Rais Magufuli: Wanaotunyima misaada muwaonee huruma

Rais Magufuli: Wanaotunyima misaada muwaonee huruma

hapana siku ngapi zimeita kabla ya siku 3? Ni kama wiki

Naukuuliza mkuu, hivi kutoa faili kabatini inachukua siku 3 kweli!
Faili lina mkataba uliotumika kuchukulia pesa! Siku 3 kweli au kunakuficha na kutaka kufanyia kazi nyaraka!

Mkuu hili wamekimbia , wengine wapo majimboni! kaa la moto si mita za bandarini

LUGUMI ! itatueleza mengi , ukweli, uongo na unafiki! Toeni mkataba! Toeni maagizo mkataba utoke haraka, faili lipo kwanini ichukue siku 3 kulitoa kabatini! why
Kuleta mkataba ingewezekana palepale kikaoni Makamu Mwenyekiti wa PAC aagize kuwa naahirisha kikao kwa SAA moja wajumbe wakanywe chai na IGP nenda katuletee faili la mkataba wa Lugumi full stop. Siku tatu kama vile mkataba unahifadhiwa Geneva?
Naanza kuona kuwa kwa vile bei ya wajumbe wa kamati za bunge inafahamika ni milioni 30 (refer to Lugola & others) sasa kama kamati inao wajumbe 20 basi ni kutafuta milioni 600 tuu kuwapoza.
Business as usual
 
...mkuu si ndio kamati ya Bunge jana wameandika barua kwa jeshi la polisi, baada ya zile siku saba za mwanzo kupita bila majibu,jana wamepewa siku tatu kwenye hiyo barua,wawe wametolea ufafanuzi hayo mambo,hebu tusubiri tuone kitakachotokea,subira yavuta kheri.
Huo ni mchezo wa paka na panya tu na tutaishia kusikia hayo hayo kila kukicha
 
JPM ni mtata na mtu anayejikinzani mara kwa mara. Kwa hakika tunamshukuru sana kwa hatua anazozichukua kurejesha uadilifu, nidhamu, uwajibikaji hususan katika utumishi wa umma. Ni kweli kwa anayoyafanya na kauli zake ni njia ya kukiri makosa yaliyofanywa na serikali ya CCM (ambayo na yeye alikuwemo ndani yake kwa muda wa miaka 20) na hivyo kuwa tayari kuyarekebisha. Huu ni ujasiri ambao nchi ilikuwa haijawahi kuushuhudia tokea mwisho wa awamu ya kwanza. Kwa hilo anastahili pongezi kubwa na sisi wananchi tunamuunga mkono.

Lakini cha ajabu na pengine cha kusikitisha katika suala la kunyimwa misaada na washiriki wa jadi wa maendeleo (a.k.a wahisani) anawalalamikia na kuhamasisha wananchi wawaone kuwa ni wabaya (maadui wa Tanzania) kutokana na hatua walizozichukua za kusitisha au kupunguza misaada kutokana na serikali hiyo hiyo ya CCM kubaka ama kudhoofisha mwelekeo mzuri tuliokuwa tunaufuata wa demokrasia na utawala bora.

Kwa mtu anayekiri makosa ili asiyarudie, ungemtarajia aongelee suala hili la wahisani kwa mtazamo chanya kwamba, kwa mfano, ndiyo misaada yao ilikuwa ni sehemu kiduchu ya bajeti yetu (kwa hivyo haina athari kubwa katika kuendesha nchi yetu), lakini uamuzi wao ni ujumbe (a.k.a message) tosha na muhimu kwetu kwamba kuna mahali katika eneo la demokrasia tumeteleza na tutaangalia ni wapi tumeteleza.

Kwa kufanya hivyo, angetupa matumaini kuwa yuko tayari kuimarisha na kurutubisha demokrasia. Mtu asikudanganye kuwa unaweza ukapanda mbegu za uadilifu, uzalendo, na utawala bora na zikastawi na kushamiri hususan katika utumishi wa umma bila kuwa na demokrasia imara. Katika dunia ya karne ya 21 huwezi kujivunia ubakaji wa demokrasia, tena mchana kweupe, na bado ukajihesabu ni miongoni mwa jamii zilizostaharabika - yaani ukatembea kifua wazi. Utachekwa na kuonekana kama mwendawazimu mbele ya jamii ya kimataifa.
Ninakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa.

