Nimewaona Rais Magufuli, Prophet T.B Joshua na Profesa John Atta Mills

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
NIMEWAONA RAIS MAGUFULI,PROPHET T.B JOSHUA NA PROFESA JOHN ATTA MILLS.

Leo 13:15hrs 31/10/2021

Kisha nikatazama juu urefu wa ghorofa tatu nikawaona Rais Magufuli,Prophet T.b Joshua na Profesa John Atta Mills wakiwa wamevaa vazi jeupe wamevikwa wingu wakikaza mwendo kuelekea mbele,walikuwa kwenye ghorofa jeupe lenye urefu kwenda mbele sikuweza kuona mwisho wake, they seem to be very busy,they look very serious,ni kama niliona malaika,niligeuka pembeni kumuuliza mtu niliyehisi yupo pembeni yangu lakini sikumuona tukiwa sehemu ya kuingia kwenye makazi fulani ya ghorofa,sehemu ya kibanda cha mlinzi na nilihisi nipo na mlinzi na nilimuuliza swali "Wale hawawezi kudondoka" akasema hapana,lakini niliendelea kujiuliza mbona Mimi nipo hapa wao wapo kule juu,nilihisi Mimi nipo salama zaidi,niliendelea kuwaza pasipo kujua nilikuwa nawaza nini hadi nilipoamka asubuhi.

- Ibada mbinguni Ufunuo 4:1-11

Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni,na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta,ikasema,"Njoo hapa juu,nami nitakuonesha Mambo yatakayotukia baadaye." Mara nikakumbwa na Roho,Kumbe uko mbinguni kuna kiti cha enzi na juu yake ameketi mmoja,Huyo aliyeketi juu yake alikuwa kama almasi na jiwe zuri jekundu,Upinde wa mvua ulikuwa unang'aa kama zumaridi na ulikizunguka kiti cha enzi pande zote,kulikuwa na duara la viti ishirini na vinne kukizunguka kiti cha enzi,na juu ya viti hivyo wazee ishirini na wanne walikuwa wameketi wamevaa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani,Umeme,sauti na ngurumo,vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi,Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi,Taa hizo ni roho saba za Mungu,mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo,angavu kama jiwe ling'aalo sana.

Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka,kulikuwa na viumbe hai wanne,viumbe hao walikuwa wamejaa macho mbele na nyuma,kiumbe wa kwanza alikuwa kama Simba,wa pili kama ng'ombe,wa tatu alikuwa na sura ya mtu,na wa nne alikuwa kama tai anayeruka,Viumbe hao wanne walikuwa na mabawa sita kila mmoja,na walikuwa wamejaa macho,ndani na nje,Usiku na mchana bila kupumzika,huimba: "Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,Bwana,Mungu mwenye nguvu,aliyekuwako,aliyeko na anayekuja!" Kila mara viumbe hao wanne walipomtukuza na kumheshimu na kumshukuru huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi ambaye anaishi milele na milele,wale wazee ishirini na wanne hujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kumwabudu huyo ambaye anaishi milele na milele;na huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema; "Wastahili ee Bwana na Mungu wetu kupokea utukufu na heshima na nguvu,Maana wewe uliumba vitu vyote,na kwa matakwa yako viliumbwa na vipi."

- Tuombee kifo Chema

Kifo chema ni kile ambacho unajua unapokwenda,kwa imani umevipiga vita vilivyo vibaya,mwendo umeumaliza na imani umeilinda,imani si ile ya uislam na ukristu bali imani ya kwamba ninatenda sawa sawa na Mungu anavyopendezwa,upendo wa Mungu utakuwa kifo chema,utaona unapokwenda ukiwa ndotoni,utaliona wingi likishuka kuja kukufuata,muda wako wa kufa ukikaribia utaona na kwa ishara na matendo Mungu atakuandaa nawe utakufa kifo chema kama alivyokufa Mfalme Daudi,Mfalme Daudi alipokaribia kufa aliwaifa familia yake akawaambia Mimi nakwenda katika njia waliyokwenda Baba zangu Ibrahim,Isaka,Ishmael na Yakobo,nawaomba mkazishike njia za bwana.

-Kifo cha Rais wa Ghana,Profesa John Atta Mills.

Rais,Profesa John Atta Mills siku moja kabla ya kuondoka kwake duniani aliita Baraza lake la Mawaziri akaongea nao,baadae akaita familia yake akaongea nayo,akaenda kulala na akapumzika milele,watumishi wa Mungu akiwemo T.b Joshua walimpigia Simu siku chache kabla ya kuondoka kwake akimkumbusha ndoto yake ya wingu likishuka juu ya nyumba yake na kisha kuondoka nae,kiimani uko ni makaribisho mema ya shujaa wa Mungu hapa duniani katika ufalme wa Mungu,a warm welcome to heaven.

- Kifo cha Rais John Magufuli
Rais John Magufuli alienda likizo ya Krismasi kijijini kwao Chato, Geita.Rais John Magufuli akakaa uko kwa miezi miwili na baada ya likizo akaanza ziara Kanda ya Ziwa,akawatembelea Wananchi Mkoani Kagera, akarudi Kanda ya kati Dodoma, akaenda kuwasalimu Wananchi wa Morogoro akifungua viwanda na Soko kuu la Morogoro, Kisha akaja Dar es Salaam akionekana mwenye afya, akazunguka Dar es Salaam kufungua Stendi ya Mkoa, Kota za polisi na Soko la Kisutu baada ya hapo hatukumuona tena hadi taarifa ya familia iliposema aliita familia yake hospitali,akamuita Kardinali Pengo, Mkuu wa kanisa katoliki na akamuita Sheikh Mkuu, Kiingozi wa Waislamu, akasali nao pamoja baada ya hapo akaimba nyimbo na familia yake, akalala, akapumzika milele.

-Kifo cha Prophet T.b Joshua
Prophet T.b Joshua aliitisha mkutano mkubwa wa maombi wa familia yake na marafiki wa kanisa lake (Emmanuel tv partners) alikuja kwenye mkutano akionekana mwenye afya tele,akaanza na Neno "Time for every thing,there is time to come here to worship and time to return home" "kila muda na wakati wake,Kuna muda wa kuja kuabudu na muda wa kurejea nyumbani" baada ya hapo alianza kuongea na umati wa watu katika mkutano ule,baada ya muda kidogo akakabidhi microphone kwa mhudumu na kuelekea chumba cha maombi na uko akisali akapumzika milele,baadhi ya watu kwenye mkutano ule wakasema kabla hajaja Prophet T.b Joshua waliona miale ya moto minne mfano wa radi ikipiga kwenye bustani na malaika walitokea katika miale ile ya moto upande ambao alikuja kwenye mkutano na kuondokea,tunaamini ilikuwa ni namna nyingine ya kukaribishwa kwake mbinguni.

Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi,na kwa Mwanakondoo,Muumba Mbingu na dunia,na vyote vyenye uhai na visivyo na uhai,iwe sifa na heshima na utukufu na enzi,milele na milele,Amina.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effects of micro-financing on Poverty Reduction.
 
Kama yule tapeli Joshua alikuwa kwenye ndoto yako, basi bila shaka shetani atakuwa alihusika na ndoto hiyo. Sio yule Mungu wa haki tumjuae.
 
Ben Saanane hukufanikiwa kumuona?

Je waliojaribu kumuua Tundu Lissu umepata kufunuliwa kuwaona?
Hao mbona bado wapo hapa hapa duniani na tayari karma ishaanza kufanya kazi yake. Hauoni alieshambuliwa haoneshi kuguswa sana na kesi zao. Ashamjua m'baya wake lkn analazimika kukaa kimya ili kulinda ugali wake. Sumu haionjwi kwa ulimi kijana.
 
Wewe ni muongo mkubwa,na pengine unataka kuugua ugonjwa wa akili.
Magufuli hawezi kuwa sehemu moja na mtumishi wa Mungu,TB Joshua, Magufuli was a serial killer akae vp na mtumishi wa Mungu,?
Sijui hata Kama alipata muda wa kutubu
TB Joshua aliishi maisha ya anasa na utajiri wa kutupa na familia yake, huku wafuasi wake wakiishi maisha ya ufukara na umasikini wa kutisha . Hii ni kwa sababu yeye na genge lake walifanikiwa kuwahadaa watu wenye akili na mawazo kama yako. Katika dunia ya leo don't play with Nigerians pastors bro.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom