Rais Magufuli: Wanaotunyima misaada muwaonee huruma

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Wakati akiongea baada ya kupokea hundi ya shilingi bilioni sita kutoka kwa Katibu wa Bunge la Tanzania kwa ajili ya kununulia madawati, Rais Magufuli amewaomba watanzania wasishangilie pale nchi inaponyimwa misaada bali wawaombee kwa Mwenyezi Mungu wale wanaotunyima misaada kwa sababu Tanzania itapiga hatua mbele na serikali imejipanga kuhakikisha nchi inasonga mbele kwa haraka.

Rais amewaomba waandishi wa habari wawe wazalendo kwa taifa lao na waisaidie serikali katika juhudi zake za kuleta maendeleo ya haraka na pia wawe tayari kukosoa na kuelimisha katika mlengo wa kujenga Taifa na sio kubomoa Taifa.

''Niwaombe waandishi muwe wazalendo kwa Tanzania yetu kwa sababu na ninyi pia mnapata shida za kimaisha’’ Rais alisema.

''Kuna watu wachache walizoea vihela vya hovyo hovyo na ninaamini wanachukia tunapochukua hatua kali. Tuwaache wachukie ili tuivushe Tanzania yetu mahali pazuri kwa faida yawatanzania wote na tusipochukua hatua kali tutakuwa hatuna uhalali wa kuitwa viongozi. Nia ya serikali yangu ni kuhudumia wananchi wote na siyo wachache’’ alisema.

Aliendelea kusema, ''Ni aibu kwa Rais kwenda kila mahali nchini na kukuta wananchi wake wanalia kwa sababu ya shida wanazozipata katika maisha yao wakati kuna watu wachache nchini wanafanya mambo ya hovyo’’. Ni lazima viongozi tujenge tabia ya kuwajibishana na tusipowajibishana hatuwezi kuivusha Tanzania yetu mahali pazuri''.

Alimalizia kwa kusema, ''Nia ya serikali yenu ni nzuri kwa faida ya Tanzania yetu’’

VIDEO:

NOTE:
Baada ya maneno ya Rais Magufuli, kwa sasa Marekani wameufyata na kusema wataendelea kutoa misaada kwa Tanzania baada ya kugundua Masikini Jeuri, Rais Magufuli hatikisiki wakati huo huo wana hatari ya kupoteza mengi kuliko kupata kutokana na msimamo wao wa kuondoa misaada.
 
Wise people admit their mistakes easily. They know progress accelerates when they admit their mistake.

Admission of a mistake makes learning possible by moving the focus away from blame assignment and towards understanding.

Tunajifunza kutokana na makosa tuliyoyafanya baada ya kukili makosa tuliyofanya.

Tunapoanza kulaumu watu wengine kwa makosa yetu tunakuwa tunajiondoa kwenye funzo ambalo lingetuwezesha kupiga hatua mbele.

Rais Magufuli amekuwa muwazi kuhusu madudu ya serikali na makosa yaliyofanyika ndani ya serikali ya CCM.

Kuyakubali makosa ambayo yamelifanya taifa kuwa tegemezi kimaendeleo kunamfanya Rais Magufuli apate fursa na uwanja wa kushughulikia tatizo.

Wahenga walisema mficha maradhi kifo kitamuumbua.

Kwa kuficha uozo wa serikali kwa muda mrefu, taifa lilikuwa linaelekea kufa!

Kwa kusema nchi yetu ni masikini wakati ni tajiri, taifa lilikuwa linadumaa kifikra huku wachache wakinufaika na utajiri wa Taifa!

Kwa kusema nchi yetu haiwezi kuendelea bila kutegemea misaada wakati ni nchi tajiri ni kuendeleza inferiority complex ambayo imepandikizwa na mabeberu ili tuendelee kudumaa kifikra wakati wao wakipiga hatua zaidi za kimaendeleo.
 
MsemajiUkweli Tumemsikia mara nyingi na maneno hayo hayo(whining)
Tunataka atoke atuambie LUGUMI kilitokea nini.

Hili la Lugumi wote wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.
Tunahitaji kusikia nini kimetokea?
Mambo yanafanyiwa kazi taratibu. Vyombo husika vinafanya kazi zao. Kama kuna tatizo wahusika watachukuliwa hatua.
 
MKuu, mimi nadhani tatizo lako unataka kusikia yanayokupendeza ndani ya roho na nafsi yako.

Unaposema mmesikia mara nyingi una maana wewe na nani mmesikia? Jisemee nafsi yako kuwa wewe ndio umechoka kwa sababu ni kosa kimantiki/kihoja kuwaweka wananchi wote katika mwanvuli wa fikra zako.

Kuhusu mambo ya LUGUMI, unatakiwa utafute wahusika ambao ni Bunge au unataka Rais aingilie kazi za watu ili upate hoja za kusema Rais Magufuli hafahamu dhana ya separations of power kama ilivyoainishwa katika andiko la spirit of the Laws.

Kwa kukusaidia zaidi kuhusiana na LUGUMI, angalia hii video;
 
...."ni aibu kwa Rais wa nchi kwenda mahali na kukuta wananchi wake wanalia shida..."-Magufuli.
....."urais sio kazi ndogo,unapita mabarabarani huko,unaona wananchi wana maisha magumu,unawaangalia,unajua huu ni mzigo wangu"-Mwalimu Nyerere.
 
...mkuu si ndio kamati ya Bunge jana wameandika barua kwa jeshi la polisi, baada ya zile siku saba za mwanzo kupita bila majibu,jana wamepewa siku tatu kwenye hiyo barua,wawe wametolea ufafanuzi hayo mambo,hebu tusubiri tuone kitakachotokea,subira yavuta kheri.
 
Shukrani kwa kuleta andiko linalofanana katika ujumbe kwa wananchi.
 
MsemajiUkweli Tumemsikia mara nyingi na maneno hayo hayo(whining)
Tunataka atoke atuambie LUGUMI kilitokea nini.

Hili la Lugumi wote wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.
Tunahitaji kusikia nini kimetokea?
Sasa unahitaji kusikia kwa nani mbona umeshasikia tayali unataka kusikia tena.
 
Sasa unahitaji kusikia kwa nani mbona umeshasikia tayali unataka kusikia tena.
Mimi nadhani huyo hataki kumsikia Rais Magufuli akisema atawashughulikia wezi na mafisadi.

Hao ni wale hawapendi mafanikio ya serikali ya Rais Magufuli.

Hao ni wale ambao kazi yao ni kutafuta udhaifu wa serikali ya Rais Magufuli na kuanza kujenga hoja za mfumo.

Hao ni wale wamekaa tayari kwa hamasa kubwa wakisubiri scandal ndani ya serikali ya Rais Magufuli ili waseme, TULISEMA.
 
...mkuu si ndio kamati ya Bunge jana wameandika barua kwa jeshi la polisi, baada ya zile siku saba za mwanzo kupita bila majibu,jana wamepewa siku tatu kwenye hiyo barua,wawe wametolea ufafanuzi hayo mambo,hebu tusubiri tuone kitakachotokea,subira yavuta kheri.
Mkuu jeshi la Polisi ni chombo anachosimamia. Kauli yake ilikuwa rahisi sana, 'toeni mkataba' kwa kamati ya bunge!

Hili la kusbiri kamati ya bunge ni kutaka kukwepa ukweli kwa kubabaisha. Unakumbuka ESCROW ilivyobabaishwa na akina Makinda? Mbona bandarini hakusbiri alikuwa na majina kupitia Maja!

Tusitwike kamati ya bunge mzigo. Aliposikia Kilango anadanganya akatuma tume mara moja
Mbona hili wana kigugumizi?
 
pia tuwaonee huruma ving'ang'anizi wa madaraka wasio aibu..
siku waking'olewa watapita barabara ipi ?
 
MKuu, mimi nadhani tatizo lako unataka kusikia yanayokupendeza ndani ya roho na nafsi yako.

Unaposema mmesikia mara nyingi una maana wewe na nani mmesikia? Jisemee nafsi yako kuwa wewe ndio umechoka kwa sababu ni kosa kimantiki/kihoja kuwaweka wananchi wote katika mwanvuli wa fikra zako.

Kuhusu mambo ya LUGUMI, unatakiwa utafute wahusika ambao ni Bunge au unataka Rais aingilie kazi za watu ili upate hoja za kusema Rais Magufuli hafahamu dhana ya separations of power kama ilivyoainishwa katika andiko la spirit of the Laws.

Kwa kukusaidia zaidi kuhusiana na LUGUMI, angalia hii video;
Hapana hapa mnataka kuhamisha goli

1. Hakuna suala la separation of power kwasababu kamati ya bunge inahitaji kuona mkataba kutoka jeshi la Polisi.

Katika kufanikisha 'team work' Serikali inatakiwa itoe vielelezo kupitia jeshi la Polisi
Ni suala la Rais kuagiza 'toeni vielelezo' kwa kamati, siyo kuingilia kazi za mhimili mwingine hapo.

2. Kama ni separation of power iweje wabunge wa CCM walalamike kuhusu Rais kufanya matumizi bila kuidhinishwa na bunge yakiwa si dharura?

3. Rais aliagiza hazina itoe pesa mara moja kwenda mahakamani.
Agizo lile kama unakumbuka lilikuwa na 'walakini' kimantiki.
Separation of power iko wapi

Hapa hili si suala la separation of power, kinachoendelea ni kutaka kukwepa ukweli na kubabaisha kama ilivyokuwa kwa Escrow.

LUGUMI ipo meza kuu, kukaa kimya au kukimbilia Ruangwa hakutoi picha nzuri. Watuambie LUGUMI ni nini? Wananchi wamechanganyikiwa kuhusu nini kinaendelea LUGUMI. Kilitokea nini kiasi kwamba jeshi la Polisi halijui mkataba upo wapi

Jeshi laPolisi lenye dhamana haijui mkataba upo wapi.

Mheshimiwa tusaidie kujua nini kimetokea LUGUMI
 
Pamoja na nia nzuri ya Magufuli kwa taifa hili bado amezungukwa na watu wenye tamaa za mali kias cha kutisha, watu hao wanampamba kwenye social media na newsroom, lakin ukwel ni kwamba hawamsaidii
Wanapinga kila kinachozungumzwa dhidi yake,
wapinzani wanakosoa kumuongezea kas, bila kukosolewa hatafika kokote.
Ukwel ni kuwa bado kazi ngumu hajaianza..NSSF, Lugumi, ni chache sana, bado viporo vya mkwere..akianza hivyo nitamuombea na missa kabisa......

Your Excellency watch your boys hapo kwa whitehouse .......
 
MsemajiUkweli Tumemsikia mara nyingi na maneno hayo hayo(whining)
Tunataka atoke atuambie LUGUMI kilitokea nini.

Hili la Lugumi wote wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.
Tunahitaji kusikia nini kimetokea?
Wabongo tunatabu sana, issue ya Lugumi inashughulikiwa tena kwa kasi sana jana tumejuzwa bunge kutoa siku tatu kwa wahusika kutoa docs wewe leo unasema kila mtu yuko kimnya. Ni kweli wanaposema huwezi kumridhisha kila mtu.
 
Mambo yanafanyiwa kazi taratibu. Vyombo husika vinafanya kazi zao. Kama kuna tatizo wahusika watachukuliwa hatua.
Bandarini hayakusbiri vyombo husika. TRA hayakusbiri vyombo husika. Anne Kilango hakusubiri vyombo husika, hili la LUGUMI kila mmoja analikimbia.

Hakuna suala la vyombo husika, kamati inataka kuona mkataba. Nini kinafichwa?
Mkataba upo sasa wanaogopa kuutoa kwa nini?

Na kwanini serikali isitoe amri aliyeficha huo mkataba autoe?

Nini kinafichwa, na nini kinaogopwa na watumbua majipu?

LUGUMI itaueleza umma mengi ! Tunahitaji kujua ni kitu gani kinafichwa na kwanini serikali inaogopa! Kuna nini hasa kinafichwa? Sasa hivi 'wanapika mkataba' kusetiriana

LUGUMI tunahitaji majibu, hatuhitaji ubabaishaji. Toeni mkataba vinginevyo wanaoficha mkataba majipu, wanaosita kushinikiza mkataba utoke majipu. Turudi tulikozoea

LUGUMI jamani!
 
Wabongo tunatabu sana, issue ya Lugumi inashughulikiwa tena kwa kasi sana jana tumejuzwa bunge kutoa siku tatu kwa wahusika kutoa docs wewe leo unasema kila mtu yuko kimnya. Ni kweli wanaposema huwezi kumridhisha kila mtu.
Kwani mkataba si upo? Kitu gani kinachosumbua kuotoa! Kwanini ichukue siku tatu kutoa karatasi kabatini? Nini kinaogopwa hapa

Hatuhitaji unafiki, tunataka ukweli. Leo tunaambiwa hakuna muda wa kusubiri kutokana na kasi, halafu tunasikia kamati ya bunge hadi itoe siku 3 kutoa karatasi kabatini

LUGUMI itatueleza mengi kuhusu ukweli wa serikali hii!

Yaani kutoa karatasi kabatini inachukua siku 3! ubabaishaji huu utaisha lini

Wahusika wamekaa kimyaa! Lipo neno LUGUMI.

Wananchi tunataka kujua kutoa mkataba kwanini imekuwa nongwa?

Nini kinafichwa na serikali ya awamu ya tano? Nini hasa kinafichwa kuhusu LUGUMI?
 
Back
Top Bottom