Tatizo la Zanzibar linahitaji mjadala mpana bila kuweka hisia.

Hatufahamu Serikali ilisema nini kwenye vikao vyake na uongozi wa MCC.

Kwa upande wangu ninadhani Tanzania tuna tatizo la Katiba zetu kwa maana kuwa Katiba ya Tanzania na Katiba ya Zanzibar zinakinzana ndiyo maana kama taifa tunajikuta kwenye no man's land pale masuala kama ya uchaguzi yanapokuwa na matatizo. Katiba zetu hazijaweka sawa namna ya kukabiliana na mazingira kama yaliyojitokeza huko Zanzibar.
 
Huu mchezo hauitaji hasira mkuu .... Wewe lini umeona zuri la serikali ya Magufuli?

Wewe kizuri ni kinachotoka kwa chadema na friends of Lowassa tu.

Hakuna anayetafuta mazuri au mabaya ya serikali,hivi kwa nini mtu anapojaribu kuutafuta Ukweli kuna baadhi ya watu mnaumia horo?Ifike mahali watu wawe tayari kuutoa Ukweli hata kama Ukweli huo utakuwa unagusa mboni za macho yao.

Ni kweli tumeshuhudia tofauti kubwa iliyopo kati ya serikali ya awamu ya nne na hii ya awamu ya tano,ila kuna link inayozifanya serikali hizi zisivuke mstari wa uwajibikaji,link hiyo ni Ukweli kwamba serikali hizi ni serikali za Chama Cha Mapinduzi(CCM)

Matatizo makubwa ya nchi hii ambayo kimsingi ndiyo yaliyolifikisha Taifa letu hapa lilipo hayapo katika utendaji wa mtu mmoja mmoja,mtu mmoja hajawahi na hataweza kuwa kikwazo cha Maendeleo yetu kama Taifa.Ndiyo maana linapokuja suala la kuwajibishana,serikali huchukua hatua mara moja ikiwa tu anayepaswa kuwajibika ni mtu mmoja na si mfumo.

Aliyepata kuwa waziri mkuu Mh.Pinda aliwahi kusema kuwa kuwa"mafisadi si watu wadogo,na unahitajika uangalifu katika kupambana na mafisadi,vinginevyo mafisadi wanaweza kuiyumbisha nchi"

Tusifikiri eti mtu huamka tu asubuhi toka kitandani kwake na kuamua kuwa fisadi,ufisadi hasa ule unaominya ustawi wa watu wetu una "koneksheni" na wale tuliowapa dhamana.Dili zote za kifisadi hazianzishwi na mtu kapuku kama Mimi,ufisadi ni miradi na biashara za wakubwa.

Ni rahisi mtu kuitaja LUGUMI,EGMA,KAGODA,ESCROW,IPTL na mengine mengi.Lakini je,tumeshajiuliza ni kwa nini huwa vigumu kuyawajibisha makampuni hayo na hata pale inapotokea wakawajibishwa hufanywa hivyo kwa shinikizo tu la kisiasa lakini kimsingi bado wahusika watalindwa? Mh.Pinda aliposema mafisadi wanaweza kuyumbisha nchi alijuwa na anafahamu mifumo inayoanzisha na kuulea ufisadi nchini.

Rais akitaka kutumia "falsafa ya mbanano" kupambana na mafisadi,Mwisho wa siku atashangaa kukuta ufisadi wote uliasisiwa ndani ya "korido za ikulu"

Tulishuhudia mawimbi ya upepo wa Escrow yalivyovuma pande zote za nchi na kwenda kuishia katika viunga vya ikulu kiasi cha kutishia kuing'oa ikulu.Hili la LUGUMI tayari linaonesha kuwa Na tufani ambalo likiruhusiwa kuvuma,upepo wake unaweza kuezua paa la ikulu na makao makuu ya jeshi la polisi.Hapo ndipo tunapofikia hatua ya kukubaliana na Mh.Pinda kuwa mafisadi wanaweza kuyumbisha nchi.

