Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 950
- 2,866
Leo dola 1 sawa na tzs 2500 sawa na tofauti ya tshs 292 toka Hayati Rais Magufuli alivyoondoka (2500 - 2208 = 292) hii inasababishwa na kinachoendelea duniani juu ya dola,hivi sasa mataifa kama China yameanza kutumia pesa yao, Urusi vivyo hivyo na tumesikia habari ya brics(China, Urusi, India, Brazil, South Africa) kukubaliana kutumia sarafu moja, pengine ni mpango wa kuondoa nguvu ya dola duniani, lakini tusijifungie kwenye boksi la mawazo ya sababu hizo tu, twende kwenye sababu za kiuchumi,
Ku-import(kununua vitu vingi kuliko ku-export(kuuza) hili kwenye sababu za kiuchumi ni tatizo namba moja lakini, shida kubwa tumekosa ubunifu kabisa nashauri yafuatayo;-
1. Serikali lazima iwekeze kwenye madini iwe na migodi yake yenyewe.
Yaani watanzania tuchimbe na kuuza dhahabu, gesi, chuma nk Lakini kufanikisha hili ni lazima iwekeze kwenye utafiti wa kutosha nasisitiza utafiti wa kutosha, hii itasaidia kuingiza fedha nyingi za kigeni kwenye nchi yetu hasa uuzaji wa dhahabu.
2. Serikali iboreshe bandari ya Dar es salaam, tusiiuze bali tuwekeze wenyewe kwa kununua vifaa vya kisasa na kufanya kazi 24hrs lakini pia itengenezwe bandari kavu kubwa kabisa Morogoro ili mizigo inapotoka bandarini ipelekwe Morogoro wahusika wa mikoa ya kanda ya ziwa kati na nje ya nchi watachukua mizigo hapo. Hii itaongeza ufanisi wa bandari na kuwavutia wateja zaidi.
3. Serikali ni lazima iwekeze kwenye kilimo na viwanda ili kupunguza uagizaji wa bidhaa nje ya nchi, kwanza kutoa ruzuku kwenye pembejeo zakilimo na kuandaa mazingira wezeshi kwa wazawa kufungua viwanda vya bidhaa zinazozalisha kwa wingi nchini mfano mkonge, pamba, alizeti, chikichi na karafuu, tukifanya hivyo tutaongeza uzalishaji, tutapata fedha nyingi za kigeni na tutaongeza mzunguko wa biashara na fedha nchini.
Tuzungumzie matumizi ya dola kwenye manunuzi ya bidhaa kutoka nje ya nchi importation na sio manunuzi ya ndani ni sawa kuzuia matumizi ya dola kwa manunuzi na malipo ndani ya nchi lakini huwezi kufanya manunuzi ya nje kwa kutumia Tsh, mfanyabiashara akitoka Tanzania kwenda Uturuki kununua nguo atakwenda na dola kwakua ndio pesa unayoweza kuibadili na kupata fedha nchi yoyote duniani kwa urahisi, matumizi ya dola hayaepukiki.
Tuzungumzie reserve yetu ya taifa ukifuatilia data za BOT utaona, hifadhi ya fedha za kigeni Tanzania kwa sasa na baadae inapaswa itosheleze miezi mitano mpaka sita,
Tuzungumzie bibi, babu, Mama na dada wanaovaa nguo, hizo nguo zinatoka China nk
tunahitaji dola kuzinunua na kuzileta hapa Tanzania ili bibi, babu, Mama, Baba, Mimi na wewe tuzinunue na tuzivae.
Tuzungumzie bibi, babu, Mama, Baba, Mimi na wewe tukiumwa tunatumia dawa lakini hatuna viwanda vingi vya dawa, zinaagizwa nje Ili bibi, babu, baba, mama, Mimi na wewe tuzipate ni lazima ziagizwe nje kwa dola.
Tuzungumzie kilimo, bibi, babu, baba, Mama, Mimi na wewe tunahitaji mahindi Ili tupate mahindi tunahitaji mbolea, mbolea zinaagizwa nje ya nchi kwa kutumia dola.
Tuzungumzie usafiri sio? Bibi, babu, baba,Mama,Mimi na wewe Magari, pikipiki nk yanatumia mafuta lakini hatuchimbi mafuta,serikali inatumia fedha nyingi sana (dola) kuagiza mafuta ili bibi, babu, baba, Mama, Mimi na wewe tupande gari kwenda sokoni kununua mahitaji uliyoorodhesha, nadhani nimetumia lugha rahisi kuona thamani ya tshs yetu mbele ya dola.
Nimalizie kihesabu; ina tafsiri ya kuwa, tunatumia sana vitu vya nje kuliko wao kutaka vya kwetu, sijui ni kweli au rasilimali zetu tumezikalia ama sisi ni wajinga,labda tutaamka akija Magufuli mwingine, ila ningekuwa na maamuzi basi biashara zote za kuagiza vitu nje na kuingiza nchini ningezipiga chini na kuwapa kipaumbele wale wote wanaofanya biashara ya kupeleka vitu nje.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
- Bachelor of business administration in International business.
- Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.