Rais Magufuli na Lissu wakutanishwe

Rais Magufuli na Lissu wakutanishwe

Rais akutanishwe na kibaraka wa mabeberu ili iweje? Acheni kumtafutia promo za kitoto hapa. Amekimbia, amejipanga kuichafua nchi yetu kwa kutumiwa na mabeberu wanotaka kuja kuchuma. Hana uzalendo wowote kwa nchi yetu. Yeye aishi huko huko, hatumhitaji.
Tutaijenga upya CHADEMA aliyoibomoa. Let him go to hell
Chokooooo
 
Tunaweza kukataa na kupinga Ila dalili zote ziko bayana Taifa limemegeka kisiasa, kihisia, kimitazamo, na kivitendo.

Kuna roho ya ubinafsi na majivuno inazidi kusimika mizizi katika taifa hili. Kuna wanojiona ni bora na wanastahili vyote, na wengine wanajiona kuchukiwa, kutotambulika, kutokuwa na haki hata ya kuheshimiwa mitazamo yao.

Kilichotufikisha hapa hakijaanza leo wala jana. Tunachokishuudia ni matokeo ya roho iliyopaliliwa na kunyeshewa maji kwa muda Sasa. Na kadri tunavyochelewa kuchukua hatua hali itakua mbaya Sana.

Siasa zetu zimekua chanzo Cha utengano huu. Sio kwetu tu siasa imekua chanzo Cha anguko la umoja wa kitaifa bali duniani kote siasa ugawa watu. Hili utokea kwa kuwa siasa pasina shaka ni ulaji na mamlaka. Wahenga husema palipo na ulaji hapakosi fitina, Ila ni wajibu wetu kuonyesha ustaarabu na utu.

Wazee wako kimya, watumishi wa Mungu tayari wamekubali ku take side na kuendeleza mpasuko huu. Wasomi wamekubali kubaki neutral. Wengine wamechagua kuwa kimyaa kabisaa ili kuzipa amani fake familia zao na kujihakikishia mkate mezani. Kifupi njaa na uchu wa madaraka umefubaza kalamu zao na kuamua kuisariti Taifa hili.

Nani anaweza kututoa kwenye janga hili?

Bila kupepesa macho JPM na LISSU wanaweza kulisahidia Taifa hili.

JPM- unazo nyenzo, unawajibika kikatiba, unawajibika kisiasa, na unawajibika kiimani kuongoza juhudi za kulijenga taifa hili na kuziba mpasuko. Kuchukua wajibu huu sio udhaifu na kujishusha Ila ni kuonyesha njia na kuwajibika. Utakumbukwa zaidi ukilifanikisha ili kuliko kuamua kukaa kimyaa. Heri wapatanishi maana wataitwa wana wa Mungu.

LISSU- Kama mwanasiasa unawajibika kikatiba kuilinda amani ya taifa hili. Unawajibika kiimani kusamehe na kuachilia. Unawajibika kiraia kutii na kukubali kunyenyekea mamlaka. Utakumbukwa zaidi kwa kuongoza maridhiano ya kitaifa kuliko kufanikisha mashindano.

Kwa wanaowazunguka wawili hawa, mnao wajibu wa kutuliza majeraha, kuponya nafsi zao, na kusisitiza malidhiano, na sio kuwajaza sifa, hasira na viburi.

Msione kwa kuwa mnafaidika leo kwa kushabikia umwamba huu mkaona haya ndo maisha. Hakika hiyo itakua dhambi kubwa sana mbele za Mungu na Jamii ya Watanzania.

Tunapenda kuona umoja na mshikamano wa taifa hili kuliko uhasama na maumivu tunayoyashuudia leo katika kona nyingi za taifa hili.

Mwisho wa waraka huu, nitoe rai kwa wanajeshi wanobeba silaha kwa jina la Tanzania kamwe mtusaidie kurejesha tumaini na heshima ya taifa hili. Tulisifiwa na mataifa mengi duniani coz jeshi letu liliheshimu uhai wa raia zake , na liliwalinda kwa adui awaye yote. Ila leo ni haibu kuona raia zetu wanauawa na wanajeshi wetu na maafisa usalama. Tafadhari mjizuie, mtangulize weledi na utu na muwalinde raia wa taifa hili bila upendeleo.

Nashusha kalamu yangu chini. Nimetimiza wajibu wangu na ninaomba record iwekwe bayana.

Heri mpatanishi maana ataitwa mwana wa Mungu.

Ainone:

1: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jonh Pombe Magufuli

2: Mh. Tundu Antipas Lissu

3: Marais wastaafu

4: Wakuu wa majeshi ya Tanzania

5: Viongozi wa vyama vya siasa

6: Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ukapimwe kidogo
 
Mkuu,

Wakutanishwe kwa sababu zipi ukiwaacha wengine 13 waliogombea Urais?

Unayetamani akutanishwe na mh. Rais je, amekiri kwamba uzushi wa tuhuma alioutoa hadharani kwamba alifanya makosa ya kijinai?

Baadhi ya tuhuma alizotoa Tundu Antipas Mughwai Lissu ni hizi ambazo anatakiwa azithibitishe kwenye mamlaka ya mahakama
1. Kupora ardhi hekari 25,000 huko Kihanga Karagwe akishirikiana na Innocent Bashungwa bila ushahidi wa tuhuma hizo
2. Kajenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato kwa ajili ya mama yake na mkewe
3. Kwamba aliamuru vyombo vya ulinzi na usalama yeye apigwe risasi;
4. Kwamba anateua viongozi mbalimbali kwa kada tofauti ambao ni ndugu zake au wanaotoka kanda ya ziwa pekee bila kuzingatia, sifa, vigezo, uwezo na utendaji bora wa kazi;
5. Kwamba ni mbaguzi wa dini kwa kuwanyima waislamu nafasi za uongozi na kupendelea wakiristo tu;
6. Kudhalilisha, kutukana, kufokea viongozi na maaskari wa vyombo vya ulinzi na usalama (kitendo hicho hakikuwa ni kukemea ikla kujivika mamlaka asiyokuwa nayo);
7. Kuchafua sifa za nchi ya Tanzania kwa sababu binafsi za kisiasa na washirika wake wenye nia OVU na taifa la Tanzania kwa kufiklia hatua kushawishi taasisi mbalimbali na wawakilishi wa mbalimbali kuisuia, kutoshirikiana nayo hasa viongozi wa ngazi za juu ili kufanikisha nia yake isiyo bayana kwa manufaa ya nchi;

Sasa wito wa mh. Tundu Lissu kufanya maridhiano kwa kitu gani kilichotokea kusababisha wakutanishwe wawili pekee wakati yeye ndiye aliyeongoza kumshambulia kwa tuhuma zisizothibitishwa wakato wote aliposimama jukwaani?

Tundu Lissu anatakiwa awe na nidhamu, mtiifu na aache kiburi, ujeuri, majivuno, dharau nakujiona msomi zaidi ya yeyote; alichokuwa anakionesha shuleni na JKT kule Makutupora ambako kutokana na misimamo yake kulikuwa na migongano mingi sana na makamanda (koplo an MP)
6. Kwamba
Umesema vizuri sana. Kitendo jamaa alichofanya hawa BAVICHA hawatakaa waelewe mpaka visikizio vyao visafishwe. Si ajabu Mr Mzungu kajisepea zake mapema.
 

AskProfWolff: Mussolini: From Socialism to Fascism



Source: Democracy at work

Ukikumbatia na kung'ang'ania umoja bandia usiokidhi vigezo rahisi vya uzalendo wa kweli, siasa safi na matarajio ya umma, basi utalazimika kununua ushawishi na uungwaji mkono wa wananchi kwa gharama aghali isiyolipika. JPM watajua uzuri wake hawa wazugaji wakiwa wamechelewa sana. Hata hawajui wanataka nini.
 
Back
Top Bottom