mlimilwa
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,078
- 3,142
atakaezembea kwenye nafasiyake namfukuza malamoja.Rais Magufuli anasifiwa na kuliliwa kwa kasi aliyoanza nayo. Anatazamwa na watanzania kama mwenye nia ya wazi ya kupambana na rushwa,ufisadi na uzembe Serikalini. Hata hotuba yake Bungeni ilimchora kama bora na mwenye dhamira. Mchezo kamili bado haujaanza. Yote hayo yalikuwa ni sawa na timu kuingia uwanjani na kupasha misuli. Mpira kamili haujaanza.Mpira utaanza pale watakapoteuliwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri. Hawa watakuwa ndiyo wakuu wa Wizara zao. Watakuwa ndiyo wanaoongoza na kuelekeza Wizara. Rais itampasa kuwaacha Mawaziri kuenjoy madaraka yao.Rais hataweza,na haipendezi kutokea,kufuatili jambo au mambo fulani moja kwa moja kwakuwa kutakuwa na Waziri husika. Kinachotokea sasa ni sawa na Mwalimu wa zamu kusimamia kazi zote shuleni bila uwepo wa viranja wa zamu.Mkwamo wa Rais Magufuli,kusipokuwa na umakini kwenye uteuzi,utaanzia litakapopatikana Baraza la Mawaziri. Na Rais hataweza kubadilibadili kila mara!Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam