Rais Magufuli: Wanaotunyima misaada muwaonee huruma

PAC walikwendaje?
Hili ni swali lisislojibiwa. Kama kamati zinajulikana PAC walikwendaje?

Tulianza kusema jana, ficha ficha ya mkataba ilikuwa kutafuta namna ya kusetiri mkataba na wahusika. Sasa wamepata mahali pa kuwaficha Watanzania

LUGUMI imefikia mwisho, wameshalindwa mjadala wa LUGUMI uishie hapa

Mjadala unaotakiwa kuendelea ni , je, kuna tofauti ya uozo wa awamu ya nne na huu?
Tumbua majipu ina maana yoyote katika kulindana huku?

Wahusika watataka tuwaombee kwa mungu! kwa hili mungu gani atatusikiliza?

Je hatujafeli! Hatujafeli? Atoke mtu aseme kwanini Hatujafeli
Kwa hiyo unataka kusema unaimani na PAC kuliko Kamati ya Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama?

Wapinzani hawawezi hata kupinga lolote kuhusu maamuzi ya kupeleka mkataba kwenye Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwa sababu mwezi uliopita walituambia hawana imani na wajumbe PAC.

Hata wale wa upinzani waliopangwa walidai hawana uwezo na kwa sababu hiyo mpaka leo walikataa kuchagua Wenyeviti wa Kamati za PAC na LAAC kutoka kambi ya upinzani kama Kanuni za Bunge zinavyotaka kwa sababu waliamini hazina wajumbe kutoka kambi ya upinzani wenye uwezo.

Siasa za Tanzania zinafurahisha kweli!
 
Sina tatizo na kamati yoyote

Nina tatizo na mchezo uliochezwa.
PAC wamekwenda almost a week wakitafuta nyaraka
Ina maana walikuwa wanafanya kazi wakijua haiwahusu?

Ninatatizo majukumu yalivyohamishwa. Baada ya kufichwa kwa mkataba kwasababu zisizoingia akilini kwa mwanadamu mwenye kufikiri mkataba umepelekwa ulinzi na usalama

Maana yake ni simple, walikuwa anatafuta njia ima ya kuharibu nyaraka, ikashindikana, wakaona njia rahisi ni kupeleka kamati ya ulinzi na usalama ili waweze kuwafunga wabunge na wananchi midomo

Kamati ya ulinzi na usalama ikisema hilo ni jambo la usalama wa nchi nyaraka hazitoki

Hapo ndipo wataficha kila kitu, halafu wanatoka na kutuomba tuwaombea kwa mungu

Baada ya hapo tunarudi kule kule kwa miaka 10 iliyopita.

Ninyi mtashangaa sisi wengine hatushangai maana hawa wamekulia katika mfumo wa kifisadi, wanajua ABCD zote , wanajua kupumbaza umma na kulindana

Tunamashaka sana kama si wanufaika, ingawa tunaambiwa wafanyabiashara hawakuchangia. Hii ficha ficha imechafua. Tunaishi jana tuliyozoea

#HapaKulindana ufisadi ni utamaduni wetu. Wamechafuka tayari
 
Mkuu, mimi sifahamu kwa sababu sina uelewe mzuri kuhusu Kanuni za Bunge.

Nadhani Polisi iko chini ya Kamati ya Bunge inayoshughulika na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Mkuu hilo la polisi kuwa chini ya kamati ya nje,ulinzi na usalama nadhani sio sahihi. Hapa inajadiliwa ripoti ya CAG ambayo ndio imeibua madufu ya fedha huko polisi, jee kwa maana hiyo wizi ukigundulika TANAPA itabidi jambo hilo lipelekwe kamati ya maliasili? au ripoti ya wizi wa bandari ipelekwe kamati ya miundo mbinu?
Ninavyofahamu mimi hiyo kamati ya nje,ulinzi na usalama hizo ripoti za CAG haziwahusu hata kuzisoma nadhani hawazisomi maana ni nje ya majukumu yao
 
Mkuu, Kwa kweli siwezi kusema uko sahihi au hapana kwa sababu sifahamu kwa undani kilichokuwa kinaendelea na pia sifahamu majukumu ya PAC na Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika hii tenda ni yapi kwenye taasisi kama polisi.

