Rais Magufuli na Lissu wakutanishwe

Rais Magufuli na Lissu wakutanishwe

No, hii Ni roho ya visasi tu
Watanzania tusiipe nafasi
Umesahau kauli za huyo Mzungu wako, au? Alisema uchaguzi huu ni "Make or break!" "Patachibika!" "Patawaka moto!" "Hapatatosha!" "Hawatatuua wote, maana hawana jeshi kubwa kama sisi!" "Lazima Magufuli, Afande Sirro na Mkuu wa TISS waishie ICC!" Pls, usijifanye eti humjui huyo mchonganishi!!!
 
pureman2 umeanzisha mjadala murua kabisa wa kizalendo hujulikani upo upande upi,umesimama katikati ya maslahi mapana ya taifa,Hao ni wanasiasa wawili wanaosigana,na wote wana wafuasi wengi wasioelewa maslahi mapana ya taifa,ama wamejitoa ufahamu ili kufanya upotoshaji kwa ajili ya maslahi yao binafsi,pengine wanatumikia ajira zao, ndoyo maana wanapinga na kubeza maridhiano.Hii nchi si ya wawili hao wala kikundi fulani,nchi ni ya watanzania katika ujumla wao.Maridhiano ni haiba njema kisiasa
 
Tuache kufanya kazi tukae vikao na wasiokubali kushindwa? Jamani jamani jamani, uchaguzi umeisha, maisha lazima yaendelee. Viongozi wa upinzani tafuteni mbinu nzuri ya kudeal na umafia wa CCM. Mmeingia kwenye uchaguzi na katiba ile ile na tume ile ile iliowanyoosha siku zote, mlikua mnategemea nini?

Watanzania wa kawaida hawana hata mawazo na ubunge wa Zitto, Sugu au Mdee. Wako masokoni, viwandani, minadani, kwenye maofisi ya umma wakipambania ugali wao na watoto wao, watawaza vipi kuhusu ugali wa Mbowe na Esther Matiko.

Wapinzani wa Tanzania hamko serious na huenda mnautreat upinzani wenu kama solely source of income.
 
Rais akutanishwe na kibaraka wa mabeberu ili iweje? Acheni kumtafutia promo za kitoto hapa. Amekimbia, amejipanga kuichafua nchi yetu kwa kutumiwa na mabeberu wanotaka kuja kuchuma. Hana uzalendo wowote kwa nchi yetu. Yeye aishi huko huko, hatumhitaji.
Tutaijenga upya CHADEMA aliyoibomoa. Let him go to hell
Nyie ndiyo watetea tumbo, amawataja hapo juu, na akasema furaha yenu ni sawa na maua mazuri asubuhi maana yanakuwa yamechanua vizuriiii, ila ikifika jioni yamenyauka yoooteee.
 
Kwanza wazungu wamemtolea nje hoja za kuiwekea vikwazo tanzania, raia wa marekani na ulaya kwa sasa tanzania is their second home hawawezi kukubali ku-distabilize nchi hii yene asali na maziwa, nchi ambayo kwa utalii ni bora duniani, rushwa imepungua hadi kuwa nchi ya 26 out of 173 countires in the world. Sera za uwekezaji zinatoa usawa kwa wote, wawekezaji wanalindwa. Tanzania ni sehemu salama zaidi duniani kwa sasa hasa kwa ugonjwa wa corona na pia kiulinzi, hakuna mauaji ya wazungu wala kubaguliwa.


Kifupi lissu amegundua kuwa kuwa nje ya mfumo wa kufanya maamuzi makubwa kwa nchi kama bunge chadema wanajifuta wenyewe, hawatakuwa tofauti na chauma kwani platform ya kufanya siasa hawatakuwa nayo maana bungeni hawapo. Yeye atulize mshono jpm ana huruma sana anaweza kuwasikiliza lakini kizabina zabina cha kuchafua nchi wakome kabisa.

Jpm atawasikiliza kama watamtambua kuwa rais wa nchi na amiri jeshi mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama na ni mwajiri namba moja serikalini
Thanks so VERY much!
 
Ningeelewa kana mtu angependekeza Rais akutane na viongozi wa vyama vya upinzani walioko nyumbani, Mbowe, Zitto, nk; lakini siyo Lissu. Yeye aachwe atimize nia yake aliyonayo kwa taifa let, then tutaona kama atatia mguu Tanzania tena.
Mnaweka majina makubwa kwenye Avator zenu, huku nyie wenyewe ni mapimbi na wapumbavu wakubwa....
 
Tuache kufanya kazi tukae vikao na wasiokubali kushindwa? Jamani jamani jamani, uchaguzi umeisha, maisha lazima yaendelee. Viongozi wa upinzani tafuteni mbinu nzuri ya kudeal na umafia wa CCM. Mmeingia kwenye uchaguzi na katiba ile ile na tume ile ile iliowanyoosha siku zote, mlikua mnategemea nini?

Watanzania wa kawaida hawana hata mawazo na ubunge wa Zitto, Sugu au Mdee. Wako masokoni, viwandani, minadani, kwenye maofisi ya umma wakipambania ugali wao na watoto wao, watawaza vipi kuhusu ugali wa Mbowe na Esther Matiko.

Wapinzani wa Tanzania hamko serious na huenda mnautreat upinzani wenu kama solely source of income.
Hasa ukizingatia ruzuku ile ya 300 milioni hajulikani ilipo na chama hakina hata sura. Walizoea siasa za mkumbo, enzi hizi za JPM hizo mambo ni zilipendwa.
 
Marekebisho namba 4 badala ya Makuu weka Mkuu.
 
Ungetusaidia sana iwapo ungeanza kwa kufafanua neno MPASUKO. Baada ya hapo utueleweshe huo MPASUKO uko wapi? Maana Uchaguzi Umekwisha, maisha yanaendelea kama kawaida na intact tumeshajisahaulia Uchaguzi maana tumeshampata Rais Magufuli chaguo la wengi.

Queen Esther
Badala wajikusanye kwa ile 2025, wanagwayagwaya mpaka watabung'aa tena uchaguzi mwingine huo.
 
Huwezi kumdanganya mtu wewe. Huyo kibaraka ni sly pretender na mzushi mwanzo mwisho. Hawezi hata kulionea huruma taifa lake anachotaka ni watu waandamane, machafuko yatokee, watu wafe ili ajizolee pointi za kisiasa. Huo ni unafiki usio na kiwango. Unasema anaipenda nchi yake??? Usiwe mwepesi kusahau kiasi hicho!
No matter awe kibaraka or not, kinachotakiwa ni maridhiano,maridhiano sasa itakuwa ndiyo wimbo,utaimbwa na wazalendo wapenda amani na maendeleo.Ishu ya maandamano si hulka ya watanzania, hata uitishe maandamano ya amani au kupongeza hakuna atakayejitokeza labda kama kuna posho au uponi waandamanaji watapatikana na kusiwepo vitisho.Ki ukweli wanasiasa hawa wawili wakutanishwe kwa maridhiano nchi ipate heshima,siyo mpaka madhara makubwa yatokee ndiyo wapatanishwe ni aibu kwa taifa linalojinasbisha ni kisiwa cha amani.
 
Mtemi ati akutane na nani? hebu acheni utani.
 
No matter awe kibaraka or not, kinachotakiwa ni maridhiano,maridhiano sasa itakuwa ndiyo wimbo,utaimbwa na wazalendo wapenda amani na maendeleo.Ishu ya maandamano si hulka ya watanzania,hata uitishe maandamano ya amani au kupongeza hakuna atakayejitokeza labda kama kuna posho au uponi waandamanaji watapatikana na kusiwepo vitisho.Ki ukweli wanasiasa hawa wawili wakutanishwe kwa maridhiano nchi ipate heshima,siyo mpaka madhara makubwa yatokee ndiyo wapatanishwe ni aibu kwa taifa linalojinasbisha ni kisiwa cha amani.
Kinachotakiwa jamaa akiri tu kwamba mdomo umemponza, hata akiwa hukohuko, kila Mtanzania atamwelewa kabisa.
 
Tunaweza kukataa na kupinga Ila dalili zote ziko bayana Taifa limemegeka kisiasa, kihisia, kimitazamo, na kivitendo.

Kuna roho ya ubinafsi na majivuno inazidi kusimika mizizi katika taifa hili. Kuna wanojiona ni bora na wanastahili vyote, na wengine wanajiona kuchukiwa, kutotambulika, kutokuwa na haki hata ya kuheshimiwa mitazamo yao.

Kilichotufikisha hapa hakijaanza leo wala jana. Tunachokishuudia ni matokeo ya roho iliyopaliliwa na kunyeshewa maji kwa muda Sasa. Na kadri tunavyochelewa kuchukua hatua hali itakua mbaya Sana.

Siasa zetu zimekua chanzo Cha utengano huu. Sio kwetu tu siasa imekua chanzo Cha anguko la umoja wa kitaifa bali duniani kote siasa ugawa watu. Hili utokea kwa kuwa siasa pasina shaka ni ulaji na mamlaka. Wahenga husema palipo na ulaji hapakosi fitina, Ila ni wajibu wetu kuonyesha ustaarabu na utu.

Wazee wako kimya, watumishi wa Mungu tayari wamekubali ku take side na kuendeleza mpasuko huu. Wasomi wamekubali kubaki neutral. Wengine wamechagua kuwa kimyaa kabisaa ili kuzipa amani fake familia zao na kujihakikishia mkate mezani. Kifupi njaa na uchu wa madaraka umefubaza kalamu zao na kuamua kuisariti Taifa hili.

Nani anaweza kututoa kwenye janga hili?

Bila kupepesa macho JPM na LISSU wanaweza kulisahidia Taifa hili.

JPM- unazo nyenzo, unawajibika kikatiba, unawajibika kisiasa, na unawajibika kiimani kuongoza juhudi za kulijenga taifa hili na kuziba mpasuko. Kuchukua wajibu huu sio udhaifu na kujishusha Ila ni kuonyesha njia na kuwajibika. Utakumbukwa zaidi ukilifanikisha ili kuliko kuamua kukaa kimyaa. Heri wapatanishi maana wataitwa wana wa Mungu.

LISSU- Kama mwanasiasa unawajibika kikatiba kuilinda amani ya taifa hili. Unawajibika kiimani kusamehe na kuachilia. Unawajibika kiraia kutii na kukubali kunyenyekea mamlaka. Utakumbukwa zaidi kwa kuongoza maridhiano ya kitaifa kuliko kufanikisha mashindano .

Kwa wanaowazunguka wawili hawa, mnao wajibu wa kutuliza majeraha, kuponya nafsi zao, na kusisitiza malidhiano, na sio kuwajaza sifa, hasira na viburi.

Msione kwa kuwa mnafaidika leo kwa kushabikia umwamba huu mkaona haya ndo maisha. Hakika hiyo itakua dhambi kubwa sana mbele za Mungu na Jamii ya watanzania.

Tunapenda kuona umoja na mshikamano wa taifa hili kuliko uhasama na maumivu tunayoyashuudia leo katika kona nyingi za taifa hili.

Mwisho wa waraka huu, nitoe rai kwa wanajeshi wanobeba silaha kwa jina la Tanzania kamwe mtusaidie kurejesha tumaini na heshima ya taifa hili. Tulisifiwa na mataifa mengi duniani coz jeshi letu liliheshimu uhai wa raia zake , na liliwalinda kwa adui awaye yote. Ila leo ni haibu kuona raia zetu wanauawa na wanajeshi wetu na maafisa usalama. Tafadhari mjizuie, mtangulize weledi na utu na muwalinde raia wa taifa hili bila upendeleo.

Nashusha kalamu yangu chini. Nimetimiza wajibu wangu na ninaomba record iwekwe bayana.

Heri mpatanishi maana ataitwa mwana wa Mungu.

Ainone:

1: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jonh Pombe Magufuli

2: Mh. Tundu Antipas Lissu

3: Marais wastaafu

4: Wakuu wa majeshi ya Tanzania

5: Viongozi wa vyama vya siasa

6: Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mchawi kukaa na malaika kipenzi wa watanzania inawezekana kweli? Yeye alishajijuwa kuwa ni msaliti ndiyo maana kakimbia nchi.
 
Napenda sana siasa za upinzani wenye hoja ila upinzani unaopinga maendeleo na kukejili maendeleo kila kukicha nasema hapana narudia tena hapana.

Tulionya humu mara kadhaa kwa spidi ya JPM inabidi wapinzani wabadili mbinu za kumchallenge kama kweli wanataka kuendelee kusikika lakini wao hawakusikia. Wakaendelea na mbinu zile zile walizozitumia enzi za utawala wa JK. Bahati mbay kipindi hiki wakajikuta wanaishia kuzusha mara kuna upotevu wa 1.5 tril, na kutengeneza matukio madogo madogo ya kutafuta huruma kwa wananchi kitu ambacho wananchi wengi waligundua ni uzushi.

Taifa ambalo wananchi wake bado wanashida kubwa ya maji eti wapinzani wanadai democracia, Taifa ambalo wanananchi wake zaidi ya asilimia 80 ni wakulima wanatumia zana duni za kilimo ikiwemo pembejeo eti wapinzani agenda yao kubwa ni democracia, taifa ambalo mpaka sasa kuna shule ambazo hazina milango sakafu wala madirisha achilia mbali umeme na miundombinu ya kujifunzia eti wapinzani agenda yao kuu ni democracia.

Wakati JPM akipambana kuimarisha maisha ya raia kwa siku zijazo kwa kuimarisha sekta ya miundombinu, ikiwemo ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli SGR, ukarabati wa reli MGR, ujenzi wa bwawa kubwa la la umeme la Nyerere 2115Mw, ujenzi wa daraja la Tanzanite, ujenzi wa dara refu kuliko yote EA daraja la Busisi nk, badala ya wapinzani kumuunga. mkono au hata kutoa ushauri wao wanapinga na kukejeli kana kwamba kinachofanyika hakina maana.

Kifupi wapinzani wa Tanzania hasa wa awamu hii ya tano wameshindwa kabisa kutoa mawazo mbadala wametumia mda mwingi kukosoa, kukejeli, kutukana na kutaka kukwamisha juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maamendeleo, ni vyema wakatafakari na wakaja na sura ya kizalendo sio kupandikiza chuki miongoni mwa raia ndani ya taifa hili, Namna viongozi wa upinzani walivyounzungumzia muuungano wetu ni jambi ambalo halikubaliki kabisa na sio jambo la kuzungumzwa na chama kilichojiandaa kuchukua dola.

Tutajie uzi uliowahi kuchangia kuwa unaukubali upinzani. Naona umetaja mambo mengi ili kuhalalisha Utetezi wako hasi dhidi ya upinzani. Inaonyesha huna mtazamo wako binafsi, bali utetezi wako unatokana na propaganda mfu za kiccm ndio maana umefikia hilo hitimisho. Hata mimi sioni kwanini wakutanishwe watu hawa maana kila mtu anaamini cha kwake. Tusubiri tu muda muafaka hayo yatatokea.
 
Mbona bila maandamano yoyote mmeuwa watu kule Pemba, Tunduma, Tarime, Rorya, nk?!!!
Nani alikuwa anadai hawatawaua wote? Patachimbika mwaka huu??? Mchochezi wa ghasia, fujo, machafuko na mauaji nani??? Usijitoe upofu, sawa?
 
Back
Top Bottom