Rais Magufuli: Wanaotunyima misaada muwaonee huruma

Rais Magufuli: Wanaotunyima misaada muwaonee huruma

Nifahamishwe, kwanini ichukue siku 3 baada ya ubabaishaji wa wiki nzima kupata mkataba uliotumika kwa malipo ambao kama kitu halali. Leo mkataba umekwenda wapi?

Hatusemi kuna tatizo katika mkataba, tunajiuliza kwanini unafichwa na wanafanya nini wakati huu kwa mkataba uliotumika kutoa mabilioni ya fedha. Hakuna siri hapao

Wamekimbia hawataki kusema 'Toeni mkataba' wamekimbia kabisa! LUGUMI si mchezo
Weye unajuwa mkataba uko kwenye kabati Basi nenda kautoe. Maana hiyo Lugumi lazima ilikutowa nishia katika biashara zako ukaiombea dua ishuke Sasa inashuka unataka Kwa kasi zako .
Mkuu hii nchi Ina sheria Kama sikuzote nyie Watu wa Upawa mnavyo lilia.Wabunge wamewapa jeshi la polisi siku 3.Kama huwezi kusubiri kajinyonge Au kunywa SUMU yaishe.
 
MsemajiUkweli Tumemsikia mara nyingi na maneno hayo hayo(whining)
Tunataka atoke atuambie LUGUMI kilitokea nini.

Hili la Lugumi wote wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.
Tunahitaji kusikia nini kimetokea?

Hivi kwa akili yako unadhani Magufuli anaogopa? Unadhani alivyoenda Rwanda alienda kutembea tu? Hapo watu wako kazini and it is a matter of time issue ya escrow, Lugumi, Richmond itakuwa hewani.

Bahati mbaya haya makitu yanagusa familia ya mstaafu ndo maana anasubiri muda muafaka. hukumbuki wakati mh rais anazungumza na majaji juu ya mahakama ya mafisadi??

Subiri!
 
Rais amewaomba waandishi wa habari wawe wazalendo kwa taifa lao na waisaidie serikali katika juhudi zake za kuleta maendeleo ya haraka na pia wawe tayari kukosoa na kuelimisha katika mlengo wa kujenga Taifa na sio kubomoa Taifa.

''Niwaombe waandishi muwe wazalendo kwa Tanzania yetu kwa sababu na ninyi pia mnapata shida za kimaisha’’ Rais alisema.

Aliendelea kusema, ''Ni aibu kwa Rais kwenda kila mahali nchini na kukuta wananchi wake wanalia kwa sababu ya shida wanazozipata katika maisha yao wakati kuna watu wachache nchini wanafanya mambo ya hovyo’’. Ni lazima viongozi tujenge tabia ya kuwajibishana na tusipowajibishana hatuwezi kuivusha Tanzania yetu mahali pazuri''.
Rais naye awe mzalendo kwa kuonyesha mshahara wake na marupurupu, na pia kuonyesha analipa kodi kiasi gani. Siyo anasema uzalenda kwa wengine tu. Lazima awe mfano.
Akimaliza hilo, awe mzalendo pia katika kushiriki kubana matumizi kwa kupunguza mshahara na marupurupu yake. Apige mnada hizo BMWs na Benzs zilizo kwenye fleet yake; kisha aanze kuendeshwa kwenye Suzuki Vitara ama Rav4. Zoezi liende sehemu zote serikalini; apige marufuku matumizi ya magari ya design ya Land Cruisers. Kisha atoe agizo la kuanzishwa ama kutekelezwa kwa mfumo wa government car pool, ambapo viongozi waandamizi watakuwa wakikodi magari kutoka kwenye pool na kuyatumia pale panapouhitaji tu.
Bila kusahau aigize utaratibu wa mawaziri na viongozi wengine waandamizi (wakurugenzi, mameneja n.k.) kuwa wanajiendesha wenyewe, siyo lazima waendeshwe.
 
Wise people admit their mistakes easily. They know progress accelerates when they admit their mistake.

Admission of a mistake makes learning possible by moving the focus away from blame assignment and towards understanding.

Tunajifunza kutokana na makosa tuliyoyafanya baada ya kukili makosa tuliyofanya.

Tunapoanza kulaumu watu wengine kwa makosa yetu tunakuwa tunajiondoa kwenye funzo ambalo lingetuwezesha kupiga hatua mbele.

