Nimesoma hoja zako hapa na nimekuelewa...Lakini ni wazi kuwa kuna issues nyingine inabidi ujiongeze zaidi...Kwa mfano katika masuala ya uhuru wa watu na suala la kuvifungia vyombo vya habari kwa kutaja machache tu....
Anayozungumza JPM kuhusu Libya ni kweli tupu...binafsi nilibahatika kufika Libya wakati wa Gadhafi na nikakaa Tripoli na maeneo mengine machache kwa karibu wiki mbili hivi...Ni siku chache kuweza kuifahamu nchi, lakini ni wazi Libya wakati wa Ghadafi ilikuwa ni 'heaven' ukilinganisha na hali ya sasa....Ni kweli Libya wakati wa Ghadafi walikuwa wanakosa mambo mengi ya anasa kwa vigezo vya nchi za magharibi...kama pombe, vyombo huru vya habari kwa, na yale mambo mengine ya anasa ambayo siwezi kuyaweka hapa...Lakini Libya wakati huo walikuwa na karibu kila kitu kwa bidhaa madukani..vyakula, nguo za bei rahisi kutoka Italy, Spain, Turkey na kadhalika...Kulikuwa hakuna tatizo la ajira..maji na umeme karibu ni wa bure na wanaume kulipiwa mahali wakati wa kuoa...
Ni kweli walikuwa hawana uhuru kwa maana ya kukosoa uongozi...sikuona pia uhuru katika masuala ya internet...hakukuwa na madawa ya kulevya...vyombo vya habari vilikuwa controlled na kadhalika...
Wamarekani na nchi za magharibi hawakupenda ustawi wa Libya...na pale Ghadafi alipojaribu kupendekeza kuwa dhahabu ndiyo itumike kwenye biashara ya mafuta, ndipo walipokula njama za kumuodoa....
Sijafika Libya ya sasa lakini kwa kupitia vyombo vya habari ni wazi Walibya wanajuta...hakuna serikali pale..Kule Benghazi nadhani wana serikali yao...kuna makundi mengi yenye silaha yenye itikadi tofauti na yanapambana yenyewe kwa wenyewe...mafuta yanachotwa ovyo na mabepari wa nchi za magharibi...
Ndiyo maana walibya wengi wanajuta kwa kuona kuwa walihadaiwa.....Pengine ni vema tujiulize hivi tunapodai uhuru tunamanisha nini???? Libya sasa wana uhuru wa kutukana viongozi, kuchukua silaha na kupigana na kuuana wao kwa wao...Yaani kilichoko Libya sasa ni vurugu...Je, sisi Tanzania ndio uhuru tunaoutaka??? Yaani tunataka uhuru wa kutotii mamlaka??? Tunataka uhuru wa ghasia???? Je, sisi watanzania tunataka hayo??? Uhuru ni jambo jema lakini uhuru pasipo wajibu ni vurugu....
Vyombo vya habari vina nafasi ya kujenga mshikamano na kukemea maovu, lakini vyombo hivyo vikianza kutumika katika kuhakikisha kuwa amani na usalama wa nchi unapotea ni lazima vyombo hivyo vya habari 'vishughulikiwe' kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za nchi yetu.....