Rais Magufuli nisikilize kwa makini, Sitaki upoteze muda bure

Ulianza kutafakari ukiwa mtoto, kama sikosei 16 yrs ukiwa Sekondari!!

Ndo maana unaandika mada ndeefu kama unafundisha watoto wenzako. Hayo mambo waachie wachumi wabobezi. Unatupotezea muda aisee
 
Ulianza kutafakari ukiwa mtoto, kama sikosei 16 yrs ukiwa Sekondari!!

Ndo maana unaandika mada ndeefu kama unafundisha watoto wenzako. Hayo mambo waachie wachumi wabobezi. Unatupotezea muda aisee

Mtu mbobevu hawezi shindwa kusoma makala fupi kama hii isiyo na maneno hata elfu kumi.

Watoto ningeweza waandikia aya mbili tuu zingewatosha
 
Wewe unaijui historia gani sasa, badala ya kunijibu kuwa Israeli imejengwa na nani au china, Rusia,
Dermak na Norway zimejengwa na nani unakuja kuleta maswali hapa.

Wewe ni kama umeandika gazeti tu hapa ila hujui nini unacho omba, eti uzi wa kikubwa wakati ulikiri kuwa wewe ni mtoto sasa tunakuelimisha namna ya kuwalisha hoja zako ili ziwe namantiki unakuja kubisha hapa unatuletea fikra za kitumwa hapa, sisi tunataka tujenge taifa la watu wanao jiamini unatuletea ushauri tegemezi hapa, inamaana katika elimu yako ulicho ambulia ni kuandika fasihi tu na sio uwezo wa kupambanua mambo. Ni aibu kwa mtu kama wewe kuandika uzi wa kutaka wageni waje kufanya kazi wakati inafahamika kuna wageni kibao wapo wanafanya kazi katika taasisi mbalimbali hapa nchini, hii inaonesha ni kaasi gani hauko familiar ni miradi mbalimbali inayoendelea hapa nchini.

Sipo hapa kukufundisha, niliowaandikia wanajua nini nimelenga na wanaelewa naongelea nini.

Huko juu nimeshaeleza kuwa China ilishavamia nchi kama Vietnam, Burma, Mongolia, Taiwan n.k. Unajua maana ya kuvamia na kutawala?
Hiyo Russia pengine huijui ndio hiyo iliyokuwa inaitwa USSR, pengine hujui kilichoifanya iingie katika vita ya kwanza na ya pili ya Dunia, unafikiri vita hivyo sababu kuu ilikuwa ni nini kama sio maslahi ya kiuchumi katika kutawala makoloni mengine?

Najua hujui kuwa kabla ya vita ya pili ya dunia, Taifa la japan ndilo lilikuwa linaongoza kwa masuala ya uvuvi, lakini baada ya vita ya pili kuisha najua hujui kilichopelekea taifa hilo kushuka katika nafasi hiyo, na nafasi hiyo kushikiliwa na hiyo nchi ya Norway, hata hivyo sina uhakika kama unajua wakazi wa Norway na Denmark asili yao ni jamii zipi.

Kuhusu hiyo Miradi inayoendelea ndani ya nchi labda wewe ndio huijui, au pengine unahadithiwa tuu na kuiona kwenye luninga, mimi mpaka kuishuhudia nimeishuhudia. Kuanzia huo mradi wa umeme katika bonde la Rufiji, vituo vyote vipya vya mabasi mikoani, kuanzia Hiko cha mbezi Luis, Igumbilo, Dodoma, kituo cha mabasi cha kibaha, kituo cha mabasi Mpanda, kituo cha mabasi Singida n.k

Mradi wa SGR kILa mtu kaushuhudia hasa wakazi wa Dsm, Pwani na morogoro. Usafiri wa anga, ukarabati wa terminal 3 na ndege mpya tena kupanda nimeshazipanda, sijui unataka nielewe kwa namna gani hiyo miradi.

Miradi inafanya vizuri lakini ushauri wangu naona kwako hauna maana kwa sababu sio mtu husika, wahusika wanajua nazunguzia nini.

Kuhusu Historia naomba uachane napo maana huko utajitia aibu
 
Sipo hapa kukufundisha, niliowaandikia wanajua nini nimelenga na wanaelewa naongelea nini.