Kinachoshangaza zaidi ni kuwa haya tunayojadili kwa sasa yamefanyika mwaka 2011.

Ndio maana nikasema ni vema tukasubiri findings otherwise, nitakuwa ninajadili jambo ambalo hisia zangu ndizo nitakuwa ninazijengea hoja.

Sipendi kujenga hoja kwa kutumia hisia.
 
Sina tatizo na kamati yoyote

Nina tatizo na mchezo uliochezwa.
PAC wamekwenda almost a week wakitafuta nyaraka
Ina maana walikuwa wanafanya kazi wakijua haiwahusu?

Ninatatizo majukumu yalivyohamishwa. Baada ya kufichwa kwa mkataba kwasababu zisizoingia akilini kwa mwanadamu mwenye kufikiri mkataba umepelekwa ulinzi na usalama

Maana yake ni simple, walikuwa anatafuta njia ima ya kuharibu nyaraka, ikashindikana, wakaona njia rahisi ni kupeleka kamati ya ulinzi na usalama ili waweze kuwafunga wabunge na wananchi midomo

Kamati ya ulinzi na usalama ikisema hilo ni jambo la usalama wa nchi nyaraka hazitoki

Hapo ndipo wataficha kila kitu, halafu wanatoka na kutuomba tuwaombea kwa mungu

Baada ya hapo tunarudi kule kule kwa miaka 10 iliyopita.

Ninyi mtashangaa sisi wengine hatushangai maana hawa wamekulia katika mfumo wa kifisadi, wanajua ABCD zote , wanajua kupumbaza umma na kulindana

Tunamashaka sana kama si wanufaika, ingawa tunaambiwa wafanyabiashara hawakuchangia. Hii ficha ficha imechafua. Tunaishi jana tuliyozoea

#HapaKulindana ufisadi ni utamaduni wetu. Wamechafuka tayari
Kama nilivyosema, una haki ya kuwa na wasiwasi kwa kile kinachoendelea kuhusiana na suala hili lakini wasi wasi wako usitumike kujenga hoja kwa kutumia hisia na kuzifanya kama ndio ukweli.

Mimi sifahamu kinachoendelea na kutokana na mabandiko yako, ninaamini pia hufahamu kinachoendelea.

Siwezi kuanza kutoa lawama kwa mtu au chombo ambacho sina ukweli wake.

Labda maswali ya kujiuliza, kama huu mradi umekuwepo toka mwaka 2011, Zitto na Kamati yake ya PAC walifanya nini kuhusiana na suala hili?

Je, hawakuliona wakati wanapitia mahesabu ya Polisi?

Je, inawezekana kweli Kamati ya PAC iliyokuwa inaongozwa na Zitto haikuwa na uwezo kikanuni kupitia vitabu vya idara ya Polisi na kwa sababu hiyo ndio maana kwa sasa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inashughulikia suala hili badala ya PAC?
 
Yes kwa asiye na hofu na hili atakuwa mgonjwa sana. Tuna sababu

1. PAC ya leo iliwezaje kwenda kufanya kazi bila muongozo wa uongozi wa bunge?

2. Hadi walipoomba nyaraka, kwanini hakutokea mtu kusahihisha makosa kama yapo?

3. Kwanini imechukua masiku kutoa mkataba kabatini?
Kwanini isielezwe kuwa PAC haihusiki bali ni mambo ya nje, ulinzi na usalama

4. Nne, kwanini kumekuwa na unyemela wa kuficha mkataba. Ukapelekwa ulinzi na usalama haraka sana huku PAC wakiwa wameomba wiki nzima

5. Kwanini watumbua majipu wapo kimyaa wengine wamekimbilia ''nyumbani''

Kwanini hili jambo linawekewa uzio tena kutoka ngazi za angani? Why

Hapa hakuna utetezi, lipo jambo linafichwa chini ya zulia. Ni utamaduni wetu na wanaotekeleza ni wale wale waliousimamia utamaduni huo ukastawi

Leo kweli tunazungumza ya jana! real ! tuliambiwa sasa basi! tumerudi kwenye tamaduni zetu for real! Tunaishi jana, tunatenda jana. Funika kombe!
 
Nimeuliza maswali ambayo hukunijibu!

Nauliza tena kama una jibu unisaidie ili niweze kupata mwanga kihoja.

Kama huu mradi umekuwepo toka mwaka 2011, Zitto na Kamati yake ya POAC/PAC walifanya nini kuhusiana na suala hili katika miaka mitano?

Je, hawakuliona wakati wanapitia mahesabu ya Polisi?

Je, inawezekana kweli Kamati ya PAC iliyokuwa inaongozwa na Zitto haikuwa na uwezo kikanuni kupitia vitabu vya idara ya Polisi na kwa sababu hiyo ndio maana kwa sasa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inashughulikia suala hili badala ya PAC?
 
Wewe kama Mtanzania unayejua hilo la Lugumi umefanya nini?na taifa hili umelifanyia nini isiwe kazi kuloloma tu wewe unaloloma hapa hujui nini kinaendelea ,sio kila kitu tupigiwe baragumu kuwa jamani eh sasa Nguruvi tunamsweka ndani sababu ya ufisadi au kaiba,kuna mambo ya uchunguzi n,k mambo ya uwizi na kisiasa ni tofauti,watu sijui kwanini bado hamuoni kazi inayofanywa na uongozi awamu ya tano,naona kama tuna upofu wa makusudi uliochagizwa na misimamo tofauti ya kisiasa.Hata akitoka na tamko la Lugumi bado hamturidhika mtarukia kwingine kisa mumeshakuwa na mawazo hasi kwenye utawala huu ,hata viongozi wafanye mema mengi hawatasifiwa hata siku moja bali Lema akitoa gari la wagonjwa au Kubenea akitoa milioni 2 inakuwa kama kipofu kaona mwezi hapa JF panakuwa hapatoshi. Penye kupongeza wacha tupongeza na penye kulaumu wacha tulaumu lakini tuwe fair chuki hazisaidii.
Kinachonishangaza kidogo ni kuwa, hili suala la LUGUMI limekuwepo tokea mwaka 2011.

Kuna maswali mengi kuhusiana na kuibuka kwake wakati huu.

Kuna uwezekano tukawa tunacheza ngoma za kisiasa zinazopigwa na watu wenye malengo yao bila sisi kufahamu.

Nimeanza kupata wasi wasi katika kuicheza hii ngoma!
 
Nimeuliza maswali ambayo hukunijibu!

Nauliza tena kama una jibu unisaidie ili niweze kupata mwanga kihoja.

Kama huu mradi umekuwepo toka mwaka 2011, Zitto na Kamati yake ya POAC/PAC walifanya nini kuhusiana na suala hili katika miaka mitano?

Je, hawakuliona wakati wanapitia mahesabu ya Polisi?

Je, inawezekana kweli Kamati ya PAC iliyokuwa inaongozwa na Zitto haikuwa na uwezo kikanuni kupitia vitabu vya idara ya Polisi na kwa sababu hiyo ndio maana kwa sasa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inashughulikia suala hili badala ya PAC?
Yes inawezekana hawakuwa na uwezo, sina uhakika na hilo.

Hata hivyo ukumbuke kuwa kamati zinabadilika ikiwa ni pamoja na majukumu.

Unafahamu PAC ya Zitto ilivyowahi kuvunjwa, majukumu yalivyobadilishwa
Suala la kamati ya Zitto, tujue majukumu yalikuwaje na mipaka yake

Ni makosa kutumia PAC ya Zitto kutaka kusafisha uchafu huu.

Huu uchafu upo katika awamu ya tano na unapaswa ushughulikiwe na awamu hi

kama Zitto alivyohangaika na Escrow wao walikuwa kimyaaaa! Hawana rekodi
In fact wengine walikuwa wanahamisha mafungu ya wizara kwa matakwa yao

Tukianza kumyooshea Zitto kidole tutafika pabaya kuliko hapa pa LUGUMI
Tutarudi nyuma kutafuta rekodi za Zitto, halafu tutatafuta zao pia.

Nadhani huko si mahali pa kwenda, tafadhali tuache maana tuna rekodi!Trust me

Nimekuuliza , hii PAC ilikwendaje kufanya ukaguzi ikiwa haina mwongozo wa Bunge?
Tunajua kamati hizi zinakwenda kwa idhini ya bunge

Mwenyekiti alisema mawasiliano hupitia bungeni, ilikuwaje ikafika hapo?
Hakuna kiongozi wa bunge aliyetoa mwongozo, wanajua ukweli upoje

Tatu hutaki kujibu, kulikuwa na sababu gani za kuficha mkataba ikiwa ilijulikana unatakiwa kamati ya ulinzi na usalama.

Kwanini wahusika wasiseme mkataba utakwenda wanakodhani ni sahihi

Nne, kwanini ilichukua malumbano kutoa mkataba tu wa karatasi huku Polisi wakitupiana mpira na wizara ya mambo ya ndani?

Je, kuna guideline ya nani afanye nini ?
Na kwa muktadha huo mradi ulisimamiwaje ikiwa hakuna mawasiliano ya Polisi Wizara

Hapa nikueleza jambo moja wakati unatafakari hoja zangu hapo juu

Mkataba umepelekwa ulinzi na usalama katika malengo haya kwa maoni yetu

1. Isemewe ni nyaraka nyeti kiusalama ,wananchi na bunge litafungwa midomo
Watafanya yao kadri wanavyotaka

2. Kule kuna mwenyekiti aliyekuwa DCI. Makorokoro yote yaliyowahi kufanyika nchi hii anayajua kama DCI, yalivyoanza na yalivyomalizwa . Umeelewa?
 
Kinachonishangaza kidogo ni kuwa, hili suala la LUGUMI limekuwepo tokea mwaka 2011.

Kuna maswali mengi kuhusiana na kuibuka kwake wakati huu.

Kuna uwezekano tukawa tunacheza ngoma za kisiasa zinazopigwa na watu wenye malengo yao bila sisi kufahamu.

Nimeanza kupata wasi wasi katika kuicheza hii ngoma!
Wala wengine hatukuwa na hisia zozote. Kilcihotushtua ni jitihada za kuficha mkataba.

Tunaambiwa mkataba uliotoa pesa hazina haujulikani upo wapi.
Eti kuutoa kabatini ni tatizo. Hapo ndipo hofu ikaanza kutuingia maana ukishaona serikali inasita sita tena majina makubwa yakiwa katika orodha wengine wakikanusha , lipo neno

Wasi wasi ni ukimya wa wahusika, wametulia tuli kana kwamba hakuna wanachokijua

Wasi wasi umefikia kikomo pale mbinu za kamati za bunge zinapoingia

Tunaambiwa eti ni jukukumu la kamati ya ulinzi na usalama.
Hatuambiwi PAC ilikoseaje njia kwenda huko.

Uongozi wa bunge upo kimyaa, kamati zake zinasigishana! kulikoni?

Hapa lipo jambo! ukishaona wamekaa kimya au wanakimbia lipo neon

Lugumi ni mauza uza gani
 
Kama nilivyosema, una haki ya kuwa na wasiwasi kwa kile kinachoendelea kuhusiana na suala hili lakini wasi wasi wako usitumike kujenga hoja kwa kutumia hisia na kuzifanya kama ndio ukweli.

Mimi sifahamu kinachoendelea na kutokana na mabandiko yako, ninaamini pia hufahamu kinachoendelea.

Siwezi kuanza kutoa lawama kwa mtu au chombo ambacho sina ukweli wake.

Labda maswali ya kujiuliza, kama huu mradi umekuwepo toka mwaka 2011, Zitto na Kamati yake ya PAC walifanya nini kuhusiana na suala hili?

Je, hawakuliona wakati wanapitia mahesabu ya Polisi?