Ni afadhari mh.aendelee kufagia uchafu uliopo barabarani kwa kuvitumbua vipele jamii ya "kilango", kuliko kujaribu kutumbua jipu lililopo moyoni mwake ambalo ni sehemu ya uhai wake pale ikulu.Jipu aina ya LUGUMI lenye chembe chembe za " mawe matatu,Liz 1,mkwere na kamanda mwema sana" huku likihusisha ofisi nyeti ni Hatari.Ni bora kubaki na uvundo wa ufisadi ikulu,kuliko kuivua nguo ikulu yetu kwa kuanika mikataba miovu iliyofichwa kwenye kabati za ikulu.

Kuiamini serikali ya ccm kuwa itapambana na ufisadi papa ni sawa na kuitaka serikali hiyo ilikate tawi ililokalia,serikali yote ni zao la ufisadi wa kimfumo uliofanywa na waliopewa dhamana ya kuliongoza Taifa,ndiyo uti wa mgongo wa serikali,ndiyo uliotumika kuwaingiza serikalini kwa kutoa hongo za kanga,t-shirts,kofia,chumvi Na viberiti.CCM na ufisadi ni sawa na mwili na ngozi,kujaribu kuitenganisha serikali ya CCM Na ufisadi ni jaribio ovu na katili lenye lengo la kuiuwa CCM yenyewe.
 
Mwenyekiti wa CCM aombe msamaha kwa makosa yote. Akishindwa Rais Magufuli aombe watanzania msamaha kwa niaba ya chama chake. Hapo ndipo tutakapoanza upya. Bila ya hivyo ni maigizo tu! Maana hayo yote anayoyalalamikia yamesababishwa na serikali za CCM, ambazo naye kwa miaka 20 alikuwa sehemu ya serikali hizo. Na sijamsikia akiomba radhi.
Rais Magufuli ameishasema serikali ilifanya makosa kwenye masuala fulani na kwa sasa akiwa kama Rais anajaribu kurekebisha, kwa maana nyingine katika mtazamo wangu hii statement inatoa ujumbe wa kuomba msamaha.

Mimi sioni umuhimu wowote kwa Mwenyekiti wa CCM kuomba msamaha kwa sababu hata akiomba msamaha hawezi kubadilisha mazingira yaliyopo na yanayokuja bila kuitegemea serikali.
 
Ndicho hata mimi ninakipenda kwa Rais Magufuli. Rais lazima kwanza akubali madhaifu ya serikali yake baada ya kuyatambua ili aweze kutafuta njia ya kuyaondoa.

Nilimsikia akisema hata kwenye ofisi yake kulikuwa na wafanyakazi hewa.
Sometimes kampeni za JPM nilikuwa najiuliza bila majibu jinsi alivyokuwa anashangaa duh aisee utazani amekodiwa tu toka nchi nyingine.
 
Nchi haiendeshwi hivyo wewe, suala lipo mikononi mwa kamati ya Bunge wewe unataka Magu afanye nini? Muda mwingine ni vyema ukajielimisha kuhusu mambo ya unayoyapenda kuzungumzia yana taratibu zipi. Kwani hili la Lugumi wewe ulilipataje au limeibuliwaje? Ukiwa na ashki ya kukosoa tu ipo siku utamkosoa mpaka Mungu kwa jinsia aliyokupa.
Hawezi kukuelewa kwa sababu ametaka tu ili asikuelewe.

Nia yake ni kujaribu kuweka link kati ya LUGUMI na ofisi ya Rais wa Awamu ya Tano ili atimize malengo yake yenye hitimisho linalosema, ''NILISEMA Rais Magufuli hawezi kuleta mabadiliko ya kweli''.
 
Mkuu pole sana kwa kupitia mabonde na milima ila hawa jamaa wa UKAWA ni zaidi ya wafuasi wa iblis wao wapo kwenye ubaya tu.
 
Ndugu mambo yanakwenda kwa ngazi. Ngoja tuone hizo siku tatu kama police watapeleka mikataba kwa kamati. Hapa naona kuna kununiana misuli. Jamaa waliingia bungeni na kuburuza watu. Sasa inakula kwao!
 
Kuna mahali nakubaliana na JPM 100%, ingawa kwenye baadhi ya maeneo nakuwa siko naye. Kwa mfano, bado naamini Tanzania inahitaji misaada. Kujiamini kwamba tunaweza sisi wenyewe bila misaada ni jambo zuri, lakini hatuoni kwamba tungekwenda haraka zaidi kimaendeleo kama tungepata pia misaada? Na tena ninaamini, misaada wakati huu ambao tunajivuna kuwa na rais anayesimamia vizuri raslimali za nchi, ingekuwa na manufaa mkubwa zaidi katika kuharakisha maendeleo ya nchi. Lakini tunaponyimwa misaada baada ya kufanya mambo ya "hovyo hovyo" hatupaswi kuweka utetezi wa "hatuzitaki mbichi hizi" bali viongozi wetu waangalie na kutathimini mambo wanayoyafanya na athari zake.
Ninakubaliana na wewe kwa namna moja au nyingine lakini pia nadhani kunyimwa misaada kutatufanya tuamshe fikra zetu (blessing in disguise)

Kwa mfano, wananchi wa nchi kama za kwenye mabara ya Ulaya na Asia waliamusha fikra zao ili kupambana na mazingira ya winter kwa sababu hawakuwa na msaada mwingine na kwa kufanya hivyo, waliweza kutafuta njia ya kujikinga na baridi kali.

Tanzania tumebarikiwa maliasili nyingi tu ambayo ina demand sana lakini kwa sababu mawazo yetu ni tegemezi ndiyo maana tunaridhika na kile Rais Magufuli anaita vimusaada vya masharti magumu.
 
Ninakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa.

Tatizo la Zanzibar linahitaji mjadala mpana bila kuweka hisia.

Hatufahamu Serikali ilisema nini kwenye vikao vyake na uongozi wa MCC.

Kwa upande wangu ninadhani Tanzania tuna tatizo la Katiba zetu kwa maana kuwa Katiba ya Tanzania na Katiba ya Zanzibar zinakinzana ndiyo maana kama taifa tunajikuta kwenye no man's land pale masuala kama ya uchaguzi yanapokuwa na matatizo. Katiba zetu hazijaweka sawa namna ya kukabiliana na mazingira kama yaliyojitokeza huko Zanzibar.
Usemalo ni kweli lkn jamaa zako wa CCM hawaamini hiki ulichoandika Nafasi tuliyoipata yakuandika KATIBA tungeitumia vzr angalau matatizo mengi yangepungua....Sijui Magufuli.....Kama atakuwa na hill wazo manake chama chake kimegeuza issue ya Katiba kama ILANI ya CHAMA chao
 
Hakuna anayetafuta mazuri au mabaya ya serikali,hivi kwa nini mtu anapojaribu kuutafuta Ukweli kuna baadhi ya watu mnaumia horo?Ifike mahali watu wawe tayari kuutoa Ukweli hata kama Ukweli huo utakuwa unagusa mboni za macho yao.

Ni kweli tumeshuhudia tofauti kubwa iliyopo kati ya serikali ya awamu ya nne na hii ya awamu ya tano,ila kuna link inayozifanya serikali hizi zisivuke mstari wa uwajibikaji,link hiyo ni Ukweli kwamba serikali hizi ni serikali za Chama Cha Mapinduzi(CCM)

Matatizo makubwa ya nchi hii ambayo kimsingi ndiyo yaliyolifikisha Taifa letu hapa lilipo hayapo katika utendaji wa mtu mmoja mmoja,mtu mmoja hajawahi na hataweza kuwa kikwazo cha Maendeleo yetu kama Taifa.Ndiyo maana linapokuja suala la kuwajibishana,serikali huchukua hatua mara moja ikiwa tu anayepaswa kuwajibika ni mtu mmoja na si mfumo.

Aliyepata kuwa waziri mkuu Mh.Pinda aliwahi kusema kuwa kuwa"mafisadi si watu wadogo,na unahitajika uangalifu katika kupambana na mafisadi,vinginevyo mafisadi wanaweza kuiyumbisha nchi"

Tusifikiri eti mtu huamka tu asubuhi toka kitandani kwake na kuamua kuwa fisadi,ufisadi hasa ule unaominya ustawi wa watu wetu una "koneksheni" na wale tuliowapa dhamana.Dili zote za kifisadi hazianzishwi na mtu kapuku kama Mimi,ufisadi ni miradi na biashara za wakubwa.