Huko juu nimeshaeleza kuwa China ilishavamia nchi kama Vietnam, Burma, Mongolia, Taiwan n.k. Unajua maana ya kuvamia na kutawala?
Hiyo Russia pengine huijui ndio hiyo iliyokuwa inaitwa USSR, pengine hujui kilichoifanya iingie katika vita ya kwanza na ya pili ya Dunia, unafikiri vita hivyo sababu kuu ilikuwa ni nini kama sio maslahi ya kiuchumi katika kutawala makoloni mengine?

Najua hujui kuwa kabla ya vita ya pili ya dunia, Taifa la japan ndilo lilikuwa linaongoza kwa masuala ya uvuvi, lakini baada ya vita ya pili kuisha najua hujui kilichopelekea taifa hilo kushuka katika nafasi hiyo, na nafasi hiyo kushikiliwa na hiyo nchi ya Norway, hata hivyo sina uhakika kama unajua wakazi wa Norway na Denmark asili yao ni jamii zipi.

Kuhusu hiyo Miradi inayoendelea ndani ya nchi labda wewe ndio huijui, au pengine unahadithiwa tuu na kuiona kwenye luninga, mimi mpaka kuishuhudia nimeishuhudia. Kuanzia huo mradi wa umeme katika bonde la Rufiji, vituo vyote vipya vya mabasi mikoani, kuanzia Hiko cha mbezi Luis, Igumbilo, Dodoma, kituo cha mabasi cha kibaha, kituo cha mabasi Mpanda, kituo cha mabasi Singida n.k

Mradi wa SGR kILa mtu kaushuhudia hasa wakazi wa Dsm, Pwani na morogoro. Usafiri wa anga, ukarabati wa terminal 3 na ndege mpya tena kupanda nimeshazipanda, sijui unataka nielewe kwa namna gani hiyo miradi.

Miradi inafanya vizuri lakini ushauri wangu naona kwako hauna maana kwa sababu sio mtu husika, wahusika wanajua nazunguzia nini.

Kuhusu Historia naomba uachane napo maana huko utajitia aibu
Mkuu nchi haiongozwi kwa historia unazozitaja hapa sio kila kitu ni cha kuiga hamasisha watu kujitambua na kufanya kazi sio swala la kuwa tegemezi na fikra za kitumwa. Unaweza kuwa na ushauri mzuri lakini uwasilishaji ukawa unatia mashaka. Sitakujibu tena sababu umeshasema wewe ni mtu wa fasihi.
 
Mhe. Rais, naomba nifupishe habari hii, huu ni wakati wa kutumikisha watu wa mataifa mengine, kwani kwa kufanya hivyo ndio uhakika wa kuiendeleza nchi upo kwa kiasi kikubwa.
Kijana wa miaka 26!

Kuna mambo mengi uliyoandika yanafikirisha, hata kama ni nadharia kuliko uhalisi wenyewe. Kwa mfano, ni huo hapo juu nilioku'quote'. Hujaeleza hayo mataifa mengine utawatumikisha vipi: utakwenda kuwafanya wawe makoloni kama wao walivyofanya mataifa mengine kuwa makoloni?
Kama kwa mfano huo ulioutoa una maana ya "ushirikiano na mataifa mengine", basi sema hivyo waziwazi, lakini sio "kuyatumikisha" inavyoeleweka hapa.

Pengine ungesoma historia ya China, ingekufungua mawazo kidogo na kujua kwamba wao walijifungia kwa muda mrefu sana, walipojifungua taifa lao likawa lipo tayari kupaa juu kama roketi kimaendeleo. Walipokuwa wamejifungia ("hawatumikishi wengine") walikuwa wakiweka miundo imara)

Nikiri, sikusoma bandiko lako refu lote, huenda kuna mambo kadhaa uliyoandika yanayoeleza undani wa nadharia hii uliyoweka hapa.

Inawezekana sana kukawa na tofauti kati ya uliyoandika na baadhi ya yale ninayoyadhania mimi kama chachu ya kuleta maendeleo ya nchi haraka.

Kwa ufupi niaminiyo mimi:
1. Maendeleo ya nchi ni 'process' ambayo haitokeii "ghafla bin vuuu". Ni mwendelezo na kuongezea kwa yale yaliyokwishafikiwa. Kwa mfano. Mtu hawezi sasa hivi akasema hatujapiga hatua katika kuendeleza elimu yetu ukilinganisha na wakati Mwalimu Nyerere anatwaa nchi toka kwa wakoloni. Ndiyo, elimu yetu imekuwa ni ya kusuasua katika sehemu mbalimbali, lakini mtu hawezi kusema kwamba hatujaendelea. Kinachotakiwa hapa sasa hivi katika eneo hili ni kuifanya iwe bora zaidi na kuwaandaa wasomi wetu katika nyanja mbalimbali kuwa na uwezo wa kuligeuza kwa kasi zaidi kimaendeleo taifa letu. Maana yangu ni kwamba, hatuwezi kuwa na kasi (speed) au (rate) ile ile tuliyokuwa nayo miaka ya sitini au sabini. "Rate" yetu sasa inatakiwa kuwa ya juu zaidi katika kuleta maendeleo.

