Rais Magufuli kateleza kuomba viwanda vya pikipiki na Bajaji; tulitakiwa kuomba za dawa au Trekta

no sawa watuletee na lesen za india
 

Ebu jaribu kufikiri beyond enemy line.
Je unajua sekta nzima ya Bodaboda imetoa ajira nyingi kiasi gani?

Fikiria tena itakuaje iwapo serikali itapiga marufuku ajira hii.wangapi watakuwa jobless?

Am sick and tired to deal with people of your type.

Hapa kazi tu.
 

Nikweli, angeongezea light/heavy trucks assembly bila kusahau kijiji cha ICT. Bajaj wa-import tu, cha angeweka msisitizo kwenye sekta ya kumanfacture solar cell Panels, invertors na deep cycle batteries vyote hivyo vinatumika kwenye mfumo wa solar - huu umeme A Grid utachukua muda sana kufikia kila kaya nchini - mkombozi ni umeme jua tatizo initial costs ni kubwa mno.
 
Nilicho Muona akisema mimi, kwenye taarifa ya habari kupitia Itv, ilikua ni viwanda vya dawa na vifaa tiba

Hili la mambo ya bajaj sijui n ibilis yuko kazini au ni kweli

Sasa mleta mada kwa nini analeta taarifa za kutunga - sisi watu wa ajabu wakati mwingine.
 
kumbe ndio viwanda alivyomaanisha ?!
kweli Tanzania ya viwanda..
ngoja nikatafute kerosine nitarudi..
 
naona watu wanalitafsiri hili neno la hapa kazi tuu vibaya.Sasa hiyo nguvu kazi inayokufa kila siku kwa bodaboda ndo ziongezwe kisa ajira wakati hazipo walikua wanafanya nini?usishabikie kimahaba huko kwao hizo toyo zimesaidia nini ?viwanda ndo vinatoa ajira zenye risk ndogo sasa toyo tena si shughuli.
 
Vyovyote ilivyo, kama mheshimiwa aliahidi serikali yake itakuwa ya viwanda halafu anakaa hapa mpaka viongozi wa nje waje ndio awaombe wajenge hivyo viwanda itabidi tusubiri sana. Vinginevyo labda angekuwa anatembelea mataifa makubwa labda ingewezekana kuwashawishi hao wawekezaji Haiwezekani wewe ukae tu kwako huna mipango yoyote aje mgeni kwa utaratibu wake wewe ndipo uombe msaada. Je kama asingekuja hayo maombi yangejulikana vipi?
 
Agro

Tatizo kubwa la nchi hii ni export ya raw materials badala ya finished goods. Tuna- export mbao badala fanicha, pamba badala ya nguo, bulk black tea badala ya packed blended teas, matunda badala ya juice, madini badala ya vidani, mahindi badala ya unga, ngozi bdala ya viatu,mkoba, mabegi n.k n,k. Kwa hiyo priority yetu inatakiwa kuwa value additional factories haya megine yatakuja baada ya uchumi kupata multiplier effect ya viwanda hivi
 
Priorities za Magufuli kwa kweli zinanipa wasiwasi kama tutafanikiwa huko mbele.

Imagine, kununua Ndege za ATC badala ya kuwekeza kwenye kilimo!! Kufufua General Tyre badala ya kufufua viwanda vya korosho!!
 
Hata angeomba matrekta na madawa vado mngemlaumu tu mgesema anatembeza bakuli,ngulumbili hawana shukrani kabisa
 
Anataka kumakiza vijana viungo bodaboda walipigia kura ukawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…