Rais Magufuli kateleza kuomba viwanda vya pikipiki na Bajaji; tulitakiwa kuomba za dawa au Trekta

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Jana Rais Magufuli alimuomba Waziri Mkuu wa India aanzishe viwanda "assembling centre" za pikipiki na bajaji. Nafkiri ni vyema angeeomba zaidi katika eneo la dawa au trekta....

Dawa nyingi zinazotumika nchini zinatoka India, na ni bei ghali sana. Sasa ingekuwa vyema kama tukipata uzalishaji hapa, ingesaidia kupunguza gharama na zingepatikana kwa wingi...

Pili, kwenye eneo la trekta, lingesaidia wakulima wengi kupata matrekta kwa uraisi na pengine kwa bei nafuu na kupelekea kukua kwa kilimo..

Ila binafsi, pamona na kwamba Mimi ni mfuasi Mkubwa wa Rais Magufuli, naona sio sahihi kuomba assembling centre za pikipiki. Pikipiki ni janga kwa vijana, inauwa vijana wengi sana, inapelekea vijana wengi sana kuwa walemavu, ingawa kwa upande mwingine ni chanzo cha kipato kwa vijana wengi...

Kama hatujaweka mikakati madhubuti ya kuwasadia waendesha bodaboda sio sahihi kwa sasa kuomba assembling centre. Tungeanza na kuomba centre za dawa na trekta kutoma India...
 
Ndio tayari ameshaomba.
Inawezekana alikuwa na maana yake na faida zake kwa alivyoviomba
 
Elimu ya kuandika huna basi hata kusikiliza umekosa ndugu....Rais jana kasema ameomba waje kujenga viwanda vya dawa hapa nchini pamoja na vifaa tiba...hayo mapikipiki ni point za nyongeza...huku ni kukurupuka kwa mwendokasi

Mkuu ukipata na Video itupie
 
Nilicho Muona akisema mimi, kwenye taarifa ya habari kupitia Itv, ilikua ni viwanda vya dawa na vifaa tiba

Hili la mambo ya bajaj sijui n ibilis yuko kazini au ni kweli
 
sijaona au kusikia hiyo hotuba ila kama ameomba hivo na kusahau viwanda vya tractor kubwa na power tiller kweli amekosea maana karibu watanzania 80% wapo involved kwenye kilimo ila ni kilimo kile kilichokuwa kinafanyika kabla ya kuzaliwa Kristo yaani jembe la mkono au ngombe!
Unapozungumzia mapinduzi ya viwanda bila mapinduzi ya kilimo na bure kabisa. ni sawa na kununua gari bila injini. Anyway sijui sera zake lakini sijawahi kumsikia akiweka msisitizo kwenye kilimo kama sekta zingine. Tanzania tunaweza kuwa soko kubwa sana la chakula kwa nchi zinazotuzunguka ambazo hawajitoshelezi kwa chakula kutokana na hali ya hewa mbaya au machafuko ya kisiasa. Ndoto hiyo inawezeweza kutimia endapo tuta mechanize kilimo chetu,,,jembe la mkono au ngombe halitaweza kutusaidia hata kujitosheleza sisi wenyewe kwa chakula!!!
 
HIVI DAWA TUNASHINDWAJE KUTENGENEZA WAKATI KUNA MASPECIALISTS KIBAO WA LAB
unaweza kuwa na wataaalamu wa kutengeneza dawa lakini usiwe na capital (mataji wa kujenga hivo viwanda) na raw materials hapo ndipo dhana ya uwekezaji inaingia
 
sijaona au kusikia hiyo hotuba ila kama ameomba hivo na kusahau viwanda vya tractor kubwa na power tiller kweli amekosea maana karibu watanzania 80% wapo involved kwenye kilimo ila ni kilimo kile kilichokuwa kinafanyika kabla ya kuzaliwa Kristo yaani jembe la mkono au ngombe!
Unapozungumzia mapinduzi ya viwanda bila mapinduzi ya kilimo na bure kabisa. ni sawa na kununua gari bila injini. Anyway sijui sera zake lakini sijawahi kumsikia akiweka msisitizo kwenye kilimo kama sekta zingine. Tanzania tunaweza kuwa soko kubwa sana la chakula kwa nchi zinazotuzunguka ambazo hawajitoshelezi kwa chakula kutokana na hali ya hewa mbaya au machafuko ya kisiasa. Ndoto hiyo inawezeweza kutimia endapo tuta mechanize kilimo chetu,,,jembe la mkono au ngombe halitaweza kutusaidia hata kujitosheleza sisi wenyewe kwa chakula!!!
Yeye bado yuko kwenye kilimo cha jembe la mkono na kutegemea mvua za masika na vuli.
Ndiyo maana kila siku utasikia anasisitiza vijana mkalime bila kujua tabia nchi ilishaleta mushkeri siku nyingi
 
Jana Rais Magufuli alimuomba Waziri Mkuu wa India aanzishe viwanda "assembling centre" za pikipiki na bajaji. Nafkiri ni vyema angeeomba zaidi katika eneo la dawa au trekta....

Dawa nyingi zinazotumika nchini zinatoka India, na ni bei ghali sana. Sasa ingekuwa vyema kama tukipata uzalishaji hapa, ingesaidia kupunguza gharama na zingepatikana kwa wingi...

Pili, kwenye eneo la trekta, lingesaidia wakulima wengi kupata matrekta kwa uraisi na pengine kwa bei nafuu na kupelekea kukua kwa kilimo..

Ila binafsi, pamona na kwamba Mimi ni mfuasi Mkubwa wa Rais Magufuli, naona sio sahihi kuomba assembling centre za pikipiki. Pikipiki ni janga kwa vijana, inauwa vijana wengi sana, inapelekea vijana wengi sana kuwa walemavu, ingawa kwa upande mwingine ni chanzo cha kipato kwa vijana wengi...

Kama hatujaweka mikakati madhubuti ya kuwasadia waendesha bodaboda sio sahihi kwa sasa kuomba assembling centre. Tungeanza na kuomba centre za dawa na trekta kutoma India...
Anataka muendelee kuwa vilema
 
Back
Top Bottom