Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Tatizo Tanzania na mara nyingi Afrika kwa ujumla, tumezoea kufanya mambo kwa mazoea au kwa matarajio kwamba kama leo tumekula basi hata kesho tutakula tu. Ndio maana wengi wetu mambo ya kuandika wosia hatutaki. Hatutaki kufikiri mambo mbele kiasi hicho, au kudhani tukifa leo au kesho kutakuwa ni tatizo kwa familia zetu tutakazoacha. Na mara nyingine hatudhani kama tunaweza kufa leo au kesho!
Ndio maana hili la raisi wa Tanzania katika mazingira ya Zanzibar kuwa na serikali na raisi wake, hatukulifikiria mbali, labda tukiona kwamba tulikuwa na raisi Mkapa, kisha Kikwete na baadae Magufuli, na mambo yalikuwa sawa tu. Tuliamini kwamba siku zote raisi wa Tanzania atatoka bara, japo makamu wake alitoka visiwani. Hatukuona kwamba raisi wa Tanzania anaweza kutoka visiwani ikiwa raisi aliechaguliwa toka bara atakufa akiwa madarakani na makamu wake toka visiwani akawa raisi wa Tanzania,au raisi wa bara.
Sasa, hili sasa la kuwa na raisi wa Tanzania toka visiwani lazima tukiri linatuletea matatizo mengi sana. Na chimbuko la matatizo haya ni ukweli kwamba kimsingi, raisi wa Tanzania ni raisi wa bara, na anapaswa kuwa mtu kutoka bara. Huu ndio ukweli. Na sababu mojawapo ni kwamba kwa muundo wa muungano tulio nao sasa, raisi wa Tanzania hana sauti tena na mambo ya Zanzibar.
Tukisema raisi ni wa Jamhuri yaa Muungano ya Tanzania hivyo anaweza kutoka bara au visiwani, huko ni kujidanganya. Jiulize, ni mambo mangapi ya muungano raisi Samia anaweza kuyatolea tamko ambalo itabidi raisi wa serikali ya Zanzibar atii na kutekeleza? Hakuna hata moja! Ona kwamba hata mkataba wa Tanzania na DP World haukuhisisha Zanzibar, kwa sababu raisi Samia hana mamlaka na bandari za Zanzibar japo zinasemekana kuwa chini ya muungano.
Sasa basi, kama kweli tunataka tuwe na raisi wa Jamhuri ambaye ana sauti bara na visiwani kuna mawili - aidha kusiwe na raisi wa Zanzibar, au kuwe na raisi wa Tanganyika. Na hii ndio inachochea baadhi ya watu kudai serikali ya Tanganyika.
Kama ambavyo watu hatutaki kuandika wosia, Tanzania hatukuwahi kufikiria nini kitatokea ikiwa raisi wa Tanzania toka bara atakufa, na tukiwa na makamu wa raisi toka Zanzibar anaepaswa kuchukua nafasi yake. Kama tungefikiria mbali ju ya hili, na tukijua kwamba raisi wa Tanzania ni raisi wa bara na anapaswa kutoka bara, basi tungepaswa kusema ikiwa raisi wa Tanzania atakufa akiwa madarakani, kama uchaguzi mkuu uko mbali zaidi ya miaka miwili, makamu wa raisi atakaimu nafasi ya raisi wa Tanzania katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja, ambapo ndani ya muda huo uchaguzi mdogo wa raisi utafanyika, pasipo kuwa na uchaguzi wa wabunge. Raisi mpya atakapochaguliwa, kaimu raisi ataendelea na nafasi yake ya makamu wa raisi, ikiwa raisi aliechaguliwa atatoka tena chama tawala; la sivyo kutakuwa na raisi mpya na makamu wa raisi mpya kama uchaguzi mdogo wa raisi utatoa raisi toka chama cha upinzani.
Sasa tukijua hili, na kuelekea uchaguzi wa 2025, ingependeza ikiwa Raisi Samia asigombee tena kiti cha uraisi wa Tanzania, bali CCM walete mgombea mpya kutoka bara na mgombea mwenza mpya kutoka visiwani. Najua wengi watasema ooh, Katiba haisemi hivi. Ndio, lakini CCM wakifanya hivi hawatakuwa wamevunja katiba, bali watakuwa wameinusuru Tanzania katika mitafaruku na issues nyingi zinazoendelea kutokana na uraisi wa Samia, akiwa raisi wa bara kutoka visiwani. Na kama raisi Samia ana uchungu na mapenzi na nchi hii, ni suala la yeye kusema jamani eeh, nimeamua sintagombea uraisi 2025 ili CCM ifanye mchakato mpya kupata wagombea wapya. Baadae hili linapaswa kuwekwa kwenye katiba.
Hakuna mtu asieona kwamba uraisi wa Samia analeta mitafaruku mingi mno. Kwanza watu wengi wa bara hawamwamini kwamba anafanya kazi kwa maslahi ya Tanzania bara na si Zanzibar. Pili watu wanaona anapendelea sana Zanzibar katika miradi na uteuzi. Tatu watu wanaona ameanza kutumia njia za Magufuli. Nne watu wanaona anashindwa kudhibiti viongozi mafisadi wa bara kwa sababu anataka support yao. Tano watu wanaona anaingiza sana watu wa Zanzibar kwenye nafasi za kazi za bara. Sita watu wanaona anatumiwa vibaya na ndugu zake toka nchi za kiarabu. Saba watu wanaona anajitajirisha sana binafsi na ndugu zake ndio maana hawezi kuwakemea viongozi mafisadi kwa sababu wanafanya anachofanya yeye, nk, nk.
Soma Pia: Tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano
Watu wengi wa bara wameanza kuona kuwa support anayopata Samia toka kwa watu wa bara ni kutoka kwa wale tu wanaofaidika na nafasi yake kama raisi wa Tanzania, watu ambao inasemekana wako tayari hata kuteka na kuua Watanzania wenzao ikiwa wataonekana kupinga utawala wa raisi Samia. Sasa hali kama hii si sawa kwa nchi yetu, na inazidi kuharibika. Na ni wazi CCM inajua hili ndio maana wanatumia nguvu kubwa na fedha nyingi sana kumfanyia Samia kampeni, kabla hata ya uchaguzi mkuu.
Raisi Samia, kwa heshima na taadhima, nakuomba ujitoe kwenye kugombea uraisi 2025 ili tujipange upya. Uwepo wako katika nafasi ya uraisi una mambo mengi mazuri yanayoonekana, lakini mabaya makubwa mengi yasiyoonekana!