Rais Magufuli hatofanya lolote ndani ya miaka 5

Rais Magufuli hatofanya lolote ndani ya miaka 5

Jmaaa hasomeki formula yake vizuri lakini kajitahidi baadhi ya mambo tusimkatishe tamaa na kukasirisha watu, mfano Wafanyakazi hewa, fyeti feki, madawati shuleni, naia yatafuata madarasa, ubadhirifu kupunguzwa, rushwa kadhaa mfano ya yule masamaki na ule wa risiti feki za milioni saba kwa dakika....mengine yanakuja

Tatizo la watanzania wanataka kila kitu kifanyike kwa siku mmoja na hawa jui kua ni hao wanai lalamika ndiio wanao angusha nguvu za raisi.
 
Ibilisi, ngoja niwe "mtetezi wa ibilisi". Kwa kweli hata mimi ninaona changamoto unayoielezea na jinsi ambavyo unahitimisha kuwa jpjm hajafanya chochote na hatafanya chochote. Mimi nataka niyofautiane na wewe kama ifuatavyo:
JPJM amefanikiwa kusafisha serikali kwa kuweka watu wapya karibu kila ofisi kubwa ili kuhakikisha haachi masalia ya Jk kama vile wote walikuwa hawafai.
Matendo na maneno ya JPJM na "wanafunzi" yanaonyesha kuwa makao makuu ya nchi hii yatahamia dodoma ndani ya miaka hii mitano, hata kama si kipaumbele cha taifa kwa sasa (na hata hakikutengewa pesa ya ki vile kwenye bajeti).
Raisi ameshaagiza ndege mbili kwa ajili ya kufufua ATC, bila hata kufuata sheria ya manunuzi ya umma kwa maana kwa namna fulani katiba inamweka juu ya sheria zote.
Mkuu, kwa kushirikiana na chama anachokiongoza wamebaka democrasia na kuhakikisha wapinzani hawawaambii wananchi mikakati yao ya kuchukua dola ifikapo 2020; na hivi leo TAL inasemekana amekamatwa huko ikungi kwa maagizo ya mamlaka za uteuzi wa RPC wa Singida.
Je, Umesahau jinsi alivyoifanya sukari ikaadimika sana katika nchi hii kinyume cha kawaida ya miaka mingi kwa sababu ya kupiga marufuku uagizaji wa sukari toka nje?
Je, umesahau jinsi alitumbua majipu tena kwa namna dhalili sana huku wadanganyika tukishangilia kama mazuzu.
Dah, umesahau alivyowaita "vil aza" watoto wetu wa UDOM, watoto wa wapiga kura masikini na wanyonge anajiapiza kuwatetea?
Yeye kwa kujua au kutokua anaona anafanya kazi nzuri sana na kuna wadanganyika wengi wanaounga mkono namba yake ya utendaji (kwa kujua au kutojua).

Kwa mifano hiyo machache (mingine ongezea mwenyewe) nihitimishe kwa kusema kuwa JPJM atafanya mengi sana yatakayowaumiza wengi ilimradi tu yanamfurahisha yeye na wachache wanaomtukuza na kuimba sifa zake. Wajibu wetu ni kuendelea kujipanga kisaikolojia maana jamaa ndo ameanza na hana wa kumwekea gavana.

Inawezekana hivi ndivyo Mungu ameruhusu tuongozwe? Mm mimi nina mashaka lakini hatimaye wakati utasema na historia itahukumu kwa haki.

Mungu ibariki Tanzania!
 
Kwa sababu huu ni utabiri wa ibilisi ngoja mimi nisikilizie Tu.ukitimia nitaamini kumbe na ibilisi ana maono
 
Nimekuwa nikasema kuwa under CCM no deep revolutionary, tutasubili sana, tena Magufuli atashindwa mbaya, na haya ni matokeo ya visasi na unafiki wa CCM. Najua hata nyie wafuasi wa chama cha Magufuli CCM mnajua. Endelea kucheza sarakasi na filam za Nigeria, Tutaeshimiana tu #TujengeUkutaSeptembamosi.
 
