Napenda sana siasa za upinzani wenye hoja ila upinzani unaopinga maendeleo na kukejili maendeleo kila kukicha nasema hapana narudia tena hapana.
Tulionya humu mara kadhaa kwa spidi ya JPM inabidi wapinzani wabadili mbinu za kumchallenge kama kweli wanataka kuendelee kusikika lakini wao hawakusikia. Wakaendelea na mbinu zile zile walizozitumia enzi za utawala wa JK. Bahati mbay kipindi hiki wakajikuta wanaishia kuzusha mara kuna upotevu wa 1.5 tril, na kutengeneza matukio madogo madogo ya kutafuta huruma kwa wananchi kitu ambacho wananchi wengi waligundua ni uzushi.
Taifa ambalo wananchi wake bado wanashida kubwa ya maji eti wapinzani wanadai democracia, Taifa ambalo wanananchi wake zaidi ya asilimia 80 ni wakulima wanatumia zana duni za kilimo ikiwemo pembejeo eti wapinzani agenda yao kubwa ni democracia, taifa ambalo mpaka sasa kuna shule ambazo hazina milango sakafu wala madirisha achilia mbali umeme na miundombinu ya kujifunzia eti wapinzani agenda yao kuu ni democracia.
Wakati JPM akipambana kuimarisha maisha ya raia kwa siku zijazo kwa kuimarisha sekta ya miundombinu, ikiwemo ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli SGR, ukarabati wa reli MGR, ujenzi wa bwawa kubwa la la umeme la Nyerere 2115Mw, ujenzi wa daraja la Tanzanite, ujenzi wa dara refu kuliko yote EA daraja la Busisi nk, badala ya wapinzani kumuunga. mkono au hata kutoa ushauri wao wanapinga na kukejeli kana kwamba kinachofanyika hakina maana.
Kifupi wapinzani wa Tanzania hasa wa awamu hii ya tano wameshindwa kabisa kutoa mawazo mbadala wametumia mda mwingi kukosoa, kukejeli, kutukana na kutaka kukwamisha juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maamendeleo, ni vyema wakatafakari na wakaja na sura ya kizalendo sio kupandikiza chuki miongoni mwa raia ndani ya taifa hili, Namna viongozi wa upinzani walivyounzungumzia muuungano wetu ni jambi ambalo halikubaliki kabisa na sio jambo la kuzungumzwa na chama kilichojiandaa kuchukua dola.