Rais Magufuli: Watanzania kuamini kila kitu cha kwenye mtandao ni kutokana na sisi kutoi-control mitandao

..uzuri wa mitandao ya kijamii ni UHURU wa kutoa mawazo.

..kuna kipindi Magufuli alikuwa anakubalika sana ktk mitandao ya kijamii.

..kukubalika huko kunaelekea kupungua sasa hivi.

..sasa anachotakiwa kukifanya ni kujisaili kuelewa ni wapi amepungukiwa na kupafanyia marekebisho.

..hatakiwi kuichukulia mitandao ya kijamii kama MAADUI, WAHUJUMU, au WASALITI.

..badala yake aichukulie mitandao kama TOCHI inayomulika maeneo yanayohitaji marekebisho kutoka kwa watawala.

Kwa mtu aliye kulia kwenye RTD, Daily News na Uhuru kama Magufuli, mitandani kwake ni wembe. Mitandao ya leo ni kama moto wa mstituni unoongezeka ukubwa kadidiri upepo unvyo vuma, tofauti na magazeti au redio ambavyo vinaweza kudhibitiwa haraka zaidi kuliko mitandao. Mitandao ni pressure sio hapa Tanzania pekee, hata nchi zilizoendelea kuna watu wazito na maarufu wameshindwa na pressure ya mitandao wameamuwa kujitoa kabisa. Nchi kama china inaonekana katili na haitowi uhuru wa kujieleza, lakini siku zijazo utasikiwa china imeweza kuokoa kizazi out of Internet stress huku nchi za mgharibi wameshindwa kuokwa watu wao. Ni kama mikopo nafuu kwa nchi za magharibi miaka ya 80-90, leo hii watu wa hizo nchi wanalia na wengine kujiuwa kwa kushindwa kulipa madeni.
 
Rais na serekali pamoja na bunge la JMT, wanatakiwa wajiulize kwa nini watanzania wanaamini zaidi habari zinazo toka kwenye mitandaao ya kijamii kuliko habari zinazo toka serekalini au Bungeni? I hope, THINKING it's not illegal yet!
 
Acha uwehu wewe mimi nilikuwa PAC miaka nane?

Na wewe unajiita mamba wakati sio mamba ni uhuni

dawa itawaingia tuu.
Sasa tutajuaje kama haukuwa PAC? Huwezi kuchukua kauli ya mtu kama ilivyo halafu unabandika tu bila kumtambua. Kama shule au chuo ni umefeli maana ni wizi wa uandishi na uhuni. Inaitwa Plagirism. Hamna cha dawa kuingia wala nini!
 
Kwa nini umetolea mfano wa marehemu na sio mfano wa hili lililopo mbele yetu
Hii ni pesa ingemtiba baba yako bibi yako mke wako watoto wako tungeweza kuwa na shule bora (zifundishe hiyo elimu uliyotaja)Tunapozungumzia upo tegu was pesa ya Mtz maskini mkulima mvuja jasho wakati wengine wanazifuja kwa kujenga nyumba za kifahari Mwanza Chattle na keingineko wakati vijijini watu wanateseka please msije hapa kuwabeza WaTz eti hawajui matumizi ya mitandao.
Trump ni mfano tu nimekupa sasa wewe utakuwa unajua social media kuliko mzungu mwenyewe aliyeileta
Wewe kazana kusoma Uhuru na Mzalendo tupishe sisi na social media zetu
Mnawaziba watu midomo kwa maovu yenu
Hii dhambi mtailipa even 50 years down the road kama hutailipa wewe atalipa mwanao au mjukuu wako au kitu kuu chako

Mfano wa marehemu ndio mfano halisi na kile alichokuwa anazungumzia JPM, kwamba mtu anaona Ah achana nibandike hili mtandaoni bila kufikiri madhara yatakayo tokea upande wa pili. Ndio maana nikasema kama kungekuwa na somo la kujifunza jinsi ya kujali kile tunacho andika labda upotoshaji ungepunguwa kwenye mitandao.

Swala la fedha kupotea ni swala la watanzania na mimi silipingi, nacho kipinga ni kutokuwa na uhakika na swala lenyewe. Je ni kweli hizo fedha zimepotea? ni kweli kuna mtu serikalini au kwenye taasisi yoyote aliyenufaika na upotevu huo? haya ni maswali halali na ya msingi. Lakini mtu ukiandika halafu inakuja kujulikana hakuna kilichopotea, yule aliyeandika uwongo tumfanye nini au atakuja kuandiaka samahani kwa upotoshaji wake? ELimu ya mitandao ni muhimu kwetu sote, mitandano ni moto wa msituni ukiwaka umewaka, hakuana atakayejitokeza kuuzima.
 
Watanzania wenzangu,

Kwenye ripoti yake, CAG hajasema popote kuwa TZS 1.5trn zimeibiwa. Alichosema leo Ikulu ndio msimamo wake uliopo kwenye Taarifa yake ukurasa wa 34. Fedha hizo HAZIONEKANI kwenye matumizi ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Ndio maana tunahoji zipo wapi. Tunataka Ukaguzi Maalumu ili kuhakiki majibu ya Serikali na kujua hela zetu zipo wapi. Hilo tu, hakuna lingine.

Vitisho vya hatua za kisheria ni tambo tu za watawala, hazina maana yeyote. Kumsimamisha CAG Ikulu na kumhoji mbele ya Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ni kumtisha CAG, ni kinyume na misingi ya Katiba yetu. Ripoti ya CAG ikishakuwa mbele ya Bunge sio Ripoti ya Executive tena. Ni mali ya Bunge. Kama Rais ana majibu aende akayaseme Bungeni mbele ya PAC.

Rais sio wa kumchekea chekea anapovunja misingi ya nchi yetu. Ni lazima ADHIBITIWE na Taasisi za Kikatiba ikiwemo Bunge. Rais leo amekosea. CAG naye amekosea kwenda Ikulu.

Watanzania sikilizeni, mimi nimekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC miaka 8, ninajua kusoma, kuchambua na kutafsiri Taarifa ya CAG. TZS 1.5trn hazina maelezo, hazipo Benki Kuu na Maelezo ya Naibu Waziri Fedha leo ni kujikosha tu.

Nikiwa Mwenyekiti wa PAC, Mwaka 2013 Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli alikutwa na Hoja ya ukaguzi ya TZS 252 bilioni ya ujenzi wa barabara hewa ambayo mpaka sasa haijajibiwa na utaikuta kwenye Hoja za CAG za mwaka 2016/17. Hivyo ni Kawaida yake kutoheshimu sheria za Fedha na kutojibu Hoja za Ukaguzi.

Kama Serikali ina uhakika kabisa hii hoja ya TZS 1.5trn haipo inipeleke mahakamani hata leo. Nitawashinda hata Jaji akiwa mmoja wa majaji wapya walioapishwa leo.

Mimi siogopi. Nitasema UKWELI daima fitina kwangu mwiko.

Zipo wapi TZS 1.5trn?
jamaa ni cancer kwa CCM "" sio kwa hoja hizi aiseee
 
..uzuri wa mitandao ya kijamii ni UHURU wa kutoa mawazo.

..kuna kipindi Magufuli alikuwa anakubalika sana ktk mitandao ya kijamii.

..kukubalika huko kunaelekea kupungua sasa hivi.

..sasa anachotakiwa kukifanya ni kujisaili kuelewa ni wapi amepungukiwa na kupafanyia marekebisho.

..hatakiwi kuichukulia mitandao ya kijamii kama MAADUI, WAHUJUMU, au WASALITI.

..badala yake aichukulie mitandao kama TOCHI inayomulika maeneo yanayohitaji marekebisho kutoka kwa watawala.
hana akili huyo yeye anawaza negative tu"" kama haoni umuhimu wa hiyo mitandao" KWANINI ALIITUMIA MITANDAO HIYO HIYO KUTOA RAMBI RAMBI KTIKA MSIBA WA WINIE MANDELA....

bangi mbaya sana aiisee"""
 
Mfano wa marehemu ndio mfano halisi na kile alichokuwa anazungumzia JPM, kwamba mtu anaona Ah achana nibandike hili mtandaoni bila kufikiri madhara yatakayo tokea upande wa pili. Ndio maana nikasema kama kungekuwa na somo la kujifunza jinsi ya kujali kile tunacho andika labda upotoshaji ungepunguwa kwenye mitandao.

Swala la fedha kupotea ni swala la watanzania na mimi silipingi, nacho kipinga ni kutokuwa na uhakika na swala lenyewe. Je ni kweli hizo fedha zimepotea? ni kweli kuna mtu serikalini au kwenye taasisi yoyote aliyenufaika na upotevu huo? haya ni maswali halali na ya msingi. Lakini mtu ukiandika halafu inakuja kujulikana hakuna kilichopotea, yule aliyeandika uwongo tumfanye nini au atakuja kuandiaka samahani kwa upotoshaji wake? ELimu ya mitandao ni muhimu kwetu sote, mitandano ni moto wa msituni ukiwaka umewaka, hakuana atakayejitokeza kuuzima.
ili kuondoa huo mkanganyiko "" siwaruhusu hilo swala kuchunguzwa na kamati ya bunge ...kuna haja gani ya kuendelea kuchambua mambo kwa hisia mkuu"" wanachokiogopa nini ""?? umewahi kuona wapi mtu anayetuhumiwa kwa uhalifu akakubali kuwa yeye ni muhalifu wakati anajua fika kuwa kitendo cha uhalifu ni moja ya vitendo vyenye sifa mbaya na ya haramu mahala popote pale duniani"""
 
Madikteta siku zote uwa wanaminya vyombo vya habari na pia hawapendi kukosolewa kama JPM ametoa bunge live ila mambo yake ya kiki za kufungua vitu ambavyo vinawahusu mawaziri yeye kudandia kufungua ili tu hapate kiki.Ameona mitandao ya jamii kwa sasa inapeleka habari kwa jamii kwa haraka sana.Suluhisho alilonalo JPM kwenye halmashauri ya ubongo wake ni kuminya uhuru wa habari kwa wananchi wake ili hapige fedha za uma kirahisi
 
Watu wanapenda kutoa mifano ya China, halafu wanasahau ingekuwa CHINA wote wale walio tufisidi kwa njia moja au nyingine tungekua hatunao. Kule masisadi wanakula shaba moja kwa moja.
kwanza nimifano ya kipuuzi na yakijinga kabisa..kwahiyo kama China wanaishi kwakula Nyama za watu na sisi tule ""tunapaswa kuishi chini ya muongozo wa katiba ya nchi yetu nasio chini ya muongozo wa katiba ya china..katiba ya nchi yetu inatambua "" uwepo wa haki ya kujadiliana kwa hoja na kupingana kimitazamo"" inatambua kuwa kila mwananchi wanchi husika anayo haki ya kushauri ama kukosoa utendaji unaofnyika serikalini"" so inakuwaje leo atueleze habari za china wakati katiba yetu inajieleza wazi katika suala zima la majadiliano....
 
Rais Magufuli leo akiwaapisha Majaji 10 aliowateua pamoja na Mawakili amesema kuwa Watanzania tunaamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii. Hii inatokana na kutoku-control mitandao hiyo wamiliki wako huko wao interest yao ni kutengeneza biashara wala hawajali consequences zitakazotokea

> Rais Magufuli ameongeza kuwa hadhani kama ukienda kwenye nchi kama China utakuta wana 'Google' na 'WhatsApp' kama hizi za kwetu huku

> Rais Magufuli: Kila Mtu anapojifikiria anapost chochote kwenye mitandao ya kijamii

Rais ameelezea tabia ya kuamini mijadala ya mitandaoni kama ugonjwa ambao hafahamu umetoka wapi. Ameeleza kuwa siku moja alikua akisoma mtandaoni kuhusu serikali kuiba Trilioni 1.5 ikabidi ampigie CAG kuuliza kuhusu wizi huo

======
Ikumbukwe kuwa mnamo Septemba 28 mwaka 2016 Rais Magufuli alinukuliwa akisema kuwa ''Anatamani Malaika washuke wazime mitandao ya kijamii, irudi baada ya mwaka 1 ikute hatua kubwa za kimaendeleo tulizopiga''
[/QQUOTE
Where there many people you can not stop stealing instead control
 
Kwa mtu aliye kulia kwenye RTD, Daily News na Uhuru kama Magufuli, mitandani kwake ni wembe. Mitandao ya leo ni kama moto wa mstituni unoongezeka ukubwa kadidiri upepo unvyo vuma....

..tatizo ninaloliona ni kuwa Magufuli ana focus zaidi kwa wale wanaompinga, and ignoring the fact kuwa wapo wengi sana ktk mitandao wanamuunga mkono.
 
Mimi sikatai umuhinu wa mitandao ya kijamii, lakini je ni wangapi wanajuwa kupanga na kupanguwa kilicho kwenye hiyo mitandao? hata huyo Trump mwenyewe, mara ngapi anadika vya uwongo na baadhi ya watu wanaamini. Kuna kijana mmarekani alianika mwili wa mjapani aliye jingonga bila kujali madhara ya hizo picha kwa wanadugu wa marehemu, Je kwako wewe huo ndio matumizi stahiki ya mitandao. Hata kama watu wanataka kuibuwa wizi Je aliye andika kama kadanganya na nchi ikavurugika kwenu hili ni jambo jema?
Wewe unatakaje?..hakuna kitu kisicho na kasoro hapa duniani..ukiwemo wewe mwenyewe!..Nadhani hulijui lengo la mzee baba..hataki kukosolewa kabisaa..anataka kusifiwa tu!..nakuhakikishia kama watu wangekuwa wanamsifia kwenye mitandao..angekuwa anarukaruka kama ndama na hata angeweza kuzirudia zile pushups za wakati wa uchaguzi kwa furaha!Tunahitaji maelezo ya kutosha 1.5 trilion zimeenda wapi?na sio miamala kuiva sijui nn..slowslow hatutaki porojo!
 
Ahsante sana Pakawa.

Kwa nini umetolea mfano wa marehemu na sio mfano wa hili lililopo mbele yetu
Hii ni pesa ingemtiba baba yako bibi yako mke wako watoto wako tungeweza kuwa na shule bora (zifundishe hiyo elimu uliyotaja)Tunapozungumzia upo tegu was pesa ya Mtz maskini mkulima mvuja jasho wakati wengine wanazifuja kwa kujenga nyumba za kifahari Mwanza Chattle na keingineko wakati vijijini watu wanateseka please msije hapa kuwabeza WaTz eti hawajui matumizi ya mitandao.
Trump ni mfano tu nimekupa sasa wewe utakuwa unajua social media kuliko mzungu mwenyewe aliyeileta
Wewe kazana kusoma Uhuru na Mzalendo tupishe sisi na social media zetu
Mnawaziba watu midomo kwa maovu yenu
Hii dhambi mtailipa even 50 years down the road kama hutailipa wewe atalipa mwanao au mjukuu wako au kitu kuu chako
 
Mfano wa marehemu ndio mfano halisi na kile alichokuwa anazungumzia JPM, kwamba mtu anaona Ah achana nibandike hili mtandaoni bila kufikiri madhara yatakayo tokea upande wa pili. Ndio maana nikasema kama kungekuwa na somo la kujifunza jinsi ya kujali kile tunacho andika labda upotoshaji ungepunguwa kwenye mitandao.

Swala la fedha kupotea ni swala la watanzania na mimi silipingi, nacho kipinga ni kutokuwa na uhakika na swala lenyewe. Je ni kweli hizo fedha zimepotea? ni kweli kuna mtu serikalini au kwenye taasisi yoyote aliyenufaika na upotevu huo? haya ni maswali halali na ya msingi. Lakini mtu ukiandika halafu inakuja kujulikana hakuna kilichopotea, yule aliyeandika uwongo tumfanye nini au atakuja kuandiaka samahani kwa upotoshaji wake? ELimu ya mitandao ni muhimu kwetu sote, mitandano ni moto wa msituni ukiwaka umewaka, hakuana atakayejitokeza kuuzima.
Pesa zimepotea zimeibiwa whatever the case is CAG ndio muongo au mnatetea kujinufaisha wachache
Raisi asije na majibu mepesi mepesi yeye kama kiongozi hupashwi kujibu ya mtandaoni alipashwa aamuru Bunge lichunguze ukweli sio kusingizia mitandao.
He has to be responsible, own his mistakes period!
 
ili kuondoa huo mkanganyiko "" siwaruhusu hilo swala kuchunguzwa na kamati ya bunge ...kuna haja gani ya kuendelea kuchambua mambo kwa hisia mkuu"" wanachokiogopa nini ""?? umewahi kuona wapi mtu anayetuhumiwa kwa uhalifu akakubali kuwa yeye ni muhalifu wakati anajua fika kuwa kitendo cha uhalifu ni moja ya vitendo vyenye sifa mbaya na ya haramu mahala popote pale duniani"""

Swala muhimu, kuna taratibu za kibunge kuhoji chochote ambacho inakiona sio sawa. Ndio moja ya kazi za kamati za kudumu za bunge. Lakini kuna watu wameamuwa kujichukulia umaarufu wa haraka haraka kwa kupaza sauti pasipo hitaji kupazwa sauti. Hii sio mara ya kwanza bunge kuhoji au CAG kutowa mapungufu kwenye mapato na matumizi ya serikali.
 
Usiwe mpumbavu kama bosi wako. Walioanza kupaza sauti wakitetea huu upotevu wa mabilioni ya kodi zetu unawajua vizuri kabisa nao ni mawaziri wake dikteta uchwara.
 
Back
Top Bottom