Rais Magufuli: Polisi kamateni hata gari la Rais

Happy Nation kuna mkono wa Said ..............ma. Ila Bufalo ilikuwa kampuni ya Mpare fulan sijajua kama kuna wakubwa waliingiza mikono yao huko.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Thanks.

Ninaamini comment yako itasaidia wengi katika uelewa pamoja na kwamba huna uhakika kuhusu Buffalo.
Kuna uzi hapa jf uliongelea kwa undani juu ya happy nation na huyu bwana. Sikuwahi kutegemea kabisa aisee na hasa ukiunganisha na hili swala ya sare za polisi hewa, ni wazi katika watz milioni 50 waaminifu huenda wasizidi elfu tano!
 
Vigogo wengi wastaafu na waliopo kazini wamejiingiza sana kwenye biashara ya Mabasi kwa kupitia migongo ya makampuni yaliyokuwepo zaman. Ndio maana kuna magar hayakamatwi kabisa hata yakifanya makosa,.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Wakati akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema kipindi cha nyuma jeshi la polisi lilikuwa linaweka historia mbaya.

Kuna baadhi ya polisi waliowahi kuumizwa siku za nyuma kutokana na kusimamia sheria. Kuna magari au mabasi ya wakubwa ndani ya polisi ambayo ilikuwa ukiyakamata unapata msukosuko.

Rais akatolea mfano akisema kulikuwa na mabasi yanayoitwa Buffalo, Happy Nation au Happy Tanzania ambayo ukiyagusa lazima utaondolewa kwenye cheo ulichopo.

Rais akawaomba Makamishna kwenda kufanya kazi bila woga na wahakikishe pia hawawabughudhi Maaskari walio chini yao wakati wanatimiza majukumu yao ndani ya sheria na Kanuni za utumishi wao.

‘’Hata kama askari atakamata gari la IGP, RPC, Waziri au Rais, mwacheni atimize majukumu yake ili wahusika wa hayo magari wakajieleze wenyewe mbele ya sheria. Sheria ni msumeno’’. Rais alisema.

Rais aliendelea kusema, ‘’tunawanyima nguvu hawa Maaskari wa chini wanapotimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria halafu tunawaambia liachie hilo gari. Akishatoka pale yule aliyekuwa amekamatwa huanza kutamba kweli kweli huku askari akiwa amevunjika moyo na nguvu katika kusimamia sheria. Niwaombe sana, Vyeo vyetu tuweke pembeni na sheria tuziweke pembeni’’.

Its a nice presidency lakini sikuzote watu hatulingani......mfano polisi anaanzaje sasa kulikamata gari la mtoto wa rais tu........achilia mbali rais mwenyewe.. ni ukweli pia
 
NINAZIDI KUPATA WASIWASI MKUBWA SANA NA MASHAKA KILA SIKU ZINAVYOZIDI KWENDA NA KAULI TATA ZINAZOTOLEWA NA KIONGOZI MKUU WA NCHI.
SIJUI NINI HATMA YA KAULI HIZI NA MATOKEO YAKE, MIMI YANGU MACHO NA MASIKIO HADI MWISHO.
 
Ni kweli huyo mkubwa anayemiliki hilo basi hafurahii akisikia gari limepiga mzinga kisa mwendo kasi, hafurahii akisikia trafik kapigwa makofi kisa basi limezidisha abiria.
 
Wakubwa wasipokuwa na miradi sisi watoto wa mjomba na shangazi tutaishije? Akituajiri mnasema ooh undugunizasheni, mara watoto wa vigogo wamejazana, wakitufungulia miradi nako shida oooh ile sheli ya rizimoja mara basi lile la ngunguri, au mnataka mjomba ale pekeyake na wanae? Ila mkumbuke huyo mkubwa babangu ndie aliyemsomesha.
 
Hivi katika msafara wa rais unamkamata nani? Yule eskota wa pikipiki au lile gari la ffu lililotangulia au ile ya rais yenyewe?
 
Wakati akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema kipindi cha nyuma jeshi la polisi lilikuwa linaweka historia mbaya.

Kuna baadhi ya polisi waliowahi kuumizwa siku za nyuma kutokana na kusimamia sheria. Kuna magari au mabasi ya wakubwa ndani ya polisi ambayo ilikuwa ukiyakamata unapata msukosuko.

Rais akatolea mfano akisema kulikuwa na mabasi yanayoitwa Buffalo, Happy Nation au Happy Tanzania ambayo ukiyagusa lazima utaondolewa kwenye cheo ulichopo.

Rais akawaomba Makamishna kwenda kufanya kazi bila woga na wahakikishe pia hawawabughudhi Maaskari walio chini yao wakati wanatimiza majukumu yao ndani ya sheria na Kanuni za utumishi wao.

‘’Hata kama askari atakamata gari la IGP, RPC, Waziri au Rais, mwacheni atimize majukumu yake ili wahusika wa hayo magari wakajieleze wenyewe mbele ya sheria. Sheria ni msumeno’’. Rais alisema.

Rais aliendelea kusema, ‘’tunawanyima nguvu hawa Maaskari wa chini wanapotimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria halafu tunawaambia liachie hilo gari. Akishatoka pale yule aliyekuwa amekamatwa huanza kutamba kweli kweli huku askari akiwa amevunjika moyo na nguvu katika kusimamia sheria. Niwaombe sana, Vyeo vyetu tuweke pembeni na sheria tuziweke pembeni’’.

umesahau na pale aliposema rushwa ya buku 5 ni pesa ya kubrashia viatu. ongezea na kipande hiki ili stori yako inoge zaidi
 
Sikurudisha kadi wakati wa dhiki na shida na foleni za chakula kila kukicha, ntarudisha leo? Mimi ni CCM wa asili, toka haijaundwa CCM nilikuwa TANU na wazee wangu walikuwa AA kabla ya TAA na Taa kabla ya TANU, mimi ni zao la Al Jamiatul Islamiya fi Tanganyika, hunitowi CCM.

Hiyo kauli ya CUF ndicho anachomaanisha Rais. Simply put.

Upinzani ulianzishwa ili kuwe na wigo na fikra pana na si kila la upinzani ni baya, halikadhalika kwa chama tawala.
Faiza wewe ni fundi na unajua sana kuchagua sehemu za kupenyeza ngumi zako.
Naipenda sana misimamo yako.
 
umesahau na pale aliposema rushwa ya buku 5 ni pesa ya kubrashia viatu. ongezea na kipande hiki ili stori yako inoge zaidi
Kachukue rushwa halafu useme hii ni pesa ya kubrashia viatu ambayo Rais alisema.

Tatizo lako unasumbuliwa na ufahamu wa tamathali za semi.
 
hizo tamathali unapaswa kumfundisha mtu wako aliyetamka hayo maneno. si miye!
 
Back
Top Bottom