Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,845
Inashangaza sana Raisi hataki ku-deal na kiiini cha matatizo yote ya nchi hii matatizo ambayo chanzo chake kikubwa ni mikataba mibovu na badala yake kila siku utamsikia kaibua hili na kesho kaibua lile na yanakoishia yote haya wengine hata wala hatuelewi.
Raisi angekuwa na dhamira ya kweli ya kunyoosha nchi kama anavyodai, basi angehakikisha Katiba mpya inapatikana maana hii katiba ya sasa ni chanzo kimojawapo kikubwa cha huu wizi na ufisadi unaoendelea hapa nchini pamoja na uwajibikaji mbovu wa watu waliopewa dhamana lakini cha ajabu swala la Katiba Raisi hana habari nalo kabisa kwa sasa.
Jambo lingine.Kama Raisi angekuwa na nia ya dhati ya kutuvusha watanzania basi angeangalia uwezekano wa kupeleka mikataba yote yenye utata Bungeni ili ipitiwe upya na pia utawala wake ungekuja na sheria inayotaka mikataba yote serikali inayoingia kwa niaba ya wananchi wake shariti ipite Bungeni kupata baraka za Bunge,Bunge ambalo ndio chombo cha uwakilishi wa wananchi.
Badala yake Raisi yuko kimya kabisa juu ya jambo hili kama vile halijui na wakati huo huo utamsikia kila wakati anahoji juu ya mikataba yenye harafu ya ufisadi!!
Binafsi mimi huwa simuelewi mh.huwa anasimamia nini na hata dhamira yake katika kile anachokita kunyoosha nchi kwangu ni utata mtupu.
Mimi namtahadharisha ya kuwa bila ku-deal na kiini cha matatizo haya,si ajabu kesho na keshokutwa hata hii mikataba inayosainiwa leo hii yeye akiwa madarakani, baadhi yake inaweza kuja kugundulika kuwa ina harufu ya rushwa na ufisadi na ikitojea hivyo sijui atamlaumu nani zaidi ya yeye mwenyewe.
Hata sheria za utumishi wa umma nazo zinapaswa kupitiwa vinginevyo hata hao mafisadi unaowatumbua (kama kweli wote ni mafisadi) utalazimika kuendelea kuwalipa mishahara japo hawako maofisini na wengine watakuja kukushinda mahakamani na ukalazimia kuwarudisha makazini na pengine hata kuwalipa na fidia.
Nchi zilizofanikiwa kimaendeleo sidhani kama zilifanikiwa kwa style ya mtu mmoja kuwa ni watchdog wa kila kitu katika nchi nzima badala ya kuwa na mifumo thabiti ya kuzibiti rushwa na ufisadi na inayowafunga watu kuwajibika.
Tukiendelea na mtindo huu wa kuibua tukio moja baada ya lingine badala ya kushughulika na viini vya matatizo yote haya,miaka mitano itaisha na hakuna la maana tutakolokuwa tumefanya na huenda tukajikuta tunawalipa watu fidia kwa kuvunja mikataba.
Tubadilike vinginevyo hatufiki popote na tunaweza kujikuta tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele.
Likiisha hili la mchanga wa dhahabu sijui litafuata tukio gani lingine.
Wacheni tusubiri.