Ni rahisi mtu kuitaja LUGUMI,EGMA,KAGODA,ESCROW,IPTL na mengine mengi.Lakini je,tumeshajiuliza ni kwa nini huwa vigumu kuyawajibisha makampuni hayo na hata pale inapotokea wakawajibishwa hufanywa hivyo kwa shinikizo tu la kisiasa lakini kimsingi bado wahusika watalindwa? Mh.Pinda aliposema mafisadi wanaweza kuyumbisha nchi alijuwa na anafahamu mifumo inayoanzisha na kuulea ufisadi nchini.

Rais akitaka kutumia "falsafa ya mbanano" kupambana na mafisadi,Mwisho wa siku atashangaa kukuta ufisadi wote uliasisiwa ndani ya "korido za ikulu"

Tulishuhudia mawimbi ya upepo wa Escrow yalivyovuma pande zote za nchi na kwenda kuishia katika viunga vya ikulu kiasi cha kutishia kuing'oa ikulu.Hili la LUGUMI tayari linaonesha kuwa Na tufani ambalo likiruhusiwa kuvuma,upepo wake unaweza kuezua paa la ikulu na makao makuu ya jeshi la polisi.Hapo ndipo tunapofikia hatua ya kukubaliana na Mh.Pinda kuwa mafisadi wanaweza kuyumbisha nchi.

Ni afadhari mh.aendelee kufagia uchafu uliopo barabarani kwa kuvitumbua vipele jamii ya "kilango", kuliko kujaribu kutumbua jipu lililopo moyoni mwake ambalo ni sehemu ya uhai wake pale ikulu.Jipu aina ya LUGUMI lenye chembe chembe za " mawe matatu,Liz 1,mkwere na kamanda mwema sana" huku likihusisha ofisi nyeti ni Hatari.Ni bora kubaki na uvundo wa ufisadi ikulu,kuliko kuivua nguo ikulu yetu kwa kuanika mikataba miovu iliyofichwa kwenye kabati za ikulu.

Kuiamini serikali ya ccm kuwa itapambana na ufisadi papa ni sawa na kuitaka serikali hiyo ilikate tawi ililokalia,serikali yote ni zao la ufisadi wa kimfumo uliofanywa na waliopewa dhamana ya kuliongoza Taifa,ndiyo uti wa mgongo wa serikali,ndiyo uliotumika kuwaingiza serikalini kwa kutoa hongo za kanga,t-shirts,kofia,chumvi Na viberiti.CCM na ufisadi ni sawa na mwili na ngozi,kujaribu kuitenganisha serikali ya CCM Na ufisadi ni jaribio ovu na katili lenye lengo la kuiuwa CCM yenyewe.
Mkuu asante kwa hii umeandika..unajua NCHI hii bado ccm inamini wapumbavu bado wapo wengi..kwenye Nchi..Watu wanamshangilia Magufuli nahawatamani wengine tumkosoe....Hawa hawa ndio waliokuwa wanarukaruka kumsifia Mkwere kipindi cha Uongoz wake Leo nihawa wanamponda Wakati mwingine najidharau sana kuwa mtanzania kwa kuona watu wanavyolazimisha watu tukubaliane nao.....Wajinga wengine wanatwambia Tumpe muda Rais muda upi ikiwa Chama chake kiko mamlakani tangu Uhuru nayy alikuwa kwenye Uongoz km 20yrd apewe muda wa nini.... Wengine sisi tumechoshwa na maigizo tunataka kazi...naingekuwa Amri yangu....Habari yoyote inaelezea kwamba Serikali au Rais atafanyakitu flan ningeizuia isitoje badala yake ziandikwe zile za matukio ambayo tayari yameshafanyika.....
 
Kwanza ndugu yangu ndumbaye ilifaa kwanza uelewa neno huruma lina maana ipi.
Kwa mujibu wa tafsiri ya neno huruma maana yake ni kua tayari kusaidia na kusamehe.

Sasa Mheshimiwa alikua na maana kwamba hawa wakoloni pamoja na mambo yao ya kipuuzi tuwe tayari kusaidizana inapo bidi na kusameana tunapokoseana.

All human beings are not perfect.
Kwa hiyo Rais kwa kauli yake hiyo alitumia hekima sana na anastahili pongezi.
Mkuu, Ninashukuru kwa kunisaidia kutoa elimu mulua.

