Rais Magufuli: Wasiotutakia mema wanatumia Asasi za Kiraia na NGO kutuhujumu ili kufifisha jitihada zetu kujikomboa kiuchumi kwa maslahi yao binafsi

Kwa nini kila azungumzapo yeye ni kulialia tunahujumiwa, hatupendwi, mabeberu wanatuonea nk nk?
Hivi tuna nini sisi hapa duniani kilicho cha kipekee hadi tushambuliwe kiasi hicho?
Tumeharibu biashara wenyewe, tumeua kilimo cha biashara chenye kuweza kubadili maisha ya watu wetu wenyewe na tumevunja mahusiano ya kijamii na kikanda kwa ubaguzi tulio anzisha wenyewe halafu tunatupia lawama za kilaghai kwa wengine?
CCM mtaacha lini usanii?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mahusiano gan ya kikanda yamevunjwa?
 
Tunahujumiwa sawa, lakini si kila wanalosema au kutufanyia lisipotupendeza ni hujuma. Mwisho tunajenga paranoia na kutenda bila kufikiri.
 
Elimu tunayotoa kwa vizazi vijavyo, hasa ukilinganisha na wanayopata wa kwao, inawahakikishia mabeberu kesho yenye neema ya kuendelea kutubeberu pengine kirahisi zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
 
Sisi Tukitazama Juu, Vibaraka wa Mabeberu Wanatazama Chini

Walifurahi sana kusikia imekamatwa. Walikesha wakiomba isitolewe ili wacheke. Wamefeli sana.

Leo hii aibu zimewajaa. Wanainamisha vichwa chini kwasababu hawana la kusema. Wameumbuka sana.

Sisi tunaangalia juu tukiwa na nyuso zenye furaha na tabasamu. Tunafurahia kurudi kwa ndege yetu. Tuna uzalendo.

Tarehe 14/12/2019 ni kesho. Nadhani watajifungia ndani jinsi aibu ilivyowajaa.

Ndege ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Niliona ACTL ikitoa gawio ili fedha hizo zikasaidie maendeleo ya jamii. Pongezi kwao.

Waendelee kutazama chini na sisi tunatazama juu. Tunawapa vidonge vyao. Wakimeza wakitema shauri yao. MAGUFULI SAFIIIIIII. Kama mzalendo wa kweli itikia...ukinyamaza mnafiki.
 
Hizi NGO zilikuwa na nguvu sana enzi za diplomat Kikwete na diplomat Mkapa, awamu hii ya mwana wa Chato zinakutana na muafrika halisi asiyezuzuliwa na u-magharibi.
 
Bado kuna watu wachache tu wanaoisumbua Nnchi hii ila kingine hakuna anaefurahia maendeleo ya mtu ni muda wa watanzania kuungana kwa pamoja nasi kuleta mgawanyo usio na maana..
 
On the contrary kauli za namna hii si za kizalendo bali ni kibaguzi na kugawa watu, ionekane kuna kundi fulani ndiyo linaipenda nchi na lingine linahujumu nchi. Hii si kweli, when i read between lines anataka kuwafanyia ubaya kundi fulani la watu kwa kisingizio cha uzalendo.

Hakuna mtanzania asiyeipenda nchi yake, wanaokosoa wanakosoa ili taifa lisonge mbele na hii ni kawaida kwa mtu yeyote aliyepitia development studies misuguano ni jambo la kawaida. Na kwa waliosoma physics they know that there is no movement without friction. We unataka kuongoza nchi ambayo watu wametulia kama maji ya mtungi we ni nani? hakuna nchi ya hivyo, ajifunze kupanua kifua cha kupokea anayoyataka na asiyoyataka. That is what leadership entails.
Waliosema "AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE" hawakukosea kabisa!
 
Haya maneno ya Raisi Magufuli yana ukweli mwingi sana, na haya kuanza leo, nyerere alihujimiwa sana lakini alivumilia sana na tukipata shida sana.

Huko Somalia Siad Barre 1977, alishawishiwa na Jimmy Carter aivamie Ethopia, Urusi ilipo badilisha kambi kuwahama Somalia na kwenda kwa Mengistu Ethopia, na baadaye America wakamtelekeza Barre mpaka machafuko yakaanza somalia.

Waingereza walimshawishi Iddi Amin ampindue Obote hatimaye tuliona yaliyotokea, na wakamshawishi Nyerere aivamie Uganda, wakatutelekeza peke yetu, hadi uchumi wetu ukaharibika.

Leo hii wanatumia NGO na WHO kutudhibiti kwa kutumia chanjo za Polia na maradhi mengineyo, huku wachanganya dawa za kufunga uzazi, tuzizaane.

Kuna mengi yanafanywa tusiendele na wazidi kutudhibiti.

Mradi wa Steigle Gorge unapigwa vita, eti mazingira na utawateketeza wanyama, mbona mradi wa REINASENCE DAM wa Ethopia hawaupingi wala kuuzungumzia, kwa sababu wanaodhurika ni waafrika, na hakuna wanyama pori kwa starege zao, lakini Waafrika zaidi ya million 120 hakuna neno wakiteseka kukosa maji kwa maisha yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom