokea tukafanya hivyo na CCM kuchakachua na kuendelea kung'ang'ania madarakani walau tutakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuishinikiza mpaka itoke. Ila kwa sasa inakuwa vigumu kwa sababu hata bunge limejaa hao hao CCM na hivyo kuifanya hoja ya chaguzi kutokuwa huru na haki kukosa nguvu kidogo.

Yaani kwa kweli ingekuwa ni juu yangu mimi basi ningependa sana kujaribu na watu wengine [zaidi ya CCM] ili tuone na wao wana nini la kutupa Watanzania.
 
Opinions. Uncle Ngosha yuko sawa. Ninamuelewa kwa sababu nilishamuelewa kabla hajawa Raisi. Ni ngumu kuielewa management style yake, mimi huwa naiita "JUST DO IT style"
Management By Walking About (MBWA)
 
Na sasa hivi hospital hakuna chanjo ya watoto,,kila kitu shidaa,vijana wanabaniwa kusoma aajiandae kukabiliana na majambazi ,,maana vijana wengi wapo tu na hawana pa kwenda
 
Utawala wa mwendokasi. Ni mwendo wa kuisigina katiba kila uchao.
 
Rais ni Magufuli na ataendelea kuwa magufuli. huko anakopita ni shangwe na vigelegele. wananchi wanatamani aseme neno roho zao zifrahi. huku mko busy kutunga ngonjera na hadithi zisizo na vichwa wala miguu......
Mmmh nahisi unaishi nje ya Tanzania,sio kwa mahaba haya. Duuuh[emoji15] [emoji15]
 
Mimi kila siku naomba asifike kituo cha mabasi cha Ubongo saa kumi na mbili asubuhi. Maana akiona mabasi yanavyokwenda mikoani na idadi kubwa ya wasafiri, anaweza kusema " Marufuku mabasi kuondoka Dar, watu wote hawa wakiondoka nani atafanya kazi?"
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Yakimshinda wewe unafaidika na nini? Tuambie Watanzania ili tujue. Toa lugha za kumpa moyo sio kuwazia mabaya.. Yule ni Rais wako na pia ni baba yako, lazima uwe na fikra za kinidhamu.
 
leo mpaka huyu jamaa kasema kitu! ni sawa na kumkuta chief mkwawa anahubiri siasa
 

tusiwe wajinga..hata yeye mwenyewe alisema kwa hali ilivyosasa ni bora kufanya maamuzi kama kunamakosa basi yatarehekebishwa kuliko kutofanya maamuzi yeyote kwa kuogopa
 
Jamaa nchi kaiweza. Mfano jana nilikwenda beach escape 1 moja ya beach yenye wapenzi wengi lkn kwajana mambo yalikuwa ni kinyume . Nilikuta viti havina watu. Nikasogea mchangani bahari imekuwa tupu. Nikitupa jicho baharini. Hakuna hata meli moja iliyosubiri kutia nanga.

Jamaa nchi kaiweza. Na inaonekana kama nchi kasusiwa hata naawaziri wake. Na kwakweli anaejua tunakoelekea aje atufafanulie.
 
wengi tu wanayaelewa, wewe endelea kutoyaelewa
Thubutuu amnyooshe nani? Watu wanajuwa ni roho yake mbaya hawezi kufanya lolote.sisi tunachoshindwa kumuelewa matamko yake hayaeleweki.
 
Na akionaa mnamsema sana jf ,anaipiga marufukuuu
Baba j hapendi mawazo kinzani yeye anajiona correct, ana create situation ambayo ikija kubuma itakua hatari. Na anaweza sema kweli ifungwe mana hulka ya wasiotaka kukosolewa huwa kuwanyamazisha opponents wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…