Keep it up!
 
Ninakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa.

Tatizo la Zanzibar linahitaji mjadala mpana bila kuweka hisia.

Hatufahamu Serikali ilisema nini kwenye vikao vyake na uongozi wa MCC.

Kwa upande wangu ninadhani Tanzania tuna tatizo la Katiba zetu kwa maana kuwa Katiba ya Tanzania na Katiba ya Zanzibar zinakinzana ndiyo maana kama taifa tunajikuta kwenye no man's land pale masuala kama ya uchaguzi yanapokuwa na matatizo. Katiba zetu hazijaweka sawa namna ya kukabiliana na mazingira kama yaliyojitokeza huko Zanzibar.
Asante sana kwa maoni na hoja za kujenga. Lakini niongeze tu kwamba kwa hivyo basi JPM, kama kiongozi wa JMT, angeshauriwa kubadilisha lugha (kauli) - badala ya kuwaaminisha wananchi kuwa nchi 'wahisani' hawatutakii mema, wanatuonea gere au kutulaumu watu kama sisi kuwa sio wazalendo kwa kuunga mkono hatua za 'wahisani' (ambazo tunaamini ni za nia njema na hivyo sisi ni wazalendo), anaweza kuacha kabisa kulitolea kauli suala hilo kila anapokuwa anahutubia hadharani au tumewasikia na tunayafanyia kazi yote yaliyobainishwa. Hapa nitakubaliana nawe kuwa JPM ana hulka ya kukiri makosa (hata yaliyofanywa na watangulizi wake) - yawe ni ya kiuchumi, kisiasa, kiutawala, na hata kijamii - na huo ni mwanzo mzuri wa kuyatafutia dawa. Nikiri hapa kwamba nina matumaini makubwa kuwa atakua na kukomaa kisiasa! Muda bado ni mchanga.
 
Mkuu pole sana kwa kupitia mabonde na milima ila hawa jamaa wa UKAWA ni zaidi ya wafuasi wa iblis wao wapo kwenye ubaya tu.
Were akili huna yaani unataka wote waimbe mapambio yamkusifu?...Nyakati za nyuma watu walipokuwa wanaanika maDhaifu ya Mkwere..simlikuwa mnamwaga mitusi namna hii kikowapi sasa hivi Mliokuwa mnamtukuza ndio mnaongoza kumnanga.....Sasa nani mwenye akili nzito kama uji
 
Nimesoma kwenye gazeti la Raia Mwema nadhani, kuna nukuu moja inasema hivi (hapa sio rasmi na aliye na nukuu rasmi atuwekee):

"Uliyoyasema nimeyasikia na yote yamesababishwa na sisi wenyewe na miongoni mwa wahusika wamo humu ndani..." JK

Nilivyosoma nika najaribu kujiuliza kama ni kweli au la maana magazeti siku hizi yanaweza kuandika lolote. Lakini kama ni kweli basi ina maana matatizo yote JK alikuwa anayajua lakini alishindwa kuchukua hatua. Sasa kama alijua yaliyokuwa yanaendelea na waliokuwa wakiyafanya ni wazi hakujua ni kwa nini alishikishwa Quran Tukufu mchana kweupee kula kiapo cha kuilinda katiba!
 
Mkuu hii issue ya Lugumi si inashugulikiwa? au unataka results overnight, turudi kule kule kwenye yale yaliyomkuta mama malechela kwa kukurupuka?
Mkuu tunachosema hapa ni kuwa kwanini mkataba unachukua siku 3 kutolewa kabatini!

Tunachoogopa ni hizo nyaraka kuwa 'doctored' ili kuficha ukweli. Tena watu wakumbuke kamati ipo zaidi ya wiki, leo wanaongeza muda hawataki kutoa mkataba

Hivi kwanini watu hawaoni mchana? Yaani mkataba uliotumika kumlipa LUGUMI mabilioni unatafutwa siku 3 katika makabati! Kwamba hakuna anayejua upo wapi tena katika jeshi la Polisi! Hamuoni kuna walakini hapo?

Wahusika wamekimbia, mwingine anafungua maduka ya dawa kama mfamasia, mwingine kimyaa! Lugumi baba! kaa la moto
 
Back
Top Bottom