Rais Magufuli amekuwa muwazi kuhusu madudu ya serikali na makosa yaliyofanyika ndani ya serikali ya CCM.

Kuyakubali makosa ambayo yamelifanya taifa kuwa tegemezi kimaendeleo kunamfanya Rais Magufuli apate fursa na uwanja wa kushughulikia tatizo.

Wahenga walisema mficha maradhi kifo kitamuumbua.


Kwa kuficha uozo wa serikali kwa muda mrefu, taifa lilikuwa linaelekea kufa!

Kwa kusema nchi yetu ni masikini wakati ni tajiri, taifa lilikuwa linadumaa kifikra huku wachache wakinufaika na utajiri wa Taifa!
JPM ni mtata na mtu anayejikinzani mara kwa mara. Kwa hakika tunamshukuru sana kwa hatua anazozichukua kurejesha uadilifu, nidhamu, uwajibikaji hususan katika utumishi wa umma. Ni kweli kwa anayoyafanya na kauli zake ni njia ya kukiri makosa yaliyofanywa na serikali ya CCM (ambayo na yeye alikuwemo ndani yake kwa muda wa miaka 20) na hivyo kuwa tayari kuyarekebisha. Huu ni ujasiri ambao nchi ilikuwa haijawahi kuushuhudia tokea mwisho wa awamu ya kwanza. Kwa hilo anastahili pongezi kubwa na sisi wananchi tunamuunga mkono.

Lakini cha ajabu na pengine cha kusikitisha katika suala la kunyimwa misaada na washiriki wa jadi wa maendeleo (a.k.a wahisani) anawalalamikia na kuhamasisha wananchi wawaone kuwa ni wabaya (maadui wa Tanzania) kutokana na hatua walizozichukua za kusitisha au kupunguza misaada kutokana na serikali hiyo hiyo ya CCM kubaka ama kudhoofisha mwelekeo mzuri tuliokuwa tunaufuata wa demokrasia na utawala bora.

Kwa mtu anayekiri makosa ili asiyarudie, ungemtarajia aongelee suala hili la wahisani kwa mtazamo chanya kwamba, kwa mfano, ndiyo misaada yao ilikuwa ni sehemu kiduchu ya bajeti yetu (kwa hivyo haina athari kubwa katika kuendesha nchi yetu), lakini uamuzi wao ni ujumbe (a.k.a message) tosha na muhimu kwetu kwamba kuna mahali katika eneo la demokrasia tumeteleza na tutaangalia ni wapi tumeteleza.

Kwa kufanya hivyo, angetupa matumaini kuwa yuko tayari kuimarisha na kurutubisha demokrasia. Mtu asikudanganye kuwa unaweza ukapanda mbegu za uadilifu, uzalendo, na utawala bora na zikastawi na kushamiri hususan katika utumishi wa umma bila kuwa na demokrasia imara. Katika dunia ya karne ya 21 huwezi kujivunia ubakaji wa demokrasia, tena mchana kweupe, na bado ukajihesabu ni miongoni mwa jamii zilizostaharabika - yaani ukatembea kifua wazi. Utachekwa na kuonekana kama mwendawazimu mbele ya jamii ya kimataifa.
 
Wise people admit their mistakes easily. They know progress accelerates when they admit their mistake.

Admission of a mistake makes learning possible by moving the focus away from blame assignment and towards understanding.

Tunajifunza kutokana na makosa tuliyoyafanya baada ya kukili makosa tuliyofanya.

Tunapoanza kulaumu watu wengine kwa makosa yetu tunakuwa tunajiondoa kwenye funzo ambalo lingetuwezesha kupiga hatua mbele.

Rais Magufuli amekuwa muwazi kuhusu madudu ya serikali na makosa yaliyofanyika ndani ya serikali ya CCM.

Kuyakubali makosa ambayo yamelifanya taifa kuwa tegemezi kimaendeleo kunamfanya Rais Magufuli apate fursa na uwanja wa kushughulikia tatizo.

Wahenga walisema mficha maradhi kifo kitamuumbua.

Kwa kuficha uozo wa serikali kwa muda mrefu, taifa lilikuwa linaelekea kufa!

Kwa kusema nchi yetu ni masikini wakati ni tajiri, taifa lilikuwa linadumaa kifikra huku wachache wakinufaika na utajiri wa Taifa!
Mwenyekiti wa CCM aombe msamaha kwa makosa yote. Akishindwa Rais Magufuli aombe watanzania msamaha kwa niaba ya chama chake. Hapo ndipo tutakapoanza upya. Bila ya hivyo ni maigizo tu! Maana hayo yote anayoyalalamikia yamesababishwa na serikali za CCM, ambazo naye kwa miaka 20 alikuwa sehemu ya serikali hizo. Na sijamsikia akiomba radhi.
 
MsemajiUkweli Tumemsikia mara nyingi na maneno hayo hayo(whining)
Tunataka atoke atuambie LUGUMI kilitokea nini.

Hili la Lugumi wote wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.
Tunahitaji kusikia nini kimetokea?

Nchi haiendeshwi hivyo wewe, suala lipo mikononi mwa kamati ya Bunge wewe unataka Magu afanye nini? Muda mwingine ni vyema ukajielimisha kuhusu mambo ya unayoyapenda kuzungumzia yana taratibu zipi. Kwani hili la Lugumi wewe ulilipataje au limeibuliwaje? Ukiwa na ashki ya kukosoa tu ipo siku utamkosoa mpaka Mungu kwa jinsia aliyokupa.
 
Kwani mkataba si upo? Kitu gani kinachosumbua kuotoa! Kwanini ichukue siku tatu kutoa karatasi kabatini? Nini kinaogopwa hapa

Hatuhitaji unafiki, tunataka ukweli. Leo tunaambiwa hakuna muda wa kusubiri kutokana na kasi, halafu tunasikia kamati ya bunge hadi itoe siku 3 kutoa karatasi kabatini

LUGUMI itatueleza mengi kuhusu ukweli wa serikali hii!

Yaani kutoa karatasi kabatini inachukua siku 3! ubabaishaji huu utaisha lini

Wahusika wamekaa kimyaa! Lipo neon LUGUMI.

Wananchi tunataka kujua kutoa mkataba kwanini imekuwa nongwa? Nini kinafichwa na serikali ya awamu ya tano? Nini hasa kinafichwa kuhusu LUGUMI?

Kamati yenyewe ya Bunge ilikosea, haikufuata taratibu kuomba mkataba, Mwenyekiti alifanyia kazi mazoea kwa kuwakilisha mahitaji yake kwa mdomo kama vile anashughulikia suala la mboga na mkewe nyumbani kwake
 
Kuna mahali nakubaliana na JPM 100%, ingawa kwenye baadhi ya maeneo nakuwa siko naye. Kwa mfano, bado naamini Tanzania inahitaji misaada. Kujiamini kwamba tunaweza sisi wenyewe bila misaada ni jambo zuri, lakini hatuoni kwamba tungekwenda haraka zaidi kimaendeleo kama tungepata pia misaada? Na tena ninaamini, misaada wakati huu ambao tunajivuna kuwa na rais anayesimamia vizuri raslimali za nchi, ingekuwa na manufaa mkubwa zaidi katika kuharakisha maendeleo ya nchi. Lakini tunaponyimwa misaada baada ya kufanya mambo ya "hovyo hovyo" hatupaswi kuweka utetezi wa "hatuzitaki mbichi hizi" bali viongozi wetu waangalie na kutathimini mambo wanayoyafanya na athari zake.
 
Hapana hapa mnataka kuhamisha goli
Wewe ndio unataka kuhamisha goli kwa sababu mada iliyopo haihusu LUGUMI ila wewe umeleta hoja ya LUGUMI ili kuhamisha mjadala wa hotuba ya Rais Magufuli.

1. Hakuna suala la separation of power kwasababu kamati ya bunge inahitaji kuona mkataba kutoka jeshi la Polisi.

Katika kufanikisha 'team work' Serikali inatakiwa itoe vielelezo kupitia jeshi la Polisi
Ni suala la Rais kuagiza 'toeni vielelezo' kwa kamati, siyo kuingilia kazi za mhimili mwingine hapo.
Officially Public Accounts Committee wameliomba Jeshi la Polisi lakini kinachoshangaza unaingiza ofisi ya Rais.

Kwa maana nyingine unataka kutuambia kuwa PAC hawafahamu kazi yao.

2. Kama ni separation of power iweje wabunge wa CCM walalamike kuhusu Rais kufanya matumizi bila kuidhinishwa na bunge yakiwa si dharura?
Matumizi yapi?

Kwa hiyo hukubaliani na wabunge wa CCM wanaolalamika?

3. Rais aliagiza hazina itoe pesa mara moja kwenda mahakamani.
Agizo lile kama unakumbuka lilikuwa na 'walakini' kimantiki.
Separation of power iko wapi

Hapa hili si suala la separation of power, kinachoendelea ni kutaka kukwepa ukweli na kubabaisha kama ilivyokuwa kwa Escrow.
Sisi tunaongea utawala wa Awamu ya Tano, wewe bado unaleta ngonjera za utawala wa Awamu ya nne. Husikii kama Rais Magufuli anakwambia kuna madudu yalikuwa yanafanyika serikalini?

Kwa hiyo kama serikali ya Awamu ya Nne ilifanya madudu, basi na Rais Magufuli ayaendeleze? Wewe vipi?

LUGUMI ipo meza kuu, kukaa kimya au kukimbilia Ruangwa hakutoi picha nzuri. Watuambie LUGUMI ni nini? Wananchi wamechanganyikiwa kuhusu nini kinaendelea LUGUMI. Kilitokea nini kiasi kwamba jeshi la Polisi halijui mkataba upo wapi

Jeshi laPolisi lenye dhamana haijui mkataba upo wapi.

Mheshimiwa tusaidie kujua nini kimetokea LUGUMI
Umejuaje kama LUGUMI iko meza kuu? Haya ndio matatizo ya kujenga hoja kwa kutumia hisia.

Umejuaje kama wananchi wamechanganyikiwa? Sema wewe ndio umechanganyikiwa kwa suala ambalo hujataka kujielimisha ili ufahamu kinachoendelea kati ya PAC na Polisi.
 
Kamati yenyewe ya Bunge ilikosea, haikufuata taratibu kuomba mkataba, Mwenyekiti alifanyia kazi mazoea kwa kuwakilisha mahitaji yake kwa mdomo kama vile anashughulikia suala la mboga na mkewe nyumbani kwake

Mkuu, wewe unatetea nini hapa? hebu declare interest yako. Maana unasema "Kamati yenyewe... " kama vile kile kinachofanywa na kamati ni kitu kisichokuwa na maslahi kwa nchi yetu.
 
Pamoja na nia nzuri ya Magufuli kwa taifa hili bado amezungukwa na watu wenye tamaa za mali kias cha kutisha, watu hao wanampamba kwenye social media na newsroom, lakin ukwel ni kwamba hawamsaidii
Wanapinga kila kinachozungumzwa dhidi yake,
wapinzani wanakosoa kumuongezea kas, bila kukosolewa hatafika kokote.
Ukwel ni kuwa bado kazi ngumu hajaianza..NSSF, Lugumi, ni chache sana, bado viporo vya mkwere..akianza hivyo nitamuombea na missa kabisa......

Your Excellency watch your boys hapo kwa whitehouse .......
Yes, ninakubaliana na wewe.

Hata Rais Magufuli anafahamu hivyo ndio maana amesema kuna baadhi ya wafanyakazi serikalini bado hawajabadili mentality zao. Bado wanadhani ni business as usual.
 
Wabongo tunatabu sana, issue ya Lugumi inashughulikiwa tena kwa kasi sana jana tumejuzwa bunge kutoa siku tatu kwa wahusika kutoa docs wewe leo unasema kila mtu yuko kimnya. Ni kweli wanaposema huwezi kumridhisha kila mtu.
Mbaya zaidi anataka Rais aingilie kati na Rais akaingilia kati atakuja hapa na kusema, Rais anaingilia madaraka ya muhimili mwingine wa dola au anafanya kazi za Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Huyo huyo utamsikia tena akisema, Rais anapenda one man show!
 
Mkuu, wewe unatetea nini hapa? hebu declare interest yako. Maana unasema "Kamati yenyewe... "

Hiyo ya kusema 'kama vile kile kinachofanywa na kamati ni kitu kisichokuwa na maslahi kwa nchi yetu' ni tafsiri yako. Ninachosema polisi kupiga chenga kutoa mkataba kumechangiwa na kamati nayo kutokuwa makini, badala ya kufuata taratibu zinazotakiwa ikafanya mazoea mpaka imetuchelewesha kupata ukweli na pengine kutoa nafasi kwa watu kufanya 'michezo'. Hata kama kamati inafanya jambo zuri lakini isipofuata taratibu zinatakikana haiki 'immune' na kukosolewa. Nilikuwa na respond kwamtu ambaye anamkosoa Rais eti hafanyi kitu kuhusu Lugumi kwa vile polisi haikutoa mkataba wa kamati at the first place.Ilikuwa ni suala la muktadha!
 
Rais naye awe mzalendo kwa kuonyesha mshahara wake na marupurupu, na pia kuonyesha analipa kodi kiasi gani. Siyo anasema uzalenda kwa wengine tu. Lazima awe mfano.
Kwa hiyo wewe sio mzalando kwa sababu hujaonyesha mshahara wako?

Nani alikuambia kuwa mzalendo ni lazima uonyeshe mshahara wako?

Ni wapi Rais amewataka wananchi/wafanyakazi waonyeshe mishahara yao ili wawe wazalendo?

Hisia zako usifanye ziwe kama sheria au utaratibu!
Akimaliza hilo, awe mzalendo pia katika kushiriki kubana matumizi kwa kupunguza mshahara na marupurupu yake. Apige mnada hizo BMWs na Benzs zilizo kwenye fleet yake; kisha aanze kuendeshwa kwenye Suzuki Vitara ama Rav4.
Cha kushangaza unadai Rais aonyeshe mshahara wake halafu kumbe unaofahamu!

Huwezi kusema Rais apunguze mshahara wake kama huufahamu, otherwise unajenga hoja kwa kutumia hisia zako kitu ambacho ni kosa kimantiki katika nguvu za hoja.

Kwa sababu wewe unaofahamu mshahara wa Rais niambie, unataka apunguze kiasi gani?

Kwenye masuala ya ulinzi, Rais hana mamlaka katika kuamua gari gani atumie kwenye msafara wake.

Kitengo kinachohusika na ulinzi wa Rais ndicho huamua ni dhana gani zitumike katika kurahisisha kazi zao za kumlinda Rais. Aina ya gari anayotumia Rais na walinzi wake ni moja ya dhana/vifaa vinavyorahisisha kazi ya ulinzi wa Rais.
Zoezi liende sehemu zote serikalini; apige marufuku matumizi ya magari ya design ya Land Cruisers. Kisha atoe agizo la kuanzishwa ama kutekelezwa kwa mfumo wa government car pool, ambapo viongozi waandamizi watakuwa wakikodi magari kutoka kwenye pool na kuyatumia pale panapouhitaji tu.
Government car pool na Serikali iwe inakodi magari ya kutumia?

Unaleta nadharia kwenye uhalisia!

Unashangaza kweli!
 
Huu mchezo hauitaji hasira mkuu .... Wewe lini umeona zuri la serikali ya Magufuli?

Wewe kizuri ni kinachotoka kwa chadema na friends of Lowassa tu.
Halafu mbaya zaidi anashika bango kwenye serikali ya Rais Magufuli kama vile mkataba uliingiwa na Serikali ya awamu ya Tano.

Kuna baadhi ya watu wanashangaza kweli.
 
Rais naye awe mzalendo kwa kuonyesha mshahara wake na marupurupu, na pia kuonyesha analipa kodi kiasi gani. Siyo anasema uzalenda kwa wengine tu. Lazima awe mfano.
Akimaliza hilo, awe mzalendo pia katika kushiriki kubana matumizi kwa kupunguza mshahara na marupurupu yake. Apige mnada hizo BMWs na Benzs zilizo kwenye fleet yake; kisha aanze kuendeshwa kwenye Suzuki Vitara ama Rav4. Zoezi liende sehemu zote serikalini; apige marufuku matumizi ya magari ya design ya Land Cruisers. Kisha atoe agizo la kuanzishwa ama kutekelezwa kwa mfumo wa government car pool, ambapo viongozi waandamizi watakuwa wakikodi magari kutoka kwenye pool na kuyatumia pale panapouhitaji tu.
Bila kusahau aigize utaratibu wa mawaziri na viongozi wengine waandamizi (wakurugenzi, mameneja n.k.) kuwa wanajiendesha wenyewe, siyo lazima waendeshwe.
Mmhh huyu atakuwa mtoto wa sekondari tena O level, childish way of presenting ideas.
 
Mmhh huyu atakuwa mtoto wa sekondari tena O level, childish way of presenting ideas.
Sawa mzee. Mimi ndiyo kwanza nimemaliza darasa la saba. Sekondari hata bado sijafika. Darasa la saba lenyewe nimemaliza kimagumashi. Lakini asante kwa elimu bure nina uhakika wa kwenda kukua zaidi katika shule yetu ya Kata hapa Kibakwe.
 
Back
Top Bottom