Rais Magufuli kutembea na kipaza sauti chake kwenye Madhabahu yetu ni kutukosea Heshima, sisi TAG si Wauaji

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Salaam Wakuu.

Leo Rais Magufuli amekuja hapa Miyuji mjini Dodoma na kutoa Hotuba kwa baraza kuu la kanisa la TAG leo ikiwa ni kilele cha mkutano mkuu wa kanisa ambalo limetimiza miaka 81 tangu kuingia nchini Tanzania.

Kilichonisikitisha ni Kitendo cha Rais wetu kukataa kutumia Kipaza Sauti Kilichotumiwa na Mkuu wetu wa Kanisa, badala yake akaja na Kipaza sauti chake.

Baada ya Mkuu wetu wa kanisa kutoa Hotuba ya kumsifia rais wetu na kumpa Tuzo ya kupambana na Corona na kuitokomeza Nchini, alimkaribisha rais kuhutubia. Ile Rais anainuka, kabla hajfikia kipaza sauti, akatokea Mlinzi mmoja mwenye briefcase yenye kipaza sauti akafungua kwa namba akabadilisha ile iliyopo akaiweka chini. Kisha akaondoka. Akaja mwingine akaikotoka ili Baba Askofu mkuu aliyoitumia, akachukua na briefcase akaondoka navyo. Nmesikitika sana.

Hii imetuchafua sisi Waumini wa Dhehebu la TAG. Nmejiuliza maswali mengi.

1. Je, rais anahisi sisi kama kanisa tunaweza kumuua au kumuwekea Sumu kwenye Kipaza sauti?

2. Je, rais hana Imani na Kiongozi wetu Mkuu wa Kanisa,

3. Kwanini akienda kwenye Shughuli Nyingie kipaza sauti hakibadilishwi?

Naomba hili suala lisijitokeze tena.

KWANINI KWETU T.A.G TU? MIKUTANO MINGINE HAWAFANYI, HATA YA CCM

1597401896370.png

mic1.PNG
Mic2.PNG

 
Ukae ukijus kwenye msafara wa mamba na kenge wapo
Ila ujue askofu sio fundi mitambo
Mafundi mitambo wengi nivijana tu wamawdza kununuliwa na mabeberu ...kijana akipewa milioni20
Anaona kama kafika tayari mbinguni
Anamaliza kabisa biashara
 
Kwa uzoefu wangu, hilo ni jambo la kawaida sana, mbona haujahoji kwanini wameenda na hiyo stand (podium) ya kutolea hotuba yenye nembo ya ngao wakati kanisani kuna madhabahu au sehem ya kutolea hotuba?

Rais ana utaratibu wake kiprotokali.
 
Ukae ukijus kwenye msafara wa mamba na kenge wapo
Ila ujue askofu sio fundi mitambo
Mafundi mitambo wengi nivijana tu wamawdza kununuliwa na mabeberu ...kijana akipewa milioni20
Anaona kama kafika tayari mbinguni
Anamaliza kabisa biashara
 
Ukae ukijus kwenye msafara wa mamba na kenge wapo
Ila ujue askofu sio fundi mitambo
Mafundi mitambo wengi nivijana tu wamawdza kununuliwa na mabeberu ...kijana akipewa milioni20
Anaona kama kafika tayari mbinguni
Anamaliza kabisa biashara
Kwani Mungu hawezi kuzuia Hilo Jambo baya
 
Back
Top Bottom