Pamoja na matatizo yake kwenye swala zima la demokrasia na haki za binadamu,kuna mengi aliyoyafanya ,anaonekana ana nia ya dhati shida ni njia ipi atumie ndio kikwazo ,halafu pia aache tabia ya kuwapiga watu mikwara ,yeye kwake kila mtu ni kijitu fulani hivi ,hao wanaomzunguka ni watu wazima wanaohitaji heshima pia ,mfano ni ile alipokwenda BOT ,alimuuliza Beno Ndulu swali utafikiri ni mwanae

Au lile la Mahiga na mkewe kisanga cha Trafiki ,unakuja public oh nimwambia na waziri sijui amkanye mkewe , ishu ya Wilson Kabwe na Makonda wake oh nitumbue nisitumbue ?"
 
Tangu aingie naona life lnazid kuwa tyt mfano mkwere aliacha sukari kg1 =Tsh 1800-1900 alipoapishwa huyo jamaa akaleta misifa yake now kg1 tsh 2500-3000.unafuu uko wapi ss!!
 
Kabla hata ya kumshukuru ninaye Muamini, naomba Mods Msiupoteze uzi huu ili iwe kumbukumbu katika jukwaa hili.

Wana Jukwaa, niseme na nikiri tu kwamba katika makosa yote ambayo aliyo fanya Kikwete katika mihula yake kama kashfa za ufisadi, kukithiri kwa rushwa, kushuka kwa thamani ya Shilingi, na hata mengine uyajuayo ninaweza kumsamehe na kuyasahau makosa hayo kabisaa.

Kosa kubwa ambalo hata nishikiwe bunduki ambalo sitaweza kumsamehe JK ni la kutuletea Magufuli. Nasema hivi kwa sababu Kkwete anamjua Magufuli fika.

Natambua kwamba majeraha ambayo aliyaacha Kikwete alipaswa kutuletea mtu wa kuyatibu kwa utaalamu na busara ya hali ya juu. Lakini Ninacho shuhudia mimi Majeraha yale yameanza kuongezeka taratibu na kuwa makubwa zaidi ingawa kwa njia nyingine tofauti na JK.

Magufuli huyu ambaye tunamuona Shujaa wa kupambana na Ufisadi na kutaka maendeleo ya gafla hatofanikiwa chochote zaidi ya kulalamika kwenye majukwaa na kipiga mikwara.

Naamini asilimia kubwa ya wanajukwaaa hili wengi ni wasomi. Na kama ni ndivyo naamini mnatambua kwamba nchi huongozwa na Mipango thubuti (Strategies) yenye kutoa dira na njia ya kufikia yale tunayo yataka.

Tuliambiwa serikali hii ni ya viwanda, serikali ya kutoa ajira kupitia viwanda, watu wafanye kazi (hapakazi tu). Lakini mpaka sasa hatuoni mikakati ya viwanda hivyo vitakujaje eidha wavijenge serikali au wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Mara nyingi tumemshuhudia waziri wa viwanda akisimulia kapokea simu nyingi kutoka kwa wawekezaji wa nje na tena wengine wamemfata kwenye ofisi yake wakitaka ardhi kwa ajili ya kuwekeza.
Ukweli ni kwamba wawekezaji wengi wameingia uoga na wengine kutokomeaa kutokana na uchumi wa nchi hautabiriki na hasa pia serikali kupanga bei za bidhaa za soko, kubana matumizi na kutoa vitisho vingi kwa wawekezaji waliopo.

Bado hali haijakaa sawa, tunaambiwa Serikali kuamia dodoma ndani ya mwezi mmoja tena kwa amri pasipo mipango yenye kukamilisha hilo. Bado najiuliza ajenda za awamu hii ni zipi hasa, yaani tuna target kufika wapi hasa?

Rais amekuwa akitoa matamko kila siku mpaka wakati mwingine anapoongea unajikaza mwili mzima ukihofu ataongea nini, yaani unaogopa asitoe kauli zenye ukakasi ambazo mataifa mengine kutushangaaa. Yaani haipiti siku bila kusikia Magufuli kasema nini.

Hakuna mipango na mikakati thabiti ya kutufikisha kule tunapo pataka au anapopataka yeye, inaonekana kwamba dereva tuliye naye anayo nia ya kufika ila hajui njia ya kupita kufika tunapotaka, anabahatisha njia, lakini mbaya zaidi abiria tuliopo ndani ya gari ni wachache tunaona tunapotea ila tunahofu ya kumweleza dereva huyu njia sahihi kwa maana mbili, kwanza tunajua hawezi kutusikiliza zaidi ya kichapo, pili abiria wengine ambao ni wengi watatubwatukia kwa matusi mengi na kutukejeli kwamba nasi tunautaa udereva.

Nimalizie kwa kusema kwamba, nchi hujengwa kwa misingi na mipango thabiti. Marekani ya leo anaweza kuongoza hata Jay Z au Kanye West na Marekani isitetereke, kwa sababu moja tu, Nchi ina mising, Kila Rais ajaye pamoja na ajenda zake hukua ajenda kuu za nchi kwenye meza yake ambayo lazima aitekelezee. kuna mengiya kueleza lakini naomba niishiee hapa, ila wote ambao tutausoma uzi huu tusipoteze kumbukumbu, hakuna kitakacho badilika iwe ni maisha bora, uchumi, huduma za jamii, demokrasia, haki za binadamu na vitu vingine vinavyo maanisha maendeleo, zaidi ya kudidimia.

Tutakwenda kwa mikwara na kuanzisha ajenda ambazo zitakufa kibudu kwa muda mfupi, na kwakua CCM ina take advantages ya uoga na umbumbumbu wa watanzania waliowengi, 2020 watabadili maneno tu, kwamba ni HAPA NI KAZI ZAIDI.

Ibilisi

Uko serious? Mbona miradi ya maendeleo iko mingi sana tena katika hatua za utekelezaji?...basi hata barabara tano toka Moroco mpaka Mwenge zishakamilika
 
mmmmh mi naogopa hata ku like. duuuh halafu kumbe ndio nimeisha comment.
 
Sitaki kuamin kama hata wewe umetoka kapa!
Mpwaaa kamaa nduguyoo anafanyaa yaliokuwepoo kitabuchakoo joithem kusaidia maendeleo wanapokosea tupigekelele lakini tupigekelele KISA IT ZA DILI AZIPITI TENA WAEEENDEEE WASIONEKANE KABISA

TUMUUNGE MKONO KWAMAZURI NANI ALIJUA WAFANYAKAZI HEWA ...NDOA HEWA ELIMU HEWA...HADI IDADI ZA WANANFUNZI WAVYUO NAOO HEWA..HAKUNA ....MWOMBEEN HUYUBABA MUNGU AMTIENGUVU KUMBUKA ANAYOFANYA AKUNA ANAEFURAHIA....MAANA KIZURI KINA.....MPENISIFA ZAKE SHIKAMOO DK JPM

POPOTE ULIPO
 
Juzijana tumeana treni mjini pugu...bado mbagala wanakuja wakimaliza ndiowanakuja zilenjia za guest zenu Sinza walinde hats hivi vigari vyamkopo msipaki kabla amjamalizia kulipa
 
Mkuu Ndio kwanza nimemaliza chuo mwaka huu, Sina mpango hata wa kuandaa CV ya kuomba kazi, nilicho somea ni ajira tosha, nilijua haya ,mapema.

Mark my words, hata watendaji aliowatumbua ambao wengi hakuna sababu za msingi hakuna mabadiliko yoyote tutakayo shuhudia kwa miaka hii mi 5
Kaa hivyo hivyo wakati meli ilishang'oa nanga tayari. Aliyofanikiwa kuyafanya katika mda mfupi ni ishara kwamba atafanikiwa.
 
Dah.....bado hamjakubali tuu...kunyimwa nafasi ya kupiga ndiyo mmechanganyikiwa hivyo? Mijitu ya wapi nyie mnaoishi kwa ndoto za kuwa DC au rc au mkurugenzi??? Mlijiaminisha sana mkaweka akili zenu zote huko kwenye upigaji sasa mnatapata kutafuta namna nyingine ya kuishi....JPM ndiyo huyo kafyeka mirija yenu yote YA WIZI na NDIYO MKOME SASA [emoji4]
 
Back
Top Bottom