Rais Magufuli nisikilize kwa makini, Sitaki upoteze muda bure

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Heshima kwako, Mkuu wa nchi, Pole na hongera na Majukumu yako ya kila siku. Naomba uniruhusu nichukue muda wako kidogo kwa kusoma jumbe hii. Natumai hekima na busara yako hazitashindwa kuelewa nini nimekusudia kusema.

Mara kwa mara nimekuwa nikikufuatilia katika hotuba zako, imekuwa ni desturi kusikia kutoka kwako kuwa unataka taifa hili liendelee. Nafiikiri kama sipo peke yangu kuwa,, usemapo kauli hiyo, watu huliona taifa likiwa limefika mbali katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, Siasa, kijamii, Utamaduni, Sayansi na Teknolojia, Sanaa, michezo na Burudani miongoni mwa Nyanja zingine. Usemapo kauli zako, watu huchora picha vichwani mwao na kuona maisha yao yakiwa mazuri mno. Lakini mara umalizapo hotuba yako watu hushtuka kama waliotoka usingizini wakiwa wameota ndoto za utajiri lakini wameamka na kujikuta bado ni masikini na fukara wanaonuka shida na tabu za kila namna. Hotuba zako ni nzuri, lakini ni kama ndoto za mtu aliyelala mwenye matamanio makubwa katika maisha yake.

Nakiri, mimi ni kijana mdogo, huenda nikaonekana nina akili za kiutoto, Lakini sikosi cha kushauri kwa akili zangu hizi hizi ambazo ndio kwanza zina miaka 26. Mhe. Rais John Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania. Naomba unisikilize kwa utulivu.

Hakuna taifa lolote duniani lililoendelea kwa kutumikisha tuu raia wake, hakuna na halijawahi na kamwe halitawahi kutokea Dunia ingalipo. Kwa umri mdogo niliokuwa nao (nakubali kurekebishwa na kufunzwa pia kama nitakosea sehemu) nimechunguza kwa muda sasa, ni zaidi ya miaka kumi nimetafakari na kuchunguza kwa nini mataifa mengine yamekuwa makubwa kiuchumi, kijeshi, kiushawishi, kisayansi na Kiteknolojia, kiutamaduni n.k Baada ya kufanya uchunguzi wangu binafsi nimegundua mambo kadhaa, ambayo hayo ndio nataka nikuelezee siri ndoto tuu, ambayo ukiifahamu hiyo basi nchi hii itapiga hatua kubwa sana.

Siri yenyewe nimeshaieleza; Huwezi kuiendeleza nchi kwa kutumikisha Raia wako pekee yake, haiwezekani na kamwe haitakuja kuwezekana, huko ni kupoteza muda tuu.

Ni sawa na kusema, Mtu hawezi kuwa tajiri kwa kujitumikisha yeye peke yake, mtu ili aweze kuwa tajiri ni lazima ajitumikishe yeye kidogo, kisha awatumikishe wengine kwa ajili yake. Mtu huyo lazima awe tajiri.

Taifa lolote ili liendelee, lazima lisijitumikie lenyewe bali lihakikishe kuwa linatumikisha mataifa mengine kwa maslahi yake. Yaani Tanzania kamwe haitaweza kuendelea kwa kutumikisha Raia wake peke yake. Mara kwa mara nimekuwa nikisema, nchi haiwezi kuendelea kwa kutegemea wananchi wake pekee. Kama ilivyo kwa mtu binafsi kuwa, huwezi kuendelea kwa kujitegemea wewe peke yako, lazima utafute namna ya kutegemewa na wengine ili uweze kuendelea zaidi ya hao wanaokutegemea. Kutajirika ni kutegemewa, ni uwezo wa kuwafanya wengine wakutumikie na kukutegemea.

Halikadhalika na Taifa, ili taifa letu litajirike, liendelee na kuwa na maendeleo, basi hakuna namna tutaweza kukwepa; sharti tuwe na uwezo wa kuyatumikisha na kuyafanya mataifa mengine yatutegemee kwaa vyovyote vile, kwa wema au kwa ubaya, kwa sheria halali au kwa sheria haramu, yaani kwa vyovyote.

Ninafurahia kuona Baadhi ya jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha taifa hili linaendelea, lakini jitihada hizo hazitatufikisha popote kama tusipoelewa jambo nililolisema kwa ukomavu wa kifikra na kijitihada. Sio lengo langu kumtukana mtu, wala sio lengo langu kujikweza kwa wakubwa, bali msingi wa hoja yangu ni, kushauri na ikiwezekana kuhimiza hatua za haraka zichukuliwe katika hoja yangu. Nategemea watu wenye akili ndani ya mfumo, waijadili hoja yangu kiweledi, waichambue na kuichanganua, kisha waiundie mikakati ya namna ya kuitekeleza.

Taifa letu tangu limeundwa lina miaka takribani miaka 60. Sio miaka michache, na sisemi kuwa ni mingi. Tumejitahidi kulijenga taifa hili mpaka tulipofikia, kiasi tunaweza kusema tuna ahueni, lakini hatuwezi kujidanganya kwa maneno ya jukwaani tuu kwamba tutaweza kuiendeleza nchi hii na kuifanya kuwa taifa kubwa kwa kutumikisha raia wetu pekee yake. Labda tuamue tuu kujidanganya, lakini kamwe hatutaweza kufanya hivyo, hatutaweza kulifanya taifa letu kuwa taifa kubwa, tajiri kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kisanaa, michezo na buruda, kisayansi na teknolojia.

Mhe. Rais, Nakuambia kwa ya upole na uzalendo, hatuwezi kuiendeleza nchi hii kwa kutumikisha Raia wetu peke yake. Kama tutaendelea kuwatumikisha Raia wetu pekee yake ni kuwafanya waendelee kuwa watumwa wa nchi yao, ni lazima tutawapunja mishahara, sio waalimu, sio madaktari, sio Maaskari wetu, sio wahasibu, sio mainjinia wetu, wote tutawasotesha kwa kuwalipa mishahara midogo na kuwafanya kama watumwa kumbe ni raia wa nchi hii.

Kama tutaendeleaa kutegemea Raia wa taifa letu pekee bila kutafuta namna ya kutumikisha mataifa mengine, basi ukosefu wa ajira utazidi kuongezeka maradufu. Vijana wetu watazidi kusota, kuhenyeka na kuyachukia maisha kwa kukosa hela za kuendesha maisha yao na familia zao.

Zamani nikiwa kijana mdogo nikiwa nasoma Biblia, nilipata kujiuliza kuwa ni kwani mataifa ya zamani yalikuwa yanachukua WATUMWA kutoka katika nchi zingine au kuzikalia kimabavu. Mathalani, taifa la shinari, Ninawi, ambalo lilikuwa Dola la Ashuru(Syria ya leo) ndio huo ufalme wa Babeli. Taifa la Misri, Ufalme wa kifarao, Taifa la wamedi na waajemi(Iraq na Iran ya leo), Taifa la Wayunani(wagiriki) hapa yupo Mfalme Alexandar the Great Mfalem wa Macedonia, aliyefia Babeli. Ufalme wa Rumi, Dola la kirumi, Ufalme wa Ottoman ambapo mji mkuu ulikuwa Konstantinopoli au Bizanti( Instanbul kwa sasa), Kisha vikazuka vitawala kutoka nchi za magharibi mwa ulaya, Utawala wa waingereza, Wafaransa, Wajerumani, Kisha likazuka taifa la Marekani.

Mataifa hayo makubwa karibu yote yametumia mbinu hii, kwa namna mbalimbali. Mbinu ya kuyatumikisha mataifa na raia wa nchi zingine kujenga nchi zao. Kwa mfano walitumia mbinu za biashara ya utumwa kwa lengo la kuchukua watumwa(Raia wa mataifa mengine) Kuja na kujenga miji yao, miji karibu yote mikubwa duniani ya kale imejengwa na watumwa kwa gharama sawa na bure. Mbinu ya kuvamia mataifa mengine na kuyakalia kimabavu kisha kutumikisha nchi hizo kwa kulipa kodi kwenye mataifa yao, Dola la Kirumi, Kiashuru, Misri ya kale, zote zilitumia mbinu hizo. Yaani taifa linalokaliwa kimabavu linalipa kodi kwenye taifa lenye nguvu.

Mbinu ya ukoloni, ambapo taifa moja linatawala taifa jingine kwa kila nyanja. Mbinu hii wametumia Waingereza, wajerumani, Wafaransa, wareno, Wajapan kuwatawala wachina, n.k.Mbinu hii ilitajirisha sana mataifa tajwa hapo.

Mbinu ya Kutawala nchi zingine kwa kisingizio cha kusambaza dini, Mbinu hii imetumiwa na Dola la Kirumi, na Dola la Ottoman, ambapo mataifa hayo yalijifanya kana kwamba yanaeneza dini zao kumbe ni utamaduni wao kinguvu kwa kisingizio cha miungu yao. Dola la Kirumi liliitumia dini ya Kikristo, wakati dola la Ottoman likiitumia dini ya Kiislam. Baada ya kuteka na kutiisha nchi walizovamia kilichofuata ni kuchukua sadaka, yaani sehemu ya sadaka zilikuwa zinaenda makao makuu ya madola hayo. Nafikiri hata kwa sasa baadhi ya dini hufanya hivyo. Waliokataa dini hizo kwa zama hizo walikiona cha mtema kuni, waliuawa kwa vifo katili.

Taifa letu lazima tutafute namna ya kulifanya liheshimike, na ili kitu kiheshimike lazima kitegemewe. Sasa katika kulitegemeza taifa kuna njia kuu mbili, kwa kuwatumikisha watu wa mataifa mengine mpaka waone hayo ndio maisha, pili, kuwafanya watu wetu wawe na sifa maalumu ambazo mataifa mengine hawana, na sifa hizo ziwe ndio mahitaji ya msingi kwa mataifa mengine.

Kwa sasa mataifa makubwa, yanavamia nchi ndogo kwa kile kiitwacho Ukoloni mamboleo. Nayapongeza mataifa hayo kwa hatua hizo. Kwa sababu kwenye maisha usipokubali kuongoza basi lazima uongozwe, yaani upende usipende.

Kama taifa, hatuwezi jiwekea mipaka katika kuliimarisha taifa letu, kulifanya taifa letu liwe taifa kubwa na tajiri. Hata kama halitakuwa kubwa kuliko yote lakini angalau liwe kwenye nafasi bora katika kumi za mataifa makubwa.

Nilishawahi kusema pia, Hatuwezi kuondoa umasikini kama hatujui pa kuupeleka. Viongozi wa taifa lazima kwa makusudi makubwa yenye dhamira, wasemapo tunataka kuuondoa umasikini katika nchi hii, lazima moyoni wawe na jibu kuwa tunauondoa kuupeleka wapi. Hatuwezi kuuondoa umasikini bila kujua wapi tunaupeleka. Kama tutakuwa tunafanya hayo, yaani kuuondoa umasikini bila kujua pahala pa kuupeleka maana yake ni kusema, tunagawiana wenyewe kwa wenyewe umasikini bila ya kujijua.

Tunagawanaje umasikini? Ipo hivi, serikali yoyote ili ijiendeshe inahitaji kodi, kodi ni pesa wala sio kitu kingine. Kodi ni watu, na watu ndio kodi. Sasa ni lazima tujue namna ya kuzipata kodi kwa watu bila kuwapa umasikini. Mbinu bora zaidi ni kutenga watu, "divide and Rule" lakini ni watu wapi hao? Hatuwezi wagawanya watu wetu wenyewe, hawa ndio furaha yetu, hawa ndio watakao jivunia sisi wenyewe. Sasa lazima tuzitafute kodi kwa watu wa mataifa mengine. Huwa nasemaga; taifa bora ni lile lenye uwezo wa kuchukua kodi kwenye mataifa mengine zaidi kuliko ndani ya taifa. Yaani siku zote tajiri bora ni yule aliyeupata utajiri nje ya watu wake. Kumbuka utajiri ni unyonyaji. Yaani ili mtu awe tajiri lazima anyonye wengine.

Sasa hatuwezi kuwa nchi tajiri kwa kunyonya watu wetu wenyewe. Ni lazima tulinde watu wetu kwa nguvu kubwa, lazima tulinde vijana wetu, kinamama na wazee. Lazima tuwalinde wafanyabiashara wetu kwa vyovyote vile, lazima tulinde watumishi wa umma, huwa nasemaga, kiongozi mzalendo ni yule mwenye uwezo wa kulinda maslahi ya watu wake kwa vyovyote. Kiongozi bora ni yule anayeweza kubuni namna ya kunyonya watu wa mataifa wengine ili kunufaisha watu wa taifa lake.

Tukisema nchi yetu inaendelea lazima tujue inaendeleaje, kwa vipi, nani aliyeendelea, je ni watu wetu wenyewe au wageni?

Hatuwezi kuendeleaa kwa kutawaliwa na wageni, nafikiri ni wakati wa kujitathmini na kuyaangalia maendeleo yetu ni yepi na kwa nini tunayaita maendeleo.

Mhe. Rais, maendeleo halisi ni kujitawala, na maana halisi ya kujitawala ni uwezo wa kuwatawala wengine. Nchi haiwezi kujitawala kama haitawali nchi zingine. Sijawahi kuona popote pale. Kigezo kikubwa cha nchi kupaa kwenda juu basi ni uwezo wa kudidimiza nchi zingine. Kama ilivyo kigezo kikubwa cha mtu kuwa tajiri ni uwezo wake wa kutawala na kunyonya watu wengine. Hatuwezi kuishi kama tupo mbinguni, kufanya hivyo ni kujidanganya. Kwa sasa tupo duniani. Kanuni ya dunia ni kuwa ili uwe mshindi basi lazima ushinde wengine. Huwezi kuwa mshindi kwa kuishi maisha bila kuwashusha washindani wako. Sijawahi kuona jambo hilo, pamoja na kuwa nina umri mdogo.

Mhe. Rais, nafikiri mpaka naandika mambo haya, ni kuwa ninajua tunaouwezo wa kuzitawala nchi zingine kwa namna yoyote ile, kwa hila, njama, mabavu, hiyari, au kwa kutumia soko la giza. Nafikiri hii ndio ingekuwa njia ya lazima kwa nchi hii kuendelea.

Taifa la uchina, linatumikisha mataifa mengine kwa namna nyingi tuu, aidha kwa kutoa mikopo yenye riba ngumu, au kwa makubaliano ya kuendesha miradi mikubwa ambayo pesa yao itarudi kwa kuajiri watu wao kutoka china. Pia hutumia mbinu ya uwekezaji ambapo, huagiza vijana wao kuja Afrika kuanzia makampuni ya namna mbalimbali kisha huwapa mikopo, wakija huku huajiri vijana wetu ambao huitwa watumishi lakini kwa mishahara wanayolipwa sio watumishi bali WATUMWA. Ni aibu kwa nchi na taifa makini kuona vijana wake wanageuzwa watumwa na wageni katika nchi yao.

Mbinu hii pia huitumia Wahindi, ambao huanzisha makampuni yao tena wengine kwa kuchukua mikopo kwenye bank za ndani, kisha huajiri vijana wa taifa hili na serikali itasema vijana wamepewa ajira, lakini sio ajira bali wameingizwa utumwani ndani ya taifa lao wenyewe. Mishahara yao ni 100,000/= wengine 140,000/= wakizidi sana, 180,000/= kwa siku sita wakifanya kazi masaa 12, kwa kupokezana, wengine usiku wengine asubuhi. Kwa vyovyote vile iwavyo hakuna maisha mazuri kwa vijana na watu wake ikiwa watakuwa watumwa ndani ya nchi yao. Taifa haliwezi kujitawala ikiwa watu wake wametawaliwa, labda tuseme viongozi ndio wamejitawala ambao kimsingi hawafiki hata asilimia 1% ya watu wote.

Ili taifa lijitawale, lazima watu wake waweze kujitawala. Na dalili ya mtu anayejitawala ni uwezo wa kudai haki zake, na ili mtu aweze kudai haki zake basi ni lazima awe huru. Na ili mtu awe huru basi lazima aweze kujikimu na kuendesha maisha yake yaani asiwe masikini. Nchi haiwezi kujiendesha bila kuendesha nchi zingine. Taifa haliwezi kujiendesha ikiwa watu wake wanaendeshwa na wageni, au hawawezi kujiendesha. Pengine waite kujiendesha kwa kujidanganya.

Utulivu wa mataifa makubwa unatokana na uwezo wao wa kuvuruga mataifa mengine. Taifa lolote lile haliwezi kuwa tulivu kama lina uwezo mdogo waa kuvuruga utulivu wa nchi zingine. Jitihada na mikakati ni muhimu sana katika mambo haya.

Mhe. Rais, suala la maendeleo ya kijamii ni suala pana na nyeti sana. Lazima tuchukua jitihada madhubuti katika kuleta heshima ya taifa hili kijamii. Taifa haliwezi kusema limeendelea kwa kigezo cha ongezeko kubwa la wasomi wenye elimu yenye asili ya kigeni. Taifa haliwezi ujivunia wasomi wenye elimu za kigeni, kujivunia elimu ya kigeni ni kujivunia utumwa, ni kujivunia kutawaliwa kiakili na wageni. Inashangaza sana kuona vijana wakijivunia ma-degree huku wazee wakijivunia Uprofesa. Degree ya utumwa, na uprofesa wa utumwa. Mhe. Rais hushangai hizo degree na Phd bado hazina impact chanya ndani ya jamii yetu. Jibu ni kwa sababu, hakuna utumwa wenye impact chanya kwenye jamii.

Elimu ya kitumwa hutengeneza kizazi cha kitumwa. Ndio maana vijana wengi wamemaliza elimu zao na bado wanashindwa kukabiliana na mazingira. Mhe. Rais, unamkumbuka yule Mkurugenzi wa Morogoro ulivyomtumbua alivyolia na kugara gara, huku akikulilia wewe kama mungu wakati wewe ni binadamu kama yeye? Unamkumbuka? Yale ndio matokeo ya elimu ya kitumwa.

Huwezi kuwa mzalendo ilhali unaelimu na fikra za kigeni, popote pale sijawahi kuona. Niliwahi kuandika kuwa, ili tuondoe ujinga katika taifa letu lazima tujue ujinga huo tunaupeleka wapi. Wazungu walituletea ujinga wao, wakauita majina mbalimbali mengine ni elimu, dini, na vikoro koro vyao vyote ambavyo waliona havina msaada

Mhe. Rais, naomba nifupishe habari hii, huu ni wakati wa kutumikisha watu wa mataifa mengine, kwani kwa kufanya hivyo ndio uhakika wa kuiendeleza nchi upo kwa kiasi kikubwa.

Naomba niishie hapa,

Niwatakie watanzania wote kheri ya sikukuu za kumaliza mwaka

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dodoma
Kwahiyo una maanisha hata ikulu ya chamwino badala ya kujengwa na JKT wangejenga wachina, waarabu au wazungu? tutatumikisha watu wengine pale tunapokuwa hatuna ujuzi wa jambo husika lakini kama ujuzi tunao sio vibaya tukifanya wenyewe.
 
Bado! dogo Bado! Nilidhani unatoa mapendekezo kumbe unaandika historia ambayo tunaijua kuliko wewe! Andika kifanyike nini na siyo kuleta historia ya ulaya na dunia, ili iweje. KWani unadhani rais na washauri wake ktk serikali hawayajui hayo?

Ukipewa heko, likes, usidhani kuna lolote hapo!
 
Kijana wa miaka 26!

Kuna mambo mengi uliyoandika yanafikirisha, hata kama ni nadharia kuliko uhalisi wenyewe. Kwa mfano, ni huo hapo juu nilioku'quote'. Hujaeleza hayo mataifa mengine utawatumikisha vipi: utakwenda kuwafanya wawe makoloni kama wao walivyofanya mataifa mengine kuwa makoloni?
Kama kwa mfano huo ulioutoa una maana ya "ushirikiano na mataifa mengine", basi sema hivyo waziwazi, lakini sio "kuyatumikisha" inavyoeleweka hapa.

Pengine ungesoma historia ya China, ingekufungua mawazo kidogo na kujua kwamba wao walijifungia kwa muda mrefu sana, walipojifungua taifa lao likawa lipo tayari kupaa juu kama roketi kimaendeleo. Walipokuwa wamejifungia ("hawatumikishi wengine") walikuwa wakiweka miundo imara)

Nikiri, sikusoma bandiko lako refu lote, huenda kuna mambo kadhaa uliyoandika yanayoeleza undani wa nadharia hii uliyoweka hapa.

Inawezekana sana kukawa na tofauti kati ya uliyoandika na baadhi ya yale ninayoyadhania mimi kama chachu ya kuleta maendeleo ya nchi haraka.

Kwa ufupi niaminiyo mimi:
1. Maendeleo ya nchi ni 'process' ambayo haitokeii "ghafla bin vuuu". Ni mwendelezo na kuongezea kwa yale yaliyokwishafikiwa. Kwa mfano. Mtu hawezi sasa hivi akasema hatujapiga hatua katika kuendeleza elimu yetu ukilinganisha na wakati Mwalimu Nyerere anatwaa nchi toka kwa wakoloni. Ndiyo, elimu yetu imekuwa ni ya kusuasua katika sehemu mbalimbali, lakini mtu hawezi kusema kwamba hatujaendelea. Kinachotakiwa hapa sasa hivi katika eneo hili ni kuifanya iwe bora zaidi na kuwaandaa wasomi wetu katika nyanja mbalimbali kuwa na uwezo wa kuligeuza kwa kasi zaidi kimaendeleo taifa letu. Maana yangu ni kwamba, hatuwezi kuwa na kasi (speed) au (rate) ile ile tuliyokuwa nayo miaka ya sitini au sabini. "Rate" yetu sasa inatakiwa kuwa ya juu zaidi katika kuleta maendeleo.

Na ili nieleweke vizuri juu ya jambo hili; jaribu kufikiria baadhi ya nchi ambazo siku nyingi sana zimekuwepo huru kabisa na hata kihistoria zinafahamika kuwa ni mataifa kamili: Turkey (uturuki), kwa mfano, ni muda huu wa karibuni ndio wameanza kuonekana kupiga hatua za kuwa nchi iliyoendelea, baada ya miongo na miongo mingi ya taifa hilo kuwepo kimuundo kama taifa. Na Misri je? Unaijua nchi inayoitwa Haiti? Inawezekana kabisa kwa hali waliyonayo sasa taifa hilo, ikawachukua miaka mingi sana kubadili hali zao kimaisha.
Unaweza ukasema Tanzania haiwezi kamwe kuwa kama Haiti?

2. Maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe, sio viongozi. Viongozi ni kusaidia kuweka mipango mizuri na kusimamia utekelezaji wake tu wa maendeleo wanayoyaleta wananchi wenyewe. Kwa hiyo, Rais Magufuli hawezi kamwe kuiletea Tanzania maendeleo, hata kama angeanzisha makambi ya kuwatumikisha wananci wake.

3. Nci zetu hizi kamwe hazitakiwi kwenda kuvumbua "tairi" upya. Tairi tayari lipo linalofanya kazi vizuri. Lengo letu sasa ni kujua jinsi ya kuyatumia haya "matairi" ya kuleta maendeleo vizuri. Na hili ndilo jukumu kubwa ambalo wasomi wetu wangelikazia ili kuwafikishia wananchi nyenzo hizi za kuharakisha maendeleo yao.
Wakulima wetu wapate ushauri wa kila aina ili wazalishe mazao kwa wingi na kuhakikisha mavuno yao hayaharibiwi kabla ya kufikishwa sokoni.
Tunanunua kila aina ya dawa toka nje, miaka zaidi ya 60 baada ya kupata uhuru wetu. Tunasomesha kila mwaka wataalam wetu katika nyanja hii ya kutengeneza madawa, lakini kama taifa hawa watu hatuwapi nyenzo za kuwawezesha kufanya kazi yao ya kutengeneza madawa aina mbali mbali, badala yake hawa watu tuliowasomesha kwa gharama kubwa wanaishia kwenda kuwa "wauza duka"! Huu ni utuzizi mbaya wa raslimali zetu. Na huu ni mfano mmoja tu katika mingi! Wengi wa hawa watu sasa mawazo yao ni kuingia kwenye siasa, kama akina Magufuli, badala ya kuvumbua na kutengeneza mafuta yanayozuia kutu yatokanayo na zao letu la korosho! Sasa, si angalao Magufuli mwenyewe angewekea mkazo baada ya kuingia kwenye siasa, ili watu (wasomi) wa aina yake wapewe fursa zaidi kuitumia elimu yao katika maeneo mbalimbali ili taifa lifaidike na utaalam wao? Badala yake, tunaona maprofesa ndio wanaojazwa kwenye vyeo vya kuteuliwa, badala ya kufanya kazi muhimu la kuligeuza taifa hili katika nyanja walizosomea!

Kama taifa, kwa nini viongozi wetu hawa wasingekazia tuandae mfumo mzima wa kuwa na "Chemical industry" yetu wenyewe - mali ghafi ya kutosha ipo ya kufanya hivyo Nchi kama Israel, Taiwan na nyinginezo wameweza, kwa nini sisi tusiweze..., ni umaskini wetu tu wa kifikra ndio unaotukwamisha.
Hatuwezi kama taifa kukubali kutojiandaa kwa mabadiliko haya makubwa yanayoletwa na ''technology" sehemu mbalimbali duniani. Ni wajibu wa viongozi wetu kuweka mipango sahihi na kuhakikisha kwamba hatupitwi na fursa kama hii itakayowezesha watu wetu kuwa wavumbuzi (innovators).
Kwa hiyo unaposikia nchi zinatofautiana, tofauti hizi zinatokana na maono ya viongozi wa nchi hizo.

Ngoja nikuache utafune haya kwanza. Lakini la muhimu, pengine kuliko mengine yote--- sahau kabisa swala la Magufuli kukuletea maendeleo au kuiletea maendeleo Tanzania. Hili ni jukumu la waTanzania wenyewe.
Jee mkuu umewahi kupitia National blue print 2015 to 2025? Ukipata nafasi pitia itakusaidia kujua tuu tunaelekea wapi .

Na juu ya kelele nyingi za sisi raia lakini mkuu anatembea kwenye blue print ya nchi hatua kwa hatua.

Kuna taabu ya kuvumilia kufika tunako kwenda lakini kama yalivyo pangwa ndio yatafuata moja baada ya lingine, mwisho wetu utakuwa mzuri, sasa hapa ni kwa wanao amini.
 
Asiyefanya kazi na asile;

Nadhani hujaelewa huo mstari wa Biblia.
Alipokuwa na makutano, ilikuwa jioni sana Yesu aliwaambia mitume wapeni ninyi chakula, mitume wakamwambia hatuna chakula Cha kututosha sisi na watu wote Hawa maana tunavisamaki vichache na mikate.

Yesu akawaambia leteni hapa.
Akavibari akawapa wavigawe makutano wote walikula na mabaki vikapu12 vikusanywa.

HAPO NAPO UNAELEWA NINI?
 
Bado! dogo Bado! Nilidhani unatoa mapendekezo kumbe unaandika historia ambayo tunaijua kuliko wewe! Andika kifanyike nini na siyo kuleta historia ya ulaya na dunia, ili iweje. KWani unadhani rais na washauri wake ktk serikali hawayajui hayo?

Ukipewa heko, likes, usidhani kuna lolote hapo!

Sijakataa kwamba mimi ni dogo, haya sasa nambie wewe unayejua historia, ni wapi uliwahi kueleza hata hicho kidogo ukijuacho kwenye jamii?
Je kwa vile wewe unajua historia unafikiri kila mtu anaijua au amesoma historia hivyo hakuna haja ya kuieleza?

Sijaandika ili nipewe like au watu wakoment, nimeandika watu wasome, watakaopenda wapende, watakaochukia wachukie, watakaojifunnza wajifunze, watakaopuuzia wapuuzie.

Ninaandika makala nyingi, zipo ambazo hazijasowa kabisa wala kupewa like humu humu Jf, So ni mpuuzi pekee yake anayeandika ili apewe like au apewe heko.

Nafikiri ungenijua kwanza kabla ya kuandika upumbavu kwa kisingizio cha kutumua Fake ID
 
Eeenh, wewe huoni hata kaweka 'contact information' yake hapo? Huyu akishateuliwa sehemu fulani sahau kabisa ndoto alizoweka JF. Akina Kala Maganda na Popole hujawahi kuwasikia?

Siwezi kuteuliwa Mkuu,
usifikiri watu wote wapo sawa, kama ningekuwa nataka kuteuliwa ningekuwa nimeshajiunga na chama fulani na kukipigia chapuo. Na ofa hizo sio kwamba hazipo..
 
Unabisha kitu ambacho kipo wazi kabisa ,wachina wanafanya kaz sana tena kwa juhud lkn kaz izo pia mojawapo kutumia nchi nyngne ,mfano apa africa wachina wapo karbu kila sehem na wapo karbu kila sekta

Huyo anaongea mambo kama hajasoma mada.

Nimeandika kwamba hatuwezi kutegemea nguvu kazi ya ndani TUU au PEKEE, Sasa sijui yeye anaelewaje kwenye ubongo wake
 
Umetumia muda mwiiingi kuandika lakini msingi wa ushauri wako unajipinga wenyewe!!

Lazima mtu anapotaka kujitegemea ni sharti afanye kazi na baada ya zile kazi kuleta matunda, mwenyewe tu bila kuambiwa na mtu ataweka watu wa kusaidia ili azidi kuimarika na kujiletea utajiri

Kwa akili nyingine ambayo nilitaka nielewe ingawa hata hukikisema, ni Tanzania na Jeshi lake waende Tu kwenye ki nchi tukakikalie na kuchukua Mali huko ili tutajirike kama zifanyavyo nchi zenye nguvu
Mkuu ulsoma kweli andiko lote
 
Mkuu nchi haiongozwi kwa historia unazozitaja hapa sio kila kitu ni cha kuiga hamasisha watu kujitambua na kufanya kazi sio swala la kuwa tegemezi na fikra za kitumwa. Unaweza kuwa na ushauri mzuri lakini uwasilishaji ukawa unatia mashaka. Sitakujibu tena sababu umeshasema wewe ni mtu wa fasihi.

Mkuu, hakuna kisichoongozwa na Historia sijui kama unajua unachokisema.

Nenda Hospitali ukiwa unaumwa, Daktari akiwa anaku-diagnosis lazima atake Patient history, historia ya mgonjwa ambapo atakuuliza umeanza kuumwa lini, unajisikia, usiku unakuwaje, hiyo ndio History. History inahusu mambo yaliyopita, yaliyopo na yajayo.

Njoo kwenye sheria, kwenye hukumu mahakimu huweza kutumia hukumu zilizopita kama Case study ya hukumu iliyopo.

Taifa lolote lile linaongozwa na Historia, huwezi kuwa Kiongozi mkubwa kama watu hawajui historia yako, lazima waangalia asili yako, Rekodi yako, maadili yako,, na hapa vinaangaliwa vitu vya nyuma.

Katika mipango na mikakati ya nchi lazima wawepo wataalamu wa Historia kwa kila kitu kinachoenda kufanyika.

Mkuu sio dhamira yangu kugombana, ni katika hali ya kueleweshana.

Kumbuka, mimi ni moja ya wanafunzi wasiopenda kupelekwa pelekwa, hivyo ukiona nakubishia ujue bado naona kuna jambo hujaeleza sawia
 
Herieli kakojoe ukalale. Kwanza utambue mjenga nchi ni mwananchi. Pili umasikini haupelekwi sehemu bali unatokomezwa. Tatu sijamalizia kusoma wosia wako
 
:D:D:D

Mkuu nikakojoe nchi kavu au baharini?

Sijakataa nchi inajengwa na wananchi ila nimependekeza mawazo yangu kwenu
 
Ulianza kutafakari ukiwa na umri wa miaka 16 na sasa una umri wa miaka 26 hongera Sana kuanza utafiti ukiwa kinda nadhani ukiwana umri wa miaka 36 utakuwa tegemeo nchini mwetu keep on
 
Jee mkuu umewahi kupitia National blue print 2015 to 2025? Ukipata nafasi pitia itakusaidia kujua tuu tunaelekea wapi .

Na juu ya kelele nyingi za sisi raia lakini mkuu anatembea kwenye blue print ya nchi hatua kwa hatua.

Kuna taabu ya kuvumilia kufika tunako kwenda lakini kama yalivyo pangwa ndio yatafuata moja baada ya lingine, mwisho wetu utakuwa mzuri, sasa hapa ni kwa wanao amini.
Umesema kweli:"sasa hapa ni kwa wanaoamini"; na hapo hapo umekwishabainisha kuhusu "kelele nyingi za sisi raia"! kama sio maajabu hayo sijui niyaite kitu gani.

Huko unakokuita "mkuu anatembea kwenye 'blue print' ya hatua kwa hatua", usidhani 'blue print' hiyo ndiyo ya kwanza kwenye uhai wa taifa letu.

Nikukumbushe tu kama hukunisoma na kunielewa nilichoandika hapo juu. Huyo unayemwita "mkuu" hana uwezo kabisa wa kuwaletea maendeleo waTanzania. Ni waTanzania wenyewe ndio watakaojiletea maendeleo.

Lakini kama ulivyoandika hapo juu kuhusu "kelele" za hao wananchi, na wewe pamoja na huyo "mkuu" bado mnadhani hao wapiga kelele ni vichaa wasiotaka kuletewa maendeleo?

Wewe ni 'Gerald M Maghembe,'; pamoja na kwamba sijajibishana nawe kwa kina ndani ya ukumbi huu wa JF, maoni yako sio mageni kwangu. Kwa hiyo ninafahamu unakotokea kwa maoni haya. Ni maoni yaliyofungwa, hayako huru. Sasa hapa sijui kama utanielewa ninachoandika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom