Rais Magufuli Mgeni Rasmi Uzinduzi Wa 'Nchi Yangu Kwanza'

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ inatarajiwa kuzinduliwa siku ya Ijumaa hii Disemba 8 2017 kupitia ‘Usiku wa Kitendawili’ mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Screen-Shot-2017-12-02-at-06.08.54.png

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto akifafanua jambo kuhusu Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’.

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kupitia Kikundi cha Sanaa cha Mpoto Theatre Gallery na wadau wa sanaa za Ubunifu ndio wataouratibu Usiku huo wa Kitendawili.

Akiongea na wadau wa sanaa katika Maandalizi ya Kampeni hiyo ya Kitaifa itayokuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere, Mrisho Mpoto amesema kampeni hiyo ina lengo la kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza ndani ya Taifa letu.

Alisema mambo ambayo yatayozingatiwa katika kampeni hiyo ni pamoja na kudhubiti na hatimaye kukomesha kabisa mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa Umma, kuongezeka kwa tuhuma za rushwa, kuibuka ufisadi, ubadhilifu wa mali za Umma pamoja kuongeza hari ya kufanya kazi na Uzalendo.

“Usiku wa Kitendawili utatumika kama jukwaa la kuwaleta pamoja watanzania pamoja na viongozi wao ili kukumbushana kuhusu wajibu na kujadili mustakabali wa Taifa. Kutakuwa na vivutio mbalimbali pamoja na wimbo maalumu kutoka kwa wasanii maalumu Mwaka Huu,” alisema Mpoto.

[HASHTAG]#Uzalendo[/HASHTAG] "Mimi ni mmojawapo wa waanzilishi wa kuhamasisha uzalendo kwasababu nimekataa kufa bila kuacha historia katika nchi yangu" Mpoto pic.twitter.com/a4zXJbiOTj

— Bodi ya Filamu Tz (@Bodi_FilamuTz) December 1, 2017

Aliongeza,”Tumekuja kuunadi Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ kwasababu tunaamini Uzalendo na Utaifa lazima uwepo ili kufanikisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ili kuunga mkono juhudi za Raisi Dkt. John Pombe Magufuli za kujenga Taifa lenye Uzalendo, Utu, Weledi na Uadilifu uliotukuka. Mimi ni mzalendo ndio maana hata kwenye hizi harakati nipo toka nimetoa wimbo wangu wa kwanza, ukiangalia nyimbo zangu zote ni za kuonganisha jamiii 120 za watanzani,”

Screen-Shot-2017-12-02-at-06.05.59.png

Maandalizi ya kampuni hiyo ya uzalendo

“Naamini kwenye kufanya kazi ambayo itawafanya watanzania pamoja na kizazi kijacho kitambue kuna watu ambao walifanya kazi kubwa kwenye hili taifa, kuacha alama ambazo haziwezi kufutika katika maisha ya historia ya nchi hii, kwa sababu hivi vyote ambavyo vinaenda kufanywa ni kufufua upya na kuiweka pamoja mitazamo ya watanzania ili kujenga Taifa la Wazalendo na Wachapakazi kuiga nyayo zilizoachwa na hayati Baba wa Taifa,” alifafanua zaidi.

Mpoto amesema lengo kuu la maadhimisho hayo kuambatana na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa kuanzia mwaka 2018 ni kutumia jukwaa hilo kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kujenga na kuendeleza Utaifa.

Alisema baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo wiki hii huko Dodoma, itafanyika kwenye mikoa yote nchini na itasimamiwa na Kamati za Utamaduni chini ya Uwenyekiti wa Mkuu wa Mkoa na Wilaya
 
Imani zake huyo mpiga dili

Nimemsikiliza Maulid Mtulia akitangaza kujiuzulu Ubunge wake kupitia CUF na kujiunga na CCM, nikakumbuka namna CCM haohao anaowasifia walivyotaka kumpora ushindi wake kwa mkono wa chuma, mwaka 2015. Nikakumbuka jinsi vijana wa UKAWA walivyompigania kwa jasho na damu hadi kuwa mbunge.

Nikakumbuka vurugu zilizotokea vituoni, polisi wakilazimisha vijana waondoke ili wamtangaze Azan. Lkn wafuasi wa UKAWA wakashikamana kwa umoja kumtetea Mtulia. Hawakuogopa mabomu, virungu wala risasi. Nakumbuka baadhi ya vijana walilazwa rumande, wengine walipigwa na kugeuzwa walemavu kwa sababu ya Mtulia, wakitaka matokeo yatangazwe.

Binafsi nilikuwa nina-oversee vituo kadhaa vya Dar, vikiwemo vya jimbo la Kinondoni siku ya uchaguzi tar.25/10/2015. Maulid hakuwa na mawakala wa kutosha. Kwahiyo Chadema ilimfadhili kwa kumpa mawakala.

Vijana wa Chadema kwa mwavuli wa UKAWA wakamsaidia kusimamia kura, kuzihesabu na kulinda matokeo. Mmoja wapo ni Wiseman Ficky. Huyu na wenzie walilala nje siku tatu, wakiumwa mbu na wakiishi kwa kunywa maji tu, ili kulinda ushindi wa Mtulia.

Nakumbuka baada ya kura kupigwa na majumuisho kuonesha ameshinda, Tume ilikataa kumtangaza, wakirudia kuhesabu kura mara tatu. Siku ya 4 ukaibuka mvutano kati ya vijana wa UKAWA na polisi pale viwanja vya Biafra. Usiku wa manane vijana wakapigwa mabomu ya machozi, virungu na risasi (hewani), lkn hawakutawanyika.

Nguvu ya umma ikawa kubwa. Wakaongezeka akina mama, watoto, wazee, kuhakikisha Mtulia anatangazwa. Hatimaye baada ya kukesha kwa siku 3, siku ya 4 akatangazwa kuwa Mbunge wa Kinondoni kupitia CUF.

Kumbukumbu hizi zimenijia baada ya kumsikia akisema anamuunga mkono Rais JPM na anaiunga mkono CCM. Nikajiuliza ni CCM ileile iliyomnyanyasa, kumdhalilisha na kutaka kumpora ushindi wake au nyingine? Ni CCM ileile iliyotumia vyombo vya dola kujeruhi wafuasi wa UKAWA waliokuwa wanatetea ushindi wake au ni nyingine?

Yuda alimsaliti Yesu kwa fedha, lakini dhambi ya usaliti ilimuandama hadi akaamua kujiua bila kula hata senti 5 ya pesa za usaliti alizohongwa. Anyway makwazo hayana budi kuja, ila ole wake yeye ayasababishaye.

Kwaheri Mtulia, nenda ulipopachagua lkn kumbuka kuna watu wali-invest jasho lao, nguvu zao, damu zao, na kuweka rehani maisha yao, mpaka ukawa Mtulia ambaye CCM wamekuona na kukutamani. Sauti za watu hao zitakulilia daima.!
 
Watanzania tuache upole tunachezewa,uzalendo upi hasa huku nasari amekoswa koswa kuuawa na Lisu yupo kitandani kwa kupigwa risasi uzalendo upi??sasa watanzania tuungane tuwapige mawe wendawazimu kama hawa ili wakisogea mtaani kwenu piga mawe ili akili iwarudi.
 
Nimemsikiliza Maulid Mtulia akitangaza kujiuzulu Ubunge wake kupitia CUF na kujiunga na CCM, nikakumbuka namna CCM haohao anaowasifia walivyotaka kumpora ushindi wake kwa mkono wa chuma, mwaka 2015. Nikakumbuka jinsi vijana wa UKAWA walivyompigania kwa jasho na damu hadi kuwa mbunge.

Nikakumbuka vurugu zilizotokea vituoni, polisi wakilazimisha vijana waondoke ili wamtangaze Azan. Lkn wafuasi wa UKAWA wakashikamana kwa umoja kumtetea Mtulia. Hawakuogopa mabomu, virungu wala risasi. Nakumbuka baadhi ya vijana walilazwa rumande, wengine walipigwa na kugeuzwa walemavu kwa sababu ya Mtulia, wakitaka matokeo yatangazwe.

Binafsi nilikuwa nina-oversee vituo kadhaa vya Dar, vikiwemo vya jimbo la Kinondoni siku ya uchaguzi tar.25/10/2015. Maulid hakuwa na mawakala wa kutosha. Kwahiyo Chadema ilimfadhili kwa kumpa mawakala.

Vijana wa Chadema kwa mwavuli wa UKAWA wakamsaidia kusimamia kura, kuzihesabu na kulinda matokeo. Mmoja wapo ni Wiseman Ficky. Huyu na wenzie walilala nje siku tatu, wakiumwa mbu na wakiishi kwa kunywa maji tu, ili kulinda ushindi wa Mtulia.

Nakumbuka baada ya kura kupigwa na majumuisho kuonesha ameshinda, Tume ilikataa kumtangaza, wakirudia kuhesabu kura mara tatu. Siku ya 4 ukaibuka mvutano kati ya vijana wa UKAWA na polisi pale viwanja vya Biafra. Usiku wa manane vijana wakapigwa mabomu ya machozi, virungu na risasi (hewani), lkn hawakutawanyika.

Nguvu ya umma ikawa kubwa. Wakaongezeka akina mama, watoto, wazee, kuhakikisha Mtulia anatangazwa. Hatimaye baada ya kukesha kwa siku 3, siku ya 4 akatangazwa kuwa Mbunge wa Kinondoni kupitia CUF.

Kumbukumbu hizi zimenijia baada ya kumsikia akisema anamuunga mkono Rais JPM na anaiunga mkono CCM. Nikajiuliza ni CCM ileile iliyomnyanyasa, kumdhalilisha na kutaka kumpora ushindi wake au nyingine? Ni CCM ileile iliyotumia vyombo vya dola kujeruhi wafuasi wa UKAWA waliokuwa wanatetea ushindi wake au ni nyingine?

Yuda alimsaliti Yesu kwa fedha, lakini dhambi ya usaliti ilimuandama hadi akaamua kujiua bila kula hata senti 5 ya pesa za usaliti alizohongwa. Anyway makwazo hayana budi kuja, ila ole wake yeye ayasababishaye.

Kwaheri Mtulia, nenda ulipopachagua lkn kumbuka kuna watu wali-invest jasho lao, nguvu zao, damu zao, na kuweka rehani maisha yao, mpaka ukawa Mtulia ambaye CCM wamekuona na kukutamani. Sauti za watu hao zitakulilia daima.!
hawa ndio walipaswa kuuwawa na sio wale wengine
 
Back
Top Bottom