Mleta mada tambua kwamba mambo anayofanya Kagame Rwanda hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba. Aliiweka katiba pembeni na akajikita katika kutengeneza mazingira ya ukuzaji wa uchumi. Na amefanikiwa huku wanyarwanda wakisahau kuwa ipo katiba. Usikariri maisha ukiamini kuwa eti tatizo la nchi lipo kwenye mabadiliko ya katiba peke yake. Sio kweli, economic goals ambazo uongozi wa juu wa serikali ya Rwanda ulijiwekea hazikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na katiba.
Wengi hutumia kigezo cha kutaka kuwashughulikia viongozi wastaafu, kwa sababu ya mambo yalivyoharibika, hivyo huamini kuwa katiba ikibadilishwa ndio lengo hilo litakapofanikiwa.
Zipo nchi zenye katiba nzuri lakini dhuluma na ufisadi ndio utaratibu wao wa maisha. Zipo nchi ambazo zina katibe mbovu lakini maisha yao yanakwenda vizuri tu. JPM analo lengo la kubadilisha hali nzima ya maisha, uwepo wa katiba yetu kama ilivyo hauwezi kuwa kikwazo cha utekelezaji wa yote aliyoyaahidi kwa wananchi.
Ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha mishahara hewa haiendelei kulipwa, agizo kama hilo linao uhusiano gani na mabadiliko ya katiba. Anapambana na wauzaji madawa ya kulevya na mafisadi, je hatua hiyo inao uhusiano na mabadiliko ya katiba.
Nchi hii inahitaji committed leader, hayo mambo ya katiba na mabadiliko yanaweza kuwa na umuhimu wake lakini yasichukuliwe kana kwamba ndio muarobaini wa matatizo mengi tuliyonayo.