Good People
JF-Expert Member
- Aug 6, 2016
- 945
- 1,819
Wakuu Nilisikitishwa sana mwaka jana TRA walitoa Nafasi wakawa wanataka watu wasiozidi Umri wa Miaka 25.
Kutokana na System ya Elimu ya Bongo watu wengi wanamaliza wakiwa na miaka 24 na Kuendelea na Tatizo la ajira kufika miaka 27 hajapata kazi ni Kawaida.
So anafika miaka 27 anakua hana vigezo vya Kupata kazi (yaani anakua Mstaafu kwa Lugha nyingine) hili linaumiza sana ndo maana siku hizi nikiona kamba ipo sehemu naitamani sana.
Kinachoshangaza JKT Wanachukua hadi miaka 31. na Wote tunajua Jeshi linahitaji watu wenye Nguvu Kinachonishangaza Sehemu Kama TRA na PCCB wanataka wasiozidi Umri wa miaka 25.
Nimeongea Kwa Uchungu Baada ya Kuona Nafasi Za Kazi Leo zilizotangazwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) Likitaka Vijana wasiozidi miaka 25.
So siku hizi Ukifika miaka 26 Unakua Mstaafu? Ndo maana nimeamua Kujiajiri baada ya Kuzeeshwa na Umri wangu wa miaka 25.
Rais Magufuli Naomba Usikie Kilio Chetu wakurugenzi wanapotaka kuingiza ndugu zao ndo wanatumia Vigezo kama Hivi Mtu aliye na Umri wa miaka 26 hajazeeka kiasi hicho Tabia hii ikiota Mizizi ipo siku Taasis zitataka watu wenye Umri wa miaka 23.
Magufuli Tusikilize Wananchi wa Tanzania.