Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,586
Wewe unatakaje?..hakuna kitu kisicho na kasoro hapa duniani..ukiwemo wewe mwenyewe!..Nadhani hulijui lengo la mzee baba..hataki kukosolewa kabisaa..anataka kusifiwa tu!..nakuhakikishia kama watu wangekuwa wanamsifia kwenye mitandao..angekuwa anarukaruka kama ndama na hata angeweza kuzirudia zile pushups za wakati wa uchaguzi kwa furaha!Tunahitaji maelezo ya kutosha 1.5 trilion zimeenda wapi?na sio miamala kuiva sijui nn..slowslow hatutaki porojo!
Sifa tamu jamani hata mimi ukinisifia hapa nadani nitalala usingizi mnono, utani pembeni. Unajuwa ukitaka watu wakusikileze au waendelee kukusikiliza ongea jambo la maana, ukishaaza kuleta uswahili-swahili watu wanakuchukulia huna kitu wanakuweka pembeni. Ndio tatizo la mitandao yetu kila mtu anasema, vingine havina hata haja ya kuvitilia maanani matokeo yake hata huyo JPM mwenyewe anaacha kuwasikiliza watanzania ana kufanya ya kwake. Maana hata yeye akiperuzi mitandao haoni kitu muhimu kinacho waliza watanzania zaidi habari za upotoshaji zinazo jirudia-rudia. Mara watu wasio julikana, mara vyetu feki vya bashite, mara diamond amembusu sijuwi nani. Tunatumia hii mitandai vibaya japo ni huru kwa kila mtu kutumia