Umejichanganya. Ukoo hauwezi kuwa kabila. Kwa hiyo Muyango ni ukoo na Msubi ni kabila. Katika wasubi kuna koo zinazopatikana kote mkoa wa Kagera na Uganda kwa Wanyankole. Mfano Basita, Bayango, Basindi, Bagara, Bahutu, etc. Kumbuka Msubi akiongea Mhaya na Mnyambo watamwelewa. Hii ni pamoja na Wazinza na hata Bakerewe unaelewa lugha yao. Kama labda babu yake alikuja na kufia pale si ajabu labda alikuja kama mpagazi. Kumbuka hawa Wasubi na Wazinza ni jamii ya Watsu au Bahima na si ajabu hata Wahutu kwa hiyo kama alikuja kama mpagazi wa kihutu basi ndo watoto wake wakatawanyikia Biharamulo