Rais Magufuli: Kawafundishe Mabalozi wenzako, Wajifunze namna ya kuishi na nchi ya Tanzania ambayo hababaishwi

Nyerere alikuwa anatumia lugha fulani kuwapa wazungu ngumi za uso na hapo hapo akiwaomba msaada, unakuta wazungu wanabaki wanacheka tu wanajua hii ni akili kubwa na msaada wanatoa.
Tuko page moja mkuu
 
Mkutano wa leo is nothing to do na tuhuma tulizonazo kwenye mahakama ya kimataifa kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Balozi wa UK hana uwezo wowote kuisafisha Tanzania...yeye ni mgeni tu kama wageni wengine walioalikwa pale.
 
Watanzania wenye Akili timamu lazima wakatae hayo maneno ya mtukufu lakini kumbuka wapo baadhi ya watanzania ni wanufaika wa huu mfumo wa kuwatesa baadhi ya wafanyabiashara kwa njia mbalimbali za kishetani hao ndiyo hufurahia kila neno litokalo kinywani mwa Mtukufu
Ndiyo maana wengi hawajipi stress kwa kuendelea kumfuatilia huyu Mzee. Hawezi kubadirika leo wala kesho, kuendelea kudhani labda kuna siku atabadilisha mtazamo sio rahisi.

Kwa Watumishi wa Umma pia ambao wanadhani huyu Mkulu atakuja kuwaongezea mishahara ni kujisumbua bure, hawezi kuongeza mishahara hadi 2025 anatoka. Ndiyo maana watumishi wajanja walioshtuka mapema wameamua kujiongeza na Ujasiliamali and in fact wana make.
 
Nashauri Mh. ajikite na utekelezaji wa ilani na ahadi zake hao jamaa aachane nao hata kama yeye binafsi hana mpango wa kwenda nchi yoyote huko Ulaya.

Hawa watu wakiamua kukufanyizia wana mbinu nyingi na michezo mingi, sio wa kuchokonoachokonoa! Kuwa na urafiki na China kusitufanye tukaamini China wanaweza kutusaidia kupambana nao wakiamua kukinukisha, mchina mwenyewe anawagwaya!
Kinachomsumbua ni "laana" ya uchafuzi. Nukta.
 
Rais wa Tanzania ndugu John Pombe Magufuli amemtaka Balozi wa Uingereza hapa nchini akawaeleze mabalozi wenziye hasa wanaopenda ku-tweet tweet kwamba Tanzania ni nchi huru na inayojiamulia mambo yake yenyewe na kamwe haiyumbishwi na haitayumbishwa na yeyote!

Pia, amempongeza Balozi huyo wa Uingereza kwa namna anavyotimiza majukumu yake hapa nchini kwa weledi na ndivyo wawakilishi nchi nyingenezo hapa nchini wanapaswa wawe.
Mungu mtu anaweweseka.
 
Hawa ndiyo walikuwa wanapinga mabeberu kwelikweli,sio hawa wachumba wa sasa hivi leo anapiga mkwara kesho anaenda kupiga magoti kuomba hela ya kutengeneza vyoo vya shule!
2670536.jpg
 
Nyerere alikuwa anatumia lugha fulani kuwapa wazungu ngumi za uso na hapo hapo akiwaomba msaada, unakuta wazungu wanabaki wanacheka tu wanajua hii ni akili kubwa na msaada wanatoa.

..Nyerere alikuwa anawazidi wazungu kwa hoja.

..alikuwa akiwakoromea kwa ku-support tawala za kibaguzi na za kidikteta.

..Nyerere alikuwa ni msafi, hakuwa na tuhuma za kuvunja haki za binadamu, au udikteta.

..Wazungu walikuwa wanamtambua Nyerere kwa usomi wake na walimpa tuzo mbalimbali na shahada za uzamifu za heshima.

..Magufuli amechafuka kwa rekodi mbaya ya kubinya demokrasia nchini, na kukiuka haki za binaadamu. Sasa hali hiyo ndio inampa matatizo na nchi wahisani na marafiki wa Tanzania huko nje.
 
Si afadhali ya mwanaume Magufuli anaweza kuongea. Nyie hapa mnaweza kusema lolote kwa wake zenu tu? Manina

..mwanaume kivipi?

..kama ni mwanaume angezuia mabalozi na kumkamata Tundu Lissu wakati amesindikizwa uwanja wa ndege.

..au angeingia ubalozi wa Ujerumani na kumkamata Lissu na kumpeleka mahakamani anakushtakiwa kwa kesi za uchochezi.

..mwanaume alikuwa NYERERE ambaye aliwahi kuvunja mahusiano ya kibalozi na Ujerumani na Uingereza.
 
Rais wa Tanzania ndugu John Pombe Magufuli amemtaka Balozi wa Uingereza hapa nchini akawaeleze mabalozi wenziye hasa wanaopenda ku-tweet tweet kwamba Tanzania ni nchi huru na inayojiamulia mambo yake yenyewe na kamwe haiyumbishwi na haitayumbishwa na yeyote!

Pia, amempongeza Balozi huyo wa Uingereza kwa namna anavyotimiza majukumu yake hapa nchini kwa weledi na ndivyo wawakilishi nchi nyingenezo hapa nchini wanapaswa wawe.



"Very" and "too" are both adverbs. They come before an adjective. The basicdifference is that "very" emphasizes the word that follows it. "Too" before a word means there is more than what is wanted.Apr 10, 2020
1611069966842.png

learningenglish.voanews.com › ...

Very and Too - VOA Learning English

 
Back
Top Bottom