Rais Magufuli na Lissu wakutanishwe

Rais Magufuli na Lissu wakutanishwe

Mwizi wa kura, mjivuni, mjenga chuki, muuaji, mzandiki,na asiyefuata demokrasia hatufai. Tunataka Uhuru, Haki, na Maendeleo ya Watu. Atuachie Ikulu yetu.
Mashindano na kutosamehe uzidisha chuki . Tusitoe nafasi kwa hila Kama hizi. Utaifa na udugu kwanza
 
Sikubaliani na ushauri wako kwa sababu ya aya hiyo hapo. Umekiri na huo ndio ukweli.

Nimekuwa nikisisitiza kuwa Siasa katika demokrasia ya vyama vingi kwenye maskini au zinazoendelea ni dhana ya "wagawanye watawalike" (divide and rule). Upinzani si wa kupanua wigo wa Itikadi, Sera na Mikakati ya kimaendeleo ila wa wanasiasa kupata nafasi ya kuingia madarakani. Ushahidi ni kauli na matendo ya wanasiasa wa upinzani, kwa mifano ifuatayo:

1) Wamekuwa wakiitisha mikutano na wanahabari au kuandika kwenye kurasa za mitandao ya kijamii kudai Tume Huru ya Uchaguzi - nia ni kuwa na Tume itayowaweka madarakani na siyo wapiga kura.

2) Wameshindwa uchaguzi kwenye sanduku la kura wakahamasisha "maandamano yasiyo na kikomo" wakisahau kuwa kuna makundi ya jamii wanayodai yanaonewa (kutekwa, watumishi kunyimwa nyongeza za mishahara, nk) lakini hawakuhamasisha "maandamano yasiyo na kikomo".
3) Walioshindwa kwenye sanduku la kura wanajikusanya Dsm kuanzisha "maandamano yasiyo na kikomo" badala ya kwenye majimbo yao wanakodai wameibiwa kura ili wapiga kura wao wawaunge mkono, hakika nia yao ni ovu ya uvunjifu wa amani.

Je, hili kundi la wanasiasa unaotaka Serikali na vyombo vyake wakae meza moja ya majadiliano litawakilisha jamii au maslahi yao binafsi?
Hata kama,! Ila tunao wajibu wakuhimiza kusameheana na kujenga taifa
 
Hahaha mwizi unapaswa ukutane naye akiwa chini ya ulinzi wa polisi, au mahakamani au mahabusu, au jela kabisa.

Yani mkutane na mwizi aliyekuibia mnazungumza nini, akurudishie alivyokuibia, akutibu majeraha aliyokupa wakati akiiba au mnazungumza nini hasa?!

Hakuna haja kukutana na Magufuli.
 
Hizi ni porojo za alinacha..unakimbia nchi yako kwenda kwa wanafiki wa ulimwengu huu kisha wewe unataka akutanishwe na Rais!! Hivi huwa watu wengine wanawaza kwa kutumia nini?
Hakuna sababu ya kukutanishwa na mnafiki kama huyo. Kwanza hana sifa ya kuwa karibu na Rais.
Ni afadhali ungesema mbowe atleast we see a patriotic traits within him.
Not that colonial pupet.
We do not even want him in TZ.
Nenda kakutane nae wewe mkuu
 
Mwambie Lissu awe na siasa za heshima, lugha nzuri.akajifunze kwa Slaa

Nje ya hapo mtaomba po sana, mtaongea lugha zote, watu washa wa ignore

Kama Lissu wazazi wake wako ubelgiji sawa

Aache kuongea shits, mpaka anakufa baadae ata loose kabisa popularity kama Mrema

Yeye ndio ajishushe
Kila mmoja tuwasaidie watu hawa kulisaidia taifa liwe sehemu bora kabisaa pa kuishi
 
Hivi kwa lipi hasa mnamthamini Tundu!!

Ungeandika kuwa Tundu atatuchafulia nchi ningekuelewa sana. Huyu ni mjinga kama wajinga wengine tu. Nashukuru watanzania wamemwelewa ndiyo maana walipuza agizo lake la kuingia barabarani.

Hata hiyo kujifanya anatishiwa kuuawa ni mbinu ya kijinga ya kutaka kurudi makao yake makuu ya kuichafua nchi yetu. Ili wajinga wasijue kwamba ametoroka nchi. Iweje mtu aamuliwe kukuwa kisha mtu huyo huyo akupigie simu na kukwambia ameamliwa kukuua? Kuna Rais gani mjinga awe na wasiri wasiyo na siri?

Amepiga kampeni kwa zaidi ya miezi mi2 ikiwa ni mchana na usiku hakuuawa iweje auawe baada ya kampeni?

Huyo acha atapetape. Na ajue kuwa raisi siyo jambo la kutaka yeye bali ni jambo linalopangwa na Mungu, mfumo wa nchi na wananchi pia.
 
Kweli kabisa Binadamu tumempuuza na kumgomea ushetani wake.
Tanzania kaiona kama moto wa jehanam KAKIMBIA!
Akitaka maridhiano aje home kwanza azunguke nchi nzima kutubu mbele ya watanzania.
Tukimsamehe - ndo tutamruhusu aonane na RAIS wetu.
Acha kiburi na majigambo- tuiponye nchi yetu
 
Ndugu, CCM wamefika kiwango cha juu kabisa cha kujiamini na kiburi. Kwa hatua waliyofikia CCM hadi kufikia kuua watu na kuwapora maamuzi yao mchana kweupe alafu wakiambiwa wanaleta majibu ya kiburi, ngebe na jeuri sasa upinzani ni sahihi wachukue tu msaada kutoka nje. Hakuna wa kuwazuia CCM zaidi ya vyombo vya nje.

Tupelekane tu ICC ili watu wajue udhalimu haulipi
Ni njia ndefu ya kuliponya taifa
Tunaweza kuanza kwa malidhiano
 
Tundu Lissu hana athari yoyote nchini aendelee kuishi huko huko Ubeligiji Rais wetu hana muda wa kukaa naye Kuna miradi na mipango mingi ya kufanya ili kuendeleza nchi

Hayo mawazo yako ni mawazo mfu watzw wameamua kuchagua maendeleo na so matusi.

Rais panga Safi yako ya Uongozi tupige kazi Mambo ya Tundu Lissu tupilia mbali kabisa haya nafasi ndani ya miaka hii 5
Ushauri wako una hila ndani. mtu asiyependa amani ni mtu mbaya
 
Fascist / Fashisti ina maana kubwa na siyo kama inavyotumiwa kiutani utani. Utawala wa kifashisti kwa mfano unalazimisha sote kuunga juhudi hata kama juhudi hizo zinazofanyika tunaona kabisa zinatupeleka pabaya.

Utawala wa kifashisti hututaka tusihoji au kutumia bongo zetu bali 'tukishachagua' chama au mtawala basi hatuna tena nafasi ya kuhoji au kutumia bongo zetu bali kutekeleza maagizo ya mheshimiwa. Kwenda kinyume na hivyo tutahesabiwa wasaliti, tunakwamisha maendeleo, hatuna mapenzi na nchi, uzalendo wa mashaka n.k

Utawala wa kifashisti huenda mbali na kulazimisha viongozi wa dini kuunga na kutetea juhudi za mtawala na chama-dola, maana ktk utawala wa kifashisti hakuna chama cha kisiasa cha kweli ( hapa ikiwemo CCM pia ambayo tayari imeuliwa ) bali chama-dola CCM Mpya kinachoendeshwa kama idara ya serikali na watawala wachache wakubwa.

Tujiulize Tanzania haijafika hapo? Hatuoni viongozi wa kidini mmoja mmoja au kwa makundi ktk 'Kamati za Amani' au ' Kongamano za Viongozi wa Kidini kuzungumzia mafanikio ya miaka mitano' lakini huwasikii viongozi hao wa kidini wakikosoa kama haki haitendeki, raia kuumiza n.k

Wenye viwanda, biashara , wachimbaji Madini, Wasafirishaji wa Mizigo kwa Malori, Bodaboda n.k wote wanaundiwa 'Makongamano huru' kusifia hali nzuri ya kibiashara na mazingira mazuri yaliyopo kufanyia shughuli zao.

Tutafakari kuhusu utawala wa kifashisti kama upo au haupo Tanzania kufuatana na yanayoendelea toka mwaka 2016.
Ufashisti ni wewe ha timu yako wasalatamtaa mnaoshindwa kutambua ustawi na maendeleo ya Tanzania. Mtakujaga kugutuka wakati wengine ndo wanaondoka mchezoni!
 
Sishauri hata kidogo kwa rais mzalendo kama JPM kukutana na lissu(Jonas Savimbi) msaliti na mwenye chuki ambaye ana nia ovu juu ya taifa letu,kwanza lissu ana jipya gani hadi akutanishwe na jpm ,kwanini isiwe mahona,rungwe au membe? ,mtu aliyekataliwa na watanzania kwa asilimimia 80+ akutanishwe na rais kwa jipya lipi?

Mwacheni ale jeuri yake,lissu ni jamii ya watu wasiofaa kuigwa hata kidogo, na tena hili ni fundisho kwa viongozi wa vyama vya siasa kuwa licha ya ushindani wa kisiasa bado uzalendo unahitajika ,kwa hili la mbowe kumpa mtu ridhaa ya kugombea urais ilikhali mtu mwenyewe hana nidhamu ,uzalendo wala staha eti agombee urais wa jmt na baadae kukiua chama nifundisho kubwa sana kwake.
Punguza asira. Sisi bado ni ndugu
 

Napenda sana siasa za upinzani wenye hoja ila upinzani unaopinga maendeleo na kukejili maendeleo kila kukicha nasema hapana narudia tena hapana.

Tulionya humu mara kadhaa kwa spidi ya JPM inabidi wapinzani wabadili mbinu za kumchallenge kama kweli wanataka kuendelee kusikika lakini wao hawakusikia. Wakaendelea na mbinu zile zile walizozitumia enzi za utawala wa JK. Bahati mbay kipindi hiki wakajikuta wanaishia kuzusha mara kuna upotevu wa 1.5 tril, na kutengeneza matukio madogo madogo ya kutafuta huruma kwa wananchi kitu ambacho wananchi wengi waligundua ni uzushi.

Taifa ambalo wananchi wake bado wanashida kubwa ya maji eti wapinzani wanadai democracia, Taifa ambalo wanananchi wake zaidi ya asilimia 80 ni wakulima wanatumia zana duni za kilimo ikiwemo pembejeo eti wapinzani agenda yao kubwa ni democracia, taifa ambalo mpaka sasa kuna shule ambazo hazina milango sakafu wala madirisha achilia mbali umeme na miundombinu ya kujifunzia eti wapinzani agenda yao kuu ni democracia.

Wakati JPM akipambana kuimarisha maisha ya raia kwa siku zijazo kwa kuimarisha sekta ya miundombinu, ikiwemo ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli SGR, ukarabati wa reli MGR, ujenzi wa bwawa kubwa la la umeme la Nyerere 2115Mw, ujenzi wa daraja la Tanzanite, ujenzi wa dara refu kuliko yote EA daraja la Busisi nk, badala ya wapinzani kumuunga. mkono au hata kutoa ushauri wao wanapinga na kukejeli kana kwamba kinachofanyika hakina maana.

Kifupi wapinzani wa Tanzania hasa wa awamu hii ya tano wameshindwa kabisa kutoa mawazo mbadala wametumia mda mwingi kukosoa, kukejeli, kutukana na kutaka kukwamisha juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maamendeleo, ni vyema wakatafakari na wakaja na sura ya kizalendo sio kupandikiza chuki miongoni mwa raia ndani ya taifa hili, Namna viongozi wa upinzani walivyounzungumzia muuungano wetu ni jambi ambalo halikubaliki kabisa na sio jambo la kuzungumzwa na chama kilichojiandaa kuchukua dola.
You deserve Gold Medal of true patriotism. Thank you!
 
Mpasuko nyumbani kwako ukikosa cheo wewe ndio uite mpasuko kura za Lisu milioni moja akutane na Magufuli aliyepata kura milioni 12 waongee Nini?

Magufuli piga kazi
Ni moja ya watu myopic kabisaa. Wale wengine aliowapa mkono siku ya kupewa hati ya ushindi walikua na ata kura laki tano ?

Tunataka jamii yenye mshikamano, utengamo hauna faida kwa taifa
 
Back
Top Bottom