Je, inawezekana kweli Kamati ya PAC iliyokuwa inaongozwa na Zitto haikuwa na uwezo kikanuni kupitia vitabu vya idara ya Polisi na kwa sababu hiyo ndio maana kwa sasa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inashughulikia suala hili badala ya PAC?
Hapo kuhusu Zitto na kamati yake unapoilaumu unapotoka kabisa. PAC kwa kawaida haikagui vitabu Bali inapitia ripoti ya CAG na kuhoji Yale ambayo hayakupatikana majibu.
Kwanza kwa utaratibu ni kuwa CAG huwa ana raise Audit querry kwa Accounting officer husika katika jambo alilokagua na kutoridhika nalo. Kisha majibu yanapotoka asipo ridhika ana re-issue Audit querry kuonyesha wapi ana mashaka napo. Hivyo ukiona jambo limefika kuingia katika ripoti yake ya mwaka ujue hajaridhika na majibu na hapo PAC ndipo inaingia kazini baada ya ripoti kusomwa na rais kwanza.
Kwa hiyo yaweza kuwa mkataba ni wa 2011 lakini CAG kahoji katika ripoti inayofanyiwa kazi sasa ambayo ni wazi ilipita kwenye mikono ya rais JK na akadharau kama kawaida yake
 
Taratibu watu watatuelewa tunapoongelea mfumo tuna maana gani. Ni ajabu watu waliokuwa mstari wa mbele kumtetea Kikwete kwa kila kitu kama Ritz, FaizaFoxy na wengineo wanavyolazimika kumtetea Magufuli kwa kila kitu. Jibu ni kwamba hawamtetei mtu wanatetea mfumo, na wanatetea mfumo kwa sababu wanafaidika nao, period.

Unajitekenya mwenyewe unajichekesha mwenyewe!
 
Inasemekana LUGUMI kaenda nje ya nchi kununua vifaa ili wamalize kazi kwa supersonic speed and put Lugumi Gate to closure!
 
Hili suala la LUGUMI filimbi zimekuwa ni nyingi sana kiasi kwamba, hata ukweli kwa sasa haujulikani.

Kilicho cha muhimu ni kufahamu kama amevunja mkataba au la.

Ni hatari sana kuanza kuhadili hoja kwa kutumia msingi wa hisia.
 
Ndio maana sisi wengine tulihoji sana, kwanini mkataba unafichwa? Sasa unaposema tujadili mkataba uliofichwa sijui unatueleza nini

Maktaba haujulikani nani ameuhifadhi, na aliyeomba mkataba hakupewa, katafutwa mtu 'mwema' kapewa bila mombi

Uongozi wa bunge kimyaa kamati zinasigishana

Uongozi wetu ndio kabisaaa wamekimbia wengine wapo makwao. Lugumi imewakikimbiza Dar

Hakuna utata, ila upo utata wa kutengenezwa ili waendelee kubabaisha. Kuna tatizo katika hili jambo na serikali inasita sita na kujenga hisia. Kwanini mkataba uwe siri wakati malipo yameshanyika? Kuna nini kinafichwa?
 
Inasemekana LUGUMI kaenda nje ya nchi kununua vifaa ili wamalize kazi kwa supersonic speed and put Lugumi Gate to closure!
Suala lipo kwa miaka 5 kwa mujibu wa MsemajiUkweli ukweli. Kutakuwa na maswali kuhusu malipo yalivyofanyika kupitia bajeti 5. Kwamba yalikuwa contnous au yalikuwajes? Na kwanini auhusiwe kufanya hivyo? Kampuni inamilikiwa na nani? Mkataba ulisemaje wakati wanasaini?

Bado LUGUMI imenata, itaonyesha uadilifu au unafiki na wataishi na kimoja kati ya hivyo
 
Hili suala la LUGUMI filimbi zimekuwa ni nyingi sana kiasi kwamba, hata ukweli kwa sasa haujulikani.

Kilicho cha muhimu ni kufahamu kama amevunja mkataba au la.

Ni hatari sana kuanza kuhadili hoja kwa kutumia msingi wa hisia.
Awali tulisema hatua ya wahusika kuutoa mkataba husika kutoka PAC kwenda kamati ya ulinzi na usalama ililenga nini - kugeuza suala husika kuwa ni la siri na sio la media/public kama ilivyo kwa kazi za kamati nyingine.

Baadae tukaeleza kwamba tusipoteza muda kumlaumu IGP au Katibu Mkuu mambo ya ndani kwa suala linalomhusu bosi wake (Waziri) ambae mamlaka ya uteuzi haijatoa tamko au kutengua uteuzi wake.

Sasa taarifa iliyopo na ambayo baadhi ya waandishi wa habari wameanza kuipokea ni kwamba:

Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.

Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.

Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.

Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Hakika Jina lako ni tamu sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom