Rais Magufuli: Nina deni zito

kitonsa

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
1,211
2,636
Rais Magufuli leo katika sherehe ya kupewa hati ya ushindi wa uraisi, mjini Dodoma amesema ana deni zito la kuwalipa Watanzania.

Anaendelea kusema vitu alivyoahidi kwenye kampeni ni nyingi hivyo ana kazi ngumu ya kuvitekeleza.

Pia Mwenyekiti wa Tume hapo kabla aliongea mafanikio ya tume yalio tekeleza katika kipindi cha uchaguzi, ila Mwenyekiti wa Tume ameshindwa kuongelea changamoto za tume kama:

1. Shutuma za upinzani kuwa kura zilipigwa nje ya vituo kisha kuingizwa kwenye vituo
2. Mawakala wa upinzani kunywimwa barua za utambulisho
3 . Mawakala kutolewa kwa nguvu kipindi cha kuhesabu kura
4. Vyombo vya habari kutangaza mgombea mmoja tu wakati wa kampeni
5. Matumizi mabaya ya vyomba vya dola kwa vyama vya upinzani
6. Kutumia vyombo vya umma kwenya shughuli za uchaguzi

Kweli Magufuli ana deni zito
 
Deni kubwa zaidi ni kurejesha umoja na ustawi wa taifa letu.
 
Deni kubwa kufufua uchumi na kujenga upya umoja wa kitaifa.....issue kubwa sio suala nguvu ni akili zaidi ...sasa sijui kama ataweza ndani muda mfupi maana misingi uchumi ilijengwa miaka 20 amebomoa miaka 5 hawezi jenga miaka 5......au ndio anajipanga kumtengeneza Zuchu kuwa billionaire?? Muda utaongea
 
Sherehe za Wachaga kukabidhi nafasi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) kwa Wamakonde zinafanyika lini?
 
Back
Top Bottom