Tanzania ya leo

ONJO

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
215
261
Tanzania ya leo

Ni nchi ya amani kusifiwa inastahili. Nilitazama duniani kote kuangalia siasa za kweli, sikuona isipokuwa Tanzania.

Kwa misingi ya Ujamaa Tanzania ilijengwa. Mwalimu Nyerere uishi mpaka wakati usio na kipimo. Hakika ulitukuka, kila mtoto anayezaliwa anasikia habari zako. Naamu jina lako litakumbukwa vizazi vyote.

Nalifurahi waliponiambia kwa falsafa yako ya ujamaa ulifundisha kuwa, "Binadamu wote ni sawa" Ukimanisha hata wewe ulikuwa sawa na watu wengine.

Kwasababu hiyo, moyo wangu ulijawa na furaha Tanzania ilipoongozwa na mwanamke, maana ndicho ulichofundisha.

Hapa ndipo nilipogeuza macho yangu kuangalia nchi za mataifa mengine. Je nijifunze siasa za mataifa mengine?

Napo sikuona isipokuwa kujifunza kwa malkia mama Samia Suluhu Hassan.

Kwa serikali ya mama ndipo ilipo Tanzania yangu.

1. Wakati mama anahamasisha viongozi wa dini wafundishe maadili yameharibika, watu wa mataifa wanaruhusu ushoga. Hakika siasa ya kweli ipo Tanzania.

2. Wakati siasa ya Tanzania ikifanyika kwa kutukanana matusi na kwa hoja. Watu wa mataifa wanapigana kwa mitutu ya bunduki. Hakika siasa ya kweli ipo Tanzania.

3. Wakati Tanzania ikiwaona watu wa mataifa yote ni ndugu. Watu wa mataifa hujikita kutukuna nchi zingine. Hakika siasa ya kweli ipo Tanzania.

4. Vita ya Tanzania ni marumbano ya dini lakini vita vya mataifa ni kumwaga damu. Hakika siasa ya kweli ipo Tanzania.

5. Watanzania wanaumizwa na mahusiano, ndoa hazidumu, viongozi wa dini wanaaswa wafundishe watu wao. Wakati watu wa mataifa wanatengeneza wanawake bandia kutatua tatizo hilo. Hakika siasa ya kweli ipo Tanzania.

Yapo mengi mtaongezea.....

Nawasihi enyi vijana jivunieni siasa zenu. Watazameni viongozi wenu waliowahi kuliongoza taifa la Tanzania, mkamtazame na Mh. Mama Samia mjifunze.

Hakuna taifa liloko nje linaloweza kutufundisha siasa. Nyerere alisema "Hakuna taifa lenye haki ya kuamua juu ya taifa jingine, wala mtu kumwamulia mtu mwingine".

Sasa tujiamulie wenyewe inawezekana Tanzania kuifanya iwe paradiso ukiwa tutaamua. Yaani mji mtakatifu ili watu wa mataifa wajichotee baraka kutoka kwetu.

Na ONJO Mpenzi wenu.
 
Back
Top Bottom