Wewe kama Mtanzania unayejua hilo la Lugumi umefanya nini?na taifa hili umelifanyia nini isiwe kazi kuloloma tu wewe unaloloma hapa hujui nini kinaendelea ,sio kila kitu tupigiwe baragumu kuwa jamani eh sasa Nguruvi tunamsweka ndani sababu ya ufisadi au kaiba,kuna mambo ya uchunguzi n,k mambo ya uwizi na kisiasa ni tofauti,watu sijui kwanini bado hamuoni kazi inayofanywa na uongozi awamu ya tano,naona kama tuna upofu wa makusudi uliochagizwa na misimamo tofauti ya kisiasa.Hata akitoka na tamko la Lugumi bado hamturidhika mtarukia kwingine kisa mumeshakuwa na mawazo hasi kwenye utawala huu ,hata viongozi wafanye mema mengi hawatasifiwa hata siku moja bali Lema akitoa gari la wagonjwa au Kubenea akitoa milioni 2 inakuwa kama kipofu kaona mwezi hapa JF panakuwa hapatoshi. Penye kupongeza wacha tupongeza na penye kulaumu wacha tulaumu lakini tuwe fair chuki hazisaidii.
Hapana ndugu yangu, kama umenisoma vema utabaini tunachukizwa na ufisadi pengine kuliko siku 3 za kutoa karatasi kabatini.
Ni lazima tuwe wakweli wa nafsi zetu ili kuijenga Tanzania. Hatujengi nchi kwa nyimbo na mapambio kufurahisha umma.
Tumeshangilia miaka nenda rudi tupo pale pale.
Ni wakati wa kuwa na fikra mbadala, za ukubwa wa tatizo na approach
Tunakubali bila kificho ufisadi, wizi, ulaghai imekuwa sehemu ya utamaduni wetu.
Hatukubaliani na approach, si kwasababu zinazofanyika ni mbaya bali si sustainable
Huwezi kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule na watu wale wale ukapata matokeo tofauti. Hadithi za uchunguzi ni za CCM na serikali zake.
Leo hatujui EPA, KAGODA na uchafu mwingine umeishia wapi
Tuliambiwa uchunguzi wa Twiga waliochukua pipa pale KIA unaendelea.
Kwasababu sisi ni mazezeta tukashangilia, wajanja wakaja na mbinu, Tumbili sasa ni KLM.
Hatujiulizi inakuwaje!! uchunguzi ulisaidia nini nani alifanya nini.
Tunasubiri jipu liive tutumbue, mengine yana meya tunafurahia tiba isiyo na majibu
Tumeona watendaji wakisimamishwa kupisha uchunguzi.
Hizo ni hatua za awali kabisa za kupata nani amehusika na kwa njia gani.
Hili la LUGUMI linajulikana, uchunguzi hakukufanyika hadi kamati ya bunge ilipoingia
Kamati haipati ushirikiano, nyaraka zilizotumika hazina kuchota mabilioni sasa ni 'clssified'
Huu ni udanganyifu ili tuendelee kuamini uchunguzi, wao wakifanya yao
Hakuna mwenye uwezo na mkuu wa Polisi, katibu mkuu, waziri na wateule wengine isipokuwa viongozi wa juu ya hapo.
Wewe na mimi si sehemu ya lolote au chochote lakini hata kuuliza ni dhalili kwetu?
Tukifika hapo tunawauliza, mbona wamekaa kimyaa! mbona wanakimbia?
Zile mbinu za majina ya mkaontena zimeishia wapi? Kigugumizi cha nini kwa hili la LUGUMI? Mbona mzigo wa jipu anatupiwa ''daktari kamati ya bunge''
Wenzetu manataka kusikia habari njema hata kama si njema.
Kuna mauza uza,ni rahisi kutoa glass ya kunywea maji kabatini kuliko karatasi za mkataba
Hatuna wa kumuuliza isipokuwa yule aliyeapa kulinda watu na mali zao.
Pesa za umma ni zetu, hatujui zilitoka kwa namna gani , uhalali au haramu.
Ndio maana tunauliza wako wapi wahusika kwa hili? Mbona kimyaaa! kulikoni?