Na ili nieleweke vizuri juu ya jambo hili; jaribu kufikiria baadhi ya nchi ambazo siku nyingi sana zimekuwepo huru kabisa na hata kihistoria zinafahamika kuwa ni mataifa kamili: Turkey (uturuki), kwa mfano, ni muda huu wa karibuni ndio wameanza kuonekana kupiga hatua za kuwa nchi iliyoendelea, baada ya miongo na miongo mingi ya taifa hilo kuwepo kimuundo kama taifa. Na Misri je? Unaijua nchi inayoitwa Haiti? Inawezekana kabisa kwa hali waliyonayo sasa taifa hilo, ikawachukua miaka mingi sana kubadili hali zao kimaisha.
Unaweza ukasema Tanzania haiwezi kamwe kuwa kama Haiti?

2. Maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe, sio viongozi. Viongozi ni kusaidia kuweka mipango mizuri na kusimamia utekelezaji wake tu wa maendeleo wanayoyaleta wananchi wenyewe. Kwa hiyo, Rais Magufuli hawezi kamwe kuiletea Tanzania maendeleo, hata kama angeanzisha makambi ya kuwatumikisha wananci wake.

3. Nci zetu hizi kamwe hazitakiwi kwenda kuvumbua "tairi" upya. Tairi tayari lipo linalofanya kazi vizuri. Lengo letu sasa ni kujua jinsi ya kuyatumia haya "matairi" ya kuleta maendeleo vizuri. Na hili ndilo jukumu kubwa ambalo wasomi wetu wangelikazia ili kuwafikishia wananchi nyenzo hizi za kuharakisha maendeleo yao.
Wakulima wetu wapate ushauri wa kila aina ili wazalishe mazao kwa wingi na kuhakikisha mavuno yao hayaharibiwi kabla ya kufikishwa sokoni.
Tunanunua kila aina ya dawa toka nje, miaka zaidi ya 60 baada ya kupata uhuru wetu. Tunasomesha kila mwaka wataalam wetu katika nyanja hii ya kutengeneza madawa, lakini kama taifa hawa watu hatuwapi nyenzo za kuwawezesha kufanya kazi yao ya kutengeneza madawa aina mbali mbali, badala yake hawa watu tuliowasomesha kwa gharama kubwa wanaishia kwenda kuwa "wauza duka"! Huu ni utuzizi mbaya wa raslimali zetu. Na huu ni mfano mmoja tu katika mingi! Wengi wa hawa watu sasa mawazo yao ni kuingia kwenye siasa, kama akina Magufuli, badala ya kuvumbua na kutengeneza mafuta yanayozuia kutu yatokanayo na zao letu la korosho! Sasa, si angalao Magufuli mwenyewe angewekea mkazo baada ya kuingia kwenye siasa, ili watu (wasomi) wa aina yake wapewe fursa zaidi kuitumia elimu yao katika maeneo mbalimbali ili taifa lifaidike na utaalam wao? Badala yake, tunaona maprofesa ndio wanaojazwa kwenye vyeo vya kuteuliwa, badala ya kufanya kazi muhimu la kuligeuza taifa hili katika nyanja walizosomea!

Kama taifa, kwa nini viongozi wetu hawa wasingekazia tuandae mfumo mzima wa kuwa na "Chemical industry" yetu wenyewe - mali ghafi ya kutosha ipo ya kufanya hivyo Nchi kama Israel, Taiwan na nyinginezo wameweza, kwa nini sisi tusiweze..., ni umaskini wetu tu wa kifikra ndio unaotukwamisha.
Hatuwezi kama taifa kukubali kutojiandaa kwa mabadiliko haya makubwa yanayoletwa na ''technology" sehemu mbalimbali duniani. Ni wajibu wa viongozi wetu kuweka mipango sahihi na kuhakikisha kwamba hatupitwi na fursa kama hii itakayowezesha watu wetu kuwa wavumbuzi (innovators).
Kwa hiyo unaposikia nchi zinatofautiana, tofauti hizi zinatokana na maono ya viongozi wa nchi hizo.

Ngoja nikuache utafune haya kwanza. Lakini la muhimu, pengine kuliko mengine yote--- sahau kabisa swala la Magufuli kukuletea maendeleo au kuiletea maendeleo Tanzania. Hili ni jukumu la waTanzania wenyewe.
 
kama kweli una miaka 26 na umeweza kuandika hivi hongera sana maana yake utakaopo kuja fika 40 yrs utakuwa ni mwandishi mzuri sana [serekali isaidie sana wakulima ili tupate chakula kingi tuilishe afrika]
Eeenh, wewe huoni hata kaweka 'contact information' yake hapo? Huyu akishateuliwa sehemu fulani sahau kabisa ndoto alizoweka JF. Akina Kala Maganda na Popole hujawahi kuwasikia?
 
Dogo umeongoea vizuri sanaa...too bad rais wetu hana confidence ya kutosha!!! Kwenye outside world
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣

Mkuu sisemi mengi

Sikulaumu kwa kuwa najua hujui mengi kuhusu Taifa la china, najua hujui kuwa taifa la China liliwahi kuvamia na kutawala nchi zifuatazo;
  • Korea
  • Vietnam
  • Mongolia
  • Taiwan
  • Central Asia
  • Burma
Kama mataifa hayo wanaishi wachina sawa sawa nitakubaliana na wewe. Pengine unaijua Chinza kuanzia kwa Huyo Mao zedong, na kama ni hivyo sitakulaumu, lakini hata habari ya kisiwa cha Taiwan ambapo china na India wanakigombea nacho hujui? Usijedhani ni kisiwa kisichoishi watu:D:D:D Hiyo ni nchi ya Taiwan
LOoooo! Ni wewe uliyeandika haya?

Basi tena!
 
Kwahiyo unataka Mh sana Jiwe akavamie Congo na kupora dhahabu yao sio ?
Uvamizi siyo lazima ubebe rungu. Chatu anamvamia mbwa kwa kutoa harufu ya kuvutia, halafu mbwa anaenda mwenyewe huku akifurahia, na kisha anamezwa.

Uvamizi wa kutumia nguvu ulikwishaisha, unafanywa na wasio na akili. Watu werevu hufanya uvamizi wa akili ambao wale wanaosubiria uvamizi wa nguvu, hawana uwezo wa kutambua kuwa wamevamiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyekuambia hayo uliyosema siyaoni ni nani? Naomba ukisoma makala za kikubwa utulize akili yako, kama umezoea makala zenye ufupisho ninngekusihi ufuatilie hizo hizo. Hizi ndefu waachie wakubwa wako
Unavuruga mada yako mwenyewe! Pole sana!
 
Si kweli china imeendelea kwa kutumikisha wananchi wake mpaka leo hii. Hata wewe unaweza kuendelea ukijitumikisha wewe mwenyewe kufanya kazi yako ya kujiajiri kisha kuwauzia watu wenye uhutaji na bidhaa zako. Ulikuwa hujuwi hili?
Unabisha kitu ambacho kipo wazi kabisa ,wachina wanafanya kaz sana tena kwa juhud lkn kaz izo pia mojawapo kutumia nchi nyngne ,mfano apa africa wachina wapo karbu kila sehem na wapo karbu kila sekta
 
Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Heshima kwako, Mkuu wa nchi, Pole na hongera na Majukumu yako ya kila siku. Naomba uniruhusu nichukue muda wako kidogo kwa kusoma jumbe hii. Natumai hekima na busara yako hazitashindwa kuelewa nini nimekusudia kusema.

Mara kwa mara nimekuwa nikikufuatilia katika hotuba zako, imekuwa ni desturi kusikia kutoka kwako kuwa unataka taifa hili liendelee. Nafiikiri kama sipo peke yangu kuwa,, usemapo kauli hiyo, watu huliona taifa likiwa limefika mbali katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, Siasa, kijamii, Utamaduni, Sayansi na Teknolojia, Sanaa, michezo na Burudani miongoni mwa Nyanja zingine. Usemapo kauli zako, watu huchora picha vichwani mwao na kuona maisha yao yakiwa mazuri mno. Lakini mara umalizapo hotuba yako watu hushtuka kama waliotoka usingizini wakiwa wameota ndoto za utajiri lakini wameamka na kujikuta bado ni masikini na fukara wanaonuka shida na tabu za kila namna. Hotuba zako ni nzuri, lakini ni kama ndoto za mtu aliyelala mwenye matamanio makubwa katika maisha yake.

Nakiri, mimi ni kijana mdogo, huenda nikaonekana nina akili za kiutoto, Lakini sikosi cha kushauri kwa akili zangu hizi hizi ambazo ndio kwanza zina miaka 26. Mhe. Rais John Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania. Naomba unisikilize kwa utulivu.

Hakuna taifa lolote duniani lililoendelea kwa kutumikisha tuu raia wake, hakuna na halijawahi na kamwe halitawahi kutokea Dunia ingalipo. Kwa umri mdogo niliokuwa nao (nakubali kurekebishwa na kufunzwa pia kama nitakosea sehemu) nimechunguza kwa muda sasa, ni zaidi ya miaka kumi nimetafakari na kuchunguza kwa nini mataifa mengine yamekuwa makubwa kiuchumi, kijeshi, kiushawishi, kisayansi na Kiteknolojia, kiutamaduni n.k Baada ya kufanya uchunguzi wangu binafsi nimegundua mambo kadhaa, ambayo hayo ndio nataka nikuelezee siri ndoto tuu, ambayo ukiifahamu hiyo basi nchi hii itapiga hatua kubwa sana.

Siri yenyewe nimeshaieleza; Huwezi kuiendeleza nchi kwa kutumikisha Raia wako pekee yake, haiwezekani na kamwe haitakuja kuwezekana, huko ni kupoteza muda tuu.

Ni sawa na kusema, Mtu hawezi kuwa tajiri kwa kujitumikisha yeye peke yake, mtu ili aweze kuwa tajiri ni lazima ajitumikishe yeye kidogo, kisha awatumikishe wengine kwa ajili yake. Mtu huyo lazima awe tajiri.

Taifa lolote ili liendelee, lazima lisijitumikie lenyewe bali lihakikishe kuwa linatumikisha mataifa mengine kwa maslahi yake. Yaani Tanzania kamwe haitaweza kuendelea kwa kutumikisha Raia wake peke yake. Mara kwa mara nimekuwa nikisema, nchi haiwezi kuendelea kwa kutegemea wananchi wake pekee. Kama ilivyo kwa mtu binafsi kuwa, huwezi kuendelea kwa kujitegemea wewe peke yako, lazima utafute namna ya kutegemewa na wengine ili uweze kuendelea zaidi ya hao wanaokutegemea. Kutajirika ni kutegemewa, ni uwezo wa kuwafanya wengine wakutumikie na kukutegemea.

Halikadhalika na Taifa, ili taifa letu litajirike, liendelee na kuwa na maendeleo, basi hakuna namna tutaweza kukwepa; sharti tuwe na uwezo wa kuyatumikisha na kuyafanya mataifa mengine yatutegemee kwaa vyovyote vile, kwa wema au kwa ubaya, kwa sheria halali au kwa sheria haramu, yaani kwa vyovyote.

Ninafurahia kuona Baadhi ya jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha taifa hili linaendelea, lakini jitihada hizo hazitatufikisha popote kama tusipoelewa jambo nililolisema kwa ukomavu wa kifikra na kijitihada. Sio lengo langu kumtukana mtu, wala sio lengo langu kujikweza kwa wakubwa, bali msingi wa hoja yangu ni, kushauri na ikiwezekana kuhimiza hatua za haraka zichukuliwe katika hoja yangu. Nategemea watu wenye akili ndani ya mfumo, waijadili hoja yangu kiweledi, waichambue na kuichanganua, kisha waiundie mikakati ya namna ya kuitekeleza.

Taifa letu tangu limeundwa lina miaka takribani miaka 60. Sio miaka michache, na sisemi kuwa ni mingi. Tumejitahidi kulijenga taifa hili mpaka tulipofikia, kiasi tunaweza kusema tuna ahueni, lakini hatuwezi kujidanganya kwa maneno ya jukwaani tuu kwamba tutaweza kuiendeleza nchi hii na kuifanya kuwa taifa kubwa kwa kutumikisha raia wetu pekee yake. Labda tuamue tuu kujidanganya, lakini kamwe hatutaweza kufanya hivyo, hatutaweza kulifanya taifa letu kuwa taifa kubwa, tajiri kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kisanaa, michezo na buruda, kisayansi na teknolojia.

Mhe. Rais, Nakuambia kwa ya upole na uzalendo, hatuwezi kuiendeleza nchi hii kwa kutumikisha Raia wetu peke yake. Kama tutaendelea kuwatumikisha Raia wetu pekee yake ni kuwafanya waendelee kuwa watumwa wa nchi yao, ni lazima tutawapunja mishahara, sio waalimu, sio madaktari, sio Maaskari wetu, sio wahasibu, sio mainjinia wetu, wote tutawasotesha kwa kuwalipa mishahara midogo na kuwafanya kama watumwa kumbe ni raia wa nchi hii.

Kama tutaendeleaa kutegemea Raia wa taifa letu pekee bila kutafuta namna ya kutumikisha mataifa mengine, basi ukosefu wa ajira utazidi kuongezeka maradufu. Vijana wetu watazidi kusota, kuhenyeka na kuyachukia maisha kwa kukosa hela za kuendesha maisha yao na familia zao.

Zamani nikiwa kijana mdogo nikiwa nasoma Biblia, nilipata kujiuliza kuwa ni kwani mataifa ya zamani yalikuwa yanachukua WATUMWA kutoka katika nchi zingine au kuzikalia kimabavu. Mathalani, taifa la shinari, Ninawi, ambalo lilikuwa Dola la Ashuru(Syria ya leo) ndio huo ufalme wa Babeli. Taifa la Misri, Ufalme wa kifarao, Taifa la wamedi na waajemi(Iraq na Iran ya leo), Taifa la Wayunani(wagiriki) hapa yupo Mfalme Alexandar the Great Mfalem wa Macedonia, aliyefia Babeli. Ufalme wa Rumi, Dola la kirumi, Ufalme wa Ottoman ambapo mji mkuu ulikuwa Konstantinopoli au Bizanti( Instanbul kwa sasa), Kisha vikazuka vitawala kutoka nchi za magharibi mwa ulaya, Utawala wa waingereza, Wafaransa, Wajerumani, Kisha likazuka taifa la Marekani.

Mataifa hayo makubwa karibu yote yametumia mbinu hii, kwa namna mbalimbali. Mbinu ya kuyatumikisha mataifa na raia wa nchi zingine kujenga nchi zao. Kwa mfano walitumia mbinu za biashara ya utumwa kwa lengo la kuchukua watumwa(Raia wa mataifa mengine) Kuja na kujenga miji yao, miji karibu yote mikubwa duniani ya kale imejengwa na watumwa kwa gharama sawa na bure. Mbinu ya kuvamia mataifa mengine na kuyakalia kimabavu kisha kutumikisha nchi hizo kwa kulipa kodi kwenye mataifa yao, Dola la Kirumi, Kiashuru, Misri ya kale, zote zilitumia mbinu hizo. Yaani taifa linalokaliwa kimabavu linalipa kodi kwenye taifa lenye nguvu.

Mbinu ya ukoloni, ambapo taifa moja linatawala taifa jingine kwa kila nyanja. Mbinu hii wametumia Waingereza, wajerumani, Wafaransa, wareno, Wajapan kuwatawala wachina, n.k.Mbinu hii ilitajirisha sana mataifa tajwa hapo.

Mbinu ya Kutawala nchi zingine kwa kisingizio cha kusambaza dini, Mbinu hii imetumiwa na Dola la Kirumi, na Dola la Ottoman, ambapo mataifa hayo yalijifanya kana kwamba yanaeneza dini zao kumbe ni utamaduni wao kinguvu kwa kisingizio cha miungu yao. Dola la Kirumi liliitumia dini ya Kikristo, wakati dola la Ottoman likiitumia dini ya Kiislam. Baada ya kuteka na kutiisha nchi walizovamia kilichofuata ni kuchukua sadaka, yaani sehemu ya sadaka zilikuwa zinaenda makao makuu ya madola hayo. Nafikiri hata kwa sasa baadhi ya dini hufanya hivyo. Waliokataa dini hizo kwa zama hizo walikiona cha mtema kuni, waliuawa kwa vifo katili.

Taifa letu lazima tutafute namna ya kulifanya liheshimike, na ili kitu kiheshimike lazima kitegemewe. Sasa katika kulitegemeza taifa kuna njia kuu mbili, kwa kuwatumikisha watu wa mataifa mengine mpaka waone hayo ndio maisha, pili, kuwafanya watu wetu wawe na sifa maalumu ambazo mataifa mengine hawana, na sifa hizo ziwe ndio mahitaji ya msingi kwa mataifa mengine.

Kwa sasa mataifa makubwa, yanavamia nchi ndogo kwa kile kiitwacho Ukoloni mamboleo. Nayapongeza mataifa hayo kwa hatua hizo. Kwa sababu kwenye maisha usipokubali kuongoza basi lazima uongozwe, yaani upende usipende.

Kama taifa, hatuwezi jiwekea mipaka katika kuliimarisha taifa letu, kulifanya taifa letu liwe taifa kubwa na tajiri. Hata kama halitakuwa kubwa kuliko yote lakini angalau liwe kwenye nafasi bora katika kumi za mataifa makubwa.

Nilishawahi kusema pia, Hatuwezi kuondoa umasikini kama hatujui pa kuupeleka. Viongozi wa taifa lazima kwa makusudi makubwa yenye dhamira, wasemapo tunataka kuuondoa umasikini katika nchi hii, lazima moyoni wawe na jibu kuwa tunauondoa kuupeleka wapi. Hatuwezi kuuondoa umasikini bila kujua wapi tunaupeleka. Kama tutakuwa tunafanya hayo, yaani kuuondoa umasikini bila kujua pahala pa kuupeleka maana yake ni kusema, tunagawiana wenyewe kwa wenyewe umasikini bila ya kujijua.

Tunagawanaje umasikini? Ipo hivi, serikali yoyote ili ijiendeshe inahitaji kodi, kodi ni pesa wala sio kitu kingine. Kodi ni watu, na watu ndio kodi. Sasa ni lazima tujue namna ya kuzipata kodi kwa watu bila kuwapa umasikini. Mbinu bora zaidi ni kutenga watu, "divide and Rule" lakini ni watu wapi hao? Hatuwezi wagawanya watu wetu wenyewe, hawa ndio furaha yetu, hawa ndio watakao jivunia sisi wenyewe. Sasa lazima tuzitafute kodi kwa watu wa mataifa mengine. Huwa nasemaga; taifa bora ni lile lenye uwezo wa kuchukua kodi kwenye mataifa mengine zaidi kuliko ndani ya taifa. Yaani siku zote tajiri bora ni yule aliyeupata utajiri nje ya watu wake. Kumbuka utajiri ni unyonyaji. Yaani ili mtu awe tajiri lazima anyonye wengine.

Sasa hatuwezi kuwa nchi tajiri kwa kunyonya watu wetu wenyewe. Ni lazima tulinde watu wetu kwa nguvu kubwa, lazima tulinde vijana wetu, kinamama na wazee. Lazima tuwalinde wafanyabiashara wetu kwa vyovyote vile, lazima tulinde watumishi wa umma, huwa nasemaga, kiongozi mzalendo ni yule mwenye uwezo wa kulinda maslahi ya watu wake kwa vyovyote. Kiongozi bora ni yule anayeweza kubuni namna ya kunyonya watu wa mataifa wengine ili kunufaisha watu wa taifa lake.

Tukisema nchi yetu inaendelea lazima tujue inaendeleaje, kwa vipi, nani aliyeendelea, je ni watu wetu wenyewe au wageni?

Hatuwezi kuendeleaa kwa kutawaliwa na wageni, nafikiri ni wakati wa kujitathmini na kuyaangalia maendeleo yetu ni yepi na kwa nini tunayaita maendeleo.

Mhe. Rais, maendeleo halisi ni kujitawala, na maana halisi ya kujitawala ni uwezo wa kuwatawala wengine. Nchi haiwezi kujitawala kama haitawali nchi zingine. Sijawahi kuona popote pale. Kigezo kikubwa cha nchi kupaa kwenda juu basi ni uwezo wa kudidimiza nchi zingine. Kama ilivyo kigezo kikubwa cha mtu kuwa tajiri ni uwezo wake wa kutawala na kunyonya watu wengine. Hatuwezi kuishi kama tupo mbinguni, kufanya hivyo ni kujidanganya. Kwa sasa tupo duniani. Kanuni ya dunia ni kuwa ili uwe mshindi basi lazima ushinde wengine. Huwezi kuwa mshindi kwa kuishi maisha bila kuwashusha washindani wako. Sijawahi kuona jambo hilo, pamoja na kuwa nina umri mdogo.

Mhe. Rais, nafikiri mpaka naandika mambo haya, ni kuwa ninajua tunaouwezo wa kuzitawala nchi zingine kwa namna yoyote ile, kwa hila, njama, mabavu, hiyari, au kwa kutumia soko la giza. Nafikiri hii ndio ingekuwa njia ya lazima kwa nchi hii kuendelea.

Taifa la uchina, linatumikisha mataifa mengine kwa namna nyingi tuu, aidha kwa kutoa mikopo yenye riba ngumu, au kwa makubaliano ya kuendesha miradi mikubwa ambayo pesa yao itarudi kwa kuajiri watu wao kutoka china. Pia hutumia mbinu ya uwekezaji ambapo, huagiza vijana wao kuja Afrika kuanzia makampuni ya namna mbalimbali kisha huwapa mikopo, wakija huku huajiri vijana wetu ambao huitwa watumishi lakini kwa mishahara wanayolipwa sio watumishi bali WATUMWA. Ni aibu kwa nchi na taifa makini kuona vijana wake wanageuzwa watumwa na wageni katika nchi yao.

Mbinu hii pia huitumia Wahindi, ambao huanzisha makampuni yao tena wengine kwa kuchukua mikopo kwenye bank za ndani, kisha huajiri vijana wa taifa hili na serikali itasema vijana wamepewa ajira, lakini sio ajira bali wameingizwa utumwani ndani ya taifa lao wenyewe. Mishahara yao ni 100,000/= wengine 140,000/= wakizidi sana, 180,000/= kwa siku sita wakifanya kazi masaa 12, kwa kupokezana, wengine usiku wengine asubuhi. Kwa vyovyote vile iwavyo hakuna maisha mazuri kwa vijana na watu wake ikiwa watakuwa watumwa ndani ya nchi yao. Taifa haliwezi kujitawala ikiwa watu wake wametawaliwa, labda tuseme viongozi ndio wamejitawala ambao kimsingi hawafiki hata asilimia 1% ya watu wote.

Ili taifa lijitawale, lazima watu wake waweze kujitawala. Na dalili ya mtu anayejitawala ni uwezo wa kudai haki zake, na ili mtu aweze kudai haki zake basi ni lazima awe huru. Na ili mtu awe huru basi lazima aweze kujikimu na kuendesha maisha yake yaani asiwe masikini. Nchi haiwezi kujiendesha bila kuendesha nchi zingine. Taifa haliwezi kujiendesha ikiwa watu wake wanaendeshwa na wageni, au hawawezi kujiendesha. Pengine waite kujiendesha kwa kujidanganya.

Utulivu wa mataifa makubwa unatokana na uwezo wao wa kuvuruga mataifa mengine. Taifa lolote lile haliwezi kuwa tulivu kama lina uwezo mdogo waa kuvuruga utulivu wa nchi zingine. Jitihada na mikakati ni muhimu sana katika mambo haya.

Mhe. Rais, suala la maendeleo ya kijamii ni suala pana na nyeti sana. Lazima tuchukua jitihada madhubuti katika kuleta heshima ya taifa hili kijamii. Taifa haliwezi kusema limeendelea kwa kigezo cha ongezeko kubwa la wasomi wenye elimu yenye asili ya kigeni. Taifa haliwezi ujivunia wasomi wenye elimu za kigeni, kujivunia elimu ya kigeni ni kujivunia utumwa, ni kujivunia kutawaliwa kiakili na wageni. Inashangaza sana kuona vijana wakijivunia ma-degree huku wazee wakijivunia Uprofesa. Degree ya utumwa, na uprofesa wa utumwa. Mhe. Rais hushangai hizo degree na Phd bado hazina impact chanya ndani ya jamii yetu. Jibu ni kwa sababu, hakuna utumwa wenye impact chanya kwenye jamii.

Elimu ya kitumwa hutengeneza kizazi cha kitumwa. Ndio maana vijana wengi wamemaliza elimu zao na bado wanashindwa kukabiliana na mazingira. Mhe. Rais, unamkumbuka yule Mkurugenzi wa Morogoro ulivyomtumbua alivyolia na kugara gara, huku akikulilia wewe kama mungu wakati wewe ni binadamu kama yeye? Unamkumbuka? Yale ndio matokeo ya elimu ya kitumwa.

Huwezi kuwa mzalendo ilhali unaelimu na fikra za kigeni, popote pale sijawahi kuona. Niliwahi kuandika kuwa, ili tuondoe ujinga katika taifa letu lazima tujue ujinga huo tunaupeleka wapi. Wazungu walituletea ujinga wao, wakauita majina mbalimbali mengine ni elimu, dini, na vikoro koro vyao vyote ambavyo waliona havina msaada

Mhe. Rais, naomba nifupishe habari hii, huu ni wakati wa kutumikisha watu wa mataifa mengine, kwani kwa kufanya hivyo ndio uhakika wa kuiendeleza nchi upo kwa kiasi kikubwa.

Naomba niishie hapa,

Niwatakie watanzania wote kheri ya sikukuu za kumaliza mwaka

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dodoma
Mbona unarudia rudia maneno yale yale? We kweli bado mtoto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom