Rais Magufuli: Wanaotunyima misaada muwaonee huruma

Inasemekana yupo ofisini kwake usiku huu pale ATC house. Mazingaombwe ya ccm yanaendelea.

Hivi ni dharau kwa Rais au ni shule ndogo? Tafakari kauli yake hii kwenye ukurasa wake wa facebook:

"Sio kila JIPU ni la kutumbua. Hata MTUMBUA MAJIPU ANAJUA".

This is a classic headline for a major newspaper...
 
Mkuu, ni nani kaandika hivyo?
 
Yaani habari za kwenye facebook account fake unazileta hapa kwenye jukwaa la heshima!

Jamani hata kama ni kutaka kusikia kile unapenda kukisikia, hii ni zaidi ya hivyo!

Hata kwa akili yenye common sense huwezi kuamini kama hizi habari zako niza kweli.
 
Inawezekana ni fake account, asante kwa ufafanuzi. Lakini kufuatia taarifa zake za kusafiri nje ya nchi tofauti na hali ya kawaida ambapo pasi yake ya kusafiria ilibidi ishikiliwe na serikali hii makini, hatimaye amerudi baada ya inavyoonekana - kwenda kuweka mambo sawa. Taarifa zilizopo na za kuaminika ni kwamba Jana usiku alikuwa ofisini kwake ATC house kwa masaa ya kutosha.

Tumeona taarifa ya Bunge kwamba kamati ya PAC haikuhitaji mkataba per se Bali maelezo ya utekelezaji wa mradi husika. Hii ni ishara kwamba hakuna mkataba na badala yake mambo yaliendeshwa kwa vimemo na simu.

Naomba utusaidie ufafanuzi juu ya haya yafuatayo:

Maelezo ya utekelezaji yanawezekana kupatikana vipi bila ya uwepo wa mkataba?

Kwanini ofisi ya Bunge haikukanusha kauli ya PAC kwamba inahitaji mkataba?

Kwanini Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Balozi Adadi Rajabu alikiri kupokea mkataba?

Kwanini IGP mangu alisema aliyesaini mkataba husika ni Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya Ndani?

Kwanini nyinyi kama watetezi wake mmekuwa mkisema kwamba mkataba husika ni halali?

Sent from my SM-G530H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nguruvi hakuna mkataba labda kama unataka mkataba wa mdomo kwa mdomo 🙂🙂 kama upo basi uliandikwa kwa pencil na hawa wahuni wameuchukua kwenda kuuandika vizuri kwa kutumia wino.

1. Je, zabuni ya hii kazi ambapo iliamuliwa apewe Lugumi ilitangazwa lini katika magazeti yepi nchini na makampuni mangapi yaliomba kupewa hii zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37. Nani aliyeidhinisha malipo ya shilingi 37 billion?

2. Nani waliokuwemo katika hiyo kamati ya kupitia zabuni zote zilizowakilishwa kwao kabla ya kuamua kwamba mshindi ni Lugumi?

3. Nani katika polisi au wizara ya mambo ya ndani alikuwa ni mfuatiliaji kuhakikisha kazi inafanyika kwa ukamilifu? Kama utakumbuka jamaa alifanya kazi ya asilimia 12 tu kwa kufunga mashine hizo katika vituo 14 tu nchi nzima kati ya vituo 108 vya polisi. Cha kushangaza na kusikitisha tangu 2011 hakuna aliyestukia kwa miaka mitano kwamba kazi iliyofanywa ni 12% mpaka juzi hili sakata lilipobumburuka ndiyo watu wanastuka na njemba inapanda ndege eti kwenda kununua mitambo mingine ili kuja kumalizia kazi ya kufunga mashine hizo katika vituo 94 au sawa na asilimia 88 ya kazi kwa speed ya "supersonic"

4. Nani aliyeamua malipo ya 99% yafanyike kabla ya kuhakikisha hata 50% ya kazi imekamilika?

5. Je, hivyo vituo 14 ambavyo mashine zimefungwa mashine hizo zinafanya kazi vile inavyotakiwa? Mashine hizo ni mpya au zilikuwa ni mitumba? Nani alihakikisha hili?

6. Bei ya kufunga hizo mashine kila kituo kwa shilingi 342,592,592 ni ya haki nani anaweza kutathmini hili? Hii kazi ya kufunga hizi mashine katika vituo 108 nchi nzima isingeweza kufanyika kwa shilingi milioni 500 au tuseme bilioni?

Wahuni wameshafanya yao kwa mara nyingine tena na kwa sababu hawa ni watu wazito sana nchini hawawezi kuguswa maana wakiguswa nchi yetu inaweza kupotezwa katika uso wa dunia ndiyo maana unaona kuna juhudi kubwa sana za kutupia mpira vyombo vya habari ili vionekane vilikurupuka kuandika hii habari. Acha mtumbua majipu amwambie Pengo kwamba kama angelijua Urais ni hivi kamwe asingechukua form kama alivyoshinikizwa na fisadi Mkapa.

Ndiyo bongo yetu hiyo itatafunwa na wajanja wachache AKA WAHUNI. HAPA KAZI TU! amua wewe kama ni ya kuondoa umaskini kwa Watanzania au kukingia vifua wahuni, mafisadi, wapokea rushwa na mazagazaga mengine yote ndani ya chama cha wenye majipu.

Uwe na weekend njema Mkuu.

Hili la LUGUMI wala halina tabu kabisa, serikali itoe mkataba! Mkataba upo kabatini, kuutoa inachukua mbinde za barua na siku 3 !!! Kuna nini kinaogopwa hapa! Katika muda huo mkataba 'unafanyiwa ukarabati' kuficha ukweli. Kwanini mkataba uliopo na uliotumika kutoa mabilioni iwe nongwa kutolewa kwa kamati ya bunge?

Yale yale ya escrow, wanataka kubabaisha ili kupitia kamati takwimu zifanyiwe ukarabati
Wmejifungia mahali, siku 3 wanakuja na kitu majina ya wahusika ni kama yale ya Dowans

Wanajua mbinu mana wameishi katika hilo, wameona namna ya kuficha ukweli

Wote wamekimbia !!! LUGUMI nzito jamani ! Fupa lile si jipu! Lugumi wakubwa!

Msikimbie ukweli, siku 3 kutoa karatasi kabatini! halafu mnatuambia Tanzania ya neema!
 
Inawezekana ni fake account, asante kwa ufafanuzi. Lakini kufuatia taarifa zake za kusafiri nje ya nchi tofauti na hali ya kawaida ambapo pasi yake ya kusafiria ilibidi ishikiliwe na serikali hii makini, hatimaye amerudi baada ya inavyoonekana - kwenda kuweka mambo sawa. Taarifa zilizopo na za kuaminika ni kwamba Jana usiku alikuwa ofisini kwake ATC house kwa masaa ya kutosha.

Tumeona taarifa ya Bunge kwamba kamati ya PAC haikuhitaji mkataba per se Bali maelezo ya utekelezaji wa mradi husika. Hii ni ishara kwamba hakuna mkataba na badala yake mambo yaliendeshwa kwa vimemo na simu.

Naomba utusaidie ufafanuzi juu ya haya yafuatayo:

Maelezo ya utekelezaji yanawezekana kupatikana vipi bila ya uwepo wa mkataba?

Kwanini ofisi ya Bunge haikukanusha kauli ya PAC kwamba inahitaji mkataba?

Kwanini Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Balozi Adadi Rajabu alikiri kupokea mkataba?

Kwanini IGP mangu alisema aliyesaini mkataba husika ni Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya Ndani?

Kwanini nyinyi kama watetezi wake mmekuwa mkisema kwamba mkataba husika ni halali?

Sent from my SM-G530H using JamiiForums mobile app
Huu utakua mtihani mgumu kwa mh. Raisi iwapo haya mlioandika ni kweli
 
Inawezekana ni fake account, asante kwa ufafanuzi. Lakini kufuatia taarifa zake za kusafiri nje ya nchi tofauti na hali ya kawaida ambapo pasi yake ya kusafiria ilibidi ishikiliwe na serikali hii makini, hatimaye amerudi baada ya inavyoonekana - kwenda kuweka mambo sawa.
Hizi taarifa za kusafiri kwenda nje au possport yake kushikiliwa na serikali unazitoa wapi?

Naomba unipatie chanzo cha madai yako ili tujenge hoja kwa kutumia msingi wa ukweli au reliable source na sio hisia au fikra zako.

Taarifa zilizopo na za kuaminika ni kwamba Jana usiku alikuwa ofisini kwake ATC house kwa masaa ya kutosha.
Una maana gani unaposema taarifa za kuaminika?

Taarifa ya kuaminika kwa nani au kutoka kwa nani?
Tumeona taarifa ya Bunge kwamba kamati ya PAC haikuhitaji mkataba per se Bali maelezo ya utekelezaji wa mradi husika. Hii ni ishara kwamba hakuna mkataba na badala yake mambo yaliendeshwa kwa vimemo na simu.
Not necessarily labda kama una uhakika na hiki unachokisema.

Mimi huwa sipendi kujenga hoja kwa kutumia hisia kwa sababu mara nyingi hisia hupotosha hoja.

Kama nilivyosema, filimbi nyingi zimesababisha kushindwa kuelewa yupi anayesema ukweli.

Naomba utusaidie ufafanuzi juu ya haya yafuatayo:

Maelezo ya utekelezaji yanawezekana kupatikana vipi bila ya uwepo wa mkataba?
Kwani kama unadhani mkataba haupo, wamewezaje kufanya kazi bila mkataba?

Kwani hawawezi kutumia maelezo yaleyale yaliyotumika bila mkataba?

Kwa upande wa pili, maelezo ya kina yaliyoombwa na PAC yanaweza kuambatana na mkataba kama kielelezo.

Kwanini ofisi ya Bunge haikukanusha kauli ya PAC kwamba inahitaji mkataba?
Una maana gani unaposema haikukanusha wakati imekanusha.

Kwanini Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Balozi Adadi Rajabu alikiri kupokea mkataba?
Umejuaje kama alikiri? Naomba tamko lake au video ya tamko lake.

Kumbuka kila gazeti linakuja na story zake kinzani kuhusiana na suala hili.

Kwanini IGP mangu alisema aliyesaini mkataba husika ni Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya Ndani?
Alisema lini na wapi?

Nisaidie kunielewesha!
Kwanini nyinyi kama watetezi wake mmekuwa mkisema kwamba mkataba husika ni halali?

Sent from my SM-G530H using JamiiForums mobile app
Unaposema sisi watetezi wake una maana gani?

Haya ni maoni yangu na sishirikishi mtu yeyote katika fikra zangu.

Mimi sio mtetezi wa mtu bali mtetezi wa fikra na mtazamo wangu.

Kama LUGUMI na genge lake wamefanya utapeli lazima wawajibishwe kisheria lakini tutakuwa tunafanya makosa kuanza kutoa hukumu bila kupata ukweli wa suala hili.

Kwani wewe ni mtetezi wa nani?
 
*Kampuni ya Marekani yahusishwa katika sakata lake

*Infosys, Bunge watoa kauli

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SAKATA la ufisadi kuhusu mkataba kati ya Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd na Jeshi la Polisi nchini sasa limechukua sura mpya huku moja ya kampuni kubwa ya Marekani ikitajwa.

Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na utata kuhusu mkataba huo ambapo sasa Kampuni ya Biometrica LLC ya Marekani ikihusishwa na sakata hilo.

Inaelezwa mwaka 2011, Kampuni hiyo ya Kimarekani iliwasilishwa na Kampuni ya Teknolojia ya Infosys IPS Tanzania Limited, ambapo waliingia nayo mkataba wa kufunga baadhi ya mashine hizo za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi nchini.

Baada ya kukamilika kwa kazi hiyo bado haijatajwa ni vituo vingapi Infosys Tanzania Limited ilifunga mashine hiyo.

Akizungumzia mkataba huo, Naibu Meneja Mkuu wa Infosys, Sweki Donald, alisema wakati wote wakiwa wanaendelea na kazi hawajawahi kushirikiana na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

“Mwaka 2011 tulipata kazi ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi na kazi hii sisi tuliipata kupitia Kampuni ya Biometrica LLC ya nchini Marekani ambao wao walisema wamepata taarifa zetu kupitia Kampuni ya Dell ya Marekani.

“Tulifanyakazi yetu kwa mujibu wa mkataba na baada ya kumaliza tulilipwa Dola 74, 420 (sawa na shilingi 162,849,565), ila ninapenda kusema kuwa wakati wote hatukujua kama kuna mtu anaitwa Lugumi.

“Tumekuja kujua baadaye sana hivyo ninapenda kusema hapa kuwa hatuhusiki na Lugumi na wala hatumjui,” alisema Sweki wakati wa mahojiano na mwandishi aliyejitambulisha wa Focus Media.

Naibu Meneja huyo alipoulizwa kuhusu ushiriki wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, alisema waziri huyo alikuwa ni mmoja wa waasisi wa kampuni hiyo ingawa aliondoka tangu mwaka 2010.

“Charles Kitwanga ni mmoja wa founder wa Infosys Tanzania Limited, tangu mwaka 2010 aliondoka katika kampuni na amekuwa hana mawasiliano,” alisema Sweki.

Alisema wao kama Infosys Tanzania Limited, hawahusiki na kashfa ya ufisadi huo unaoripotiwa sasa.

Katika kile kinachoonekana ni filamu hasa baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kutoa siku tatu kwa kampuni hiyo kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kufunga mashine za utambuzi wa alama za vidole katika vituo 108 nchini, sakata hilo limekuwa likichukua sura mpya kila kukicha.

Uamuzi huo uliibua hisia miongoni mwa jamii ambapo katika kipindi cha siku mbili baada ya PAC kutaka ripoti hiyo, Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, iliingilia kati ambapo mwenyekiti wake Balozi Adadi Rajabu, alikiri kupokea mkataba huo.

CC: nguruvi, Chakaza, Salary Slip, Mag3 asigwa

Hali hiyo ilizua sintofahamu miongoni mwa wajumbe wa Kamati za Bunge huku baadhi yao wakihofu hatua hiyo huenda ikawa ni mkakati wa kuficha ukweli dhidi ya vigogo waliotajwa katika mkataba huo tata wa Sh bilioni 37.

Kauli ya Bunge

Pamoja na jana kuwa ni siku ambayo ilitarajiwa kampuni hiyo ingewasilisha, hatimaye jana Ofisi ya Bunge kupitia Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, ilieleza kuwa taarifa hiyo itawasilishwa Aprili 18, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba tangu lilipoibuliwa sakata hilo na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Aprili 5, mwaka huu baada ya Jeshi la Polisi kutakiwa kuwasilisha mkataba ulioingiwa kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System), kumekuwa na taarifa ambazo si sahihi.

“Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba, Aprili 5 mwaka huu, kamati hiyo ilikutana na kujadili taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi la Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine ilibaini dosari katika utekelezaji wa mkataba huo.

“Kutokana na dosari hizo, kamati iliomba Ofisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua.

“Kutokana na agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo Aprili 12 mwaka huu, ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Ofisa Masuhuli. Aidha, Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani Aprili 12 mwaka huu kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha Aprili 5 mwaka huu kabla ya Aprili 18 mwaka huu kama ilivyoshauriwa na kamati,” ilieleza taarifa hiyo.

Sarakasi zaidi

Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd inadaiwa kupewa tenda na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 vya polisi pekee na tayari kampuni hiyo imelipwa Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha za mkataba.

Kamati ya PAC ambayo ilibaini kuwapo viashiria vya ufisadi katika zabuni, iliwaagiza watendaji wa jeshi hilo kuwasilisha taarifa za mkataba huo, lakini mkataba huo ulihamishwa na kupelekwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Lugumi ambaye anatajwa kuwa na uhusiano wa kifamilia na baadhi ya vigogo nchini, aliingia mkataba tata na Jeshi la Polisi mwaka 2011 kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi, lakini kazi hiyo haikufanyika kwa ufanisi licha ya kulipwa mabilioni ya fedha.

Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili kuwa mfanyabiashara huyo amekwenda nje kununua mashine zilizosalia kama njia ya kuzima mjadala kuhusu utata wa mkataba huo ambao unaelezwa kumhusisha kigogo mmoja katika Serikali ya Rais Dk. John Magufuli.

Utata

Katika sakata hilo inadaiwa kuwa Kampuni ya Lugumi Enterprises ilipewa zabuni ya kufunga mashine za ‘Biometric Access’ kwa ajili ya kuchukua alama za vidole ikiwa haina uzoefu wa kazi hiyo.

“Wamepewa mkataba sawa, lakini mbona taarifa zinaonyesha kuwa kampuni hii haijasajiliwa kama Biometric Access Company na haijawahi kufanya kazi zozote zinazohusiana na Biometric Access Control?” alihoji mmoja wa wataalamu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
 
Mkuu, BAK nashukuru kunishitua lakini kwanini hili bandiko lako usilufungulie uzi unaojitegemea?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama kampuni husika iliyofunga mashine zile inasema ililipwa Dola 74, 420 (sawa na shilingi 162,849,565), na hawamjui Lugumi, Je, Lugumi aliingiaje kwenye huu mkataba? Na malipo ya shilingi 37 billion sawa na tofauti ya shilingi bilioni 36.837 kwanini yalifanywa ikiwa malipo halisi yalikuwa ni hayo hapo juu?
 
Ni wazo zuri Mkuu, na mimi hili bandiko sikuliweka kwenye uzi huu nashangaa limehamishiwa kwenye uzi huu. Haya ndiyo baadhi ya mambo yanayoudhi hapa jamvini. Ukiangalia bandiko hili halihusiani lolote na huu uzi, huu uzi unahusu Lugumi lakini kuna MOD kaamua kuuhamisha nilikouweka na kuliweka bandiko hili hapa.

Mkuu, BAK nashukuru kunishitua lakini kwanini hili bandiko lako usilufungulie uzi unaojitegemea?
 
Hilo kampuni la kimarekani ambalo limehusishwa kwenye sakata la lugumi linaitwaje???
 
... wawaombee kwa Mwenyezi Mungu wale wanaotunyima misaada kwa sababu Tanzania itapiga hatua mbele na serikali imejipanga kuhakikisha nchi inasonga mbele kwa haraka

Hata mugabe, chaves, ayatolah wa iran, kim ill, ... baada ya kunyimwa misaada na kutengwa nao walijinadi kwamba serikali zao zimejipanga vizuri ... lakini kila mtu anajua kilichotokea.
 
*Kampuni ya Marekani yahusishwa katika sakata lake

*Infosys, Bunge watoa kauli

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SAKATA la ufisadi kuhusu mkataba kati ya Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd na Jeshi la Polisi nchini sasa limechukua sura mpya huku moja ya kampuni kubwa ya Marekani ikitajwa.

Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na utata kuhusu mkataba huo ambapo sasa Kampuni ya Biometrica LLC ya Marekani ikihusishwa na sakata hilo.

Inaelezwa mwaka 2011, Kampuni hiyo ya Kimarekani iliwasilishwa na Kampuni ya Teknolojia ya Infosys IPS Tanzania Limited, ambapo waliingia nayo mkataba wa kufunga baadhi ya mashine hizo za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi nchini.

Baada ya kukamilika kwa kazi hiyo bado haijatajwa ni vituo vingapi Infosys Tanzania Limited ilifunga mashine hiyo.

Akizungumzia mkataba huo, Naibu Meneja Mkuu wa Infosys, Sweki Donald, alisema wakati wote wakiwa wanaendelea na kazi hawajawahi kushirikiana na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

“Mwaka 2011 tulipata kazi ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi na kazi hii sisi tuliipata kupitia Kampuni ya Biometrica LLC ya nchini Marekani ambao wao walisema wamepata taarifa zetu kupitia Kampuni ya Dell ya Marekani.

“Tulifanyakazi yetu kwa mujibu wa mkataba na baada ya kumaliza tulilipwa Dola 74, 420 (sawa na shilingi 162,849,565), ila ninapenda kusema kuwa wakati wote hatukujua kama kuna mtu anaitwa Lugumi.

“Tumekuja kujua baadaye sana hivyo ninapenda kusema hapa kuwa hatuhusiki na Lugumi na wala hatumjui,” alisema Sweki wakati wa mahojiano na mwandishi aliyejitambulisha wa Focus Media.

Naibu Meneja huyo alipoulizwa kuhusu ushiriki wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, alisema waziri huyo alikuwa ni mmoja wa waasisi wa kampuni hiyo ingawa aliondoka tangu mwaka 2010.

“Charles Kitwanga ni mmoja wa founder wa Infosys Tanzania Limited, tangu mwaka 2010 aliondoka katika kampuni na amekuwa hana mawasiliano,” alisema Sweki.

Alisema wao kama Infosys Tanzania Limited, hawahusiki na kashfa ya ufisadi huo unaoripotiwa sasa.

Katika kile kinachoonekana ni filamu hasa baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kutoa siku tatu kwa kampuni hiyo kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi wa kufunga mashine za utambuzi wa alama za vidole katika vituo 108 nchini, sakata hilo limekuwa likichukua sura mpya kila kukicha.

Uamuzi huo uliibua hisia miongoni mwa jamii ambapo katika kipindi cha siku mbili baada ya PAC kutaka ripoti hiyo, Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, iliingilia kati ambapo mwenyekiti wake Balozi Adadi Rajabu, alikiri kupokea mkataba huo.

CC: nguruvi, Chakaza, Salary Slip, Mag3 asigwa

Hali hiyo ilizua sintofahamu miongoni mwa wajumbe wa Kamati za Bunge huku baadhi yao wakihofu hatua hiyo huenda ikawa ni mkakati wa kuficha ukweli dhidi ya vigogo waliotajwa katika mkataba huo tata wa Sh bilioni 37.

Kauli ya Bunge

Pamoja na jana kuwa ni siku ambayo ilitarajiwa kampuni hiyo ingewasilisha, hatimaye jana Ofisi ya Bunge kupitia Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, ilieleza kuwa taarifa hiyo itawasilishwa Aprili 18, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba tangu lilipoibuliwa sakata hilo na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Aprili 5, mwaka huu baada ya Jeshi la Polisi kutakiwa kuwasilisha mkataba ulioingiwa kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System), kumekuwa na taarifa ambazo si sahihi.

“Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba, Aprili 5 mwaka huu, kamati hiyo ilikutana na kujadili taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi la Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine ilibaini dosari katika utekelezaji wa mkataba huo.

“Kutokana na dosari hizo, kamati iliomba Ofisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua.

“Kutokana na agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo Aprili 12 mwaka huu, ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Ofisa Masuhuli. Aidha, Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani Aprili 12 mwaka huu kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha Aprili 5 mwaka huu kabla ya Aprili 18 mwaka huu kama ilivyoshauriwa na kamati,” ilieleza taarifa hiyo.

Sarakasi zaidi

Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd inadaiwa kupewa tenda na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 vya polisi pekee na tayari kampuni hiyo imelipwa Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha za mkataba.

Kamati ya PAC ambayo ilibaini kuwapo viashiria vya ufisadi katika zabuni, iliwaagiza watendaji wa jeshi hilo kuwasilisha taarifa za mkataba huo, lakini mkataba huo ulihamishwa na kupelekwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Lugumi ambaye anatajwa kuwa na uhusiano wa kifamilia na baadhi ya vigogo nchini, aliingia mkataba tata na Jeshi la Polisi mwaka 2011 kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi, lakini kazi hiyo haikufanyika kwa ufanisi licha ya kulipwa mabilioni ya fedha.

Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili kuwa mfanyabiashara huyo amekwenda nje kununua mashine zilizosalia kama njia ya kuzima mjadala kuhusu utata wa mkataba huo ambao unaelezwa kumhusisha kigogo mmoja katika Serikali ya Rais Dk. John Magufuli.

Utata

Katika sakata hilo inadaiwa kuwa Kampuni ya Lugumi Enterprises ilipewa zabuni ya kufunga mashine za ‘Biometric Access’ kwa ajili ya kuchukua alama za vidole ikiwa haina uzoefu wa kazi hiyo.

“Wamepewa mkataba sawa, lakini mbona taarifa zinaonyesha kuwa kampuni hii haijasajiliwa kama Biometric Access Company na haijawahi kufanya kazi zozote zinazohusiana na Biometric Access Control?” alihoji mmoja wa wataalamu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Hii ngoma ukiifukua vizuri unaweza kukuta ina mikono yote miwili ya magogoni.
Mukulu wa Kwanza anaweza kuwa mkono wa kushoto wa magogoni kupitia Lugumi, na Mukulu aliyepo anaweza kuwa mkono wa kulia wa Magogoni kupitia Kitwanga kwa njia ya InfoSys.

Naona kuna sarakasi sasa ya kujaribu kumtenganisha Kitwanga na InfoSys kwa kigezo kuwa ni founder lakini hahusiki nayo, hata kama hahusiki, vipi kama hisa zake bado zimo?? na kwa kuwa hisa zimo gawiwo la faida linaingia kwenye account daily??
 
Ni wazo zuri Mkuu, na mimi hili bandiko sikuliweka kwenye uzi huu nashangaa limehamishiwa kwenye uzi huu. Haya ndiyo baadhi ya mambo yanayoudhi hapa jamvini. Ukiangalia bandiko hili halihusiani lolote na huu uzi, huu uzi unahusu Lugumi lakini kuna MOD kaamua kuuhamisha nilikouweka na kuliweka bandiko hili hapa.
Kuna kila dalili mods wameanza kufichaficha mambo kuhusu hili saga!Binafsi siwaelewi!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Juhudi zao kubwa Mkuu ni kuhakikisha wahusika wanalindwa kwa kila hali ili kuuficha ufisadi mkubwa uliofanyika hapa. Kama tunavyoona kampuni husika iliyofunga mashine zile imesema ililipwa shilingi milioni 162 tu, sasa haya malipo zaidi ya shilingi bilioni 36.8 ni ya nini? Kuna yeyote ndani ya polisi au wizara ya mambo ya ndani ambaye anaweza kutupa Watanzania maelezo ya kina kuhusu malipo hayo!? Na hii kampuni wanasema hawamjui Lugumi, je, huyu Lugumi hizi bilioni 37 alizolipwa ni za nini? Kuna yeyote anayeweza kutupa maelezo ya kina kwa kupitia documents husika ikiwemo mkataba ili Watanzania tujue sababu za Lugumi kulipwa pesa nyingi kiasi hicho!? Wameshaumbuka hawa Mkuu.

Kuna kila dalili mods wameanza kufichaficha mambo kuhusu hili saga!Binafsi siwaelewi!
 
Visa vya vijana na Bamkwe/shemeji - Namkumbuka kijana mmoja aliyeitwa Albert Marwa alivyopenyeza kwa Bamkwe Rais Kikwete. Na Saidi Lugumi akasema sikubali, naye akapenyeza kwa shemeji yake Kikwete, Bamkwe Afande Said Mwema. Sasa shauri liko mikononi mwa shemeji yake Said Mwema, Adadi Rajabu, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia mambo ya Ulinzi na Usalama, mambo yasiyoruhusiwa kujadiliwa hadharani...kichwa kinazunguka!

Kama shauri lenyewe lilianzia kwa Info Systems (T) Ltd, lilihamaje na kuwa mikononi mwa Lugumi Enterprises? Na kama Sweki Donald hamjui Saidi Lugumi, huo mkataba unaofichwafichwa ulikuwa kati ya nani na nani?
 
Back
Top Bottom